Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Ndugai ana pepo la ufukara ndio maana ana chuki na wenye mafanikio kuliko yeye
Mfuatilie uone utajiri alionao leo huyo ndugai,unatokana na kufanya biashara gani?Alisoma kwa shida,akaajiriwa tanapa na ndani ya utumishi wake akawa fogo ndipo akaenda kwao na kupata ubunge,baadaye naibu spika hadi uspika.
Takukuru matajiri wa CCM hawawachunguzi,wangekuja Anti Corruption Agents toka kokote duniani kuwachunguza wanaccm sidhani kama jela zingetosha.Rushwa na kujipendekeza ndiyo silaha yao.Wivu na ujambazi dhidi ya wapinzani wao.
 
Alidhani atabaki milele pale mjengoni, asepe zake aje Spika mtenda haki kwa Taifa lake.
Bashite.......all the way from KOLOMIJE! 😀

Everyday is Saturday........................😎
 

You are very right , Job ana inferiority complex syndrome , kwa waliosoma Goverment schools enzi hizo tunakumbuka namna watoto wa wafugaji na makabila ya pembezoni namna walivyokuwa wanakuja shule wakiwa wanyonge , mara nyingi walikuwa wanapenda kuwa wenyewe na ilikuwa ni nadra sana kujichanganya na wanafunzi wengine , kwanza hawakua na nguo nzuri zaidi ya sare , hawakua na pocket money , hawakuweza hata kukubaliwa kwenda disco [walikuwa wanachekwa hawajui kuvaaa ] ....na wengi shule zikifungwa walikuwa hawaendi kwao ......serikali ilikuwa ina sera maalum , hawa wengi walikuwa wakienda likizo ilihofiwa hawatarudi .....kwa kweli tumshukuru Mwalimu kwa kuleta usawa kama huo leo watoto waliokua wanyonge wamekua viongozi wakubwa, japo bahati mbaya wamejaa viburi

Nadharia sio lazima kuwa Job anamchukia Freeman bali tu pengine anataka kumuonyesha , maana kwa viwango Freeman alitoka familia ya kitajiri na pengine alikuwa kiongozi wa Starehe au michezo shuleni , watu wengi wajanja wajanja watoto wa dar au mjini walikuwa wana pilika za kuandaa miziki na kutoroka kwenda mjini...na watoto wanyonge kama Job walikuwa wanaonekana washamba na walijiona wanyonge mbele yao ....pengine sasa naye kapata mahali pa kumnyoosha mwenzake ...hata kama ni vyama tofauti huwezi kumfanyia mwenzako namna hiyo ..
Jakaya Kikwete naye alisoma Kibaha ila alikwa mkubwa kwao ...japo kwa viwango vyote yeye alikuwa mjanja mjanja akitokea Tanga School ....na hata walikuwa na urafiki mkubwa na mbowe kutokana na familia yao kuwa na ukumbi wa disco kuanzia Mbowe Club hadi Bilcanas ambapo Kikwete alikuwa mpenzi mkubwa hadi miaka akiwa waziri alikuwa akienda
 
Asirudi tena bungeni kamwe.
 
Amekuwa muungwana kutwambia kwanini ana hasira hasira hasa linapokuja swala la kushughulika na Mbowe na kundi lake

Nilichomsifu amekuwa muwazi mbele yetu na mbele ya familia yake

Naamini Mbowe kwa kukumbuka hali ya Spika ya enzi hizo atamsamehe bure maana waliosema maskini akipata matako hulia mbwata walimaanisha vitu vingi

Hata hivyo, Ni sahihi kuwa alivyo (uonevu, hasira, ubabe) kwa kuwa tu alipitia maisha magumu na kujificha wakati wenzake wakienda likizo?

Wa aina hiyo walikuwa wengi hata miaka ya 2000 nasisi tumesoma nao sio kwamba yeye ndo alikuwa maskini wa mwisho kuliko wote
 
Na watavunja jungu hasa, zaidi ccm
 
Kama sio Nyerere nchi hii kuna watu wangekua daraja la kutawaliwa tu , we must be grateful ....nikikumbuka unyonge waliokuwa nao wenzetu shule ....ni Tanzania tu pengine unakuta baadaye mnakutana kwenye fursa sawa .....kuanzia JKT hadi Chuo kikuu wote mnakuwa sawa ...aliyesoma Arusha School au Shaaban Robert na mzizima , waliosoma nje ...wote mnakutana kwenye maisha bosi wenu ni Job mtoto wa maskini aliyekulia nyomba ya tembe na kulalia ngozi ....nchi nyingine maskini na kizazi chake wataendelea kuwa maskini hadi mwisho wa dunia.......lakini baahati mbaaya sana baadhi ya viongozi walikuwalia kwenye umaskini uliokithiri wamekua na tamaaa sana na uonevu ....ni kufuru nadhani lengo la mwalimu kuweka sera sawia ilikuwa ni ili kwenye vyombo vya maamuzi kuwe na watu wanaowakumbuka maskini ...lakini kwa wengine ndio wanaongoza kwa tamaaa na matumizi mabaya ya madaraka tofauti na baadhi ya watu waliokulia kwenye utajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…