Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hivi Nyerere ilikuwaje akawa Rais wa TANU wakati walikuwepo kina Rupia, Kyaruzi, Sykes, n.k? Ningependa kusikia simulizi la Said kwenye hili.

Good question. Kulingana na hadithi za Mohamed Saidi, Masheikh wakubwa na Viongozi wengineo maarafu waliokuwa vinara wa TAA/TANU waliamua kumchagua Nyerere kuwa Rais wa TANU huku wakijua kuwa ni Mkatoliki, na wengineo "inasemekana" walimnyooshea vifimbo kwenye kadamnasi ya Wanachama wa TANU, ambao tunachukulia asilimia kubwa walikuwa Waislamu wakimtuhumu Nyeyere kuwa angewaasi na kuwashau Waislamu baada ya Tanganyika kuwa huru. Kwa nini? Kama "Mwanahistoria" anayejifanya kuwa ndiyo, Mohamed Said ameshindwa kupeleleza na kuja na jibu la swali hili muhimu.
 
...............Na sasa natoa ujumbe kwa wote wanaotoa hoja za kijinga kuwa na sisi tuandike historia kupinga hizi porojo. Wengine wetu uandishi si taaluma yetu, ................

Mag3
huhitaji kuwa kwenye taaluma ya uandishi na eti uandike kitabu au paper kwakuwa umeona uongo (kwenye hizi simulizi/hadithi za Brother MS) na kuukosoa.......hakuna hiyo kitu....

simulizi/hadithi za Brother MS zitachambuliwa hapa JF na kuonyesha udhaifu wake.......
 
Hivi Nyerere ilikuwaje akawa Rais wa TANU wakati walikuwepo kina Rupia, Kyaruzi, Sykes, n.k? Ningependa kusikia simulizi la Said kwenye hili.
Siyo hiyo tu, Abdul Sykes anayedaiwa na Mohamed Said kuwa ndiye aliyeanzisha TANU, hatusimuliwi je, kwa nini hakutaka kukiongoza chama ? na kama alitaka je, kwa nini hakugombea Uraisi wa TANU ? na kama aligombea alishindwaje ? na kama alishindwa aliridhika na matokeo ? na kama hakuridhika kwa nini aliendelea kubaki humo ? Sasa pamoja na majibu yanayoweza kutolewa, huo ushujaa wake ni upi na unatokana na nini kama hata chama alichodaiwa kukianzisha hakuwa hata na sifa za kukiongoza ? Angalau Mtemzu alikuwa na ujasiri wa kuzira na kuanzisha cha kwake ! Maswali, maswali na maswali zaidi.
 
Nyerere kasemwa na kuitwa kila jina la ubaya, kasingiziwa kila neno hilo halimhusu kama marhum. Wakisemwa wengine ''tuachane na hayo, si jambo jema kuongelea marehem kwa mabaya''. Haa!
double standard za mzee wetu

Can't swallow own medicine, dhambi ya ubaguzi.
 
Kwanza tukwambie wengine tunamjua mpaka mtu aliyekuwa anaitwa Geugeu, jamaa aliyekuwa anaishi Ng'ambo ya bahari. Jitu refu la miraba minne mmoja wa wababe wa mjini. Kwenye Hotuba nyingi za Nyerere utamsikia mtu anapaza sauti "ndiyo Babaa" basi ujue huyo alikuwa ni Geugeu. Lakini ni wapi kwenye historia "Rasmi" (Hata kwenye vitabu vyako) jina la Geugeu limetajwa? Au kwa kuwa yeye si wa Gerezani ndiyo maana hatajwi? Mimi binafsi nachukia sana kutaja taja majina ya watu kwa lengo la kuonyesha kwamba ni mjuvi wa mambo.

Hapo kwenye rangi ya kijani (najua unaipenda hiyo rangi) ndipo ilipo shida yangu. Unaposema au kutumia neno "Omitted' kwenye lugha ya kiingereza unamaanisha tendo la kukusudia la kutoa kitu ili kisiwepo, mara nyingi tendo hilo huwa ovu. Sasa Mohamed ni nani hasa kwa kumtaja kwa jina au ni kina nani hasa walio - omitte majina ya hao "Musilmpatriots' katika kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Tanganyika??
0
Mzee Kigarama,
Umenikumbusha mbali. Geugeu. The original vuvuzela!
 
