Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Soko la Kariakoo ambalo Rais Samia Suluhu anakusudia kulifanyia mapinduzi makubwa kwa kukarabati jengo lake la zamani na kujenga lingine jipya ambalo litapokea machinga zaidi ya 2,000, lina historia ya kipekee.
Soko Kuu hilo lipo katika kiwanja namba 32 eneo la Kariakoo, katikati ya makutano ya mtaa wa Mkunguni na mtaa wa Nyamwezi na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.
Historia ya soko la hilo inarudi nyuma hadi enzi za Wakoloni wa Kijerumani wakati wanaitawala Tanganyika.
Awali Wajerumani walikusudia kujenga ukumbi wa kuadhimisha sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim wa II wa Ujerumani kwa wakati huo.
Kaiser Wilhelm II alikuwa mfalme wa mwisho wa Prussia na Kaiser wa mwisho wa Ujerumani kuanzia mwaka 1888 hadi 1918.
Hata hivyo baada ya jengo kukamilika halikutumiwa kama ilivyokusudiwa na badala yake lilitumika kama kambi ya kikosi cha wapagazi waliobeba mizigo ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia waliojulikana kama 'Carrier Corps'.
Jina hilo ndilo lililokuja kuzaa neno Kariakoo, kwani Waswahili hawakuweza kutamka Carrier Corps, walilitohoa.
Baada ya Vita Kuu ya Dunia kuisha mwaka 1919 na Wajerumani kuondoka, Tanganyika ikaanza kutawaliwa na Waingereza, jengo hilo lilianza kutumika kama soko na kuhudumia wakazi wa Dar es Salaam, ambapo wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sakafuni kwa sababu hapakuwa na meza hadi mwaka 1960, meza zilipojengwa.
Kutokana na ongezeko la watu jijini Dare s Salaam, kulikuwa na msongamano mkubwa sokoni hapo na hivyo soko hilo kushindwa kuhudumia wafanyabiashara.
Ndipo mwaka 1970, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliagiza kujenga Soko jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya soko la zamani. Uamuzi huo ulianza kutekelezwa Machi 1971.
Ramani ya jengo la soko ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo Mtanzania Beda Amuli. Mchoraji huyo alikuwa Mwafrika wa kwanza kwa Afrika Mashariki na Kati kuwa na ofisi yake binafsi ya utaalamu wa ujenzi tangu mwaka 1969.
Baadhi ya taarifa zinasema, mkandarasi huyo alitakiwa kwenda kujifunza nchini Ghana na Zambia, kuangalia masoko yaliyojengwa katika miji hiyo miwili, ndipo atengeneze ramani yake, lakini mwenyewe aliwahi kusema kuwa alipata wazo la kutengeneza ramani ya jengo hilo kutokana na utaalamu alioupata nchini Israel alikosomea.
Amuli alifariki Julai 10, 2016, tarehe hiyo hiyo ndiyo soko la Kariakoo limeunga.
Ujenzi wa soko ulikamilika mwaka 1975 kwa gharama ya Sh22 milioni na kufunguliwa rasmi Desemba mwaka huo huo na Rais Julius Nyerere akiwa mgeni rasmi.
Soko hilo lina majengo mawili ambayo yameunganishwa katika ghorofa ya chini ya ardhi. Soko kubwa limegawanyika katika sehemu tatu ambayo ni ghorofa ya kwanza, sehemu ya kati na ya chini maarufu kama shimoni.
Sasa baada ya Rais Samia kutenga bajeti ya shilingi zaidi ya Bilioni 32, historia mpya inaenda kuandikwa kwani Kariakoo patakuwa na jengo lingine la Kisasa.