Historia ya Abbas Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere (1952 – 1999)

Joka...
Amin.
Hila niwenayo ya nini ndugu yangu?

Mkuu Ninasoma Mabandiko yako mengi sana. Binafsi kama kijana mdogo yananisaidia sana kuelewa kwa undani hali halisi ya kile kilichotokea katika hist kusema Ukweli na kutuelim
 
Kwanini wewe huendi kwa mama Maria Nyrerere ukaja kutupa uliyoyapata kwa upande wako?

Allama Mohamed Said anatupakulia vipya kila siku, kama unashindwa kuvila si ulete vyako tuvionje?
Maalim Faiza,
Hivi hawa ndugu zangu wanadhani kuwa mimi nitakaa nifanye utafiti wa historia ya wazee wangu kisha nikae kitako niandike uongo ilhali mimi mwenyewe na wazee wangu watu wanatujua?
 
Tunakusubiria mzee
London 1,
Niko ndugu yangu.
Hiyo zawadi yako London.

''If you are tired of London you are tired of life.''
Charles Dickens

1568257169224.png
 
Maalim Faiza,
Hivi hawa ndugu zangu wanadhani kuwa mimi nitakaa nifanye utafiti wa historia ya wazee wangu kisha nikae kitako niandike uongo ilhali mimi mwenyewe na wazee wangu watu wanatujua?
Allama Mohamed Said.

Tumeona viongozi wa Kiislam walivyokuwa mstari wa mbele miaka kwa miaka, mpaka kuhatarisha maisha yao. Vipi viongozi wa Kikristo kwenye kutafuta uhuru mbona hawasikiki?
 
Kwanini wewe huendi kwa mama Maria Nyrerere ukaja kutupa uliyoyapata kwa upande wako?

Allama Mohamed Said anatupakulia vipya kila siku, kama unashindwa kuvila si ulete vyako tuvionje?
Umekuja kumtetea "ndugu yako" hehehee!
Ntaenda kwa mama Siti nitakapoandika kitabu kueleza alivyouza Loliondo kwa waarabu!
 
Umepiga "about turn" ya "90 degrees". Vipi umwambie Allama Mohamed Said aende kwa mama Maria Nyerere wewe ushindwe kwenda kuutafuta ukweli.

Nafahamu, Mwinyi kakukaa rohoni kwa kuwa juzi katumbuwa jipu.
 
Sundoka hakika nimekosea na nimeshafanya masahihisho.
Wala si hatari kubwa ni makosa ya kawaida katika uandishi tunayafanya kila siku. Wewe umeliona hili kubwa kwa kuwa labda hukupendezewa na hii makala. Lakini ikiwa lipo kosa lingine nifahamishe na nitakushukuru.
Unaonekana hadithi zako unatunga mkuu.
 
London 1,
Niko ndugu yangu.
Hiyo zawadi yako London.

''If you are tired of London you are tired of life.''
Charles Dickens

View attachment 1204991
Tower hill Bridge umezunguka sana mzee hii history kwangu inavutia sana sababu haya majina mengi nishawahi kuyasikia na baadhi ya koo kama kina chaurembo tumeungana nazo ndo maana nafuatilia kwa ukaribu.Mi wazazi wangu wamekulia kariakoo mtaa wa msimbazi na wengi tumezaliwa hapo, ina mzee wangu (amefariki kwa sasa), alikuwa diwani utawala wa nyerere baada ya uhuru, hakupenda kabisa kuongerea history hii ila najua alijuana na watu wengi sana sababu biashara zake zilikiwa mtaa wa Narung'ombe na nishawahi kumuona mzee Mtemvu alikuja kazini kwake kumsalimia hiyo miaka ya themanini.
 
Unaonekana hadithi zako unatunga mkuu.
Sundoka,
Wala hapana haja ya mimi na wewe kuvutana.

Ikiwa unaona kuwa nielezayo katika historia ya TANU na historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ni mambo ya kutunga kuwa watu niwaelezao hawakuwapo na hawakufanya hayo niyasemayo mimi kwangu ni sawa hapana neno.

Lakini kuna watu wengi wananiamini na ndiyo sababu ya kitabu changu kuwa kimechapwa mara ñne.