Asante Mohamed Said kwa kufunguka hata kama ni kwa kukariri. Wengine tumejifunza mengi. Kukosolewa ni sehemu ya kuweka mambo sawa, ila ukweli unabaki pale pale.

Kama upo, ila kama "umetengenezwa" kukidhi mahitaji ya mtu au kikundi hakuna "kitakachobaki pale pale"
 
Kama upo, ila kama "umetengenezwa" kukidhi mahitaji ya mtu au kikundi hakuna "kitakachobaki pale pale"

ukweli huwa unakwepwa na haufichiki. Kwa vile hakuna aliyesema kuwa hadithi/simulizi za MS ni za uongo, na imefikiwa hatua ya kuzikosoa tu, ni wazi kuwa ukweli upo, kinachofanyika ni kukosoa maeneo fulani fulani.
 
Tembo sio mguu wake tu, bali tembo ni ujumla wake, huwezi kusifia mkia wa tembo kwa kubeza na kutukana macho na mkonga wa tembo!
 
Tembo sio mguu wake tu, bali tembo ni ujumla wake, huwezi kusifia mkia wa tembo kwa kubeza na kutukana macho na mkonga wa tembo!

Hii ni valid kwenye ideal situation when all other factors are constant, na pale unapotaka utakalo liwe.
 
ukweli huwa unakwepwa na haufichiki. Kwa vile hakuna aliyesema kuwa hadithi/simulizi za MS ni za uongo, na imefikiwa hatua ya kuzikosoa tu, ni wazi kuwa ukweli upo, kinachofanyika ni kukosoa maeneo fulani fulani.
Nadhani kuna kitu ambacho baadhi ya watu hawjakielewa.

Kwanza niweke sawa kuwa hakuna anayekataa maandiko ya Mohamed kwa ujumla wake. Sykes, Mshume, Rupia, Makaranga, Tewa, Munanka, chama cha AA, TAA, TANU, EAMWS, Shekih Takdiri, Dossa Azizi, Bibi Titi, Plantan n.k walikuwepo.
Hakuna anayekataa kuwa harakati za uhuru zilichagizwa sana kutoka Dar es salaam, hakuna anayekataa kuwa mikoa ya pwani ilikuwa na waislam wengi.Hakuna anayekataa Nyerere alihamia Dar es salaam kutoka Butiama n.k nk.

Tunachokataa ni kule kusema baadhi ya watu wameachwa kwenye historia kwasababu ya dini yao. Think about this, mshume Kiyate hakupewa jina la mtaa kwasababu ni mwaislam, tunapouliza la John Rupia lipo wapi? hakuna jibu. mambo haya na mengine ndiyo yanayohojiwa.

Tunachokataa ni kuwa baadhi ya watu wa gerezani ndio walileta uhuru kwasababu ni waislam. Tunasema hivi uhuru ulipiganiwa kupinga dhulma ya mkoloni na waliofanya hivyo hawakuwa na agenda ya udini ndiyo maana walishirikiana wote bila kubaguana tena nchi nzima. Lakini masimulizi ya hadithi za Mohamed yamelenga kuwagawa wananchi katika misingi ya dini.

Tunachokataa ni pale inaposemekana kuwa historia inaandikwa kwa ukamilifu wake wakati huo huo inaacha viungo muhimu kama ile inayotuhumiwa ilivyoacha.

Tunachokataa ni kupandikiza mbegu za chuki za kidini kwamba kuna dini inakandamiza nyingine. Inaweza kuwa ni kweli kama itaelezwa kwa uhalisia wa jambo, bahati mbaya sana Mohamed anaonyesha chuki ya wazi dhidi ya wakristo na wakatoliki hata kubambikizia hoja zake na kusema ni za waislam. Ndiyo maana sehemu kubwa ya maandiko yake ni 'inasemekana'.

