Historia ya Noti na Sarafu za Tanzania

Asante nimeona nitarudia ili niielewe vizuri zaidi.
 
Naona Wazanzirabi Walisahauliwa Kabisa Kwenye Hizo Pesa

Picha Ya Nyerere Imekuwa Ya Kudumu Lakini Maalim Abein Amani Karume Haimo Sasa Haya Ndiyo Mamabo Yanayopelekea Muungano Kuonekana Ni Wabara Tuuuu

Nichukieni Sasa Kwa Kusema Hilo
Du hamwishi manung'uniko. Kila kitu manunguniko. alikuwepo twiga mkanungu'nika, kweli ni kisiwa cha wanung'unikao.
 
Kichuguu, Hongera sana kwa kumbukumbu zuri uliyotuletea, umenikumbusha mbali sana hasa nilipoiona noti ya sh. 20 second ver (Pound) ya Nyerere maana hapo ndiyo nilipoanzia kumiliki pesa yangu mwenyewe. Enzi zetu tulikuwa tunaanza kumiliki pesa ukiwa mtu mzima kuanzia miaka 20 na kuendelea ingawa kulikuwa na watu waliokuwa wakimiliki kuanzia miaka 16 lakini walikuwa wanatunziwa na wazazi wao. Na akitaka kuitumia anaomba kwa mzazi wake na iwe kwa matumizi mhimu sana, mzazi anaweza kuitumia na akakutaarifu tu kwamba ameitumia na siyo lazima akurudishie ingawa kuna wazazi wengine walikuwa wanawarudishia watoto wao. ....nakushukuru sana asante kwa kumbukumbu.
 
Du hamwishi manung'uniko. Kila kitu manunguniko. alikuwepo twiga mkanungu'nika, kweli ni kisiwa cha wanung'unikao.

Wanasahau kuwa nchi yao ina uchumi ambao ni asilimia 5 tu ya uchumi wa Tanzania; hata kwa eneo ni chini ya 5%.
 
Nimempigia Mzee Mtei simu akanieleza maoni yake ni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ivunjwe na kwamba atapendekeza hivyo atakapopata fursa ya kutoa maoni katika Tume ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba. Kwa hiyo wale Wazanzibari wanaotaka Muungano uvunjike wakiona hii assement wanaweza kuhimiza matakwa yao na ya Mtei pia.
 
Hongera sana mkuu, manake noti za miaka ya 1905 nilikuwa hata sijawahi kuona picha zake. Ni historia nzuri iliyotulia na kuelimisha kwa kweli.

Ila tu 1992 ndio hapo wenye mamlaka walipopotea kwa kuchapa noti mpya za TSh. 5,000 (elfu tano) na Tsh. 10,000 (elfu kumi). Kwa kweli walihamasisha sana kuporomoka kwa shilingi, mfumuko wa bei na usumbufu kwa kutafuta chenji hasa vijijini.
 

Asante sana kwa taarifa ya historia ya Tanzania.
 
Kichuguu asante kwa shule nzuri, hii mada nilikuwa sijawahi kuiona, pia nashukuru mods kwa kutengeneza jukwaa la historia. kwa haraka haraka ukiangalia historia ya machapisho ya fedha yetu utaona ni nani aliyeharibu uchumi wa Tanzania.
 
Nikusahihishe mkuu Kichuguu. Hayo majengo nyuma ya noti ya shilingi 1000/= siyo kiwanda cha Tanganyika parkers. hayo ni mgodi wa makaa ya mawe Kiwira uliofunguliwa mwaka 1988 na Mwinyi. Picha hiyo iliwekwa ili kuenzi mafanikio ya kufunguliwa kwa mgodi huo. Hata leo ukienda Kiwira (alikojisevia Mkapa) ndivyo yanavyoonekana. Hilo jengo la kushoto linalofuka moshi ndipo kuna mtambo wa kuzalisha umeme. Pembeni yake kulia unaona kuna lundo la makaa ya mawe. Kakibanda kulia kabisa ni geti la kuingilia mgodini.
 
Wanasahau kuwa nchi yao ina uchumi ambao ni asilimia 5 tu ya uchumi wa Tanzania; hata kwa eneo ni chini ya 5%.
Mzee Edwin Mtei, wewe ndiwe uliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki kuu ya tanzania ilipoundwa baada ya kuvunjika kwa East African Currency Board; je unaweza kutusaidia kuelewa chanzo cha kuvunjika kwa EACB na ni namna gani mlivyoamua kusanifu pesa zetu mpya? Yaani ni nani aliyepewa jukumu la kusanifu pesa zetu mpya na ni vigezo gani vilivyotumika katika usanifu huo. Wewe unajua mengi kuhusu historia ya pesa hiyo kwani tangu mwaka 1966 hadi 1980 ulikuwa kenye nafasi inayohusu pesa hizo. Ni wewe peke yake ambaye sahihi yake inonekana pande zote mbili za pesa hiyo: upande wa waziri na upande wa gavana. Wengine wote ama walikuwa magavana tu (Nyirabu, Rutihinda, Idrisa Rashid, Balali na Benno) au Mawaziri tu ( Amil Jamal, CD msuya, Kighoma Malima, Steven Kibona, Mbilinyi, na waliofuatia)
 
Last edited by a moderator:
Nataka kununua hizo hela zazamani?nitazipata wapi?
 
Iko wapo pesa ya Tanganyika kabla ya kuchapishwa hizo hela za kijerumani? Sitaki pesa ya Dola ya zanzibar, pesa ya Dola la Tanganyika please??????

Pesa ya Tanganyika ilikuwa ikiitwa vipi kabla ya Pesa hizo za Kijerumani na kizanzibar?

Jee, munayo picha ya pesa hizo za Tanganyika?
 

Zanzibar alikuwa anatawala sultani/mwarabu kwa hiyo kulikuwa na pesa ya zanzibar chini ya sultani/mwarabu. Tanganyika alikuwa anatawala Mjerumani hivyo pesa ya mjerumani ndio iliyokuwa ikitumika.
Ukumbuke pia pesa ya zanzibar haikuanzishwa na watu wa zanzibar kabla mwarabu kuitawala zanzibar, na wala zanzibar haikuwa ikiitwa zanzibar kabla ya sultan/mwarabu kufika pale.
Kwa kifupi si wabara wala wa visiwani, hakuna ambaye alikuwa na pesa yake kabla ya wavamizi wa kijerumani na ki arabu.
 
Andate,

Labda umesahau au hukulijuwa hili, zanaibar walikuwa na sarafu kabla ya kufika kwa sulat Sayyid said Al Saidi 1806 na kufunguwa second zenj empire 1832.

Nakuomba ufungue tena vitabu vya hostoria utaona hilo
 
Mkuu Kichuguu asante sana kwa historia hii yaani ni nzuri mbaya
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…