SemvulaChole,
Hapana, acha manung'uniko. Nadhani hujafuatilia historia ya fedha zetu sawasawa. Sura za Karume na Nyerere zilifanywa za kudumu kwenye sarafu zetu shillingi 100 na 200 muda mrefu uliopita. Nyerere alikuja ongezewa baadaye kwenye noti ya Shs 1000 mara tu baada ya kufariki, nadhani ilikuwa ni mojawapo na maamuzi yaliyofanywa wakati wa maombolezo, na huwezi kusema kuwa hiyo ilikuwa ni kumsahahu Karume kama unajua mambo yanayofanyika wakati wa maombolezo. Ilifanyika hivyo pia wakati Mzee Karume alipofariki ambapo uwanja wa Ilala ulipewa jina la Karume wakati hakukuwa na uwanja wenye jina la Nyerere.
Kwa hiyo Karume hajasahaulika; picha ya Karume bado ni ya kudumu kwenye sarafu ya shillingi mia mbili hii hapa.
Unajua ni kawaida ya kuweka picha za watu muhimu katika pesa ndogo ambazo ndizo zinazosambaa haraka kwa watu, ndiyo maana picha ya George Washington iko kwenye Dola 1 badala ya dola 100.