MAANA YA BITCOIN NI NINI?
Kabla sijaanza kuelezea kuhusu bitcoin nitaanza na kueleza mapito ambayo mwanadamu amekuwa akipitia kwenye kubadilishana bidhaa yoyote na fedha au vito.
1. Barter Trade Age
Wengi tunajua mfumo huu wa manunuzi na mauzo ya vitu uliojulikana kama Barter Trade.
Barter trade ni mfumo ambao watu walibadilishana bidhaa kwa bidhaa, hapakuwa na fedha kama sasa. Kwa hiyo ukihitaji nguo inabidi umpe anayeuza nguo kile ulichonacho mfano mnabadilshana nguo kwa kuku, mahindi kwa mbuzi na kadhalika. Mfumo huo ukapita ukaja mfumo mwingine.
2.Vito vya Thamani kama Dhahabu.
Ulimwengu ulihama kutoka kwenye zama za kubadilisha vitu kwa vitu ukahamia kwenye kubadilisha vitu kwa KITO cha thamani kama dhahabu. Thamani ya vipande vya dhahabu ilipimwa kwa wingi au ubora wa bidhaa husika inayobadilishana na kipande hicho cha dhahabu. Mfumo huu au zama hizo zikapita.
3. Coin and Paper money Age.
Matumizi ya dhahabu bado yalikuwa magumu sana. Wizi na ugumu wa kusafiri na vipande vya dhahabu viliifanya dunia kuja na mfumo wa sarafu na fedha za makaratasi. Mfumo huu ndo ambao tunautumia kwa kiasi kikubwa mpaka sasa. Mfumo huu umedumu sana kwa karne nyingi!!
Hata hivyo, mfumo huu unaendelea kukosa nguvu. Tangu miaka ya 2005 mfumo mpya wa kutembea na Phone Wallets au mobile money umedhoofisha sana mfumo wa paper note au coin money!!
4. Mobile Money Age.
Huu ni mfumo ulioletwa na Internet na Mobile phones. Mfumo huu umeanza miongo kama miwili iliyopita yaani mwisho mwa miaka ya 1990.
Mfano wa Mobile Money ni: Western Union, MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, Simbanking, Pesa Fasta, na mifumo mingine mingi ya kutuma, kupokea, na kutumia pesa kwa kutumia mitandao ya simu na internet au simu.
Mobile Money imeleta mageuzi makubwa sana kwenye mfumo wa fedha duniani. Fedha inahamishika kirahisi. Biashara nyingi zimekuwa rahisi kwa sababu ya matumizi ya Mobile Money au Mobile Banking. Mfumo huu nao unataka kufika kwenye kilele chake!! Mfumo ufuatao ndio unaenda kutawala tena ulimwengu wa biashara na sekta ya fedha! Hebu twende pamoja...!
5. CryptoCurrency Age.
Kuanzia mwaka 2009 Sarafu ya Digitali iitwayo Bitcoin ilipovumbuliwa na Satoshi Nakamoto kumekuwepo mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya fedha duniani!!
Sasa dunia imeingia kwenye mfumo mpya na bora zaidi wa kutuma, kupokea na kutumia fedha ujulikanao kama CryptoCurrency. CryptoCurrency ni Sarafu ya Digitali au ni Sarafu iliyojificha ambayo huwezi kuiona kwa macho (Crypto) lakin unaweza kuuza na kununua kwa kuitumia.
Crypto ni kitu kisichoweza kuonekana kirahisi, not tangible, not visible but valuable, top secret, etc!
Kama ilivyo kwa mobile money, Cryptocurrency ni fedha ya kidigitali ambayo haishikiki lakini unaweza kuitumia kwa matumizi yako ya kila siku.
Ngoja nitoe mfano wa mobile money inavyoweza kutumika kama digital money.
Umewahi kwenda sehemu ukaona wameandika lipa hapa kwa Tigopesa? Yaani kama una hela kwenye Tigopesa au Mpesa unalipia huduma au bidhaa bila kutoa sarafu au noti ( actual coins or paper note)? Unaweza Kupata chakula hotelini na ukalipia huduma hiyo bila kutoa noti mfukoni mwako!! Nk.
Umewahi kuona kwenye super markets watu wananunua bidhaa au huduma kwa kutumia master au visa cards bila kutoa fedha mfukoni?
Hivyo ndivyo Cryptocurrency itakavyofanya kazi siku zinazokuja kuanzia sasa!!
Swali, kama Mobile Money ipo, Cryptocurreny ya nini tena?
Jibu ni kwamba, Cryptocurrency ina faida nyingi naomba nitaje baadhi tu:
1. Kutuma na kupokea fedha ni bure kabisa duniani kote!!!
2. Kutuma na kupokea pesa ni kwa haraka kama unavyotuma na kupokea ujumbe wa email kwenye internet au WhatsApp na Twitter!
3. Cryptocurrency inatumika dunia nzima wakati mobile money nyingi zinatumika eneo husika tu ambapo mtandao wa simu upo. Mf MPESA
4. Mfumo wa Cryptocurrency ni madhubuti sana kwa hiyo ni ngumu sana kuibiwa (money laundering).
5. Akaunti yako ipo mikononi mwako, huna haja ya kwenda bank kuchukua fedha!!
Je, katika mfumo huu mpya wa Sarafu duniani kuna fursa yoyote ndani yake?
Jibu lake ni ndiyo
Kuna kampuni nyingi sana zipo kwenye sekta hii ya Crypto Currency zikifanya yafuatayo:
1. Exchanging digital currency with non digital currency!!
2. Trading Crypto Currency to Crypto Currency
3. Mining Crypto Currency using special software.
Hii ni fursa kubwa sana ambayo ukijiunga na kambuni inayofanya Bitcoin Mining Pool unaweza kupata faida kubwa sana kwa muda mchache.
Kampuni nyingi zimewekeza kwenye technology ya kuchimbua Sarafu za kidigitali kama Bitcoins, Ethereum,Zcash,Monero,etc
Ukiwekeza kwenye kampuni hizo kadri Sarafu zinavyopatikana utapata Sarafu zako kulingana na mtaji wako uliowapatia kwenye kampuni!!
4. Agents for Crypto Currency to non Crypto Currency!! Pia wapo mawakala wanaofanya biashara ya hii ya uwakala wa Sarafu ya Digitali kwa Sarafu za kawaida mfano Dollars, pounds, euro nk.
........................................................................
TUKUTANE WAKATI MWINGINE TUJIFUNZE ZAID JUU YA REVOLUTION YA CRYPTOCURRENCY HASA TUKIJIKITA ZAIDI KWENYE BITCOIN.