...Ndinani, umenikumbusha mbaaali sana, miaka ya 1983 au 1984 nikiwa shule ya msingi. Nilikua nafuatilia story za hawa jamaa waliokuja kujulikana sana baadae katika 'Kesi ya Uhaini'. Moja ya story ya Captain TAMIM ya kusisimua ni ile katika kukimbia asikamatwe na askari kanzu akaona lorry/gari ya wazi nyuma ikiwa imebeba crate kibao za bia akarukia na kudandia gari lile akaanza kuwavurumishia chupa za bia askari waliokuwa wanamfukuza ili wamkamate..., it is so sad kuwa ultimately akapigwa risasi na kuuwawa!
Two weeks ago nilienda Bukoba, pale airport nilikutana na mwenzao katika kesi ile, kama sijakosea anaitwa Captain Roberts. Wameshakuwa aged sasa hawa watu, unfortunately alikuwa kalewa sana. Angekua katika akili ya kawaida nilitamani kuongea nae nijue wakati huo walikusudia kuifanyia nini nchi zaidi ya kile tulichokuwa tunafanyiwa na viongozi wetu wakati ule...