Tunachokataa ni frustration za Mohamed alizohadithiwa kuwa yeye ni best student na alinyimwa fursa kwa dini yake. Mohamed haelezi best student waliopata fursa kwa dini hiyo hiyo. Anaposema yeye anaona watu waliokuwa dhaifu wakiwa wakubwa zake wa kazi na wana magari ni frustration yake ambayo anataka kuifanya kuwa frustration ya taifa.

Tunachokataa ni frustration ya Mohamed kuwa babu yake aliongoza mgomo, na kwa matarajio yake alitakiwa awe katibu mkuu au waziri kama fadhila kwa babu yake. Frustration zake anataka kuzifanya za kitaifa.

Tunachokataa ni yeye kutunga maneno na kuwafundisha watu bila kuwaambia ukweli. Anaposema asilimia 83 ya nafasi za uongozi ni wakristo na 17 ni waislam, sasa hatujui hindu, bohara na wapagani wao wana aslilimi gani. Kibaya zaidi ni pale anapotaka nafasi za uongozi zizingatie dini na si sifa.Huku ni kuligawa taifa kwani matatizo yetu hayatokani na dini bali umasikini uliotamalaki uanoshadidiwa na maadili ya viongozi wachafu.

Tunachokataa ni Mohamed kuwafanya watu waimbe nyimbo kuwa mwislam ananunua sukari bei ya juu kuliko asiye mwislam.
Tunachokataa ni kuzua uongo ili kuleta tafrani katika taifa na mara zote ameshindwa kutetea uongo na uzushi wake kama ule wa namba za mitihani na mabucha ya nguruwe

Tunachokataa ni yeye kutumia majina ya waislam na uislam kufikia lengo la kuvuruga taifa.

Tuanchokataa nni yeye kusema serikali hii yenye miaka 50 na chama kile kile anataka aongee nayo kuhusu dhulma.Aongee nini kilichioshindikana miaka 50 kwa the same. Hapa hana hoja anachotaka ni kulifarakanisha taifa kwa kutumia taaisisi yake ya siri ambayo yeye amekiri ni kiongozi. Katika dunia ya leo hatuwezi kukubaliana na taasisi kama hizi kwani hatujui malengo yake.

Tunachokataa ni Mohamed kuwawekea marehemu maneno na kuyafanya kama kauli zao. Wale walio hai hawahoji wala kutaka maoni yao hadi pale watapoaga dunia kama alivyofanya kwa Fundikira, Kawawa na Malima.

Tunachokataa ni yeye kuwafanya watu wasifikiri wakidhani kuwa matatizo yao yanaletwa na wakatoliki hata kama matatizo na ufumbuzi upo mikononi mwao. Mfano, anasema BAKWATA ni makafri, fair enough! sasa waislam safi chombo chao ni kipi?

na mambo mengi mengi yanaayoweza kujaza kurasa 100.

Kinachotia maudhi ni pale anapowadhalilisha Watanzania wenye nchi yao kwa kusema anafanya mihadhara huko Ulaya na Marekani na kwahiyo hatuhitaji kumhoji kwasababu kwake wazungu ni bora sana kuliko hata wale waarabu anaodhani ni sehemu ya imani yake na wala si Uislam kama dini ya mwenyezi mungu

Mohamed na simulizi zake ameshindwa kabisa kujibu maswali na hoja za wananchi wenye nchi yao, hoja kubwa aliyo nayo ni kila mtu aandike kitabu. Huyu ni mtafiti asiyeweza kutetea utafiti wake lakini ameweza kuwadanganya baadhi ya watu na sasa wanaimba nyimbo wasizojua tenzi au tungo zake.

Mohamed amefikia hatua ya kutangaza hali ya hatari na kutishia UN au AU kuwepo kwa kile anachokiona ni hatari. Sisi tunajua anajua kile anachookiona kwasababu yeye ndiye anaye engineer. Ndiyo maana kama watanzania tunasimama na kumwambia, NO! HATUPO HIVYO, HATUKUBALIANI NAWE.
Kama kuna tatizo liongelewe kwa uwazi na ukweli bila kuzua uzushi au kuchomeka hisia za mtu binafsi na kuzifanya za kitaifa, kama ule wa mabucha ya nguruwe na umasikini.

