1.Nimesoma hiyo link uliyoweka unayodai imesema watutsi walikuwa laki 7 na nimeirudia kama mara tatu lakini sijaona kitu cha namna hiyo,naku-challenge mkuu naomba uainishe hiyo sentensi inayosema namna hiyo pia uambatanishe na hiyo source.
Pia baada ya mauaji ya kimbari na serikali kuwa chini ya RPF,hakujawahi kufanyika tena sensa inayoonesha idadi ya makabila Rwanda,kipengele kinachoonesha idadi ya makabila kilitolewa kama sehemu ya jitihada za serikali kuutokomeza ukabila Rwanda,hicho ulichoweka angalau ungesema ni projection labda ungeeleweka,na kama unajiamini kwenye hili tupatie source kutoka kwa serikali ya rwanda kwasababu sensa yenyewe ya 2014 ilifanywa na serikali ya Rwanda,wikipedia sio credible source.
2.Usipuuzie sababu zilizowafanya RPF wakashika silaha na kuingia vitani,RPF walikuwa na sababu za msingi sana,ukizieweka pembeni utakuwa unaunga mkono Ideology ya "0 network" yaani ni wahutu tu ndio wenye haki ya kuwepo Rwanda.
3.Hakujawahi kuwa na double genocide Rwanda,isingekuwa rahisi kwa RPF kufanya genocide rwanda kama unavofikiri,hili iitwe genocide ni lazima kwanza iwe prepared,rpf walikuwa mstari wa mbele vitani wanapigana, wanateka maeneo wanasonga mbele,isingekuwa rahisi kwao kupata details za nani hasa ni mtusi na nani ni mhutu na anapatikana wapi,wahutu wenye msimamo mkali walianza kuiandaa genocide tangu 1990,haikuwa kazi ya siku moja au mwezi,walikuwa na details zote za aliyetakiwa kuuawa awe mtusi au mhutu mwenye msimamo wa kati,waliandaa jeshi na kulipa mafunzo kwa shughuli hiyo na kupenyeza propaganda ya kutosha kwa raia wa kawaida washiriki hivyo vitu,kulipuliwa kwa ndege ilikuwa ni kichocheo cha kuhalalisha mauaji lkn hata hiyo ingeshindikana ingetafutwa sababu nyingine,Gen. Dellaire aliitahadharisha UN kuwa kutakuwa na mauaji ya watusi miezi mitatu kabla ya ndege kulipuliwa,na Bagosora aliwahi kumwambia Dellaire matatizo ya rwanda hayawezi kuisha ni mpaka watusi watapofutika rwanda kwa hiyo haya mauaji yalipangwa na tena yalipangwa kwa muda mrefu.
Mimi nilipenda iitwe Rwandan genocide hili angalau hata wahutu ambao hawakushiriki huo unyama wasijisikie wana hatia ila kwa maneno uliyoandika ndo naanza kuona kwanini imepitishwa kuwa Tutsi Genoscide,kuna hatari kubwa sana ya historia kupotoshwa,kumbe kuna umuhimu wa kuukabili ukweli ila yote kwa yote mkuu mtu awe mtusi au muhutu anabaki kuwa kama binadamu wengine,wote wanayo haki ya kuishi,hakuna aliye bora zaidi ya mwingine,hakuna anayestahili kuishi zaidi ya mwingine,mgogoro wa watusi na wahutu rwanda na burundi ni matokeo mabaya ya ukoloni,kabla ya ukoloni watusi na wahutu waliishi bila kuchinjana kwa karibu/zaidi ya miaka 100,ila iliwachukua ubelgiji miaka michache tu kuipasua Rwanda na burundi vipande vpande.