Historia: vituko ulimwenguni

Historia: vituko ulimwenguni

"FARASI ATOROKA NJE YA KIBANDA ANGANI"

Ndege inayoendeshwa na shirika maalum la ndege la Air Atlanta Icelandic, ilikuwa ikielekea Liege nchini Ubelgiji kabla ya kulazimika kurejea katika uwanja wake wa ndege ilipotoka huko New York baada ya farasi kutoroka nje ya kibanda chake katika sehemu ya kubebea mizigo na kuanza kukimbia ndani ya ndege.

Ndege hiyo aina ya Boeing 747 yenye usajili TF-AMM, ilikuwa ikisafiri kwa umbali wa futi 31,000 juu ya Boston wakati ambapo kwa ghafla farasi mmoja alitoka kwenye kontena lake.

Marubani walilazimika kumwaga tani 20 za mafuta ili kupunguza uzito wa ndege kabla ya kutua kwa usalama.

Picha ni kwa lengo la kufikisha ujumbe tu.

Chanzo:

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_1700046114736.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchoro wa karne ya 16 unaoonyesha kuchunwa ngozi akiwa hai kwa hakimu fisadi, Sisamnes, katika mwaka wa 500BC.
Sisamnes alikuwa hakimu wa kifalme fisadi wakati wa Cambyses ll katika Uajemi.

Iligundulika kuwa alichukua hongo mahakamani na akatoa hukumu isiyo ya haki. Kwa sababu hiyo mfalme akaamuru akamatwe kwa ufisadi wake na akaamuru achunwe ngozi akiwa hai. Kabla ya kutoa hukumu mfalme alimuuliza Sisamnes ni nani alitaka kumteua kama mrithi wake. Sisamnes, kwa uchoyo wake, alimchagua mwanawe, Otanes.

Mfalme alikubali na kumteua Otanes kuchukua nafasi ya baba yake. Baadaye alitoa hukumu na kuamuru kwamba ngozi iliyoondolewa ya Sisamnes itumike kuwamba kiti ambacho hakimu mpya angekalia kortini ili kumkumbusha madhara yanayoweza kusababishwa na ufisadi.

Otanes, katika mashauri yake, alilazimika kukumbuka daima kwamba alikuwa ameketi kwenye ngozi ya baba yake aliyeuawa. Hii ilisaidia kuhakikisha haki na usawa katika vikao vyake vyote, mijadala na hukumu.View attachment 2680420

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ingetumika Tanzania kukomesha ufisadi
 
Back
Top Bottom