Hatusimami hapa kumzuia asiandike hadithi za wapwa zake au familia au watoto na vijana wenzake wa Gerezani enzi hizo.
Tunachokikataa ni kutumia dini akiwa amejificha katika siasa ili kuleta vurugu. Huyu ni mwerevu sana wa kutumia kalamu yake na anaweza kubadilisha hadithi kama ile ya mwembe chai kutuleta balaa. Sio mtu wa kumdharau na kumwacha ni lazima tumkemee na tumfunze wapi maandiko yake yamekosa maadili ya kiroho japo yameandika kwa misingi ya maadili ya kiroho.

Nadhani utakuwa umeelewa vema ni nini tunachosimamia na umeona udhaifu wa Mohamed katika kukanbiliana na hoja.
Hoja ya kila mtu aandike kitabu ni ya kiwango dhaifu sana kiusomi na inatuacha wengine tujiulize kulikoni?

Ingekuwa vema ukamshauri ima ajibu hoja au akubaliane na mapungufu ili sote tuandike historia ya nchi hii bila kutanguliza frustartion, chuki za kidini zisizo na msingi dhidi ya wanadamu wengine.

Uongo na uzushi ukiachwa bila kuhojiwa utageuka kuwa ukweli, haina maana kila neno lake ni uongo, la hasha! Lakini yale ya kuchomeka ni hatari zaidi kuliko yale ya ukweli. Asifinyange historia na kusema ni ya Tanganyika. Kama ni ya mtaa wa Narung'ombe, kipata na manyema hewalaaa!

Kama yupo anayedhani anaonewa aseme, ili tuweke hoja 13 alizokubalina nasi. Kwanini tumeze tu kila kitu bila kutafuna!

Kwahakika kumuacha aendelee kumwaga sumu ni kulisaliti taifa. Wengine tunasema hata kama ni page milioni 1 tutasimama naye bila kumuonea au kumuonea huruma.
 
Ndugu Nguruvi

nadhani unakubaliana makala za bwana Said zimekosolewa. Hii inabakisha ukweli kwamba makala hizi zina ukweli ila sehemu kadhaa zimenyooshwa, kama ulivyoweka kwenye post yako hapo juu.

Na pia baadhi hatutachoka kumshukuru Bwana Said kwa kutuelimisha. Kuna wengine walikuwa wanayajua, na hasa wale wanaokosoa, tuna uhakika kabisa walikuwa wanajua historia hii ila walinyamaza, kwa sababu zao wenyewe including ''kudhani labda wote wanajua wanayoyajua na wanayoyajua ndio sahihi AU walidhani wangeitoa ingekuwa ni kumwaga sumu''.
 
Nguruvi3,
Umeandika mengi lakini mimi nitakuambia kitu kimoja tu.

Ikiwa wewe kwa hakika unataka kujua ukweli wa maneno yangu khasa kuhusu dhulma na fitna ya Nyerere dhidi ya Uislam na Waislam hebu pinda mgongo na fanya utafiti.

Ninakuhakikishia utakuja na kitabu bora kuiliko cha Bergen na Sivalon na utapata sababu kwa nini historia ya TANU haikutakiwa kuandikwa kwa ukweli na ukamilifu wake.

Utaelewa kwa nini majina ya Waislam waliopigania uhuru wa Tanganyika yakaogopwa.

Vinginevyo utadumaa hapo hapo ulipo.
Mohamed aseme wewe ndiyo upate la kusema.
Kama peke yako huwezi tafuta wenzanko humu ndani msaidiane.

Vinginevyo maisha mtabakia kupiga fidla nambari mbili.

Katika historia ya TANU Nguruvi3 wewe huwezi kunishinda mimi hata siku moja kwa hiyo ondoa kuwa unaweza kusimama na mimi.
Usimame na mimi kwa kipi ukijuacho wewe katika historia hii.

