Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Umeandika vyema sana Mkuu!
 
there is A lot between hutu and tusi that many don't know...genocide haikuua watusi tuu walikuepo wahutu waliouliwa wenye msimamo wa kati...all in all tuishi kwa upendo ndicho cha msingi. ..
Hilo huwezi kulisema ukiwa Rwanda.
Kwamba Wahutu pia waliuwawa!!
 
Hivi kuna Wahutu hapa Jamii forums walishawahi kuwa proud na Kagame?

Mostly Watutsi ndiyo wanakuwa front kumtetea Kagame!!
 
Good. This is what we want.
 
Bold shusha ya 12 kaka, daaah yaani mtu unasoma kama unaangalia movie vile.

Na nyie kina Zito na Ariana kwanini toka peji ya 30 mpaka sasa ni nyie tu? Mnamlalamikia the bold kinafiki na mnaumia akimsifia kagame? Bila shaka nyie ni wahutu asilimia mia, sasa chuki sio jambo baya ila nawasihi bakieni nayo ila tuachieni uzi wetu basi tuusome tuburudike, shida iko wapi? Kweli kila peji ukisoma ni nyie wawili tu hivi hamna kazi uko labda? Na yule mtusi anaetukana mngemkalia kimya asingekua anatukana, hakuna sababu ya kulumbana kijinga, tusome tu, kama na nyie mna ya kwenu tofauti na hii basi andikeni na nyie uzi mwingine, huu ni wa the bold na sie tumeufurahia sanaa, hamko hapa hili mumsaishe the bold anajua anachokifanya.
 
kweli bwana. Wao tu wanazodoana
 
Hahaaa...kwa hiyo wanaomchukia au kumsema negatively Kagame ni Wahutu.!!

Sasa huo umoja wa Wanyarwanda uko wapi?
 
Hahaaa...kwa hiyo wanaomchukia au kumsema negatively Kagame ni Wahutu.!!

Sasa huo umoja wa Wanyarwanda uko wapi?

yaani mkuu majamaa hata hayafikirii, alafu hawataki kuona watu wanachallange, mm nimekaa burundi nafanya kazi na rwanda cyo mwenyeji kivile, hii ishu imegeuzwa, na lkuhusu uhutu na utusi upo tena sana nashangaa watu wanaopinga
 
Mie muhutu tena?? 😀😀😀 aaah taratibu bhana

Anyway mturadhi tu kuwachafulia uzi ni vile tu kuna upotoshaji mkubwa kwa baadhi ya wanaocomment ndio tunakuwa tunaeleweshana ila hakuna anayempinga the bold humu naheshimu kazi yake

Ni hayo tu
 

Kwanza nianze kwa kukusifu,unajitahidi sana kufanya majadiliano bila kutoa maneno machafu wala kuonesha hasira,hongera sana kwa hilo,sasa turudi kwenye mada,nitajibu kwa mpangilio uliouandika:

A.kuhusu utafiti wa mahakama,je unafikiri ufaransa ni nchi sahihi kufanya uchunguzi huo hasa ukizingatia kuwa nae ana mkono kwenye mauaji ya kimbari kwani alikuwa akiiunga mkono waziwazi serikali ya rwanda ya wakati huo hata akafikia hadi kupeleka jeshi lake kupigana na RPF?Je,uchunguzi huo ulikuwa huru,namaanisha ulihusisha pia kuhoji upande wa viongozi wa rpf wa wakati huo including Paul Kagame?Je,utafiti huo ulihusisha wataalamu wa ndege na makombora?Je,utafiti huo ulifanyikia Rwanda ambapo ndio sehemu ndege ilipotunguliwa au ulifanyikia ufaransa?
Lakini hata hivyo mwaka 2012 ulifanyika uchunguzi uliowahusisha wataalamu waliopewa jukumu na mfaransa huyohuyo huku ukiwajumlisha wataalamu wawili wa mabomu,wataalamu wawili wa ajali za ndege,rubani moja,masoloveya wawili na mtaalamu moja wa sauti.Matokeo ya uchunguzi wa kitaalamu yalihitimisha kuwa ndege ililipuliwa kutoka kanombe millitary base ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa inakaliwa na wanajeshi wa serikali ya rwanda ya wakati huo na majeshi ya ufaransa na isingekuwa rahisi kwa wanajeshi wa rpf kujipenyeza kwenye base hiyo.Sasa ni kwanini imekuwa rahisi kwako kuchagua uchunguzi moja na kuutupa mwingine?

Source: 'Kagame hakudungua ndege' - Ripoti

B.Hapa umekwenda nje ya mjadala,mjadala ni mauaji ya kimbari rwanda.