Kinachonisikitisha ni huku mimi kuona jinsi watu kama wewe walivyoumizwa na kitabu changu.
 
Mzizi...
Mimi nakusihi ujizuie na kuvuka mipaka ya uungwana.
Nadhani umenielewa.

Mimi kumwelewa kwangu Mwalimu Nyerere ni ndani ya historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Namfahamu Mwalimu Nyerere kwa kwanza kumsoma yeye mwenyewe binafsi katika Nyaraka za Sykes na namfahamu Mwalimu kwa kuzungumza na wale ambao alikuwanao wakati wa harakati za kudai uhuru.

Katika utafiti huu hatoweza yeyote kuyajua niyajuayo bila ya kufanya utafiti utakaojumuisha kusoma nyaraka na kuwahoji wale aliokuwanao Mwalimu kama nilivyofanya mimi.

Katika Nyaraka za Sykes kuna barua moja ya Mwalimu nimeipenda sana nakuwekea hapo chini ili na wewe ufaidi lugha yake:

''We realise the apparent incompatibility between the implementation of the resolution and imperial prestige. But to us this is not a matter of prestige, it is both a matter of high principle and of bread and butter. As far as this Union is concerned an important principle has been violated and we will not rest until it has been put right.'' [1]

Hiyo ni kalamu ya Mwalimu Nyerere ndani ya Nyaraka za Sykes mwaka wa 1954.

Hivi ndivyo mimi ninavyomfahamu Mwalimu Nyerere kwa kusoma yale aliyoandika wakati wa kudai uhuru na kwa nyongeza nilimuuliza Bwana Ally Sykes nini sababu ya waraka ule ulioandikwa na Nyerere?

Ally Sykes akanifahamisha kisa kizima.
Unazungumza kuhusu kunidharau.

Vipi utanidharau wakati kitabu changu kimesahihisha historia ya TANU iliyokuwapo na imeongeza elimu katika historia ya Tanzania?

Vipi utakidharau kitabu ambacho kimefanyiwa ''review,'' zilizochapwa katika Cambridge Journal of African History?

Vipi utamdharau mwandishi wa kitabu ambacho kimemfanya yeye kualikwa na kuzungumza Northwestern University Evanston, Chicago na University of Iowa na mada ikiwa Abdulwahid Sykes?

Utaanzia wapi kumdharau mwandishi ambae baada ya kitabu hiki akashirikishwa katika miradi miwili ya Oxford University Press, Nairobi na Oxford University Press, New York kuandika vitabu vya historia ambavyo vimechapwa na vinasomwa dunia nzima?

Vipi takidharau kitabu ambacho sasa kipo toleo la tatu Kiingereza na toleo la nne Kiswahili?
Ombi langu kwako ni hili.

Ondoa chuki na ghadhabu ili uweze kuisoma historia hii kwa utulivu ambao utakusaidia kuona kweli.

[1] TANU memorandum to the United Nations Visiting Mission, 24th August, 1954. Sykes’ Papers. Also see Uamuzi wa Busara, pp. 7-8.
Kaka mkubwa Mohammed Saida endelea kushusha nondo tu usihofu chochote, kila nisomapo makala zako hunifunza jambo jipya ambalo sikulijua bado hadi nisomapo maandishi yako. Asante sana. Tatizo watu hawataki kuelewa kwamba TANU ilizaliwa Pwani kwenye Waislamu na hivyo lazima historia yake itawagusa sana Waislamu tu. Lau ingezaliwa kwetu Karagwe huenda ingewagusa Wanyambo, Wahaya na Wahangaza zaidi kuliko makabila mengine. Tukubali hii ndo historia ya TANU.
 
Esam,
Angalia hiyo picha hapo chini katikati ya Mwalimu Nyerere na Hastings Banda ni Abbas Sykes uwanja wa ndege Dar es Salaam walikwenda kumpokea Banda.

Miaka hii uhuru bado.
Abbas Sykes mtazame ni kijana sana bado hata hajafikisha miaka 30.

Pembeni ya Banda ni Kaluta Amri Abeid na mwisho ni Kanyama Chiume.
Vipi mtu atamtilia shaka Abbas Sykes kuhusu Nyerere?

Ally Sykes ndiye aliyenijulisha mimi kwa Kanyama Chiume ofisini kwake.

