Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

 
 
mohamed said;2811655]nguruvi3,kuhusu bakwata, ukafiri sidhani kama yanakuhusu sana wewe.
Mohamed
........
 

MS,

Katika msisitizo wa blue

Mosi, unaandika "fikra" za Nyerere wakati umekiri hukuwahi kumuhoji, hizi ni fikra zake au zako? Unaandika vipi "mawazo" ya mtu na kufikia conclusion kama msomi? Alafu unaita "kisa cha kusisimua".

Pili, huyu mzee (Nyerere) angetamani vipi historia ya mzulu, mamluki wa wakoloni anayeongea na kuandika kijerumani, kuwa na fedha ya kujenga ofisi na kujua kutunza vitabu vya hesabu eti iwe historia ya baba yake? Hii ina uzalendo gani ambao Nyerere angejivunia? Kwa wanaomjua Nyerere hakupenda ufahari wa aina yeyote..ni mtoto wa Chifu lakini aliyesoma kwa shida na hakupata wala hakupenda malezi ya kifahari, hakujivunia utajiri wala hakuwa nao, hakusita kuelezea umasikini wa mama yake na maisha yake ya shida. Wewe unaibuka na "fikra" za nyerere kutamani historia ya Kleist iwe ya Chifu Burito! Alafu unadai wazungu wanakupigia makofi!!
 
 
 

Ulisema siwezi la Mkwawa nilipoleta data zake, Mpaka leo Mko Kimyaa!!
 
NARUDIA KUBANDIKA TENA HILI BANDIKO KWANI SIELEWI NI KWANINI FAIZAFOXY NA MOHAMED SAID HAWATAKI KUNIJIBU SWALI LANGU HILI.

Waislamu wana Nguzo zao tano wanazoziamini kama ndiyo msingi wa dini yao. Kama kweli waislamu wa Tanzania tangu Tanganyika walikuwa wanakandamizwa, ni nguzo ipi kati ya hizi tano ambayo waislam wa Tanzania wanakatazwa kuitimiza na Serikali kwa sababu serikali inadhibitiwa na MfumoKristu?

1. Kushahadia

2. Kuswali swala tano

3. Kufunga

4. Kutoa zaka

5. Kuhiji kwa mwenye uwezo

Kama waislamu wangekuwa wanakandamizwa katika hizo nguzo tano za uislamu ningeelewa hoja za MS. MS na wenzake watuambie ni wapi na ni lini waslamu walikatazwa kwenda kuhiji, kuswali. kufunga kwa Sunnah na Kufunga Ramadhani, kutoa zaka au kushahadia. Sijawahi kuona mfumo wa serikali ukikataza wakristo kusilimu au waislamu kujenga misikiti au kuadhini. Naijua misikiti ambayo iko katikati ya makazi ya watu kwenye mchanganyiko wa wakristo na waislamu na sijawahi kusikia serikali ikikataza waislamu kuadhini kwa sababu 'wanawasumbua" wasio waislamu kwa adhana zao.

Waislamu wanapotaka kwenda Mecca kuhiji hakuna siku walikatazwa kwenda badala yake serikali mara kadhaa imewahi kutoa fedha kusaidia waislamu kwenda kuhiji, sasa hapo waislamu wanakandamizwaje na huo mfumokristu na inakuwaje mfumokristu unashindwa kuzuia waislamu kuhiji, kusilimisha wakristo au kuadhini?

Hivi karibuni serikali si ilishawahi kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kusafirisha mahujaji kwenda Mecca kuhiji? Kanisa lilikuwa wapi kuizuia serikali kutoa fedha hizo??
 

83% vs 17%
 
83% vs 17%

Hii umeoshwa akili na MS bila kukupa takwimu zozote zenye kuthibitisha hili. Hata hesabu ndogo zinawashinda, jiulize Tanzania ina Wakristo, Waislamu, Wasiokuwa na dini, Wanaoabudu mizimu na wengineo. Kama wakristo wamehodhi 83% na Waislamu 13%, Sasa 83+17=100, Hapa makundi haya mengine ya wasiokuwa Waislamu au Wakristo mmeyaacha wapi kwenye percentage zenu za kufikirika? Au MS kakwambia hao ni 0%? Kama hesabu rahisi kama hii unamezeshwa na unakubali utapata wapi guts ya kusimamia unachokisema? Bibi unamjua Kingunge Ngombale Mwiru? Ulizia dini yake kwa mtafiti wako MS.
 
Nguruvi3,

Prof. Haroub mie ndugu yangu.
Usitake kuleta maneno yasiyokuwa na maana yoyote.

Kuhusu BAKWATA, ukafiri sidhani kama yanakuhusu sana wewe.


