Historia mpya ya TANU na Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Utangulizi

HISTORIA MPYA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA

Utangulizi

Nami nasubiri patulie In Shaa Allah nataka niandike jinsi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyochaguliwa kuongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika katika kikao cha watu watatu Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu mwaka wa 1953 na moja ya sifa kubwa iliyotajwa ni dini yake.

Wazalendo hao wote watatu waliokubaliana kumkabidhi Baba wa Taifa uongozi walikuwa Waislam, mmojawapo akiwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Kisha nitaeleza vikao vyote vya dua alivyoshiriki Baba wa Taifa pamoja na Waislam katika kumlilia Allah awape msaada Watanganyika washinde dhulma zote za Waingereza na Allah alikubali dua ya wenye kudhulumiwa.

Katika juhudi za kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TANU alipofariki mwaka wa 1968 magazeti ya TANU yaliandika kuwa Rais Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdul Sykes.

Hakikuandikwa chochote katika historia yake katika kuasisi TANU.

Ilikuwa Tanganyika Standard chini ya uhariri wa Mwingereza, Brendon Grimshaw ndiyo iliyoandika taazia na kueleza mchango wake katika kumtia Nyerere katika siasa za Dar es Salaam na kuunda TANU.

Mwaka wa 1981 Chuo cha CCM Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU walikataa kupokea "notes," zinazohusu mchango wa Abdul Sykes katika kuunda TANU.

Wanaona tabu kusema kuwa Abdul na mdogo wake Ally ndiyo waliompokea Nyerere nyumbani kwao mwaka wa 1952.

Iweje kadi ya Ally Sykes iwe no. 2 na ya kaka yake Abdul no. 3 na ya Nyerere no.1 tena kaandikiwa na Ally Sykes halafu ikawa hawa si waliunda TANU achilia mbali kuwa kadi 1000 za kwanza alinunua Ally Sykes kwa fedha zake.

Yako mengi.

Hivi sasa kuna bango limewekwa nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Mwananyamala linalosema kuwa ati TANU ilianzishwa ndani ya nyumba hiyo.

Mwaka wa 1988 nilipoandika makala katika Africa Events iliyomtaja Abdul kama mtu muhimu katika historia ya TANU gazeti zima lilikusanywa.

1576100604144.png
BARAZA LA WAZEE WA TANU KWA MAJINA.jpg
WATU MASHUHURI.jpg
SAFARI YA JULIUS NYERERE UNO 1955.jpg
NYERERE MTONI KWA CHAUREMBO.jpg
TATU BITI MZEE.JPG
MSHUME, MAX MBWANA....jpg
 
Mzee Mohammed Said Allah akupe afya njema
Uendelee kutupatia historia adhimu za nchi yetu kwa sisi vizazi vya sasa tusiojua lolote
 
Mzee Mohamed...Heshima yako.

Mimi ninadhani hizi harakati za Uhuru "tusibinafsishe" kwa watu wachache au tusizibandike sana suala la dini fulani na dini fulani,hili jambo likae kuwa watu wengi katika Tanganyika,iwe sehemu ya pwani au sehemu ya bara,walijitoa katika kusaidia harakati za Uhuru.

Hii alilosema Padre Maliva lina nafasi kubwa kuwa Wamisionari pia,kwa kutumia Askofu Attilio Betramino aliyekuwa kama Askofu Mkaazi wa Iringa wakati huo makao makuu yakiwa Tosamaganga na sio Kihesa,alitumika kutoa msaada wa pesa pamoja na makazi ya kuishi ya familia ya Nyerere,hasa mkewe na watoto.

Pale Tosamaganga,pembeni ya Kanisa kuna Jengo la Underground ambapo familia ya Nyerere ilikuwa inaishi,na aliyewatunza alikuwa Padre mmoja anaitwa Padre Jordan,ni mzima mpaka sasa,mwaka wa jana alifikisha miaka 100.

Hapa aliishi Mama Maria Nyerere na wanae,wakihudumiwa kwa shule na chakula,na watoto wa Mwalimu wakianza kusoma shule ya msingi Lupalama ambayo ipo mbele ya kanisa.