Kwa "paper" ipi au kitabu gani ulichoandika au hata kusoma kuhusu TANU?

Nimetumia miaka mingi kuyajua haya achilia mbali kuwa nimekulia Dar es Salaam na hao waliopigania uhuru ni wazee wangu.

Ingia katika darsa niloweka kuhusu Sheikh Hassan bin Amir uone maajabu.

Mohamed

Mohamed
 
Siyo hiyo tu, Abdul Sykes anayedaiwa na Mohamed Said kuwa ndiye aliyeanzisha TANU, hatusimuliwi je, kwa nini hakutaka kukiongoza chama ? na kama alitaka je, kwa nini hakugombea Uraisi wa TANU ? na kama aligombea alishindwaje ? na kama alishindwa aliridhika na matokeo ? na kama hakuridhika kwa nini aliendelea kubaki humo ? Sasa pamoja na majibu yanayoweza kutolewa, huo ushujaa wake ni upi na unatokana na nini kama hata chama alichodaiwa kukianzisha hakuwa hata na sifa za kukiongoza ? Angalau Mtemzu alikuwa na ujasiri wa kuzira na kuanzisha cha kwake ! Maswali, maswali na maswali zaidi.

Mag3,

Yote hayo nimeeleza katika kitabu chake.

Yeye alimtaka Chief Kidaha achukue uongozi wa TAA waanzishe TANU na wadai uhuru.
Hii ilikuwa 1950.

Habari zaidi zimo kwenye kitabu.

Mohamed
 
Usipate tabu Mgalanjuka. Mwanakijiji alimaliza yote aliposema haya;

Katika kukariri, Mohamed Said ni bingwa ndiyo maana hajui hata hatari ya hiyo mbegu anayoipanda. Taabu yote hii inasababbishwa na ukweli kuwa tulipata uhuru mwaka 1961 na hakuna mzee hata moja wa Mohamed (hasa hao walowezi wa Kizulu na Manyema) aliyeukwaa hata unaibu waziri katika serikali ya kwanza ya Tanganyika huru kama walivyotegemea. Naamini Mwalimu aliwasoma sana hawa jamaa - oneni sasa vitoto na vijukuu vyao kama Mohamed Said vinavyochangamkia hizo hadithi walizopewa utotoni !

first cabinet of tanzania.jpg

Cabinet ya kwanza ya Tanganyika 1961
Msitari wa nyuma toka kushoto - Job Lusinde, Rashidi Kawawa, Nsilo Swai, Oscar Kambona, George Kahama na Derek Bryceson
Msitari wa mbele kutoka kushoto - Paul Bomani, Abdulla Fundikira, Mwalimu Nyerere, na Amir Jamal

nyerere+baraza+la+mwaziri.jpg

Cabinet ya Kwanza ya Tanzania 1964
Mstari wa mbeletoka kushoto - Tewa Saidi Tewa, H. Makame, Oscar Kambona, Amir Jamal, Abeid Karume, Solomon Eliufoo, Mwalimu Nyerere, Lawi Sijaona, Rashid Kawawa, Bhoke Munanka na Abdul Wakil
Msitari wa nyuma toka kushoto - Kasim Hanga, Dereck Bryceson, Job Lusinde, Abdulrahman Babu, Austin Shaba, Abdul Jumbe, Chediel Mgonja na Said Maswanya.

Katika kuonyesha Udini wake ambao anajitahidi kuuficha kwa kivuli cha historia anawaingiza hata watu ambao hawakuwa Watanganyika eti katika harakati za kupigania uhuru mradi tu walikuwa viongozi wa dini. Mtu kama Sheikh Hassan bin Ameir anaingizwaje katika mashujaa wa Tanganyika kabla ya uhuru ? Amekazania kuisifu TAA kwa kuwataja akina Sykes lakini aliyeiongoza TAA baada ya kuundwa kwake akiwa Raisi wake wa kwanza hatajwi, je ni kwa sababu hakuwa Muislaam ?

