Maendeleo ya viwanda yamekuwa sehemu muhimu ya mikakati ya maendeleo ya Tanzania baada ya uhuru. Hasa, hatua ambazo maendeleo ya viwanda yamepitia ni pamoja na maendeleo ya viwanda katika uchumi mchanganyiko(Mixed Economy 1961-66); mwelekeo wa uongozi wa serikali katika maendeleo ya viwanda kwa mbinu ya uingizaji wa bidhaa mbadala (State-led import substitution industrialization 1967-85); kipindi cha kudhoofika kwa viwanda chini ya mipango ya marekebisho ya kiuchumi (SAPs) na mageuzi ya sera (Associated policy reforms 1986-95).
Kuna ripoti mbalimbali zinaonyesha viwanda vilivyoacha kufanya kazi (kudhoofika) ambavyo vilibinafsishwa katika miaka ya 1990. Mnamo mwaka 1990, kati ya viwanda 24 vya nguo nchini, 22 vilifungwa kwa sababu mbalimbali kama vile ukosefu wa utaalamu wa kiufundi na uhaba wa mtaji wa kuendesha shughuli (Wangwe 2017). Mnamo 2017, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John P. Magufuli aliripoti kuwa viwanda 197 viliachwa na vingine vilibadilishwa matumizi kutokana na sera zisizofaa za serikali, hali mbaya ya uchumi, hujuma za kifedha, na mabadiliko ya kiteknolojia (Macha 2017). Kwa mfano, moja ya sababu zilizochangia kufungwa kwa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki (FTC) ni ukosefu wa mtaji wa kutosha wa kuendesha shughuli, hali iliyosababisha kufungwa kwa kiwanda mnamo Desemba 2017. Pia, mashine nyingi zilikuwa zimepitwa na wakati, usimamizi mbaya, na ushindani mkubwa katika soko la nguo la kimataifa uliosababisha hujuma dhidi ya kiwanda.
Mnamo Agosti 10, 2017, mamlaka za Tanzania zilitangaza kurejesha viwanda 10 vilivyobinafsishwa baada ya kuwa vimekaa bila kufanya kazi kwa miaka 20 (Xinhua 2017). Kulingana na ripoti iliyowasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kati ya mashirika 74 yaliyobinafsishwa, 17 yalikuwa yamesitisha shughuli zake kabisa (Mugarula 2012).
Kwa mujibu wa ripoti ya 2013 kutoka Shirika la Consolidated Holding Corporation (CHC), ambalo lilifanyia ukaguzi mashirika 170 yaliyobinafsishwa, ni mashirika 42 pekee yaliyokuwa yakipata faida, 70 yalikuwa yakipata hasara, na 58 hayakuwa yakiendesha shughuli zao kabisa (TheCitizen 2015). Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa wakati huo, Dkt. Mary Nagu, alisema kuwa serikali inazingatia kurejesha viwanda 30 vilivyobinafsishwa lakini vikaachwa bila maendeleo yoyote na wamiliki wapya (Mwakisyala 2010).
Ingawa serikali imekuwa ikitoa sera za kuimarisha viwanda hivi, bado baadhi havijaweza kufanya kazi hadi sasa.
Historia inasema kutokana na mgogoro wa kiuchumi wa mwishoni mwa miaka ya 1970, Tanzania ilisaini mpango wake wa kwanza wa marekebisho ya kiuchumi (SAP) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mnamo 1986. Marekebisho ya kizazi cha pili yalifuata, ambapo ubinafsishaji uliongezeka katika miaka ya 1990, na kufikia mwisho wa 1996, mashirika yote, yakiwemo ya huduma za umma, yaliwekwa kwenye mpango wa ubinafsishaji. Kwa hiyo, katika kipindi cha miaka kumi, serikali ilibadili kabisa sera za ujamaa za Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania (Bayliss 2008) na kuanza kutumia sera ya uchumi mchanganyiko (Mixed Economy).
Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, serikali ilibinafsisha viwanda 156. Aidha, kwa mujibu wa maagizo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, hayati Dkt. John Magufuli, wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 mnamo Novemba 20, 2015, aliiagiza serikali kufufua viwanda vilivyoachwa na wawekezaji hao. Hivyo, kuanzia 2016 hadi 2017, Ofisi ya Msajili wa Hazina, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara, ilifanya tathmini ya viwanda vyote ili kubaini hali yake. Kufikia mwaka 2019, serikali ilikuwa imefanikiwa kufufua viwanda 31. Hata hivyo, hali hii ilikuwa ya wakati huo na inaweza kuwa imebadilika. Hadi sasa baadhi ya viwanda vimeanza kufanya kazi tena, vingine vimekabidhiwa kwa taasisi na serikali imetangaza mipango ya kupata wawekezaji wapya kwa viwanda vingine.
Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Msajili wa Hazina (2019), kati ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa, viwanda 77 bado vinafanya kazi, 80 havifanyi kazi (vimeachwa) au vimerejeshwa kwa serikali. Kufikia mwaka 2024, viwanda takribani 23 vilikuwa havifanyi kazi na vilirejeshwa kwa serikali. Viwanda vya usagaji nafaka vinachukua 32% ya viwanda vilivyoacha kufanya kazi, viwanda vya divai na nyama 10%, chakula na vinywaji 13%, chuma 5%, dawa 3%, na vinginevyo.
Dar es Salaam ina asilimia kubwa zaidi ya viwanda vilivyoacha kufanya kazi (27%).