Ndani ya nyumba ile iliyo chini ya ardhi,kuna kumbukumbu nyingi na nyaraka za Julius,ni kwa sababu Kanisa bado halijataka kuzichapa au kuziachia nyaraka zile waziwazi.

Makao Makuu ya Shirika la Wakonsolata kule Torino,Italia,kuna kumbukumbu kadhaa za nyaraka zinazoonyesha misaada ya kifedha iliyokuwa inatumwa Tanganyika kwa Julius katika harakati za Uhuru.

Hii ni kusema kwamba,ama Mwalimu kwa kuweka siri,au kanisa kwa kutaka kutoonekana katika ushiriki wake wa Uhuru,haikujitangaza namna inavyotoa misaada ya kifedha kwa Mwalimu na harakati zake.

Ukipata wasaa,tembelea Tosamaganga,hojiana na Padre Jordan,mzee wa miaka 101,ana habari nyingi za maisha ya Nyerere Tosamaganga,harakati za Uhuru na familia ya Mwalimu.Padre Jordan alikuja Tanganyika miaka ya 1940's
 
Nadhani ukisoma vizuri maandisha ya bwana Mohamed Said utagundua kwamba yeye habinafsishi historia ya tanu bali anataka tutambue michango iliyofanywa na wazalendo hao ambao walianza harakati zao wakati mwalimu alikuwa anasoma.
Historia ya kweli ni ile inayotambua wale wote muhimu ambao bila kujitoa kwao tungesubiri miaka mingi kupata uhuru.
 
Nimekuelewa mkuu...labda sikuwa nimeelewa vyema.Ninadhani wote wanastahili kuenziwa
 
Nadhani kati ya mambo unayolalamikiwa Mzee said kwenye historia zako ni kwamba unajikita mno kwenye eneo moja ili hali inaonekana yapo mengi sana ambayo huenda hata wewe huyafahamu, na kwa bahati mbaya unataka jamii nzima ipuuze kwa yale usiyoyafahamu wafuatilie yale tu unayoyafahamu.

Hili la TANU na Sykes umelishikia mno bango, kama kina Sykes walitaka kuwe na TANU basi hilo halikuwezekana maana mpaka Mwalimu anajiunga nao aliikuta bado TAA ipo. Na TANU ilikuja kama hitaji la kubadili muelekeo wa TAA, na hakuna chama kipya kilichoasisiwa hapa, na sijui ni kwa nini unapenda sana kuchanganya Watu kwenye hili.

Labda pia utuambie ni kwa nini Abdul na Wenzake walitaka kuanzisha TANU ili hali TAA ilikuwepo?

Umekuwa mara kwa mara ukihusisha Mwalimu kupata uongozi wa TAA na dini yake na umeng'ang'ana sana hapo, hivi sifa ya Mwalimu ilikuwa ni dini yake tu? hivi ni jamii ipi unataka kuipotosha Mzee Said....kwamba hakuwa na ziada yoyote kuliko kina Sykes bali ni dini yake tu ndio iliyombeba.

Hivi Mwalimu bila kukutanishwa na kina Sykes asingefanya alichokifanya? isitoshe ni Mwalimu ndiye aliyewatafuta kina Sykes baada ya kuelezwa habari za TAA, Abdul Sykes ndiye alikuwa Katibu wa TAA hivyo ilikuwa ni lazima akutane na Abdul.

Mchangiaji hapo juu amekushauri uende Iringa upate baadhi ya mambo, wewe ni Mwanahistoria lakini kuna mengi umeyaacha nyuma.
 