Sisi wengine tunampa ukweli kuwa chama chochote kile kiwe TAA, AMNUT, TANC au TANU kinakuwa na Raisi moja tu anayekiongoza. Fahali wawili hawakai zizi moja na ndio maana watu kama Zuberi Mtemvu au Mohamed Chamwenyewe, mambo yalipowashinda ndani ya TANU walitafuta zizi lingine, TANC na AMNUT. Sote tunajua kuwa hata huko yaliwashinda, sasa huo umaarufu wao utoke wapi hadi wawekwe mizani moja na Mwalimu ?

Na sasa natoa ujumbe kwa wote wanaotoa hoja za kijinga kuwa na sisi tuandike historia kupinga hizi porojo. Wengine wetu uandishi si taaluma yetu, engineer uanze kuandika historia ya miaka hamsini iliyopita duh, mbona kuna ya muhimu ya kulisaidia taifa langu. Lakini nina hakika wapo watu wanaupitia huu mnakasha na ikibidi wataandika wenye taaluma hiyo, haya ya kwetu ni tahadhari tu kwa mtu yeyote yule atakayeamua kufanya hivyo, ajiepushe na porojo kama hizi za kichochezi, hazijengi.

Mag3,

Nahisi hujakisoma kitabu changu.
Kitabu changu kimependwa kwa kuwa khasa kinajibu hayo yote uloandika.

Hivi tunaingia katika chapisho la tatu.
Jiiulize kwa nini?

Mohamed
 
.............Katika historia ya TANU Nguruvi3 wewe huwezi kunishinda mimi hata siku moja kwa hiyo ondoa kuwa unaweza kusimama na mimi.
Usimame na mimi kwa kipi ukijuacho wewe katika historia hii.

Kwa "paper" ipi au kitabu gani ulichoandika au hata kusoma kuhusu TANU?

Nimetumia miaka mingi kuyajua haya achilia mbali kuwa nimekulia Dar es Salaam na hao waliopigania uhuru ni wazee wangu.

......Mohamed

This is too low kwa mtu anayejiita "mtafiti".......samahani Brother MS....hebu rudisha tafakuri zako sawasawa.........hizo statements hapo juu siamini kama zinatoka kwa mwandishi/mwanataaluma/mtafiti...........I'm sorry....its too low!
 
Jasusi,

Kwa kweli umenizindua mie nilimsahau huyu mtu kabisa kama vile namuona na shati lake la kitenge.
Geugeu alikuwa kwenye kesi ya uhaini?

Hebu nipe taarifa zake zaidi.

Geugeu anastahili kufanyiwa utafiti habari zake zikafahamika.

Mohamed
Mohamed
Sisi tukiwa vijana pale DSM enzi za 65-68 Geugeu alikuwa kama kichekesho na burudani ya aina yake kwetu. Alikuwa hakosi mikutano ya TANU, kama ni Jangwani au Mnazi Mmoja. Kwa hakika anastahili utafiti wa kipekee kwa sababu alikuwa a "character." Nakumbuka ndiye aliyezusha neno "majungu" wakati huo sisi hatuna internet, lakini mazungumzo yote ya mitaani tukiyafahamu na kupasiana kama vijana wa leo wanavyotumia facebook. Na wakati huo ukisikia neno majungu ujuwe kuna ukweli wa aina fulani. Alikuja kuhusishwa na kesi ya uhaini mwaka 1969 nadhani na baada ya hapo sikumsikia tena.
 
