Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Utangulizi
HISTORIA MPYA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA
Utangulizi
Nami nasubiri patulie In Shaa Allah nataka niandike jinsi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyochaguliwa kuongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika katika kikao cha watu watatu Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Kibwana Mwapachu mwaka wa 1953 na moja ya sifa kubwa iliyotajwa ni dini yake.
Wazalendo hao wote watatu waliokubaliana kumkabidhi Baba wa Taifa uongozi walikuwa Waislam, mmojawapo akiwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Kisha nitaeleza vikao vyote vya dua alivyoshiriki Baba wa Taifa pamoja na Waislam katika kumlilia Allah awape msaada Watanganyika washinde dhulma zote za Waingereza na Allah alikubali dua ya wenye kudhulumiwa.
Katika juhudi za kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TANU alipofariki mwaka wa 1968 magazeti ya TANU yaliandika kuwa Rais Nyerere kahudhuria mazishi ya Abdul Sykes.
Hakikuandikwa chochote katika historia yake katika kuasisi TANU.
Ilikuwa Tanganyika Standard chini ya uhariri wa Mwingereza, Brendon Grimshaw ndiyo iliyoandika taazia na kueleza mchango wake katika kumtia Nyerere katika siasa za Dar es Salaam na kuunda TANU.
Mwaka wa 1981 Chuo cha CCM Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU walikataa kupokea "notes," zinazohusu mchango wa Abdul Sykes katika kuunda TANU.
Wanaona tabu kusema kuwa Abdul na mdogo wake Ally ndiyo waliompokea Nyerere nyumbani kwao mwaka wa 1952.
Iweje kadi ya Ally Sykes iwe no. 2 na ya kaka yake Abdul no. 3 na ya Nyerere no.1 tena kaandikiwa na Ally Sykes halafu ikawa hawa si waliunda TANU achilia mbali kuwa kadi 1000 za kwanza alinunua Ally Sykes kwa fedha zake.
Yako mengi.
Hivi sasa kuna bango limewekwa nyumbani kwa Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Mwananyamala linalosema kuwa ati TANU ilianzishwa ndani ya nyumba hiyo.
Mwaka wa 1988 nilipoandika makala katika Africa Events iliyomtaja Abdul kama mtu muhimu katika historia ya TANU gazeti zima lilikusanywa.