ukweli huwa unakwepwa na haufichiki. Kwa vile hakuna aliyesema kuwa hadithi/simulizi za MS ni za uongo, na imefikiwa hatua ya kuzikosoa tu, ni wazi kuwa ukweli upo, kinachofanyika ni kukosoa maeneo fulani fulani.
Nadhani kuna kitu ambacho baadhi ya watu hawjakielewa.
Kwanza niweke sawa kuwa hakuna anayekataa maandiko ya Mohamed kwa ujumla wake. Sykes, Mshume, Rupia, Makaranga, Tewa, Munanka, chama cha AA, TAA, TANU, EAMWS, Shekih Takdiri, Dossa Azizi, Bibi Titi, Plantan n.k walikuwepo.
Hakuna anayekataa kuwa harakati za uhuru zilichagizwa sana kutoka Dar es salaam, hakuna anayekataa kuwa mikoa ya pwani ilikuwa na waislam wengi.Hakuna anayekataa Nyerere alihamia Dar es salaam kutoka Butiama n.k nk.
Tunachokataa ni kule kusema baadhi ya watu wameachwa kwenye historia kwasababu ya dini yao. Think about this, mshume Kiyate hakupewa jina la mtaa kwasababu ni mwaislam, tunapouliza la John Rupia lipo wapi? hakuna jibu. mambo haya na mengine ndiyo yanayohojiwa.
Tunachokataa ni kuwa baadhi ya watu wa gerezani ndio walileta uhuru kwasababu ni waislam. Tunasema hivi uhuru ulipiganiwa kupinga dhulma ya mkoloni na waliofanya hivyo hawakuwa na agenda ya udini ndiyo maana walishirikiana wote bila kubaguana tena nchi nzima. Lakini masimulizi ya hadithi za Mohamed yamelenga kuwagawa wananchi katika misingi ya dini.
Tunachokataa ni pale inaposemekana kuwa historia inaandikwa kwa ukamilifu wake wakati huo huo inaacha viungo muhimu kama ile inayotuhumiwa ilivyoacha.
Tunachokataa ni kupandikiza mbegu za chuki za kidini kwamba kuna dini inakandamiza nyingine. Inaweza kuwa ni kweli kama itaelezwa kwa uhalisia wa jambo, bahati mbaya sana Mohamed anaonyesha chuki ya wazi dhidi ya wakristo na wakatoliki hata kubambikizia hoja zake na kusema ni za waislam. Ndiyo maana sehemu kubwa ya maandiko yake ni 'inasemekana'.
Tunachokataa ni frustration za Mohamed alizohadithiwa kuwa yeye ni best student na alinyimwa fursa kwa dini yake. Mohamed haelezi best student waliopata fursa kwa dini hiyo hiyo. Anaposema yeye anaona watu waliokuwa dhaifu wakiwa wakubwa zake wa kazi na wana magari ni frustration yake ambayo anataka kuifanya kuwa frustration ya taifa.
Tunachokataa ni frustration ya Mohamed kuwa babu yake aliongoza mgomo, na kwa matarajio yake alitakiwa awe katibu mkuu au waziri kama fadhila kwa babu yake. Frustration zake anataka kuzifanya za kitaifa.
Tunachokataa ni yeye kutunga maneno na kuwafundisha watu bila kuwaambia ukweli. Anaposema asilimia 83 ya nafasi za uongozi ni wakristo na 17 ni waislam, sasa hatujui hindu, bohara na wapagani wao wana aslilimi gani. Kibaya zaidi ni pale anapotaka nafasi za uongozi zizingatie dini na si sifa.Huku ni kuligawa taifa kwani matatizo yetu hayatokani na dini bali umasikini uliotamalaki uanoshadidiwa na maadili ya viongozi wachafu.
Tunachokataa ni Mohamed kuwafanya watu waimbe nyimbo kuwa mwislam ananunua sukari bei ya juu kuliko asiye mwislam.
Tunachokataa ni kuzua uongo ili kuleta tafrani katika taifa na mara zote ameshindwa kutetea uongo na uzushi wake kama ule wa namba za mitihani na mabucha ya nguruwe
Tunachokataa ni yeye kutumia majina ya waislam na uislam kufikia lengo la kuvuruga taifa.
