Historia ya Tanganyika: Kubali Ukweli Hata Kama Ukweli Unapingwa na Dunia Nzima

Historia ya Tanganyika: Kubali Ukweli Hata Kama Ukweli Unapingwa na Dunia Nzima

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AMESEMA ALIYESEMA NITAWAFELISHA WANAFUNZI KWA HISTORIA ZANGU ZISIZO NA VYANZO VYA KUAMINIKA

Lupweko said:

Mzee utawafelisha watoto kwenye mitihani yao kwa historia zako ambazo hazina vyanzo vya kuaminika

Lupweko,
Mimi sina historia iliyo yangu.

Historia ni kama ilivyotendwa na wahusika hao ndiyo wenye historia yao.

Wala vitabu nilivyoandika mimi haviko katika mtaala kwa hiyo hakuna mwalimu anaesomesha kitabu changu katika shule za Tanzania kwa hiyo uwezekano wa mwanafunzi kufeli mtihani haupo kabisa.

Labda tuzungumze historia ya Maji Maji na yale ambayo mimi nimeyasahihisha katika historia hiyo na nitakuwekea ushahidi.

Majemadari wa Maji Maji walinyongwa na Wajerumani na kuzikwa katika kaburi la halaiki isipokuwa mmoja Songea Mbano ambae jina lake khasa ni Abdulrauf Songea Mbano.

Katika hao walionyongwa yuko mwanamke mmoja ambae siku zote anatambulishwa kwa jina moja tu la Mkomanile.

Jina lake huyu mama ni Khadija.

Jiulize kwa nini majina ya Kiislam yameondolewa kwa hawa mashujaa?

Majemadari hawa wote walikuwa Waislam na walipopitishiwa hukumu ya kunyongwa Father Johannes kutoka Peramiho aliwaendelea na kuwaambia kuwa endapo wataukana Uislam na kuwa Wakristo hukumu ya kuuliwa itafutwa.

Father Johannes wa Peramiho akawabatiza baadhi na kuwapa majina ya Kikristo.

Ukisoma majina ya hawa yaliyoandikwa katika mnara wa kumbukumbu ya Maji Maji, Mahenge, Songea utaona majina yao ya Kiislam hayapo yameandikwa majina ya Kikristo.

Ushahidi wa haya unatokana katika utafiti niliofanya na mwingine katika haya ninayokueleza hapo juu upo katika kitabu cha Prof. James Giblin kuhusu Maji Maji: ''Lifting the Fog of War,'' (2010).

Kuwa vyanzo vyangu haviaminiki si kweli.
Usijipotezee nafasi ya kujifunza kwa hofu isiyokuwa na sababu.

Ama kuhusu kufeli wanafunzi hawa wamashafelishwa kwa kusomeshwa historia iliyoandikwa kwa ghilba.

Nakuwekea hapo chini picha ya Prof. Giblin ofisini kwake University of Iowa akiwa ameshika kitabu cha Abdul Sykes.

Prof. Giblin ni mwalimu wa African History chuoni hapo.
Huu ni mwaka wa 2011.

PICHA:
1. Prof. James Giblin.
2. Mnara wa kumbukumu wa majemadari 66 wa Maji Maji walionyongwa na Wajerumani hapo penye mnara ndipo lilipo kaburi lao.
3. Kaburi la Abdulrauf Songea Mbano
4. Abdulrauf Songea Mbano
 
Asante mzee wangu Mohamed kwa MAARIFA haya mazuri ambayo hatujafundishwa mahala popote isipokua kwako..

Shukrani sanaa 🙏
 
udini tu unakusumbua mzee, nashauri huu ulikuwa muda wako wa kucheza na wajukuu (kama unao) kuliko kuleta mambo ya uswahilini na vijembe kwenye harakati zako wa kuaminisha watu kua uislam unaonewa. hata upewe nchi zima hii iwe mali yako peke yako wewe hautaacha kulalamika, umeumbiwa kulalamika, ndio maana hata heshima yako imeshuka kwa watu wengi.
 
Mzee unahangaika sana,kupenyeza ajenda zako ila zimeshagefeli waliokutuma waambie tz sio nchi ya hichi unachokitafuta..mlengo wako tunaujua...ni mpuuzi na punguani atakayekaa kusikiliza na kusoma porojo zako zilizojaa chuki na ulongo.
 
Mzee unazo hoja, ila wengi wanakupinga kwa mipasho tu
Iele...
Naelewa maumivu yao.
Wao hawawezi kunyanyua kalamu wakaleta historia kama hii.

