rugumye
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 561
- 179
HISTORIA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakifanya kutumia taasisi za dola ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika kutisha, kutesa, kunyamazisha na kudhoofisha upinzani wa kisiasa au wale wasio na mlengo wa CCM.
CCM, kama chama dola, kimetengeneza mfumo wa kuzif​anya taasisi zote za dola (nchi) kuwa matawi yake yakiongozwa na makada wa falsafa na itikadi yake!
Tazama mifano michache hapa chini jinsi CCM dola inavyotumia vyombo vya dola kudhoofisha upinzani.
1. Mwaka 1982 hadi 1992 kulikuwa na vuguvugu la ndani ya CCM lililochochewa na wanasiasa waliotofautiana na fikra kandamizi za demokrasia ya "chama kushika hatamu" pale nafasi za kisisasa zilipokuwa zikitolewa na kikao kimoja cha chama kwa malengo maalumu yanayotokana na utashi wa chama. CCM ilikuwa inakandamiza demokrasia ndani ya chama kwa kuzuia aina zote za upinzani wa ndani ya chama.
Nguvu za kijeshi na kipolisi zilitumika kuzima aina yoyote ya upinzani wa fikra, mawazo au imani (itikadi) kinyume na viongozi wateule wa CCM wanavyoamini! Hali hii iliwakuta kina Aboud Jumbe Mwinyi, Seif Sharif Hamad, Horace Kolimba na wengine ambao ndio waliokuwa chemchemi ya kukua kwa upinzani tunaoushuhudia leo.
2. Mwaka 1997 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitengeneza shauri la jinai Na. 279/1997 dhidi ya Machano Khamisi Ali (na wenzake 17) kwa tuhuma za uhaini dhidi ya SMZ. Shauri la uhaini Na. 7, 1999 lilikuja kubainika kwamba lilikuwa la kubambikiza na Mahakama Kuu ya Zanzibar iliwaachia huru watuhumiwa wakiwa wamesota magereza kwa zaidi ya miaka mitatu.
3. Januari 25, 2001 Mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipigwa na Polisi na kuvunjwa mkono alipokuwa njiani kwenda kwenye shughuli za kisiasa.
4. Hilo halikutosha kuonyesha jinsi CCM inavyotumia taasisi za ulinzi na usalama; mwaka 2005 aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Omar Idd Mahita alitoa tuhuma za ugaidi dhidi ya CUF na kukituhumu chama hicho kwamba kimeingiza makontena ya majambia kwa minajili ya kuendesha vitendo vya kigaidi!
Haya yalikuwa madai mazito kwa chama cha siasa. Hali hii iliifanya CUF ionekane kama chama kinachochochea vurugu. Na kulithibitisha hili mgombea urais wa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005, Jakaya Khalfan Mrisho (Kikwete), alitumia propaganda hiyohiyo alipokuwa akihutubia wananchi wa Kilombero kwenye kampeni ya uchaguzi wa mwaka huo.
Kwa nyakati tofauti na mazingira yanayotatanisha vyama vya siasa vimekuwa vikipata wakati mgumu kuendesha shughuli za kisiasa hususan kwenye kuomba ruhusa (vibali) ya kufanya mikutano ya hadhara na au maandamano ya amani katika kutimiza utashi wa Katiba ya JMT ya 1977 (2005) na Sheria Na. 4, 1992 iliyotoa nafasi ya shughuli za vyama vingi vya siasa Tanzania.
5. Mfano mwingine ni kauli ya aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Afande Abdul'Rahman A. Shimbo kutoa "tamko la kijeshi" juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010. Tamko la kijeshi lililotolewa na JWTZ kupitia kwa Afande Shimbo lilikuwa ni "amri" kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM taifa!
6. Januari 5, 2011 Jiji la Arusha lilishuhudia nguvu za Polisi na taasisi za ulinzi zinazofanya kazi chini kwa chini (under cover) zikifanya mauaji mengine! Mara hii haikuwa CUF; ilikuwa ni maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilichokuwa kinafanya maandamano ya amani yaliyogeuzwa uwanja wa majaribio yaleyale ya taasisi za ulinzi na usalama kudhibiti upinzani.
7. Tangu hapo; viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA wamekuwa wakifunguliwa mashauri (kesi) mbalimbali za jinai mahakamani katika kile kinachoonekana kwamba ni uvunjaji wa sheria, kanuni na taratibu unaochukuliwa kwa kisingizio (pretext) kwamba chama hicho kilitangaza kuwa, "nchi haitatawalika." Propaganda zilizokuwa zinatumika dhidi ya CUF baina ya mwaka 2000 hadi 2010 sasa zimegeuzwa upande wa CHADEMA!
Mwisho; kwa kuwa CCM imejijengea nguvu ya uwezo (leverage) kikatiba kwa kuchukua sehemu muhimu ya kutawala na kuendesha shughuli za ulinzi na usalama kama ilivyo kwenye Ibara ya 33(2) na ya 148 ya Katiba ya JMT ya 1977 (2005), taathira ya moja kwa moja juu ya utendaji wa taasisi za ulinzi na usalama ni kuitumikia CCM katika kulinda masilahi ya muda mrefu ya kutawala siasa.
Tazama Ibara ya 148 (2) (a) hadi (d) ya Katiba ya JMT ya 1977 (2005) yanavyompa madaraka ya kutumia majeshi mwenyekiti wa CCM taifa! Hivyo ndivyo anavyoweza kutumia Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kama inavyoanzishwa kwenye Ofisi ya Rais (kifungu cha 4(1) cha Sheria Na. 15 ya 1996).
Rais wa nchi ndiye anayemuajiri Mkurugenzi Mkuu wa TISS (tazama kifungu cha 6(1) cha Sheria Na. 15, 1996); na yeye (rais wa nchi) ndiye anayeamua kumtumia mwajiriwa huyo vile apendavyo (kifungu cha 6(2) cha Sheria Na. 15, 1996).
Kama taasisi za ulinzi na usalama zote zimeundwa kwa utashi wa CCM na zinafanya kazi kwa mfumo uleule wa "amri baada ya amri" huku mwenyekiti wa CCM taifa akiwa ndiye mtoa amri (Amiri Jeshi Mkuu) unadhani wapinzani wanaweza kupata haki?
8. 02/01/2013 katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI cha ITV naibu katibu mkuu CCM bara Mwigulu Nchemba alitoa kauli nzito ya kwamba ANAYO NA ANAMILIKI CD YENYE VIDEO ya jinsi viongozi wa CHADEMA walivyokaa na kupanga mikakati jinsi ya kutekeleza mauaji nchini. Mpaka wakati huu mwigulu hajawahi kukamatwa wala kuulizwa ukweli wa swala hili.
Ushauri kwa CCM ni kuacha kutumia vyombo vya Dora kwaani wananchi wa leo siyo wa miaka ya 80. dunia nzima imebadlika kama tunaweza kutoa maoni kupitia mitandao ya kijamii.
Tafakalini swala hili kwaani kila mwananchi anajua kuwa ni mchezo mchafu. mfano kama polisi wangekuwa makini basi wangekuwa wanashughulikia issue zote bila kuangalia upande wa kisiasa.
Vyama vya siasa viwe makini kwaani kwa mfumo huu CCM itapandikiza wanachama amabo ni informer (watu wa usalama) kusaidia kuua upinzani.