nyiokunda
JF-Expert Member
- Jun 16, 2015
- 1,976
- 1,181
okayNyio...
Kalamu yangu imevutia watu wengi sana.
Sikujua kama nawe ni mmoja kati ya hao.
Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
okayNyio...
Kalamu yangu imevutia watu wengi sana.
Sikujua kama nawe ni mmoja kati ya hao.
Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com
Kondoo...Siku moja lete uzi wa John Okello Mr. MS
Mohamed Said ninavutiwa saana na maandiko yako ya historia. Ni bahati mbaya tu maandiko yako mengi yameegemea kwa watu fulanifulani ambao ukiona wanakosekena kwenye picha fulani fulani basi kwako hiyo historia haijakamilika. Mbaya zaidi tukio fulani likimuhusisha mtu asiye wa dini unayoitaka wewe basi historia haijakamilika au utadai imepotoshwa!Kitabu hiki nimekuwancho kwa miaka mingi sana.
Lakini kwa kuwa ni kitabu cha picha nilikisoma mara moja tu katika miaka ya 1980 na kikabakia Maktaba.
Sikukigusa tena.
Jana nimeona picha za TANU katika mtandao na haraka nikatambua kuwa picha hizi nimepata kuziona katika kitabu hicho hapo juu.
Ndipo nilipokitafuta kitabu hiki na kuanza kukipitia.
Kwa hakika nilistarehe sana na picha nilizozikuta ndani ya kitabu hiki ikawa kama vile naziona picha zile kwa mara ya kwanza.
Katika moja ya picha ambayo ilinivutia kwa kosa nililoliona katika maelezo ya picha hiyo ni hiyo hapo chini:
Maelezo ya picha hii ya waasisi wa TANU ni kuwa hao ni waanzilishi wa TAA.
Vipi linaweza kufanyika kosa kama hili?
Picha hii ya Waasisi wa TANU mwaka wa 1954 ni maarufu sana.
Hili mosi.
Pili hapajakuwapo na picha ya waasisi wa African Association iliyoanzishwa mwaka wa 1929.
Ingawa nimabahatika kupata picha mbili za waasisi wa chama hicho - picha ya Kleist Sykes na picha ya Mzee bin Sudi.
Tukirejea kwenye picha hiyo ya Waasisi wa TANU kuna kisa kirefu kuhusu picha hiyo iliyowekwa hapo.
Picha hiyo imechezewa kwa kutiwa mkono.
Katika picha yenyewe ya Waasisi wa TANU Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu hawamo.
Hawa walijitoa kwa kjuwa walikuwa ni watumishi wa serikali na sheria ilikuw ainawakataza kujihusisha na siasa.
Ilipokuwa inapigwa picha wao walikaa pembeni.
Angalia picha halisi hapo chini:
Kasella Bantu kapachikwa kati ya Abdul Sykes na Chief Patrick Kunambi.
Kazi hii ilifanywa na Idara ya Picha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Siku zote kila nikiangalia picha hiyo iliyotiwa mkono hujiuliza kama haja ilikuw akuwaweka waasisi wote wa TANU kwa nini hazikuwekwa pia picha za Ally Sykes na Tewa Said Tewa.
Tuendelee kubakia katika hili suala la picha hii ya Waasisi wa TANU.
Katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere, ''Nyerere Biography,'' kitabu kinaeleza kuwa picha hii ilipigwa na kamera ya Denis Phombeah yeye mwenyewe akiwa mpigaji wa picha hiyo.
Abbas Sykes alikuwapo katika mkutano wa kuasisi TANU lakini hakuwa mjumbe bali kijana mdogo wa kutumwa na kaka yake Abdul Sykes na wajumbe wengine wa mkutano kufanya hiki na kile katika mkutano ule.
Abbas Sykes amenieleza kuwa picha ya Waasisi wa TANU ilipigwa na mpiga picha maarufu Dar es Salaam jina lake Gomez.
Abbas Sykes anaeleza kuwa walimsubiri Gomez ambae studio yake ilikuwa Acacia Avenue kwa muda hakutokea.