Huyu ndio Padre mwenyewe ni mzee sana yupo Tosamaganga Iringa,
Anaitwa Padre Jorda,
Alizaliwa 10/11/1917...
Alipadrishwa 31 /08 /1947...kabla ya kuwa Padre,alikuja Tanganyika mwanzoni mwa miaka ya 1940's wakati wa vuguvugu la vita ya pili ya dunia,wakati akija alikuwa bado Mseminari na aliletwa kufanya utume Afrika,baada ya Upadre 1947,alikuja Tanganyika mpaka leo
FB_IMG_1576161723278.jpg

Na hapa ndio Kanisa la Tosamaganga,ambalo Watoto wa Mwalimu waliishi na kusoma katika udogo wao.Huyo ni Padre Mkonsolata Tosamaganga.Hii picha inaeleza nafasi na ukaribu wa Wamisionari(chini kwa chini) katika harakati za Uhuru.Na picha hii Wakonsolata wameitoa sababu mwaka huu 2019 walikuwa wanatimiza miaka 100 toka waje na kuweka makazi yao Tosamaganga,hivyo wameanza kutoa nyaraka na picha kidogokidogo baada ya miaka 100 kupita toka waingie Tanzania
FB_IMG_1576161706522.jpg
 
Nadhani kati ya mambo unayolalamikiwa Mzee said kwenye historia zako ni kwamba unajikita mno kwenye eneo moja ili hali inaonekana yapo mengi sana ambayo huenda hata wewe huyafahamu, na kwa bahati mbaya unataka jamii nzima ipuuze kwa yale usiyoyafahamu wafuatilie yale tu unayoyafahamu.

Hili la TANU na Sykes umelishikia mno bango, kama kina Sykes walitaka kuwe na TANU basi hilo halikuwezekana maana mpaka Mwalimu anajiunga nao aliikuta bado TAA ipo. Na TANU ilikuja kama hitaji la kubadili muelekeo wa TAA, na hakuna chama kipya kilichoasisiwa hapa, na sijui ni kwa nini unapenda sana kuchanganya Watu kwenye hili.

Labda pia utuambie ni kwa nini Abdul na Wenzake walitaka kuanzisha TANU ili hali TAA ilikuwepo?

Umekuwa mara kwa mara ukihusisha Mwalimu kupata uongozi wa TAA na dini yake na umeng'ang'ana sana hapo, hivi sifa ya Mwalimu ilikuwa ni dini yake tu? hivi ni jamii ipi unataka kuipotosha Mzee Said....kwamba hakuwa na ziada yoyote kuliko kina Sykes bali ni dini yake tu ndio iliyombeba.

Hivi Mwalimu bila kukutanishwa na kina Sykes asingefanya alichokifanya? isitoshe ni Mwalimu ndiye aliyewatafuta kina Sykes baada ya kuelezwa habari za TAA, Abdul Sykes ndiye alikuwa Katibu wa TAA hivyo ilikuwa ni lazima akutane na Abdul.

Mchangiaji hapo juu amekushauri uende Iringa upate baadhi ya mambo, wewe ni Mwanahistoria lakini kuna mengi umeyaacha nyuma.
Umejenga hoja vizuri.Nimekuelewa
 
Huyu ndio Padre mwenyewe ni mzee sana yupo Tosamaganga Iringa,
Anaitwa Padre Jorda,
Alizaliwa 10/11/1917...
Alipadrishwa 31 /08 /1947...kabla ya kuwa Padre,alikuja Tanganyika mwanzoni mwa miaka ya 1940's wakati wa vuguvugu la vita ya pili ya dunia,wakati akija alikuwa bado Mseminari na aliletwa kufanya utume Afrika,baada ya Upadre 1947,alikuja Tanganyika mpaka leoView attachment 1289918

Na hapa ndio Kanisa la Tosamaganga,ambalo Watoto wa Mwalimu waliishi na kusoma katika udogo wao.Huyo ni Padre Mkonsolata Tosamaganga.Hii picha inaeleza nafasi na ukaribu wa Wamisionari(chini kwa chini) katika harakati za Uhuru.Na picha hii Wakonsolata wameitoa sababu mwaka huu 2019 walikuwa wanatimiza miaka 100 toka waje na kuweka makazi yao Tosamaganga,hivyo wameanza kutoa nyaraka na picha kidogokidogo baada ya miaka 100 kupita toka waingie Tanzania
View attachment 1289920

Kwa namna hii basi ni dhahiri kuna mengi bado kama jamii hatujayafahamu...shukran Mkuu.
 
