Uongo. Uongo. Uongo.
1. Nyerere aliondokea wapi kwenda Edinburg mwaka 1949?
2.Alipotoka Edinburg mwaka 1952 alipokewa na nani?
3. Alipokuwa anafundisha Pugu alikuwa anakaa wapi? Tukumbuke Nyerere alikuwa analipwa paundi 450 kwa mwezi, mshahara ambao ilibidi Gavana akubali alipwe. Kwa mshahara huo na nafasi yake, mnataka kutuambia kuwa kila alipofika Dar alikuwa anajibana kwenye chumba cha Abbas? Bila shaka inawezekana kuna siku alifanya hivyo kwa rafiki yake lakini huo si ushahidi kuwa Abdulwahid ndie alimpokea Dar!
4. Alichokifanya MS ni kuchukua incidence moja na kuifanya ndio kawaida. Si bure yeye kutumia neno 'inasemekana'.
Uongo mtupu.
Amandla.....
Hapo sasa, unapokuja ukasema "Uongo". "Uongo". "Uongo". inabidi uje wewe na kusema ukweli, ukweli, ukweli ulikuwa hivi. Sasa wewe unasema Uongo, ukweli wako haujauweka, unaanza kuuliza tena kabla hujatuonesha "version" yako yenye ukweli, tukuite nani?
1. Hilo utueleze wewe, kwanini utuulize sisi na wewe ndio uliolileta? au hujui?
2. Hilo utueleze wewe, kwanini utuulize sisi na wewe ndio uliolileta? au hujui?
3. Hilo utueleze wewe, kwanini utuulize sisi na wewe ndio uliolileta? au hujui? Jibu letu hapo juu ni mwaka 1955 si huko unaposema wewe na lina sema hivi:
Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid Kariakoo Market. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba Mtaa wa Stanley na Abbas Sykes ndiye aliyeambiwa na kaka yake atoke chumbani kwake ampishe Nyerere.
4. Hapo ndipo inapotakiwa wewe sasa ueleze "incidence" zingine na kama unajuwa kuwa Mohamed Said kaandika "incidence" hiyo moja ina maana hajadanganya na mbele huko anaelezea kuwa mpaka nguo za Nyerere zikifuliwa hapo, sasa hiyo "incidence" moja ilkuwa ndefu na si siku moja au mbili au wewe unayo ya kutuelezea mbadala wa huu "uongo" wa Mohamed Said? Tuelezee ukweli wako hapa.