Historia: Je, wajua historia ya taifa la Thamud? kwanini watu wa mji huu waliangamizwa na Mungu?

Historia: Je, wajua historia ya taifa la Thamud? kwanini watu wa mji huu waliangamizwa na Mungu?

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Amani itawale.

Watu wa taifa la Thamud walipata kuishi katika nchi/mji uliofahamika kama Al-Hijr kaskazini magharibi mwa taifa la Saudi Arabia hivi leo.

Ni watu waliokuwa na nguvu sana na utimaku wa viwiliwili ,walikuwa na maarifa mengi ya ujenzi kiasi kwamba majumba yao waliyajenga kwa kuchonga milima. Mabaki ya mji huu yapo mpaka hivi leo. Wanasayansi wanastaajabu uwezo wa hii jamii ya watu waliopata kuishi katika eneo hili, miongoni mwa maswali wanayojiuliza na wanakosa majibu ni kuwa waliwezaje kuchonga milima na kutengeneza majumba makubwa kwa ufasaha mkubwa sana.

Mji wa Al-Hijr ulikuwa ukisifika kwa kuwa na Rutuba sana, wakazi wake walijikita katika shughuli za vilimo,ufugaji,ujenzi,biashara n.k pia ni mji uliokuwa katikati ya njia kuu za biashara ukiunganisha njia ya kutoka Yemen kuelekea Misri na Sham na maeneo mengine hivyo wakazi wake pia walinufaika katika masuala ya biashara na kupelekea kujizolea utajiri mkubwa.

Kama ilivyo ada kwa wanaadamu pindi wanapopata neema nyingi huanza kumkufuru Mungu na kufanya ufisadi na udhalimu mwingi katika ardhi. Ndipo Mungu alipoamua kuwaletea Mtume kutoka miongoni mwao ,aliyefahamika kwa jina la Saleh. Saleh alikuwa ni kijana mchamungu na alikuwa akifanya kazi kubwa ya kuwalingania watu wake wasifanye uasi na kufuru pia waache ukatili wa kupora wafanyabiashara na wasafiri waliokuwa wakipita karibu na mji wao. Watu wake hawakutaka kumsikiliza wala kuacha mienendo yao.

Mwiso waliendelea kumdhihaki sana huyo Mtume aliyetumwa kwao na kumwambia kuwa kama ni mtume kweli basi awaletee Muujiza mkubwa wa kumtoa ngamia jike mkubwa katika Moja ya jabali lililokuwa katika mji huo.
Saleh aliwaonya kuwa pindi waliletewa wale wanayoyataka wasije wakakanusha. Kweli Mungu alilipasua jabali na kuwatolea ngamia mkubwa sana . Ngamia ambaye hajawahi kuonekana katika uso wa dunia. Ila walipewa na masharti kuwa wapeane zamu katika kuchota maji kwenye kisima kikubwa (OASIS) ya mji huo. Siku moja wamuache ngamia anywe maji peke yake na siku nyingine watumie wao peke yao. Maziwa ya yule ngamia yalikuwa yanawatosha watu wa mji wote.

Hilo sharti moja liliwashinda kuvumilia na kupanga njama ya kumuua. Waliteua watu wenye nguvu kutoka katika koo na kwenda kufanya mauaji ambayo yalimkasirisha Mungu na kupelekea kuuangamiza mji wote na watu wake , kasoro Saleh na watu wachache waliomuamini.

Mabaki ya mji huo yapo mpaka leo katika karibu na mji wa al-Ula, kaskazini mwa Saudi Arabia ikiwa ni ukumbusho kwa vizazi na vizazi juu ya watu hao walioangamizwa.

View: https://m.youtube.com/watch?v=T1emV3ZTzUg&pp=ygUTYWwgaGlqcmkgc2V0dGxlbWVudA%3D%3D
 
SOMA HIKI KISA CHA WATU WA THAMUD , JINSI WALIVYOPELEKEWA MTUME KISHA WAKAMKATAA NA NINI ULIKUWA MWISHO WAO?

MUNGU ANAELEZEA HABARI ZA WATU WA THAMUD KATIKA KITABU CHA QURAN

Quran 7:73-79

Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu.

Na kumbukeni alivyo kufanyeni wa kushika pahala pa A'adi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi.

Waheshimiwa wa kaumu yake wanao jivuna waliwaambia wanao onewa wenye kuamini miongoni mwao: Je, mnaitakidi ya kwamba Saleh ametumwa na Mola Mlezi wake? Wakasema: Hakika sisi tunayaamini yale aliyo tumwa.

Wakasema wale wanao jivuna: Sisi tunayakataa hayo mnayo yaamini.

Na wakamuuwa yule ngamia, na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.

Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na kulipo kucha wakawa majumbani mwao kifudifudi wamekwisha kufa.

Basi Saleh akwaacha na akasema: Enyi watu wangu! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha.
 
ila huyo ngamia alikuwa wa maana sana!! Maziwa yake yalitosha mji mzima kweli???👿
 
Kwa jinsi Waarabu walivyo wabinafsi, mbinguni kungekua na pepo kweli na wale ma bikra 70 basi africa wasingetuletea Hii tamaduni yao wanaaita dini na porojo zao.

Wangekua wanatupenda wasingewafunga minyororo na kuwachukua watumwa huku waki-wahasi ili wasitembee na wanawake zao.