Mohamed
Hayo ya ukafiri yanamhusu nani sasa?? Mwenzio anakukataza kutoa hukumu wewe nawe unarudi pale pale. Umeambiwa si Mtume wa Mwenyezi Mungu, Swahaba au imamu mwenye haki ya kutoa hukumu juu ya amali za mtu bali ni mwenyezimungu pekee siku ya Kiyama. Mwenzetu ni Uislam gani wewe unaoutetea?? Ndiyo maana FaizaFoxy alikutilia shaka!!
 
Kwenye Red sijui kama watatoka salama na tarakimu zao zilizozaa takwimu feki namna hii. 83+17 =100. Hapo wahindu, Baniani wanawaweka wapi? Umerusha kombora la Nyukilia sijui kama watakuwa na nguvu ya kuja kukiri kama Tarakimu zao zimezaa takwimu feki.
 

Kigarama, njia ya mwongo ni fupi. Hiyo Hesabu ya darasa la tano imeshabikiwa humu na watu wanaodai tusihoji mabandiko ya MS pamoja na yeye mwenyewe na nilimwambia MS katika post moja kwamba historia yake inaleta viroja! Aje atukokotolee hii hisabati tupige makofi.
 
Usipate tabu Mgalanjuka. Mwanakijiji alimaliza yote aliposema haya;
Katika kukariri, Mohamed Said ni bingwa ndiyo maana hajui hata hatari ya hiyo mbegu anayoipanda. Taabu yote hii inasababbishwa na ukweli kuwa tulipata uhuru mwaka 1961 na hakuna mzee hata moja wa Mohamed (hasa hao walowezi wa Kizulu na Manyema) aliyeukwaa hata unaibu waziri katika serikali ya kwanza ya Tanganyika huru kama walivyotegemea. Naamini Mwalimu aliwasoma sana hawa jamaa - oneni sasa vitoto na vijukuu vyao kama Mohamed Said vinavyochangamkia hizo hadithi walizopewa utotoni !


Cabinet ya kwanza ya Tanganyika 1961
Msitari wa nyuma toka kushoto - Job Lusinde, Rashidi Kawawa, Nsilo Swai, Oscar Kambona, Tewa Said Tewa na Derek Bryceson
Msitari wa mbele kutoka kushoto - Paul Bomani, Abdulla Fundikira, Mwalimu Nyerere, Ernest Vasey na Amir Jamal

Asiyekuwapo - C.G. Kahama.


Cabinet ya Kwanza ya Tanzania 1964
Mstari wa mbeletoka kushoto - Tewa Saidi Tewa, H. Makame, Oscar Kambona, Amir Jamal, Abeid Karume, Solomon Eliufoo, Mwalimu Nyerere, Lawi Sijaona, Rashid Kawawa, Bhoke Munanka na Abdul Wakil
Msitari wa nyuma toka kushoto - Kasim Hanga, Dereck Bryceson, Job Lusinde, Abdulrahman Babu, Austin Shaba, Abdul Jumbe, Chediel Mgonja na Said Maswanya.





Katika kuonyesha Udini wake ambao anajitahidi kuuficha kwa kivuli cha historia anawaingiza hata watu ambao hawakuwa Watanganyika eti katika harakati za kupigania uhuru mradi tu walikuwa viongozi wa dini. Mtu kama Sheikh Hassan bin Ameir anaingizwaje katika mashujaa wa Tanganyika kabla ya uhuru ? Amekazania kuisifu TAA kwa kuwataja akina Sykes lakini aliyeiongoza TAA baada ya kuundwa kwake akiwa Raisi wake wa kwanza hatajwi, je ni kwa sababu hakuwa Muislaam ?

Sisi wengine tunampa ukweli kuwa chama chochote kile kiwe TAA, AMNUT, TANC au TANU kinakuwa na Raisi moja tu anayekiongoza. Fahali wawili hawakai zizi moja na ndio maana watu kama Zuberi Mtemvu au Mohamed Chamwenyewe, mambo yalipowashinda ndani ya TANU walitafuta zizi lingine, TANC na AMNUT. Sote tunajua kuwa hata huko yaliwashinda, sasa huo umaarufu wao utoke wapi hadi wawekwe mizani moja na Mwalimu ?

Na sasa natoa ujumbe kwa wote wanaotoa hoja za kijinga kuwa na sisi tuandike historia kupinga hizi porojo. Wengine wetu uandishi si taaluma yetu, engineer uanze kuandika historia ya miaka hamsini iliyopita duh, mbona kuna ya muhimu ya kulisaidia taifa langu. Lakini nina hakika wapo watu wanaupitia huu mnakasha na ikibidi wataandika wenye taaluma hiyo, haya ya kwetu ni tahadhari tu kwa mtu yeyote yule atakayeamua kufanya hivyo, ajiepushe na porojo kama hizi za kichochezi, hazijengi.

 
Asante Mohamed Said kwa kufunguka hata kama ni kwa kukariri. Wengine tumejifunza mengi. Kukosolewa ni sehemu ya kuweka mambo sawa, ila ukweli unabaki pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…