Abdul Sykes akamwambia Abbas achukue baiskeli ya TAA amfate wakapishana.
Wakati Abbas Sykes anamfuata Gomez yeye kumbe alikuwa njiani akija New Street kuwapiga picha waasisi wa TANU.
Katika kitabu hiki cha ''Nyerere na Watanzania,'' kuna picha hapo chini ya baiskeli ya kwanza ya TANU.
Bila shaka hii ndiyo baiskeli ya kijana mdogo Abbas Sykes alipanda kumfata mpiga picha Gomez:
View attachment 2576879Ukiangalia picha hii utaona nimeshika kitabu.
Baiskeli ya TANU
View attachment 2576880
Picha niliyopigwa na Gomez 1956
Mwandishi ni huyo kushoto kulia ni ndugu yangu Kapufi Yunge
Mama anasema nilikuwa situlii kwenye kiti ndipo Gomez akanipa kitabu nishike.
Studio ya Gomez ilikuwapo hadi miaka ya 1980.
Mbussi,Mohamed Said ninavutiwa saana na maandiko yako ya historia. Ni bahati mbaya tu maandiko yako mengi yameegemea kwa watu fulanifulani ambao ukiona wanakosekena kwenye picha fulani fulani basi kwako hiyo historia haijakamilika. Mbaya zaidi tukio fulani likimuhusisha mtu asiye wa dini unayoitaka wewe basi historia haijakamilika au utadai imepotoshwa!
Siku nyingine bwana Saidi nitaomba uje na historia ya biashara ya utumwa na jinsi Waarabu walivyoshiriki ktk hiyo biashara kwa nchi za Afrika Mashariki. Ni kwann maeneo yaliyoshamiri biashara ya utumwa kama vile Pwani, Ujiji, Mombasa, Kilwa na Zanzibar etc dini ya kiislam imeshamiri pia? Je, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya biashara ya utumwa na Uislamu?
Said miye siumizwi chochote na Waislam kuwa miongoni mwa watu waliopigania Uhuru. Nachoamini Watanzania wa dini zote, makabila yote na ata wale wasiyokuwa na dini, wote walihusika kati hizo harakati. Kinachogomba ni wewe kung'ang'ania baadhi ya watu waonekane wa maana na muhimu kwenye kupigania Uhuru na kwamba majina yao yakikosekana kutajwa ni kosa la jinai. Kama nilivyokuambia, usilinganishe vyama vya siasa na vile vya kuweka na kukopa, uwa havina kugawana faida, ukiishia njiani ata kama wewe ni mwanzilishi, historia inakusahau. Unapaswa kupambana hadi mwisho.Mbussi,
Hili la Waislam kuwa na mchango mkubwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika linakuchoma sana.
Huna haja ya kuuma maneno.
Ukweli ni kuwa waliodhani wanaweza kuandika historia ya TANU bila ya Sykes wametambua ukubwa wa kosa lao.
Kuhusu historia ya utumwa nakushauri wewe usome kwanza Transatlantic Slave Trade.
Mbussi,Said miye siumizwi chochote na Waislam kuwa miongoni mwa watu waliopigania Uhuru. Nachoamini Watanzania wa dini zote, makabila yote na ata wale wasiyokuwa na dini, wote walihusika kati hizo harakati. Kinachogomba ni wewe kung'ang'ania baadhi ya watu waonekane wa maana na muhimu kwenye kupigania Uhuru na kwamba majina yao yakikosekana kutajwa ni kosa la jinai. Kama nilivyokuambia, usilinganishe vyama vya siasa na vile vya kuweka na kukopa, uwa havina kugawana faida, ukiishia njiani ata kama wewe ni mwanzilishi, historia inakusahau. Unapaswa kupambana hadi mwisho.
Trans antilantic slave trade haiusiani sana na biashara ya utumwa kwa Afrika Mashariki, ambako key prayer wa hii biashara alikuwa ni Muarabu.