May Day,
Yote unayosema kuhusu mimi ni kweli.

Mimi nimeshangazwa kuona juhudi zilifanywa kumfuta Abdul Sykes katika historia ya TANU.

Hii ndiyo sababu iliyonifanya chembelecho kuibebea bango historia yake hadi nikaandika kitabu cha maisha yake (Minerva Press, London 1998).

Kitabu hiki kimepata umaarufu mkubwa na kinakwenda toleo la nne.

Kitabu hiki kikawarudisha wengi waliokuwa wamefutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na pia kusababisha baba yake kutiwa katika Dictionary of African Biography (DAB) (Oxford University Press New York, 2011).

Mwaka huo huo pia Abdul na Ally Sykes wakatunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kutambua mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Naamini na ndiyo wengi wenu mkajua ala kumbe historia tunayosomeshwa siyo?

Mlipata kumjua Abdul Sykes au Hamza Mwapachu katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Au mlipata kumsoma Sheikh Hassan bin Ameir katika uhuru wa Tanganyika?

Au mlipata kumjua Iddi Faiz Mafungo mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955 na misukosuko aliyotiwa na Waingereza wakati anahangaika kusafiri kuchangisha fedha za safari hii?

Leo nasikia ati kuna fedha zilichangwa mahali fulani na watu fulani kwa ajili ya safari hii.

Sasa kama fedha zilikuwapo ile mikutano hadi tisa ya usiku nyumbani kwa Abdul Sykes wakati wa kuandaa safari hii kutafuta fedha ilikuwa ya nini?

Kwa nini basi TANU ikamtuma Iddi Faiz Tanga kwenda kukusanya fedha nyingine kutoka kwa Mwalimu Kihere na Special Branch wakamkamata Turiani wakati akirejea Dar es Salaam?

1576207039683.png

Mwalimu Kihere

Haya mambo yalikuwa yakifanyika majumbani kwetu tunayajua vyema ndiyo maana hatukubali kuona zinaletwa historia ambazo hazilingani na tunayoyajua.

Wewe unalalamika kwa nini nimemwandika sana Abdul Sykes mimi nalalamika kwa nini kafutwa kwenye historia na kwa nini historia yake inakutoeni raha?

Katika juhudi za kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TANU, alipofariki mwaka wa 1968 magazeti ya TANU, Uhuru na The Nationalist yaliandika kuwa Rais Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdul Sykes.

Hakikuandikwa chochote katika historia yake katika kuasisi TANU.

Binti yake Aisha"Daisy" aliumizwa kwa hili alilofanyiwa baba yake na akaamua kuandika historia ya baba yake.

Siku hizo mwanafunzi University of East African Dar es Salaam.

Mwalimu wake, John Iliffe akamtuliza akamwambia alipe muda jambo hilo lake.

Ilikuwa Tanganyika Standard chini ya uhariri wa Mwingereza, Brendon Grimshaw ndiyo iliyoandika taazia na kueleza mchango wa Abdul Sykes katika kumtia Nyerere katika siasa za Dar es Salaam na kuunda TANU.

1576207366665.png

Sunday News 20 October 1968

Mwaka wa 1981 Chuo cha CCM Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU walikataa kupokea "notes," zinazohusu mchango wake katika kuunda TANU.

Notes hizi zilikuwa za mwanajopo wa uandishi, Hassan Upeka aliyemhoji Abdul Sykes miaka mingi nyuma kuhusu historia yao.

Hivi sasa kuna bango limewekwa nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Mwananyamala linalosema kuwa ati TANU ilianzishwa ndani ya nyumba hiyo.

Mwaka wa 1988 nilipoandika makala katika Africa Events iliyomtaja Abdul kama mtu muhimu katika historia ya TANU gazeti zima lilikusanywa.

Nadhani tumeelewana.
Nashangaa sana.

