Historia ya Kiwanda cha Tanganyika packers mpaka kuja kuwa Kanisa la maombi

Historia ya Kiwanda cha Tanganyika packers mpaka kuja kuwa Kanisa la maombi

Ukitaka kazi yako iharibike mpe mbongo. Hata kitu kiwe bora vipi ataharibu tu.

SGR na miradi yote mikubwa tukiwapa wabongo waendeshe itakufa in no time.
 
Hii hoja ya kizuzu sana. Mtu ameleta hoja kuntu wewe unaleta uchawa. CHADEMA wanahusikaje na kiwanda wakati msimamzizi wa Sera za Maendeleo na Uwekezaji ni Serikali ya CCM.

Hii nchi imezaliza wajinga wengi sana.
Ndio think tank ya CCM huyo!
 
Case ya Tanganyika packers inafanana na ya Tazara, Urafiki hakikuwa kiwanda cha kujifia na kuuza eneo lake kwa watu.
Kuna mambo hayajakaa sawa kwenye ule ujamaa tulioukumbatia tulihitaji viongozi kama kina Kambona, sykes wenye mlengo wa kibepari mapema.
Akaja mungu wa chato akamleta progagabdist mwijaje atuambie cherehan ni kiwanda
 
Unachanganya mambo. Viwanda hivyo vimekufa wakati nchi siyo ya ujamaa tena. Viongozi waliofuatia baada ya ujamaa walikurupuka kubinafsisha bila kujua misingi ya uchumi wa kibepari. Walifikiria kumtafuta mtu mmoja mwenye pesa nyingi anunue na kumiliki badala ya kuuza hisa. Kwa jirani zetu Kenya airways ilikuwa ya serikali lakini walibinafsisha kwakuuza hisa na bado ipo inatamba. Viwanda vyote vile ambavyo vilikuwa chini ya NDC wakati huo vingekuwa bado vipo kama share zote zingeuzwa hata kwa watu wa nje
And the whole world operates that way in running businesses!
 
Kuna sehemu Njombe panaitwa olofea, mtu mmoja akaniambia ni All Affairs ilikuwa ni kwaajili ya recreation ya wazungu baada ya kazi
nadhani ni Welfare centre zamani zilikuwepo kama recreation centres with some education programmes ...health, artistic skills
 
Pamoja na maelezo yako yooote!! Dakika za jioooooni nimegundua una chuki binafsi na mwamposa !! Uchungu wako sio kiwanda kufa ni kanisa kuwekwa pale !! Kwa taarifa fupi viwanda vilivyokufa Tanzania vinaweza kufika hata 500! Vyote ni magofu ikiwemo zzk mbeya !! Jambo la pili mwamposa pale ni mpangaji analipa Kodi ya pango isiyopungua milioni 5 Kila wiki !! Hajapewa Bure !! Habari ya mafuta na udongo havihusiani na mada yako !! Hizo ni chuki kwa kanisa la mwamposa na sio kwa serikali iliyoruhusu kiwanda kife kizembe !! Hata kama wasingemkodishia mwamposa Bado kiwanda kisingerudi mjinga mkubwa wewe !
 
(Liebig’s Extract of Meat Corporation) l
Mazungumzo yaanze waitwe, Tukae meza moja, tuone tu nafanyaje!,
°mwekezaji aje na program za kuprocess,
-ngozi
-Kwato
-pembe
-chakula cha mifugo (kuku), kwa damu za ngombe!
-vyakula vya mbwa na paka!
Too late,walifungua kiwanda nchi nyingine.Bado wana usongo wa kunyanganywa mtambo wao.
Kibaya zaidi yule mhindi aliyepewa kiwanda aendeshe alifungua mitambo yote akaiuza uhindini yakabakiza magofu.
 