Mohamed Said;2811612]Sweke34,Mafunzo yetu yanatukataza kukumbushana enzi ya ujahilia.
Haifai sasa kuanza kuongea mambo yasopendeza ya marehemu
Mohamed Said;2813091]Nguruvi3,Ikiwa wewe kwa hakika unataka kujua ukweli wa maneno yangu khasa kuhusu dhulma na fitna ya Nyerere dhidi ya Uislam na Waislam hebu pinda mgongo na fanya
Nianzie hapa, hivi mtu anayeweza kuwa na double standard za namna hii anaweza kuandika kitu ukameza tu!
Utaelewa kwa nini majina ya Waislam waliopigania uhuru wa Tanganyika yakaogopwa. Vinginevyo utadumaa hapo hapo ulipo. Mohamed aseme wewe ndiyo upate la kusema.Kama peke yako huwezi tafuta wenzanko humu ndani msaidiane
Ahsante umethibitisha kauli zangu kuwa hiyo si 'historia' ya Tanganyika ni ya Waislam wa Gerezani na kwahiyo haifai kuitwa histtoria bali masimulizi ya Kiapata na Narung'ombe. Historia ya kweli haichagui wala kubagua inafuata mtiririko wa matukio.
Katika historia ya TANU Nguruvi3 wewe huwezi kunishinda mimi hata siku moja kwa hiyo ondoa kuwa unaweza kusimama na mimi.Usimame na mimi kwa kipi ukijuacho wewe katika historia hii.
Na pia siwezi kukaa nakukusikiliza ukinidanganya au kunichochea. Lakini Mohamed, si umekubali kuwa Rupia ni mzee wako. Si Kigarama amekupiga shule ya wazee wake wa Kalenga na sasa umetulia. Si tumekwambia mchana kweupe kuwa mwembechai ni kutokana na hasira za watu kwa kutosikilizwa malalamiko yao na ni UONGO usio na haya kusema ni kutokana na umasikini wa Tabora, Kilwa, Mtwara na Kigoma. Hujajibu kusema si kweli pamoja na utajiri wa historia yako.

Tunakupiga shule kuwa EAMWS haikuuawa na Nyerere ni usaliti wa waislam waliotanguliza matumbo yao badala ya masilahi ya umma kama alivyofanya Tewa Said. Unaficha ukweli kuwa hakuna shoka linalokata bila mpini. Unachotueleza ni makabrasha aliyokuachia Tewa.

Si tumekueleza kuwa kama Nyerere ni muovu vipi Kawawa, Fundikira na akina maswanya walishiriki vipi kuumiza umma unaodai ulidhulumiwa. Hawa unawapamba kwa kuficha ukweli na kumtwisha lawama mbaya wako Julius Nyerere.
Tunasimama na wewe kwasababu hujaweza kujibu hoja au maswali zaidi ya vipande vya 'reference' zako unazodhani ni standard.
Kwa "paper" ipi au kitabu gani ulichoandika au hata kusoma kuhusu TANU?Nimetumia miaka mingi kuyajua haya achilia mbali kuwa nimekulia Dar es Salaam na hao waliopigania uhuru ni wazee wanguKwahiyo
ukikulia Dar ndiyo mjanja! hivi niandike paper ya nini kuhusu mabucha ya nguruwe wakati tunajua ni uongo, na ukweli ni kuwa hakuna mahusiano kati ya mabucha na umasikini wa watanzania.

Niandike paper ya kujibu chuki za kupandikiza kuwa waislam walivunja makanisa wakati wa kadhia ya mabucha, nikijua huo ni uongo kutoka kwa mzee. Ukweli ni kuwa hakuna kanisa au nyumba au mali iliyoshambuliwa na waislam. Wao walikwenda moja kwa moja pale walipokuwa na hasira zao kwenye mabucha.
Nikikuonyesha paper zangu zimejaa streptococcal, trichuris truchura hutaweza kuelewa maana hazina hadithi au 'inasemekana'

Ingia katika darsa niloweka kuhusu Sheikh Hassan bin Amir uone maajabu
Maajabu nimeyaona, nayo ni ushabiki wa kidini hakuna kipya kwa wasomaji wa nyaraka mbali mbali. Kwa wanokusoma leo kwa ku browse inaweza kuwa maajabu,kwa wanaosoma between the lines nothing new, the same old story embelished with fancy language.

Kwa wale wenye shaka kuwa huenda ni kweli tupu, nawatoa wasi wasi kwa kusema, Mohamed kakariri vizuri sana masimulizi. Tatizo ni pale anapoulizwa hubaki kujichangaya na jibu rahisi andikeni vitabu. Mtafiti anayeijua TANU asiyeweza kui-defend,.

