Historia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Historia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
HISTORIA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inakifanya kutumia taasisi za dola ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika kutisha, kutesa, kunyamazisha na kudhoofisha upinzani wa kisiasa au wale wasio na mlengo wa CCM.

CCM, kama chama dola, kimetengeneza mfumo wa kuzif​anya taasisi zote za dola (nchi) kuwa matawi yake yakiongozwa na makada wa falsafa na itikadi yake!

Tazama mifano michache hapa chini jinsi CCM dola inavyotumia vyombo vya dola kudhoofisha upinzani.

1. Mwaka 1982 hadi 1992 kulikuwa na vuguvugu la ndani ya CCM lililochochewa na wanasiasa waliotofautiana na fikra kandamizi za demokrasia ya "chama kushika hatamu" pale nafasi za kisisasa zilipokuwa zikitolewa na kikao kimoja cha chama kwa malengo maalumu yanayotokana na utashi wa chama. CCM ilikuwa inakandamiza demokrasia ndani ya chama kwa kuzuia aina zote za upinzani wa ndani ya chama.

Nguvu za kijeshi na kipolisi zilitumika kuzima aina yoyote ya upinzani wa fikra, mawazo au imani (itikadi) kinyume na viongozi wateule wa CCM wanavyoamini! Hali hii iliwakuta kina Aboud Jumbe Mwinyi, Seif Sharif Hamad, Horace Kolimba na wengine ambao ndio waliokuwa chemchemi ya kukua kwa upinzani tunaoushuhudia leo.

2. Mwaka 1997 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilitengeneza shauri la jinai Na. 279/1997 dhidi ya Machano Khamisi Ali (na wenzake 17) kwa tuhuma za uhaini dhidi ya SMZ. Shauri la uhaini Na. 7, 1999 lilikuja kubainika kwamba lilikuwa la kubambikiza na Mahakama Kuu ya Zanzibar iliwaachia huru watuhumiwa wakiwa wamesota magereza kwa zaidi ya miaka mitatu.

3. Januari 25, 2001 Mwenyekiti wa taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipigwa na Polisi na kuvunjwa mkono alipokuwa njiani kwenda kwenye shughuli za kisiasa.

4. Hilo halikutosha kuonyesha jinsi CCM inavyotumia taasisi za ulinzi na usalama; mwaka 2005 aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Omar Idd Mahita alitoa tuhuma za ugaidi dhidi ya CUF na kukituhumu chama hicho kwamba kimeingiza makontena ya majambia kwa minajili ya kuendesha vitendo vya kigaidi!

Haya yalikuwa madai mazito kwa chama cha siasa. Hali hii iliifanya CUF ionekane kama chama kinachochochea vurugu. Na kulithibitisha hili mgombea urais wa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005, Jakaya Khalfan Mrisho (Kikwete), alitumia propaganda hiyohiyo alipokuwa akihutubia wananchi wa Kilombero kwenye kampeni ya uchaguzi wa mwaka huo.

Kwa nyakati tofauti na mazingira yanayotatanisha vyama vya siasa vimekuwa vikipata wakati mgumu kuendesha shughuli za kisiasa hususan kwenye kuomba ruhusa (vibali) ya kufanya mikutano ya hadhara na au maandamano ya amani katika kutimiza utashi wa Katiba ya JMT ya 1977 (2005) na Sheria Na. 4, 1992 iliyotoa nafasi ya shughuli za vyama vingi vya siasa Tanzania.

5. Mfano mwingine ni kauli ya aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Afande Abdul'Rahman A. Shimbo kutoa "tamko la kijeshi" juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010. Tamko la kijeshi lililotolewa na JWTZ kupitia kwa Afande Shimbo lilikuwa ni "amri" kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM taifa!

6. Januari 5, 2011 Jiji la Arusha lilishuhudia nguvu za Polisi na taasisi za ulinzi zinazofanya kazi chini kwa chini (under cover) zikifanya mauaji mengine! Mara hii haikuwa CUF; ilikuwa ni maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilichokuwa kinafanya maandamano ya amani yaliyogeuzwa uwanja wa majaribio yaleyale ya taasisi za ulinzi na usalama kudhibiti upinzani.