Pamoja na maelezo yako yooote!! Dakika za jioooooni nimegundua una chuki binafsi na mwamposa !! Uchungu wako sio kiwanda kufa ni kanisa kuwekwa pale !! Kwa taarifa fupi viwanda vilivyokufa Tanzania vinaweza kufika hata 500! Vyote ni magofu ikiwemo zzk mbeya !! Jambo la pili mwamposa pale ni mpangaji analipa Kodi ya pango isiyopungua milioni 5 Kila wiki !! Hajapewa Bure !! Habari ya mafuta na udongo havihusiani na mada yako !! Hizo ni chuki kwa kanisa la mwamposa na sio kwa serikali iliyoruhusu kiwanda kife kizembe !! Hata kama wasingemkodishia mwamposa Bado kiwanda kisingerudi mjinga mkubwa wewe !

Hahaa,
 
Ukitaka kazi yako iharibike mpe mbongo. Hata kitu kiwe bora vipi ataharibu tu.

SGR na miradi yote mikubwa tukiwapa wabongo waendeshe itakufa in no time.
Sio wabongo serikali sasa mtu mwanasiasa na yeye anataka awe fundi huo mchanganyo wa hapo ni tafrani
 
Wewe unadhani mafuta ya kuendesha train pamoja na posho kutoka Dar hadi Dodoma na ile convoy ya Rais eti kuzindua train ya SGR italipwaje na TRC? Kulishindikana nini mh Rais kuzindua huko Dar akaendelea na kazi yake then wenye kusafiri wakate tiketi kama abiria wa kila siku?
Utakuta mtu ni kiongozi wa serikali anaona sifa kupita njia ya mwendokasi ili awahi kazini ila wazalishaji wakubwa wao waendelee na foleni...wapo humu jamvini wanalalamika.
Mkuu wa Mkoa anajengewa nyumba private na taasisi wao wanachojali nyumba yake iishe ila taasisi washindwe kutoa huduma bora kwa jamii haiwahusu.
Katibu mkuu na waziri anapewa kiwanja bure na taasisi yeye anakenua bila kujua taasisi haitafikisha malengo yaliyokusudiwa.
Viongozi achaneni ubinafsi ili kutumikia wananchi; wakuu wa taasisi acahaneni kukipendekeza ili muendelee kuteuliwa kubaki hapo mlipo.
 
Wewe unadhani mafuta ya kuendesha train pamoja na posho kutoka Dar hadi Dodoma na ile convoy ya Rais eti kuzindua train ya SGR italipwaje na TRC? Kulishindikana nini mh Rais kuzindua huko Dar akaendelea na kazi yake then wenye kusafiri wakate tiketi kama abiria wa kila siku?
Kuna washauri wake ni washwawashwa hawawezi kutulia sehemu moja
 
Nimezikumbuka zile nyama hakika zilikuwa na viwango vya kimataifa!

CCM wameua viwanda na hata wahitimu hawapati ajira wamegeukia kamari, uchawa na ngono.
 
Ndiyo.

Kwa sababu tumeshakwama.
Kama tumeshakwama, acha tuishie hapo. Hatuwezi kutafuta mwekezaji bali mwekezaji ndiye anayekuja mwenyewe. Serikali ikimtafuta mwekezaji, basi inabidi imlipe mwekezaji huyo.
 
c&p from X by MMM





SERIKALI YA CCM KAMA SIYO KUROGWA NI NINI?

Tanganyika Packers LTD, Kawe, Dar es Salaam 1945-1975. Kilikuwa kiwanda cha kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Eneo lote la Mloganzila (Muhimbili) lilikuwa ni eneo la Tanganyika Packers na ndilo eneo lililokuwa linatumika kuwapokea na kunenepeshea ng’ombe

Walipoletwa kutoka mikoani kwa treni wakiteremshwa stesheni ya Pugu, baada ya mwezi wanaswagwa kupelekwa Kawe kuchinjwa na kuchakatwa.

Kutoka Mloganzila kwenda kilipo kiwanda wakati wa kuswagwa, waingereza waliita COWS WAY (njia ya ng’ombe). Waswahili wakashindwa na kuita “KAWE”

Tanganyika Packers (TPL) kilikuwa kiwanda kikubwa, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje mpaka kwa malkia wa Uingereza,

Kilikuwa kiwanda tanzu cha shirika la LEMCO (Liebig’s Extract of Meat Corporation) linalofadhiliwa na Uingereza, ambalo lilianzia miaka ya 1860 Uruguay.

