Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
JULIUS NYERERE NA ALI MWINYI TAMBWE, AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA (UMOJA WA WAISLAM WA TANGANYIKA) SAFARI YA KWANZA UNO 1955
Usiku uliopita kijana mmoja jina lake Victor Madaha Mtangazaji wa Bongo Plus TV kanipigia simu kaniomba afike Maktaba siku ya pili tufanya kipindi kuhusu vijana na siasa. Huyu kijana ananieleza kuwa kilichomsukuma kutaka kufanya kipindi hiki na mimi ni jinsi uchaguzi mkuu wa wa mwka huu wa 2025 ulivyovutia vijana wengi wadogo kuwania kugombea nafasi nyingi katika CCM.
Kwa hakika sikuipenda hii mada na hasa kuangalia hali ya nchi ilivyokuwa katika jambo hili la uchaguzi. Lakini yeye akaniambia kuwa watu wengi wamemuomba afanye kipindi hiki na wamemwambia kuwa anihoji mimi ifahamike huko nyuma tulikotoka vijana walifanya nini na walikuwa na gani katika siasa za Tanganyika.
Nikakubali kwani niliona ni mada nzuri kurejea katika barabara hii yenye historia ya sasa yapata miaka 100 toka Waafrika walipoanza kujikusanya kwa kitu kimoja. Kulipokucha asubuhi nikaanza maandalizi ya kipindi kwa kutalii niiyokuwanayo kuhusu wazalendo wapigania uhuru wa Tanganyika zaidi hasa nikitaka kujua miaka yao ya kuzaliwa ili nipime umri wao ulikuwa miaka mingapi wakati wanaanza kupigania uhuru wa Tanganyika kupitia chama cha TANU.
Nikaanza na kutalii historia ya Dr. Kwegyr Aggrey kutoka Achimota College Ghana alipokutana na Kleist Sykes, Dar es es Salaam mwaka wa 1924.
Jina lingine lililonijia akilini lilikuwa jina la Ahmed Rashaad Ali nataka kufahamu mwaka aliozaliwa. Mwaka aliozaliwa siujui lakini alipata kuniaeleza kuwa yeye katika watu wa rika lake Dar es Salaam ile ya miaka ya 1980 alikuwa Chief Abdallah Said Fundikira na Ali Mwinyi Tambwe.
Nikampigia simu Abdallah Miraji mdogo wake Prof. Haroub Othman anifahamishe mwaka aliozaliwa Ali Mwinyi Tambwe.
Bahati mbaya yeye akawa hajui alizaliwa mwaka gani. Abdallah akanieleza kuwa Al Mwinyi Tambwe nyumbani kwake kulikuwa na cheti chake cha kumaliza elimu ya sekondari Zanzibar kakitundikia ukutani na kilikuwa na tarehe lakini haikumbuki.
Ikawa tarehe ya kuzaliwa Ali Mwinyi Tambwe nimeikosa lakini tukaingia katika mazungumzao mengine kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na mchango wake katika siasa za Tanganyika na vipi alijuana na Julius Nyerere kwa karibu mno.
Ali Mwinyi Tambwe ana historia ya pekee katika watu wa kwanza kumjua Nyerere alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952. Ali Mwinyi na Abdulwahid Sykes walikwenda Nansio kuonana na Hamza Mwapachu ili atoe kauli yake kuhusu Nyerere kutiwa katika uongozi wa juu kabisa wa TAA kisha iundwe TANU.
Historia hii nimeieleza mara nyingi sana.
Baada ya kukosa mwaka wa aliozaliwa Ali Mwinyi Tambwe, Abdallah akaniambia kuwa ana kisa anataka kunieleza kuhusu Ali Mwinyi Tambwe na siku alipokieleza kisa hicho Prof. Haroub alikuwako.
Abdallah akaanza kunieleza kisa hicho.
Ali Mwinyi Tambwe anawaeleza Prof. Haroub na Abdallah kuwa ilikuwa mwaka wa 1955 usiku na mvua inanyesha yeye yuko nyumbani kwake kwenye jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Mtaa wa Aggrey na New Street. (Ali Mwinyi alikuwa Secretary wa Al Jamiatul kama ilivyozieleka kuitwa. Ali Mwinyi akiishi katika nyumba ya Al Jamiatul nyuma ya jengo kubwa la Al Jamuatul ambako kulikuwa na shule iliyojengwa na Waislam wenyewe kwa msaada wa Aga Khan katika miaka ya 1930.
Miaka hiyo President wa Al Jamiatul Islamiyya alikuwa Kleist Sykes na Secretary, Mzee bin Sudi viongozi hawa wawili walikuwa pia ndiyo viongozi wa African Association katika nafasi hizo hizo).
Ali Mwinyi anaeleza kuwa usiku huo wa mvua Nyerere akaja nyumbani kwake akiwa kashika mwamvuli kaja kupata taarifa za hali ya mchango wa fedha za safari yake ya UNO ilikuwaje.
Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya alikuwa Iddi Faizi Mafungo ambae pia alikuwa ndiye mweka hazina wa chama cha TANU.
Abdallah Miraji aliponieleza kuwa Nyerere alikwenda nyumbani kwa Ali Mwinyi Tambwe, jengo la Al Jamiatul Islamiyya kuuliza fedha za safari ya UNO mwili ulinisisimka.
Sababu ya mimi kusisimkwa na kisa hiki ni kuwa ilikuwa katika mazungumzo kama haya niko Upare katika utafiti nazungumza na Sheikh Shaban Rashid Msuya akanieleza kuwa hafla ya kumuaga Nyerere safari ya kwanza UNO mwaka wa 1955 ilifanyika ndani ya jingo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika yeye akiwa kati ya wanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir walioletwa pale kuwahudumia waalikwa.
Nami nikamwambia Abdallah Miraji kuwa ameniongezea jambo lingine kubwa katika historia ya Nyerere na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)
Jengo hili ambalo ilikuwa shule ya Al Jamiatual Islamiyya fi Tanganyika hivi sasa linamilikiwa na TAMISEMI. Majengo ya nyuma ilipokuwa nyumba hii ambayo akikaa Secretary wa Al Jamiatul, Ali Mwinyi Tambwe wamepewa BAKWATA na wao wanaitumia kama ofisi zao.
Ipo picha imepigwa Al Jamiatul Islamiyya katika miaka ya 1930 katika picha hiyo yuko Ali Mwinyi Tambwe, Kleist Sykes, Maalim Mohamed Matar aliyekuwa mwalimu wa kusomesha Qur’an katika shule hiyo na yuko Abdul Sykes wakati huo mwanafunzi wa shule ya msingi hapo shuleni.
Picha hii ipo katika kitabu: ‘’The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 – 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.’’
Mbele kushoto ni Ali Mwinyi Tambwe amembeba Abeid Amani Karume
Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashaad Ali na Sheikh Ahmed
Islam
Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya na TANU ni huyo kulia kwa Mwalimu Nyerere na ukienda kushoto ni Zuberi Mtemvu, Robert Makange na Rashid Sisso na baada ya Nyerere ni John Rupia na Bibi Titi Mohamed safari ya kwanza UNO Februari, 1955.