7. Tangu hapo; viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA wamekuwa wakifunguliwa mashauri (kesi) mbalimbali za jinai mahakamani katika kile kinachoonekana kwamba ni uvunjaji wa sheria, kanuni na taratibu unaochukuliwa kwa kisingizio (pretext) kwamba chama hicho kilitangaza kuwa, "nchi haitatawalika." Propaganda zilizokuwa zinatumika dhidi ya CUF baina ya mwaka 2000 hadi 2010 sasa zimegeuzwa upande wa CHADEMA!

Mwisho; kwa kuwa CCM imejijengea nguvu ya uwezo (leverage) kikatiba kwa kuchukua sehemu muhimu ya kutawala na kuendesha shughuli za ulinzi na usalama kama ilivyo kwenye Ibara ya 33(2) na ya 148 ya Katiba ya JMT ya 1977 (2005), taathira ya moja kwa moja juu ya utendaji wa taasisi za ulinzi na usalama ni kuitumikia CCM katika kulinda masilahi ya muda mrefu ya kutawala siasa.

Tazama Ibara ya 148 (2) (a) hadi (d) ya Katiba ya JMT ya 1977 (2005) yanavyompa madaraka ya kutumia majeshi mwenyekiti wa CCM taifa! Hivyo ndivyo anavyoweza kutumia Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kama inavyoanzishwa kwenye Ofisi ya Rais (kifungu cha 4(1) cha Sheria Na. 15 ya 1996).

Rais wa nchi ndiye anayemuajiri Mkurugenzi Mkuu wa TISS (tazama kifungu cha 6(1) cha Sheria Na. 15, 1996); na yeye (rais wa nchi) ndiye anayeamua kumtumia mwajiriwa huyo vile apendavyo (kifungu cha 6(2) cha Sheria Na. 15, 1996).
Kama taasisi za ulinzi na usalama zote zimeundwa kwa utashi wa CCM na zinafanya kazi kwa mfumo uleule wa "amri baada ya amri" huku mwenyekiti wa CCM taifa akiwa ndiye mtoa amri (Amiri Jeshi Mkuu) unadhani wapinzani wanaweza kupata haki?


8. 02/01/2013 katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI cha ITV naibu katibu mkuu CCM bara Mwigulu Nchemba alitoa kauli nzito ya kwamba ANAYO NA ANAMILIKI CD YENYE VIDEO ya jinsi viongozi wa CHADEMA walivyokaa na kupanga mikakati jinsi ya kutekeleza mauaji nchini. Mpaka wakati huu mwigulu hajawahi kukamatwa wala kuulizwa ukweli wa swala hili.

Ushauri kwa CCM ni kuacha kutumia vyombo vya Dora kwaani wananchi wa leo siyo wa miaka ya 80. dunia nzima imebadlika kama tunaweza kutoa maoni kupitia mitandao ya kijamii.

Tafakalini swala hili kwaani kila mwananchi anajua kuwa ni mchezo mchafu. mfano kama polisi wangekuwa makini basi wangekuwa wanashughulikia issue zote bila kuangalia upande wa kisiasa.

Vyama vya siasa viwe makini kwaani kwa mfumo huu CCM itapandikiza wanachama amabo ni informer (watu wa usalama) kusaidia kuua upinzani.
 
Ni kweli tuendelee kupashana habari km hizi muhimu na vijana waendelee kutuunga mkono tuweze kuikomboa tanganyika yetu.
 
mwakyembe, kubenea, na kwenye mabano sokoine
Kinachotatiza watanzania na kuishia kuonewa na CCM kiasi hiki ni Kuishi na mambo yakuazima kama ifuatavyo

UHURU wa NCHI..Duniani kote uhuru wenye maana na tija ni ule uliotokana na umoja,damu,jasho,ujasiri na uchungu wa Raia wote kwa kuona na kuthamini uhuru na utu wao hivyo kupambana bila kutegeana kwa hali na namna yoyote huku uzalendo wa kukubali kufa au kufungwa ukilenga thamani ya kizazi kilichokuwepo kwa maana ya muhusika mwenyewe na kama sio yeye basi umuhimu ulitunukiwa kizazi kijacho..Faida na Ishara ya uhuru w hivi huwa ni pamoja na Serikali zote zinazotawala na zitazo kuja kutawala taifa husika kutanguluza Heshima,kujali uhai,kuthamini maisha ya mtu mmojamoja na taifa kwa ujumla,kulinda uhuru,mali,uzalendo na kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya wananchi husika na kujitathmini kupitia maamuzi ya wananchi husika.

