Historia moja imebaki intact; hakuna Rais aliyefanikiwa kurithisha kiti cha Urais kwa amtakaye

Historia moja imebaki intact; hakuna Rais aliyefanikiwa kurithisha kiti cha Urais kwa amtakaye

Naomba kama Una link na hiko alichosema Mugabe unitumie..

JK alikuwa Mwenyekiti wa AU wakati Bush anataka kumlazimisha Mugabe ajiuzulu..

Nna uhakika JK alikuwa anawafanyia usanii kina Bush tukapata misadaa mingi kuliko nchi yoyote Africa..
JK katika hapo Kwa Sanaa na hadaa..za kisiasa.. anaweza kutabasam Kwa mtu nyoka kabisa
Hilo la kufanya hadaa ili tupate misaada mingi kuliko nchi yoyote Afrika siyo jambo la kujivunia, aidha kwa Kikwete mwenyewe, au kwa nchi analiyokuwa akiiongoza.

Kupewa misaada ni ishara ya udhaifu, na ni udhaifu kwa unayepewa msaada.
 
Kabisa hotiba ya kikwete ilikuwa defensive...alijaribu kuonesha kuwa Mzee kweli kafariki tarehe tajwa moja ili kuondoa sintofahamu kwamba alifariki before mentioned date...lkn pia alijaribu kujibu kuwa yeye na Mabeyo hawahusiki na tetesi zinazoendelea mitaani kuhusu kuforce kutangazwa kwa msiba as wananchi wanasema ilikuwa inatakiwa bado iwe siri hadi mambo fulani fulani yatimizwe..kuhusu Magu kuwa chaguo lake la kwanza alitaka kujibu kuwa hakuwa team Membe kama ilivyohamishwa...kwa mimi hayo yote ni maneno ya mwanadiplomasia nguli ila ukweli unabaki pale pale.
Umemaliza kila kitu.
Huyo ndio Kikwete halisi.
Ni muongeaji mzuri kuiridhisha hadhira.
Anajua kucheza muziki wa kisiasa.
Anajua kufake mambo sana.
Na jana pale msibani kudhihirisha hilo.
 
Njaa haina baunsa,hata ujitutumue vp kama hunahuna tu
Huna nini sasa? Kitu gani Tanzania haikuwa nacho hadi kwenda kupiga magoti? Mbona chini ya JPM hatukupata misaada hiyo na tumeishi? We unaamini kuna vitu vya bure duniani?
 
Watoto wa marehemu Jiwe hamna aliyezimia hata mmoja kasoro nyinyi mataga kuzimia huku mmeshikili a mifuko mkononi .
Amezimia na kamfuko cha sato mkuu kuna mwingine kazimia na soda mkononi....
IMG-20210324-WA0078.jpg
 
Katika Historia ya Tz
Jambo moja limekuwa linatokea mara Kwa mara..

Rais aliekuwepo madarakani kushindwa kumuweka anaemtaka anapoondoka...

Wengi walihisi Magufuli atatuwekea mtu wake akimaliza mda wake but haikutokea..

Nyerere alimtaka Salim..akatokea Mwinyi..

Mwinyi akamtaka Malecela akaibuka Mkapa..

Mkapa akamtaka Kigoda..
Akashindwa na mtandao wa Kikwete..
Kikwete akamtaka Membe..akaibuka Magufuli..

Magufuli hatujui alikuwa na Nani kampanga kichwani mwake Ila now
Tuna Samia...

Nna uhakika hata chaguo la Samiah
Halitapita ataibuka mwingine dakika za mwisho....

Hii ndo Tanzania....ukipanga hivi the ' ancestors 'wanapangua..

Wenye imani kama yangu tunafundishwa mamlaka pamoja na serikali za dunia hii zatoka kwa Mungu. Haijalishi sisi tunaonaje ila Mungu akisema ndio hakuna wa kusema hapana na akisema hapana hakuna wa kusema ndio

Wakati wao wanakaa vikao vinavyoonekana kujadili na kupanga wenzao wanakaa vikao visvyoonekana kuomba
 
Back
Top Bottom