Mohamed ana malengo yake. Kwanza amesema(ushahidi upo) kuwa ameelezwa na marhum sheikh wake kuwa lazima kwanza wawaamshe waislam watambue dhulma. Kauli hiyo ni ushahidi wa kutosha katika mahakama yoyote kuwa haya ni masimulizi yenye lengo la kuamsha hisia za watu yaliyopewa jina la historia kamili inayorekebisha ile iliyokosewa. Kwamba unakosea ili kurekebisha kosa.

Pili, amekiri kuzunguka mikoani na vituo vya redio kuelezea dhulma, ushahidi kuwa haya ni masimulizi ya dhulma na si historia.

Tatu, ana malengo makuu matatu
1. Kumdhalilisha Nyerere kwanza kama alivyofanya kila mara ikiwa ni pamoja na kutaja vitoweo na soksi zake ndeeeeeeeefu.
2. Kuwashambulia wakristo kama chanzo cha matatizo ya waislam. Hii si sehemu ya historiahisia ni sehemu ya chuki
3. Kuhakikisha anatumia majina na dini kuleta mtafaruku ili kukidhi kiu ya frustration zinazotokana na yeye kuwa nje ya mfumo ili hali wazee wake akiwemo babu yake walimenyaka.
4. Kuufarakanisha umma kwa hisia zake anazosema ni za waislam. Anaficha ukweli kuwa AMNUT kama walivyo BAKWATA, shura ya maimam, kamati ya haki, kamati ya mali walianza kuvurugana kuanzia mwaka 1959 na kwamba mchawi yumo ndani ya nyumba na si yule anayemsingizia.
Anataka kusukuma matatizo kwa watu wasiohusika na kuwaficha wahusika ukweli.Hadi leo hakuna chombo nje ya BAKWATA kinachoweza kusema kinawakilisha waislam. Hapo haoni tatizo anaona ya mfumokristo

Nimalizie kwa mfano mmoja, Mohamed anasema mabucha.............by christian traders. Hasemi kuna bar zinamilikiwa na muslimtraders.
Yeye ni kuonyesha ubaya wa jirani na kuficha uvundo uvunguni mwa kitanda.
Read between the lines you will realize how dangerous is this man.
 
Jasusi,

Kwa kweli umenizindua mie nilimsahau huyu mtu kabisa kama vile namuona na shati lake la kitenge.
Geugeu alikuwa kwenye kesi ya uhaini?

Hebu nipe taarifa zake zaidi.

Geugeu anastahili kufanyiwa utafiti habari zake zikafahamika.

Mohamed
Wewe kusahau si neno ila akisahau Nyerere inakuwa kwa sababu ya wivu na chuki za kidini. Haya bwana ni heri tumekukumbusha mpaka na mashati ya vitenge ya Geugeu umeyataja!!
 
Ndugu Nguruvi

nadhani unakubaliana makala za bwana Said zimekosolewa. Hii inabakisha ukweli kwamba makala hizi zina ukweli ila sehemu kadhaa zimenyooshwa, kama ulivyoweka kwenye post yako hapo juu.

Na pia baadhi hatutachoka kumshukuru Bwana Said kwa kutuelimisha. Kuna wengine walikuwa wanayajua, na hasa wale wanaokosoa, tuna uhakika kabisa walikuwa wanajua historia hii ila walinyamaza, kwa sababu zao wenyewe including ''kudhani labda wote wanajua wanayoyajua na wanayoyajua ndio sahihi AU walidhani wangeitoa ingekuwa ni kumwaga sumu''.
Unakosea sana unapotoa hukumu kwamba wanaokosoa waliijua historia wakanyamaza. Historia ya nchi ni uwanja mpana sana hakuna mtu anayeweza akaandika kila kitu kilichotokea kwa ukamilifu. Kama mtu kafanya utafiti hazuiwi na watu wengine kutoa mchango wake, lakini kujaza hisia na chuki binafsi dhidi ya watu wengine kwa misingi ya udini na kuita ni historia iliyosahauliwa, haikubaliwi na kamwe hakuna atakaye afiki. Tunamuogopa mzee Mohamed Said kwa sababu anatupeleka kubaya!
 
Back
Top Bottom