Mimi nimeandika historia ya TANU chama ambacho kina mafungamano makubwa na historia ya wazee wangu lakini wewe unataka niandike historia hii kama utakavyo wewe iwe.

Hili haiwezekani.

Si umemsikia mtu kaeleza TANU ya Tosamaganga?

Mimi nani nimzuie?

Ila kwangu mimi ninachoweza kusema ni kuwa hiyo ni historia mpya ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nasema ni historia mpya kwa kuwa inapishana na historia ya TANU ya Abdul Sykes inayoanza na kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929.

Kwa ajili hii basi tutakuwa na historia mbili tofauti za Mwalimu Nyerere katika TAA na TANU.

Ya kwanza ni hii ya yeye kuijua TANU nyumbani kwa Abdul Sykes 1952 na hiyo nyingine ya Tosamaganga bila shaka itakuwa baada ya kukutana na viongozi wa kanisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Mohamed Said nashukuru sana kwa kutuelimisha kuhusu jinsi uhuru wa Tanganyika ulivyopatika na pia umeeleza kwa undani watu mashuhuri enzi hizo walioshiriki kufanikisha uhuru wetu. Mimi swali langu kwako ni hili mbona karibu wote waliopambana nikinukuu ulivyotuelimisha hakuna aliyepata nafasi ya uongozi baada ya uhuru kupatikana ina maana Bwana Nyerere raisi waTanganyika huru aliwatosa? Balaza la mawaziri la kwanza baada ya uhuru wamo akina Kawawa na wengine wengi lakini jina la Kawawa sijaliona katika simulizi zako vipi unatuelezaje kuhusu hilo.
 
Benta,
Hukumuona Kawawa kwa kuwa hakuwapo katika kipande hicho cha historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Historia inawezaje kuwa mpya?
Keyser....
Historia inaweza kuwa mpya pale inapoletwa historia nyingine ambayo inapingana na historia iliyokuwako.

Historia hii inaweza kuwa ''corrective,'' yaani inasahihisha historia iliyokuwa si kweli au inaweza kuwa yenyewe ni historia ambayo si ya kweli.
 
Kipi sasa Mzee wangu kinaweza kutupa kipimo cha kujua historia gani ni ya kweli na ipi si ya kweli??Kwa mfano hiyo aliyotoa Padre Maliva tunaweza sema si ya kweli au tunasema inaongezea pale ambapo historia iliyokuwepo iliishia?
 
Barufu,
Njia nyepesi kabisa ya kupima ''credibility,'' ya historia ya TANU ni kusoma historia zote zilizoandikwa kuhusu TANU.

Nyaraka ya awali kabisa katika historia ya TANU ni mswada wa kitabu alioacha Kleist Sykes (1894 - 1949) kabla ya kufariki kwake.

Mswada huu ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973) ndani ya kitabu hiki utasoma historia ya Kleist Sykes kama ilivyoandikwa na mjukuu wake Aisha ''Daisy,'' Sykes na mchango wake katika siasa za Waafrika wa Tanganyika.

Mswada huu unaeleza historia ya kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929.
Nadhani unafahamu kuwa chama hiki ndicho kilichokuja kuzaa TANU mwaka wa 1954.

Kleist wanae Abdu, Ally na Abbas wote hawa wameona kila kitu katika kuundwa kwa TANU wenyewe wakiwa washiriki.

Hili la kwanza.

Pili hawa watoto wa Kleist ndiyo waliompokea Mwalimu Nyerere nyumbani kwao mwaka wa 1952.

Hapa tunaweza kurudi nyuma katika historia ya TANU kuanzia mwaka wa 1945 wakati wa WW II wakati Abdul na Ally Sykes wako Burma.

Kumbukumbu za Sykes mbali na kuwa na historia ya African Association zinaeleza kuwa Abdul Sykes alikuwa na fikra ya kuunda TANU toka Burma na mkutano wa mwisho ambao askari wa KAR 6th Battalion waliazimia kuunda chama cha siasa ulifanyika Kalieni Camp, nje kidogo ya Bombay India, mkesha wa Christmas 1945 wakati wanasubiri kurudishwa Tanganyika baada ya vita.