Tuanchokataa nni yeye kusema serikali hii yenye miaka 50 na chama kile kile anataka aongee nayo kuhusu dhulma.Aongee nini kilichioshindikana miaka 50 kwa the same. Hapa hana hoja anachotaka ni kulifarakanisha taifa kwa kutumia taaisisi yake ya siri ambayo yeye amekiri ni kiongozi. Katika dunia ya leo hatuwezi kukubaliana na taasisi kama hizi kwani hatujui malengo yake.
Tunachokataa ni Mohamed kuwawekea marehemu maneno na kuyafanya kama kauli zao. Wale walio hai hawahoji wala kutaka maoni yao hadi pale watapoaga dunia kama alivyofanya kwa Fundikira, Kawawa na Malima.
Tunachokataa ni yeye kuwafanya watu wasifikiri wakidhani kuwa matatizo yao yanaletwa na wakatoliki hata kama matatizo na ufumbuzi upo mikononi mwao. Mfano, anasema BAKWATA ni makafri, fair enough! sasa waislam safi chombo chao ni kipi?
na mambo mengi mengi yanaayoweza kujaza kurasa 100.
Kinachotia maudhi ni pale anapowadhalilisha Watanzania wenye nchi yao kwa kusema anafanya mihadhara huko Ulaya na Marekani na kwahiyo hatuhitaji kumhoji kwasababu kwake wazungu ni bora sana kuliko hata wale waarabu anaodhani ni sehemu ya imani yake na wala si Uislam kama dini ya mwenyezi mungu
Mohamed na simulizi zake ameshindwa kabisa kujibu maswali na hoja za wananchi wenye nchi yao, hoja kubwa aliyo nayo ni kila mtu aandike kitabu. Huyu ni mtafiti asiyeweza kutetea utafiti wake lakini ameweza kuwadanganya baadhi ya watu na sasa wanaimba nyimbo wasizojua tenzi au tungo zake.
Mohamed amefikia hatua ya kutangaza hali ya hatari na kutishia UN au AU kuwepo kwa kile anachokiona ni hatari. Sisi tunajua anajua kile anachookiona kwasababu yeye ndiye anaye engineer. Ndiyo maana kama watanzania tunasimama na kumwambia, NO! HATUPO HIVYO, HATUKUBALIANI NAWE.
Kama kuna tatizo liongelewe kwa uwazi na ukweli bila kuzua uzushi au kuchomeka hisia za mtu binafsi na kuzifanya za kitaifa, kama ule wa mabucha ya nguruwe na umasikini.
Hatusimami hapa kumzuia asiandike hadithi za wapwa zake au familia au watoto na vijana wenzake wa Gerezani enzi hizo.
Tunachokikataa ni kutumia dini akiwa amejificha katika siasa ili kuleta vurugu. Huyu ni mwerevu sana wa kutumia kalamu yake na anaweza kubadilisha hadithi kama ile ya mwembe chai kutuleta balaa. Sio mtu wa kumdharau na kumwacha ni lazima tumkemee na tumfunze wapi maandiko yake yamekosa maadili ya kiroho japo yameandika kwa misingi ya maadili ya kiroho.
Nadhani utakuwa umeelewa vema ni nini tunachosimamia na umeona udhaifu wa Mohamed katika kukanbiliana na hoja.
Hoja ya kila mtu aandike kitabu ni ya kiwango dhaifu sana kiusomi na inatuacha wengine tujiulize kulikoni?
Ingekuwa vema ukamshauri ima ajibu hoja au akubaliane na mapungufu ili sote tuandike historia ya nchi hii bila kutanguliza frustartion, chuki za kidini zisizo na msingi dhidi ya wanadamu wengine.
Uongo na uzushi ukiachwa bila kuhojiwa utageuka kuwa ukweli, haina maana kila neno lake ni uongo, la hasha! Lakini yale ya kuchomeka ni hatari zaidi kuliko yale ya ukweli. Asifinyange historia na kusema ni ya Tanganyika. Kama ni ya mtaa wa Narung'ombe, kipata na manyema hewalaaa!
Kama yupo anayedhani anaonewa aseme, ili tuweke hoja 13 alizokubalina nasi. Kwanini tumeze tu kila kitu bila kutafuna!
Kwahakika kumuacha aendelee kumwaga sumu ni kulisaliti taifa. Wengine tunasema hata kama ni page milioni 1 tutasimama naye bila kumuonea au kumuonea huruma.