Dini ni utumwa, wazungu na waarabu wamehamisha ile minyororo waliyofungwa wazee wetu miguuni na mikononi wametunga kichwani kwenye akili.

Africa tuna story kibao ila tuliibiwa ili tumebaki kukariri za story za wenzetu ambazo ni uongo uongo mtupu.
 
Dini imetufikia kwasababu sio ya waarabu peke yao . Ni dini ya Mungu ametaka ifikie watu wote ndio maana ukienda america ,asia,europe,aftica kote utaikuta
 
Dini imetufikia kwasababu sio ya waarabu peke yao . Ni dini ya Mungu ametaka ifikie watu wote ndio maana ukienda america ,asia,europe,aftica kote utaikuta
Ukitoa Uarabuni hakuna sehemu imeshikilia uislamu kama africa na ukitoa ulaya hakuna sehemu imeshikiria ukristo kama Africa.

Cha ajabu hizo dini zote hazikuanzia afrika..

Je waafrica walioishivkabla ya dini hukumu yao ipoje?

Au africa haikuwepo kipindi zinaanzishwa?

Dini ni tamaduni za wageni na africa tuna tamaduni zetu.

Africa hizi dini za tulizoletewa hazitusaidii chochote, angalia mataifa yaliyokataa kupokea dini za kigeni mfano, China, Japan india, Korea, wapo vizuri kiuchumi kuliko mataifa mengi ya africa ambayo walikua sawa enzi hizoo dini ndio zinaingia
 
Hilo swali lako alipata kuuliza Firauni kumuuliza Mtume Mussa.

Quran 20:51-52
"[Pharaoh] said, "Then what is the case of the former generations?"
[Moses] said, "The knowledge thereof is with my Lord in a record. My Lord neither errs nor forgets."
(Firauni) Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?

(Mussa) Akasema: Ilimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau."
Watu wengi wanadhani kuwa watu waliopita hawakupelekewa mitume kuwaonya na kuwapa habari juu ya Mungu ila ukweli ni kwamba hakuna taifa lolote hapa duniani ambalo halijawahi kupelekewa waonyaji. Mungu anasema kuwa alipeleka mwonyaji katika kila taifa ,ili kuwalingania watu wamwamini Mungu na waache kumuabudu shetani ila vizazi vingi vilivyopita viliwakataa mitume ya Mungu na wengine walifikia mpaka kuuawa.

ALLAH anasema haya katika Quran

Quran 16:36
"
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha."

ALLAH anasema " kwa hakika " kwamba ni jambo lisilo na shaka ndani yake kuwa alipeleka mtume /mitume katika kila taifa na ujumbe ulikuwa ni mmoja tu Mwabuduni MUNGU na muepukeni shetani. Ila wengi wao walikataliwa na Mungu alikuwa akivifutilia mbali vizazi hivyo vya watu madhwalimu. Mwisho anatwambia tutembee katika maskani za mataifa yaliyopita ili tujionee ulikuwaje mwisho wao.

Miongoni mwa hayo mataifa ni watu wa Thamudi ambapo walimkataa Mtume wao , ALLAH akawafyekelea mbali na ukumbusho uliobaki ni hayo majengo yao.

Elimu ya vizazi vilivyopita anayo Mungu peke yake kwasababu yeye ndiye shahidi juu ya wanadamu wote na anajua mitume aliyoipeleka kila sehemu.

Mtume Muhammad anasema kuwa ALLAH ameleta mitume na manabii 124,000 hapa duniani na Muhammad ndiye Mtume na nabii wa mwisho aliyeletwa kwa ajili ya wanadamu wote
 
Ukitoa Uarabuni hakuna sehemu imeshikilia uislamu kama africa na ukitoa ulaya hakuna sehemu imeshikiria ukristo kama Africa.

Cha ajabu hizo dini zote hazikuanzia afrika..

Je waafrica walioishivkabla ya dini hukumu yao ipoje?

Au africa haikuwepo kipindi zinaanzishwa?

Dini ni tamaduni za wageni na africa tuna tamaduni zetu.

Africa hizi dini za tulizoletewa hazitusaidii chochote, angalia mataifa yaliyokataa kupokea dini za kigeni mfano, China, Japan india, Korea, wapo vizuri kiuchumi kuliko mataifa mengi ya africa ambayo walikua sawa enzi hizoo dini ndio zinaingia
mfano mzuri tu kuwa AFRICA ilifikiwa na dini ya Mungu ni katika kipindi cha Yusuf alipata kuishi Misri ambapo kulikuwa na jamii kubwa ya watu weusi na alikuwa akilingania watu wamwabudu Mungu mmoja.

Kipindi cha Nabii Suleiman bin daudi (a.s) alipeleka ujumbe kwa malkia wa sheba anbaye alikuwa akitawala eneo lote na Ethiopia mpaka pwani ya Yemeni kuwa wamwambudu Mungu mmoja na kuacha ibada za kuabudia jua.

Hawa ni miongoni mwa mitume na manabii wachache sana ambao ALLAH ametusimulia habari zao ila wapo wengi kufika 124000. walitumwa sehemu tofauti tofauti na mwanadamu hatakuwa na udhuru siku ya mwisho ya kuwa hajawahi kufikiwa na waonyaji.
 
Back
Top Bottom