kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano anaweka rekodi ya kipekee katika historia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wajumbe wa Mkutano mkuu wa 10 kumchagua kuwa Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa chama hicho tawala. Tangu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasisiwe mwaka 1977, hakijawahi kuongozwa na mwanamke, bali Rais Dk. Samia Suluhu ambaye anachaguliwa leo katika Mkutano Mkuu wa 10 wa chama hicho.
Aidha alielezea juu ya utekelezaji wa ilani wa chama hicho kwa kipindi kifupi cha uongozi Rais Samia anasema
"Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2020 CCM iliahidi kuwa iwapo Watanzania watakichagua kazi ya serikali itakuwa ni kutekeleza ahadi zilizoainishwa ktk Ilani hiyo na kwa kweli kazi ya utekelezaji wa Ilani inaendelea kwa kasi kubwa"
Kuhusiana na uchaguzi unaofanywa na chama siku hiyo Rais Samia Suluhu anasema wajumbe wote waliochaguliwa kugombania ni washindi hata kwani waliaminiwa na chama kugombea nafasi hizo.
"Wote walioteuliwa kugombea nafasi walizoomba ni washindi, kwa sababu chama kimewaamini kuwa yoyote ambaye angechaguliwa ni mwanachama thabiti, na ambaye anaweza kuongeza nguvu yake katika kukijenga chama"
"Uchaguzi tutakaofanya hapa ni kielelezo muhimu sio tu cha ukomavu wa Demokrasia bali pia haki, usawa, amani na maendeleo, mambo ambayo ndio nguzo na itikadi za siasa zetu"- Dkt Samia Suluhu.