Taarifa hizi zipo katika shajara ya Abdul Sykes ya mwaka huo.

Lakini ukitaka kupata taarifa zaidi za harakati hizi za kuunda TANU ni muhimu pia ukajua historia ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) na mchango wake katika kuwahamasisha vijana wasomi wa nyakati zile kuhusu kudai uhuru wa Tanganyika.

Mchango huu wa Mwapachu ulifikia kileleni mwaka wa 1950 yeye na Abdul Sykes walipofanya mapinduzi na kuondoa uongozi wa Thomas Plantan aliyekuwa Rais wa TAA na Clement Mtamila Katibu wake.

1576554785874.png

Thomas Plantan
Habari zaidi ya kipindi hiki ambacho ulifanyika uchaguzi na Dr. Vedasto Kyaruzi akachaguliwa kuwa Rais na Abdul Sykes Katibu unaweza ukausoma katika mswada wa Dr. Kyaruzi, ''The Muhaya Doctor.''

Unaweza pia kupata historia zaidi ya kipindi hiki katika kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika, '' (1965).

Ikiwa utapita kwenye rejea hizi zote haitakuwa kazi kubwa kwako kujua ukweli wa historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nimeandika historia ya TANU kutokana na kumbukumbu za Sykes na kitabu hiki kina mengi ambayo hayakuwa yanafahamika kabla.

Mfano mmoja ni mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Chief Kidaha Makwaia kutaka kumtia Chief Kidaha katika uongozi wa TANU kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru.

Unaweza kusoma kitabu hiki kujua kina nini tofauti na historia iliyozoeleka.

1576554451684.png
 
Huyu ndio Padre mwenyewe ni mzee sana yupo Tosamaganga Iringa,
Anaitwa Padre Jorda,
Alizaliwa 10/11/1917...
Alipadrishwa 31 /08 /1947...kabla ya kuwa Padre,alikuja Tanganyika mwanzoni mwa miaka ya 1940's wakati wa vuguvugu la vita ya pili ya dunia,wakati akija alikuwa bado Mseminari na aliletwa kufanya utume Afrika,baada ya Upadre 1947,alikuja Tanganyika mpaka leoView attachment 1289918

Na hapa ndio Kanisa la Tosamaganga,ambalo Watoto wa Mwalimu waliishi na kusoma katika udogo wao.Huyo ni Padre Mkonsolata Tosamaganga.Hii picha inaeleza nafasi na ukaribu wa Wamisionari(chini kwa chini) katika harakati za Uhuru.Na picha hii Wakonsolata wameitoa sababu mwaka huu 2019 walikuwa wanatimiza miaka 100 toka waje na kuweka makazi yao Tosamaganga,hivyo wameanza kutoa nyaraka na picha kidogokidogo baada ya miaka 100 kupita toka waingie Tanzania
View attachment 1289920
Nashindwa kushangaa bin kuelewa hapa kitangulizi wa ukoloni akawe muondoa ukoloni,,,,
 
You're so self-centered, namekufuatilia makala zako ila sasa naamini kuna uongo wa makusudi na exaggerations alimradi kufanikisha adhma yako.
Kama hauko flexible kupokea yale usiyoyafahamu, hiyo mikutano na michango ya 'Kariakoo' ambayo japo na yenyewe ilikuwa na sehemu ya harakati za uhuru ni wajinga tu watakaoamini ndiyo ilikuwa 'kila kitu' mpaka uhuru kupatikana.
Kulikuwa na michango mingi na harakati nyingi kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika, hata makanisa yalishiriki kwa kiwango kikubwa sana.
Nitakusapoti tu pale ambapo kuna watu au matukio yamefutwa kwa makusudi ili kupotosha umma,hilo si jambo sahihi kabisa. Lakini na wewe lazuma uwe na utayari wa kuyapokea yale usiyoyafahamu.
May Day,
Yote unayosema kuhusu mimi ni kweli.