SERIKALI..Hii sio serikali ya Tanzania kama wengi tunavyo amini ni kundi la watu ambalo limejikita katika kuteka,kudhulumu,kuua na kukejeli tafsiri ya umma wa watu tunaojiita watanzania.Sifa za serikali yoyote halali huwa ni Kulinda uhai wa watu wake,kulinda rasilimali za Taifa,Kulinda mipaka,kusimamia maendeleo ya nchi,kutuza vipaumbele kwa watu,kuwajibika pale inapokosea,kushauriwa na kuboresha utendaji na hata kujiuzulu inaposhindwa kabisa..Hii inayojiita serikali ya Tanzania ni kinyume chayo yote hapo juu mfano ni serikali pekee inayosimamia wageni kuibia mali wananchi wake,ndio serikali pekee inayoteka na kuua watu wake,ni serikali pekee inayokataa ushauri wa kimaendeleo kwa watu wake mfano bungeni mambo ya Elimu,afya na maji,ajira na ulinzi ni hii serikali inayokwenda kuiba BOT na kupora demokrasia kwa watu wake..Inavunja katiba na kulitiisha bunge!!Eti serikali ndio Bosi wa Kuliongoza bunge la wananchi!!hii ina maana mbunge wako huenda kuishabikia serikali vinginevyo itamshughulikia

IMANI POTOFU..Wengi tuna imani potofu kuhusu kutawala na kutawaliwa mfano watanzania wengi wanaamini serikali ndio yenye haki ya kuamua kutawala au kuacha kutawala,kuleta maendeleo au kutoleta,kutulinda au kuacha kutulinda,kutuajiri au kuacha,na wengi tunaamini mazuri tunayoyaona ni hisani kuoka serikalini na kwamba wangeweza kutofanya na wasilaumiwe.Pia wengi huamini serikali ni watu fulani na majengo fulanifulani hivi na kwamba huongoza kwa pesa ambazo zinapatikana bila wananchi kujua na kuhusishwa hivyo kuacha kudai chochote serikalini.

ELIMU..Hii ni lazima iwe na mitazamo sahihi maana watanzania wengi huamini kazi ya elimu ni kupata ajira serikalini na kuvaa vizuri ikiwa ni pamoja na kumiliki pesa.Elimu ni uwezo wa utambuzi na ukomavu wa fikra na utayari wa kuwa huru ambao hupatikana mifumo rasmi na isiyokuwa rasmi.Mifumo isiyokuwa rasmi ya elimu na iliyo na tija ni pamoja kushika na kuenzi mawazo ya watu mifano(roll models)kama nyerere,karume,nkurumah na wengine ambapo kupitia redio Tv huweza kujua misimamo yao ilikuwaje,kusikiliza kwa makini misimamo ya kisiasa ya makundi ya upinzani hasa CHADEMA ambapo huelimisha bure haki na mahitaji na ubovu wa serikali pasipo kudanganya,kufanya kazi kwa bidii,kujitokeza kupiga kura kwa wingi baada kusikiliza sera na mazingatio ya kisiasa na histiria njema ya Chama ktk mambo ya kiuchumi nakadhalika mfano huwezi kumsikiliza mtu anayekudanganya kila siku na ukaendelea kumwamini kila siku.

NINI KIFANYIKE..Inawezekana watanzania wamekata tamaa ya nini kifanyike ili kuondoa mambo hayo..Kwanza ni Kuamini kwamba Tanzania haiko Huru,kuanzisha namna ya kupata uhuru ambapo ni kufanya liwezekanalo kupata uhuru kubwa zaidi kupiga kura CDM iingie madarakani,Kuacha woga wa kufa maana CCM inategemea kutishia watu vifo wasiisumbue madarakani..Kumbukeni hii ni njia ya udhalimu tangu enzi za mitume na manabii japo ni njia isiyonamafanikio zaidi hivyo watanzania waamini kifo hakitakuacha eti kwakuwa umekiogopa cha msingi ni dhamira na matendo yako ya kutafuta uhuru kwa njia yoyote ile kwa manufaa kwanza ya kizazi kijacho na inshallah kizazi hikihiki..

MUNGU WABARIKI WADANGANYIKA WAWE WATANGANYIKA
 
Mwandishi: Shabani Shabani.
Barua pepe: Shabanishabani3@gmail.com

1. CCM ndio Chama chenye unasaba na ukombozi wa Tanzania, Chama kilichopigania na kufanikiwa kuleta uhuru kutoka kwa Mkoloni. Sababu CCM ni zao la vyama mama,TANU na ASP.