Liebig ni heshima ya baba wa (Organic Chemistry), Justus von Liebig. Jengo la machinjio la LEMCO lipo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Sehemu kubwa ya nyama kutoka Tanganyika Packers iliuzwa Ulaya hususani katika nchi ya Uingereza. Watanganyika walipata ajira katika kiwanda hicho.

Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa na wakoloni kutoka Uingereza 1945 na kilitoa zaidi ya ajira 2,500 ambapo 1,200 zilikuwa ni ajira za kudumu.

Walifanya kazi kwa shift, walichukuliwa kwa mabasi kazini. 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.

Kiwanda cha TPL kilizalisha nyama za mabuchani, mafuta ya kutengeneza sabuni, damu ilikaushwa na mifupa ilisagwa na kuwa chakula cha kuku,

Pembe na kwato za ng’ombe zilichemshwa kwenye boiler zikatoa gundi, kiwanda pia kilisindika nyama na maharage kama ox-tail beans, ngozi nk

Katika vita ya Kagera 1978-1979, kiwanda kilitumika kuwalisha wapiganaji vitani. Chakula cha kusindika kilitoka kiwandani kwenda uwanja wa vita.

Mwaka 1975 Serikali ya Mwl, J.K. Nyerere ilitaifisha kiwanda cha Tanganyika Packers na kukifanya kuwa mali halali ya Serikali ya Tanganyika.

Baada ya Serikaki kutaifisha kiwanda, uzalishaji na ubora wa nyama iliyosindikwa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kukosa utaalam na ufundi.

Serikali walinyimwa leseni ya kusafirisha nyama iliyosindikwa. Walinyimwa (phytosanitary certificate) kuthibitisha ubora wa vyakula vya package

Waingereza wakawanyima cheti cha ubora na usafi wa nyama inayozalishwa. Soko la Ulaya ambako ndiyo walikuwa wanunuzi wakubwa likapotea.

Soko la ndani likawa gumu kiwanda kikaanza kusambaza nyama zake kwenye mabucha ya ndani ya Dar es Salaam na baadae kiwanda kikafariki 1993

Taratibu kiwanda cha Tanganyika Packers kikaanza kufariki. Baadaye kilibinafsishwa kwa mbunge wa Kawe, hata hivyo aliishia kuuza mashine na vipuri.

Mbunge wa Jimbo la Kawe wakati huo alitokana na CCM, aliitwa Zainuddin Adamjee. aliposhindwa Kukiendeleza akaamua kung’oa mitambo na vipuri.

Mapaa, madirisha, milango na vifungashio vilipelekwa Mapambano (veterinary) na kupimwa kama vyuma chakavu na mapaa kuuzwa kama used.

Picha chini, zinaonesha ng’ombe wakiwa Tanganyika Packers kabla kiwanda hakijataifishwa. Video kushoto inaonesha gofu la kiwanda hicho lilivyo leo

Leo pale Tanganyika Packers palipokuwa KIWANDA kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa KANISA. Watu wanauziwa udongo na mafuta na maji.



Leo pale Tanganyika Packers watu ndiyi wanakondoo na wanajipekeka wenyewe machinjioni. Wananyeshwa maji na kulishwa udongo wakielezwa ni UPAKO.

Kanisa hilo la MWAMPOSA (wao wanamuita MTUME) linawaombea maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira ili wapate ajira kwa maombi.

Maelfu ya vijana wanakesha na kufunga kwake, wananunua mafuta na maji ya UPAKO wapate KAZI. MWAMPOSA anajenga hoteli kubwa MBEYA.

Aliyewaroga watawala wa CCM na watanzania alikufa zamani na dawa ya kuwasaidia aliitupa katikati ya bahari na haiwezi kupatikana leo au kesho.

Mazombi. MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mada nzuri ila sijaona umuhimu wa kumchomeka Mwamposa!!
 
Sio wabongo serikali sasa mtu mwanasiasa na yeye anataka awe fundi huo mchanganyo wa hapo ni tafrani

Wabongo wote sio serikali tu. Hao serikali wanaonekana sababu wapo kwenye spotlight ila hata kwenye private sector wabongo wanazingua sana.
 
Back
Top Bottom