Mimi nimeshangazwa kuona juhudi zilifanywa kumfuta Abdul Sykes katika historia ya TANU.

Hii ndiyo sababu iliyonifanya chembelecho kuibebea bango historia yake hadi nikaandika kitabu cha maisha yake (Minerva Press, London 1998).

Kitabu hiki kimepata umaarufu mkubwa na kinakwenda toleo la nne.

Kitabu hiki kikawarudisha wengi waliokuwa wamefutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na pia kusababisha baba yake kutiwa katika Dictionary of African Biography (DAB) (Oxford University Press New York, 2011).

Mwaka huo huo pia Abdul na Ally Sykes wakatunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kutambua mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Naamini na ndiyo wengi wenu mkajua ala kumbe historia tunayosomeshwa siyo?

Mlipata kumjua Abdul Sykes au Hamza Mwapachu katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Au mlipata kumsoma Sheikh Hassan bin Ameir katika uhuru wa Tanganyika?

Au mlipata kumjua Iddi Faiz Mafungo mkusanyaji wa fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955 na misukosuko aliyotiwa na Waingereza wakati anahangaika kusafiri kuchangisha fedha za safari hii?

Leo nasikia ati kuna fedha zilichangwa mahali fulani na watu fulani kwa ajili ya safari hii.

Sasa kama fedha zilikuwapo ile mikutano hadi tisa ya usiku nyumbani kwa Abdul Sykes wakati wa kuandaa safari hii kutafuta fedha ilikuwa ya nini?

Kwa nini basi TANU ikamtuma Iddi Faiz Tanga kwenda kukusanya fedha nyingine kutoka kwa Mwalimu Kihere na Special Branch wakamkamata Turiani wakati akirejea Dar es Salaam?

View attachment 1290346
Mwalimu Kihere

Haya mambo yalikuwa yakifanyika majumbani kwetu tunayajua vyema ndiyo maana hatukubali kuona zinaletwa historia ambazo hazilingani na tunayoyajua.

Wewe unalalamika kwa nini nimemwandika sana Abdul Sykes mimi nalalamika kwa nini kafutwa kwenye historia na kwa nini historia yake inakutoeni raha?

Katika juhudi za kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TANU, alipofariki mwaka wa 1968 magazeti ya TANU, Uhuru na The Nationalist yaliandika kuwa Rais Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdul Sykes.

Hakikuandikwa chochote katika historia yake katika kuasisi TANU.

Binti yake Aisha"Daisy" aliumizwa kwa hili alilofanyiwa baba yake na akaamua kuandika historia ya baba yake.

Siku hizo mwanafunzi University of East African Dar es Salaam.

Mwalimu wake, John Iliffe akamtuliza akamwambia alipe muda jambo hilo lake.

Ilikuwa Tanganyika Standard chini ya uhariri wa Mwingereza, Brendon Grimshaw ndiyo iliyoandika taazia na kueleza mchango wa Abdul Sykes katika kumtia Nyerere katika siasa za Dar es Salaam na kuunda TANU.

View attachment 1290347
Sunday News 20 October 1968

Mwaka wa 1981 Chuo cha CCM Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU walikataa kupokea "notes," zinazohusu mchango wake katika kuunda TANU.

Notes hizi zilikuwa za mwanajopo wa uandishi, Hassan Upeka aliyemhoji Abdul Sykes miaka mingi nyuma kuhusu historia yao.

Hivi sasa kuna bango limewekwa nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Mwananyamala linalosema kuwa ati TANU ilianzishwa ndani ya nyumba hiyo.

Mwaka wa 1988 nilipoandika makala katika Africa Events iliyomtaja Abdul kama mtu muhimu katika historia ya TANU gazeti zima lilikusanywa.

Nadhani tumeelewana.
Nashangaa sana.

Mimi nimeandika historia ya TANU chama ambacho kina mafungamano makubwa na historia ya wazee wangu lakini wewe unataka niandike historia hii kama utakavyo wewe iwe.

Hili haiwezekani.