2. CCM ndio Chama ambacho kina historia
ya ukombozi wa Bara la Afrika, chini ya CCM vyama vya ukombozi vilipata mafunzo, fedha na ushawishi wa kujikwamua kutoka kwenye makucha ya Makaburu, Mabeberu na Wakoloni.
Mfano ZANU_PF ya Zimbabwe,
ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola na SWAPO ya Namibia

3. CCM ndio Chama ambacho kina nukta halali na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kikaunda mfumo wa kudumisha na kuulinda kwa sababu vyama mama vya TANU na ASP ndio vichocheo na morali ya Muungano wa Tanzania.

4. CCM ndio Chama kilichojenga Umoja wa watanzania, Mshikamano wa watanzania, Amani ya Tanzania na Utulivu wa Tanzania, kwa miaka mingi na kuvijengea misingi ya kudumu isiyo tetereka kiurahisi.

5. CCM ndio Chama pekee kinachokwenda na kubadilika na wakati ili kukidhi matakwa na maslahi ya Watanzania wengi.

6. CCM ndio Chama ambacho Mwenyekiti wake wa kwanza ni Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wake wa sasa ni Ndg. John Pombe Joseph Magufuli.

7. CCM ndio Chama ambacho kina_demokrasia pana ya kushiriki na kushirikishwa na kuchagua na kuchaguliwa kuliko chama chochote cha siasa Tanzania.

8. CCM ndio Chama ambacho kipo karibu zaidi na wananchi watanzania kutokana na mfumo na mtandao wake nchi nzima uliyo madhubuti na wakipekee wa kusikiliza na kushughulikia kero za watanzania. (Kwanzia Shina hadi Taifani).

9. CCM ndio Chama Chenye Katiba nzuri, Kanuni bora, Taratibu za kistaarabu na miongozo inayoishi katika uendeshaji wake. Vyama vyote Tanzania vimeiga vitu vingi kutoka kwa CCM.

10. CCM ndio Chama chenye Nyaraka nyingi (literature), Maktaba yake iliyopo Dodoma imesheheni taarifa za kutosha kuhusu Chama
hiki imara barani Afrika.

11. CCM ndio Chama kikubwa cha kwanza Afrika, na kati ya vyama vevye mrengo wa Kijamaaa ni Chama cha pili kwa ukubwa Duniani, cha kwanza duniani kikuwa chama cha Kikomonist cha watu wa China (CPC).

13. CCM ina Dira, ilani iliyoshiba utatuzi wa shida za watanzania, ina sera zinazotoa muelekeo wa Maisha bora kwa watanzania na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo ya watu.

14. CCM ndio Chama chenye wanachama wengi Tanzania wakikadiriwa kufika milioni 10 hadi 12 mwaka 2018 , Ukiwa mwanaCCM unakuwa umeungana na familia kubwa kabisa.

Mwisho: CCM ni Chama cha siasa Makini, kina Viongozi wenye uwezo, Wanachama wenye umoja, mshikamano na upendo miongoni mwao. Heri ya siku ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi. Miaka 42 tangu kuasisiwa si haba.

Karibu CCM


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kidumu chama cha mapinduzi...😀😀😀
 
Mwandishi: Shabani Shabani.
Barua pepe: Shabanishabani3@gmail.com

1. CCM ndio Chama chenye unasaba na ukombozi wa Tanzania, Chama kilichopigania na kufanikiwa kuleta uhuru kutoka kwa Mkoloni. Sababu CCM ni zao la vyama mama,TANU na ASP.

2. CCM ndio Chama ambacho kina historia
ya ukombozi wa Bara la Afrika, chini ya CCM vyama vya ukombozi vilipata mafunzo, fedha na ushawishi wa kujikwamua kutoka kwenye makucha ya Makaburu, Mabeberu na Wakoloni.
Mfano ZANU_PF ya Zimbabwe,
ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola na SWAPO ya Namibia

3. CCM ndio Chama ambacho kina nukta halali na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kikaunda mfumo wa kudumisha na kuulinda kwa sababu vyama mama vya TANU na ASP ndio vichocheo na morali ya Muungano wa Tanzania.

4. CCM ndio Chama kilichojenga Umoja wa watanzania, Mshikamano wa watanzania, Amani ya Tanzania na Utulivu wa Tanzania, kwa miaka mingi na kuvijengea misingi ya kudumu isiyo tetereka kiurahisi.