1.Narudia tena,tafiti zote nilizofanya kwenye vyanzo huru,hakuna sehemu nimeona RPF walitumia mapanga,rpf walikuwa na silaha za moto,walikuwa frontline kupambana na jeshi la rwanda,nakuhakikishia mkuu,rpf wangeshika mapanga na kuanza kuhangaika na raia wasio na hatia wasingeshinda hii vita,tunaweza kuwasema rpf kwa maneno yoyote mabaya tunayotaka lakini mwisho wa siku rpf lilikuwa ni jeshi lenye displine ya hali ya juu sana,na wangefanya vitu vya namna hiyo wasingepata uungwaji mkono wa kimataifa,moja kati ya vitu vilivyofanya serikali ya rwanda ya wakati huo kushindwa vita ni kujihusisha na mauaji ya raia wasio na hatia na wakashindwa kuelekeza nguvu zao kupambana na jeshi lenye silaha.Hiyo unayoiita confession ya mwanajeshi wa rpf nimejaribu sana kuitafuta lkn hakuna sehemu yoyote nimeona kama ushahidi huo ulitolewa ICTR,nilichoambulia ni kuwa "unadaiwa kuwa ni ushahidi" lkn haukufikishwa ictr na kama ulifikishwa naomba unisaidie source kutoka kwenye vyanzo huru na pia mwisho wa siku nisaidie kama ushahidi ulikuja kuthibitishwa na mahakama kama ni kweli au ulibaki kuwa ni allegation?

2.Tukikubaliana na huo uchunguzi wa davenport na miller kutakuwa hakuna maana ya majadiliano tunayoyafanya humu,wao wamekataa kabisa uwepo wa genocide rwanda lakini tukumbuke tafiti zote za kitaalamu za mauaji ya Rwanda zikiwemo zilizofanywa na na wataalamu wa UN zili-conclude kuwa kulikuwa na genocide Rwanda.
 

1.Nimesoma hiyo link uliyoweka unayodai imesema watutsi walikuwa laki 7 na nimeirudia kama mara tatu lakini sijaona kitu cha namna hiyo,naku-challenge mkuu naomba uainishe hiyo sentensi inayosema namna hiyo pia uambatanishe na hiyo source.

Pia baada ya mauaji ya kimbari na serikali kuwa chini ya RPF,hakujawahi kufanyika tena sensa inayoonesha idadi ya makabila Rwanda,kipengele kinachoonesha idadi ya makabila kilitolewa kama sehemu ya jitihada za serikali kuutokomeza ukabila Rwanda,hicho ulichoweka angalau ungesema ni projection labda ungeeleweka,na kama unajiamini kwenye hili tupatie source kutoka kwa serikali ya rwanda kwasababu sensa yenyewe ya 2014 ilifanywa na serikali ya Rwanda,wikipedia sio credible source.

2.Usipuuzie sababu zilizowafanya RPF wakashika silaha na kuingia vitani,RPF walikuwa na sababu za msingi sana,ukizieweka pembeni utakuwa unaunga mkono Ideology ya "0 network" yaani ni wahutu tu ndio wenye haki ya kuwepo Rwanda.

3.Hakujawahi kuwa na double genocide Rwanda,isingekuwa rahisi kwa RPF kufanya genocide rwanda kama unavofikiri,hili iitwe genocide ni lazima kwanza iwe prepared,rpf walikuwa mstari wa mbele vitani wanapigana, wanateka maeneo wanasonga mbele,isingekuwa rahisi kwao kupata details za nani hasa ni mtusi na nani ni mhutu na anapatikana wapi,wahutu wenye msimamo mkali walianza kuiandaa genocide tangu 1990,haikuwa kazi ya siku moja au mwezi,walikuwa na details zote za aliyetakiwa kuuawa awe mtusi au mhutu mwenye msimamo wa kati,waliandaa jeshi na kulipa mafunzo kwa shughuli hiyo na kupenyeza propaganda ya kutosha kwa raia wa kawaida washiriki hivyo vitu,kulipuliwa kwa ndege ilikuwa ni kichocheo cha kuhalalisha mauaji lkn hata hiyo ingeshindikana ingetafutwa sababu nyingine,Gen. Dellaire aliitahadharisha UN kuwa kutakuwa na mauaji ya watusi miezi mitatu kabla ya ndege kulipuliwa,na Bagosora aliwahi kumwambia Dellaire matatizo ya rwanda hayawezi kuisha ni mpaka watusi watapofutika rwanda kwa hiyo haya mauaji yalipangwa na tena yalipangwa kwa muda mrefu.

Mimi nilipenda iitwe Rwandan genocide hili angalau hata wahutu ambao hawakushiriki huo unyama wasijisikie wana hatia ila kwa maneno uliyoandika ndo naanza kuona kwanini imepitishwa kuwa Tutsi Genoscide,kuna hatari kubwa sana ya historia kupotoshwa,kumbe kuna umuhimu wa kuukabili ukweli ila yote kwa yote mkuu mtu awe mtusi au muhutu anabaki kuwa kama binadamu wengine,wote wanayo haki ya kuishi,hakuna aliye bora zaidi ya mwingine,hakuna anayestahili kuishi zaidi ya mwingine,mgogoro wa watusi na wahutu rwanda na burundi ni matokeo mabaya ya ukoloni,kabla ya ukoloni watusi na wahutu waliishi bila kuchinjana kwa karibu/zaidi ya miaka 100,ila iliwachukua ubelgiji miaka michache tu kuipasua Rwanda na burundi vipande vpande.
 
TwoB nmesoma hoja zako zilizoshiba ila ntazijibu baadae maana watu wanadai tunawajazia uzi wao na kuuchafua so tusubiri usogee sogee ntareply

Thanks
 

Wewe ni genius, unajua kujenga hoja bhana doooh... Tunahitaji kusoma mijadala ya hivi uku tukiwa tunamngojea Bold.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…