Si umemsikia mtu kaeleza TANU ya Tosamaganga?

Mimi nani nimzuie?

Ila kwangu mimi ninachoweza kusema ni kuwa hiyo ni historia mpya ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nasema ni historia mpya kwa kuwa inapishana na historia ya TANU ya Abdul Sykes inayoanza na kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929.

Kwa ajili hii basi tutakuwa na historia mbili tofauti za Mwalimu Nyerere katika TAA na TANU.

Ya kwanza ni hii ya yeye kuijua TANU nyumbani kwa Abdul Sykes 1952 na hiyo nyingine ya Tosamaganga bila shaka itakuwa baada ya kukutana na viongozi wa kanisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You're so self-centered, namekufuatilia makala zako ila sasa naamini kuna uongo wa makusudi na exaggerations alimradi kufanikisha adhma yako.
Kama hauko flexible kupokea yale usiyoyafahamu, hiyo mikutano na michango ya 'Kariakoo' ambayo japo na yenyewe ilikuwa na sehemu ya harakati za uhuru ni wajinga tu watakaoamini ndiyo ilikuwa 'kila kitu' mpaka uhuru kupatikana.
Kulikuwa na michango mingi na harakati nyingi kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika, hata makanisa yalishiriki kwa kiwango kikubwa sana.
Nitakusapoti tu pale ambapo kuna watu au matukio yamefutwa kwa makusudi ili kupotosha umma,hilo si jambo sahihi kabisa. Lakini na wewe lazuma uwe na utayari wa kuyapokea yale usiyoyafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Qwy,
Unaweza kuamini upendavyo.

Siku zote mimi huwaambia wanaonisoma na kupinga haya ninayowaeleza kama ninavyoyajua kuwa si lazima wala si muhimu kwangu kwa wao wakaniamini.

Kwa miaka mingi walikuwa wakiamini historia rasmi na hakutokea mtu kuipinga.

Lakini mimi nilipokuja na historia ya kweli na ni kweli kwa sababu wazee wangu walihusika katika African Association hadi kuja kuunda TANU kwa hiyo ninajua mengi hapo ndipo waliposimama kupinga historia hii.

Mimi sina tattizo ya kupokea nisiyoyafahamu lakini pale ninapoona kuwa hayakubaliani na historia ya TANU ya wazee wangu kwa ''facts'' na ''chronology,'' hapo sina budi kusema niyajuayo.

Kuwa yale yaliyokuwa Kariakoo ndiyo kila kitu huu ni ukweli la huamini hapana shida unaweza kuamini kuwa harakati za kuunda TANU zilianza Tosamaganga.

Mimi nitakueleza kuwa mikutano yote ya siri ya kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu na ni nyumba hii ndipo alipoishi Nyerere baada ya kuacha kazi mwaka wa 1955 na TANU ilipoundwa kadi ya TANU ya Abdul ni no. 3 na mdogo wake Ally ni no. 2 na Nyerere no.1.

1576564418065.png

Nitakueleza pia na kadi za TANU 1000 za mwanzo alichapisha Ally Sykes kwa fedha zake na hata usanifu wa kadi aliufanya yeye kutoka na kadi yake ya Tanganyika Legion.

Ikiwa historia ya TANU itaanza Tosamaganga ni wazi ni hii itakuwa ni TANU nyingine si hii iliyotokana na mazungumzo nyumbani kwa Hamza Mwapachu mwaka wa 1953 kati ya Abdul Sykes, Ali Mwinyi na Mwapachu mwenyewe kumjadili Nyerere.

Wala TANU hii haitakuwa TANU ya babu yangu Salum Abdallah ambae alikuwa akihudhuria mikutano yake ya siri kila Jumapili Town School Tabora mwaka wa 1953.

Wala sitasema kuwa mazungumzo hayo ya Tosamaganga hayakuwapo.
Labda nitauliza hiyo TANU ya Tosamaganga ilikuwa mwaka gani?

Kabla Nyerere hajafahamiana na Abdul Sykes au baadae?
 
Back
Top Bottom