Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,420
- 18,298
Spika Ndugai amesema haya,
Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza wala kuota kama nitakuwa Mwanasiasa, Mbunge na hata Spika ni Mungu tu ambaye katika uumbaji wake hutujua na kutupangia safari kadri anavyoona ni vyema, asanteni sana wana Kongwa, chama changu na Rais
Nakumbuka miaka niliyosoma Shule ya Msingi nilikuwa natembea Km 16 kwa siku 1, nimekulia maisha ya shida na dhiki, nikiwa mdogo nililala kwenye kitanda cha kamba na nyumba ya tembe, lakini baadaye nimesoma vyuo mbalimbali ndani na hata nje ya nchi
Nilipokuwa chuo cha MWEKA Moshi, nilikuwa mmoja wa Wanafunzi maskini sana, baadhi ya likizo sikuwa na nauli za kurudi Kongwa, nakumbuka jinsi ambavyo wenzangu walivyokuwa wakipanda magari kuondoka mimi nilikuwa najificha kwa aibu ya kuulizwa huna kwenu?
Mimi nyumbani nilikuwa mtoto wa pekee wa Mama yangu, tunapomaliza Bunge hili natamani ni-revenge sasa nirudi akanipokee, lakini bahati mbaya Mungu alishamchukua, kwahiyo wakati mwingine mnisamehe huwa napata hasira ninapokutana na mtu mjinga
Leo nimekuja na rafiki yangu, Mama umenivumilia sana, hata nilipokuwa ICU India alikuwa analala pembeni yangu masaa 24 amekaa kwenye kiti, amekuwa Daktari wangu muda wote, hakika wewe ni mke mwema, kwa kukopa maneno ya Dk Mpango, Asante sana kwa kunipa raha.