Mzee Chiume alikuwa kamletea ''project proposal,'' ya kuandika kitabu kuhusu wapigania uhuru Kusini mwa Sahara.

Ally Sykes alifurahi sana kwa kutokea kwangu na akafanya foto copy ya proposal ile na kunipa nakala ambayo ninayo had leo sasa zaidi ya miaka 20 imepita.

Bahati mbaya kazi hii Mzee Chiume hakuifanya na ikaja kufanywa na Brig. General Hashim Mbita:

Nimeishi na watu hawa na wakaniamini sana kama kijana wao.

1568280166636.png
 
Esam,
Angalia hiyo picha hapo chini katikati ya Mwalimu Nyerere na Hastings Banda ni Abbas Sykes uwanja wa ndege Dar es Salaam walikwenda kumpokea Banda.

Miaka hii uhuru bado.
Abbas Sykes mtazame ni kijana sana bado hata hajafikisha miaka 30.

Pembeni ya Banda ni Kaluta Amri Abeid na mwisho ni Kanyama Chiume.
Vipi mtu atamtilia shaka Abbas Sykes kuhusu Nyerere?

Ally Sykes ndiye aliyenijulisha mimi kwa Kanyama Chiume ofisini kwake.

Mzee Chiume alikuwa kamletea ''project proposal,'' ya kuandika kitabu kuhusu wapigania uhuru Kusini mwa Sahara.

Ally Sykes alifurahi sana kwa kutokea kwangu na akafanya foto copy ya proposal ile na kunipa nakala ambayo ninayo had leo sasa zaidi ya miaka 20 imepita.

Nimeishi na watu hawa na wakaniamini sana kama kijana wao.

View attachment 1205281
Oooo ubarikiwe sana kaka hakika una vitu adhimu ambavyo sio rahisi kivipata, hasa kuhusu nyakati za kabla na zile za mwanzoni mwa miaka ya uhuru
 
Oooo ubarikiwe sana kaka hakiJohnnzoni mwa miaka ya uhuru
ESAM,
Amin.

Kila msomi aliyepata historia ya hawa akina Sykes alivutiwa kutaka kujua zaidi ni nani watu hawa?

John Iliffe mwanahistoria wa University of Cambridge wakati anasomesha Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam 1960s ndiye aliufungua mlango huu.

Nina file nimelipa jina ''Sykes Obsession'':

Ndjabu...
Ondoa tu hayo matusi hayana maana lakini yote uliyoandika ni muhimu. Obsession honestly...Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.

Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).

Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.

Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile. Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.

Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.

Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu. Mwanae Abdul Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika
Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake...

Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.

Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.

Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.

Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.

Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.

Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.

Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.

Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.

Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa KwanLikunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.

Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.

Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.

Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia. Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.

Ndjabu,
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.

NB:
Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika serikali ikaamua kutunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Ally na Abdul Sykes kwa kutambua mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.''
 
Umekuja kumtetea "ndugu yako" hehehee!
Ntaenda kwa mama Siti nitakapoandika kitabu kueleza alivyouza Loliondo kwa waarabu!

Mzizi...
Jizuie na ghadhabu zinazokufanya utoke katika uungwana.

Huu uzi ni historia ya TANU na kupigania uhuru hayo mengine unayoleta hayafai kwani unashambulia watu binafsi ukiongozwa na chuki za ukabila.

Tujadili mada iliyoko mezani kwa ustaarabu.
 
ESAM,
Amin.

Kila msomi aliyepata historia ya hawa akina Sykes alivutiwa kutaka kujua zaidi ni nani watu hawa?

John Iliffe mwanahistoria wa University of Cambridge wakati anasomesha Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam 1960s ndiye aliufungua mlango huu.

Nina file nimelipa jina ''Sykes Obsession'':

Ndjabu...
Ondoa tu hayo matusi hayana maana lakini yote uliyoandika ni muhimu. Obsession honestly...Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.

Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).

Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.

Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile. Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.

Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.

Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu. Mwanae Abdul Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika
Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake...

Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.

Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.

Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.

Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.

Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.

Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.

Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.

Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.

Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa KwanLikunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.

Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.

Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.

Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia. Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.

Ndjabu,
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.

NB:
Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika serikali ikaamua kutunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Ally na Abdul Sykes kwa kutambua mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru ta Tanganyika.''
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom