Umenikumbusha kitabu cha historia ya rais wa zamani wa Marekani Harry S. Truman, kimeandikwa na muandishi nguli David McCullough. Kinaitwa "Truman". Kimetolewa mwaka 1992. Kitabu hiki pia kilifanyiwa sinema ya kampuni ya HBO.
Katika kitabu hicho, kilichoshinda nishani ya Pulitzer, muandishi David McCullough kabla ya kuanza kukupa historia ya Truman anaanza kukupa historia ya familia yake kwanza ilivyoingia na kuhamahama Marekani.
Yani kabla ya kuelezwa kuhusu Truman, unaelezwa kuhusu family tree ya Truman kwanza.
Ukija kufika kwa Truman mwenyewe inakuwa kama ushajengewa msingi wa kuanza kuelewa mtoto atakayezaliwa katika mlolongo huu anaweza kuwa vipi.
Ulivyoitaja hii point moja kwa moja nikakumbuka hicho kitabu. Hapo ndipo unaweza kuona tofauti ya muandishi nguli anayepata nishani ya Pulitzer na muandishi anayelipua lipua tu.