5. CCM ndio Chama pekee kinachokwenda na kubadilika na wakati ili kukidhi matakwa na maslahi ya Watanzania wengi.

6. CCM ndio Chama ambacho Mwenyekiti wake wa kwanza ni Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wake wa sasa ni Ndg. John Pombe Joseph Magufuli.

7. CCM ndio Chama ambacho kina_demokrasia pana ya kushiriki na kushirikishwa na kuchagua na kuchaguliwa kuliko chama chochote cha siasa Tanzania.

8. CCM ndio Chama ambacho kipo karibu zaidi na wananchi watanzania kutokana na mfumo na mtandao wake nchi nzima uliyo madhubuti na wakipekee wa kusikiliza na kushughulikia kero za watanzania. (Kwanzia Shina hadi Taifani).

9. CCM ndio Chama Chenye Katiba nzuri, Kanuni bora, Taratibu za kistaarabu na miongozo inayoishi katika uendeshaji wake. Vyama vyote Tanzania vimeiga vitu vingi kutoka kwa CCM.

10. CCM ndio Chama chenye Nyaraka nyingi (literature), Maktaba yake iliyopo Dodoma imesheheni taarifa za kutosha kuhusu Chama
hiki imara barani Afrika.

11. CCM ndio Chama kikubwa cha kwanza Afrika, na kati ya vyama vevye mrengo wa Kijamaaa ni Chama cha pili kwa ukubwa Duniani, cha kwanza duniani kikuwa chama cha Kikomonist cha watu wa China (CPC).

13. CCM ina Dira, ilani iliyoshiba utatuzi wa shida za watanzania, ina sera zinazotoa muelekeo wa Maisha bora kwa watanzania na mipango madhubuti ya kuwaletea maendeleo ya watu.

14. CCM ndio Chama chenye wanachama wengi Tanzania wakikadiriwa kufika milioni 10 hadi 12 mwaka 2018 , Ukiwa mwanaCCM unakuwa umeungana na familia kubwa kabisa.

Mwisho: CCM ni Chama cha siasa Makini, kina Viongozi wenye uwezo, Wanachama wenye umoja, mshikamano na upendo miongoni mwao. Heri ya siku ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi. Miaka 42 tangu kuasisiwa si haba.

Karibu CCM


Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo chama kilicholeta umasikini tanganyika
 
Kilaaniwe Chama cha Mapinduzi.
Cha kilichoifilisi nchi kwa sera za kijingajinga. Kimeua kila kitu, kuanzia elimu, biashara, viwanda, uhuru, demokrasia, uchumi, chaguzi huru, nk. kimeuza kila kitu, kuanzia madini, mashirika yaliyokuwa yanaleta faida, gesi, mpaka twiga walisafirishwa kwenye ndege kwa usimamizi wa chama cha mapinduzi.
Kama tungekuwa watu wanaojitambua angalau asilimia 50 ya raia, ni wazi kuwa hiki chama kungekuwa kaburini muda mrefu sana.
 
CCM inanisikitisha kwa kushindwa kukarabati viwanja vya Michezo alafu inasisitiza vijana wajiajiri..
 
Chama kilichodumaza uchumi na kudunisha hali na mali za watanzania... Chama tawala kisichowapenda raia wake!!! Chama chenye kubariki wizi, ufusadi na ubaguzi, chama ambacho umaskini, ujinga, maradhi na unyonge ni sifa ya kusifia na kujivunia!!! Chama ambacho sikio linaitwa goti na watu wanashangilia!!! Chama ambacho mkono ukiitwa mkono unakuwa adui na si mwenzao!!
Hakuna cha kujivunia... kwani watanzania walishaungana kabla hata ya hiyo Tanu... Historia wanazipotosha na zinawavisha kilemba cha ukoka!!!
Chama chenye wenyewe na wasio wenyewe!!!
Fisiemu inasifiwa sana na wachumia tumbo... huku ikishangiliwa zaidi na maz.....
 
Ukieleza sifa za ccm bila Utekaji na Unyanganyi utakua ujakitendea haki chama chetu pedwa.
 
LKN pia CCM ndicho chama pekee kisichofungamana na kabira lolote,ukanda wowote au dini yoyote, CCM ni chama cha watanźania woote,bira kujari makabira yako na dini zao
 
Back
Top Bottom