Historia yao iliyokuwapo leo haina miguu ya kusimama.

1715975460539.jpeg

 
udini tu unakusumbua mzee, nashauri huu ulikuwa muda wako wa kucheza na wajukuu (kama unao) kuliko kuleta mambo ya uswahilini na vijembe kwenye harakati zako wa kuaminisha watu kua uislam unaonewa. hata upewe nchi zima hii iwe mali yako peke yako wewe hautaacha kulalamika, umeumbiwa kulalamika, ndio maana hata heshima yako imeshuka kwa watu wengi.
Yesu...
Hapana mimi si mdini wala siandiki vijembe na Uislam kuonewa wala heshima yangu haijashuka mahali popote.

Nina nishani tano za uandishi na ya mwisho nimepokea mwezi March mwaka huu.

Vyombo vya habari havipungia nyumbani kwangu kunihoji kuhusu historia ya Tanzania.
 
Mzee wangu una mambo mazuri, ni furaha sana kumuona mwenye hekima amezeeka, We ni mkweli sana na huongei hoja zako bila uthibitisho, unaitendea haki kauli ya (no authority no right to speak). Mungu akujalie afya njema inshallah🙏​
 
maudhui na misimamo yako inafanana, sijui lengo lako ni nini hasa!
asilimia kubwa ya mabandiko unayoleta humu yako njia moja.

ok, endelea tu..
Per...
Lengo langu lilikuwa kusahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika iliyokuwa inafundishwa kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Katika hili nimefanikiwa baada ya kuandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Ndani ya kitabu hiki nimeeleza historia ya African Association hadi vuguvugu la kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ndiyo tunayoijadili na kuizungumza hapa sasa zaidi ya miaka 10.

Kutokana na historia hii wazalendo waliokuwa hawatajwi kwenye historia ya zamani kama ilivyoandikwa sasa wanafahamika.

Kutokana na uandishi wa historia hii JF wamenichagua Mwandishi Bora mara mbili.

Halikadhalika kitabu changu kinasomeshwa kama rejea muhimu katika historia ya Tanganyika.

Yapo na mengine kadha wa kadha.
 
Mzee wangu una mambo mazuri, ni furaha sana kumuona mwenye hekima amezeeka, We ni mkweli sana na huongei hoja zako bila uthibitisho, unaitendea haki kauli ya (no authority no right to speak). Mungu akujalie afya njema inshallah🙏​
Witch...
Ahsante.

No research...
 
Mzee unazo hoja, ila wengi wanakupinga kwa mipasho tu
Iele...

"Ndege pekee anayethubutu kumgonga Tai ni Kunguru.

Hukaa kwenye mgongo wa Tai na kudonoa donoa shingo yake.

Hata hivyo Tai huwa hajibu au kupigana na Kunguru.

Hufungua mbawa zake na kuanza kupaa juu zaidi, ndio inavyokua ngumu kwa Kunguru kupumua na hatimae Kunguru huanguka kwa kukosa oksijen.

Sio Vita zote unahitajika kujibu, wewe wapeleke kwenye kimo chako na watapotea."

(Maneno haya nimeyasoma kutoka kwa rafiki yangu mtandaoni).

Zaidi ya miaka 10 sasa mjadala uko hapa lakini hakuna aliyeandika kitabu kupinga kitabu changu.

Wale waliojaribu kupinga ukweli ndani ya kitabu cha Abdul Sykes wengi siwasomi tena hapa.

Hawa wa leo ni wapya kabisa.
Watakosa oxygen na wao watapumzika kama waliowatangulia.

Mimi bado nipo.
Sijachoka.

Naendelea kuifundusha historia ya kweli na nimewafunza wengi mengi ambayo hawakuwa wanayajua.

Kitabu kinakwenda toleo la tano.
 
Sasa mzee hapo napata ukakasi umesema walibatizwa na kupewa majina ya kikristo.

Sasa kwanini unalalamika watumie majina ya kiislamu wakati walishaukana uislamu wakabatizwa na kuwa wakristo?
 
Sasa mzee hapo napata ukakasi umesema walibatizwa na kupewa majina ya kikristo.

Sasa kwanini unalalamika watumie majina ya kiislamu wakati walishaukana uislamu wakabatizwa na kuwa wakristo?
Mutual...
Hapana mimi naeleza yale yaliyotokea.

Silalamiki.

Wewe unanipa hoja yako hulalamiko unaeleza fikra zako.
 
Back
Top Bottom