Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Barubaru,
Wengi wa wazee hawa hatunao duniani. Wakati Mohamed anaongea na wazee wake wale wa Kariakoo hawa niliowataja waliokuwepo pia. Hakuhangaika nao. Agenda yake isingekamilika! Pili, sina ukaribu na wazee hawa wachache waliobaki kama alivyokuwa Mohamed na wazee wake ingawa sijui kama anazikumbuka familia za wazee hawa kwenye mapato yanayotokana na kitabu hiki ambacho anadai kinauzika sana.
 

WC,

Pembea ya mzunguko.

Mohamed
 

Barubaru,

Hapo umewatwisha mlima.

Mohamed
 

WC,

Kumbuka kuwa hicho sio kijitabu cha khadithi bali ni utafiti ndio uliozaa kitabu hicho na paper kibao. Hivyo siku zote utafiti unajibiwa na utafiti mwingine na hivyo kuandika kile kilicho sahihi na kuondoa kile kilicho kosewa kwa kutumia hoja katika tafiti yako.

Ndio maana hapo awali uliwataja baadhi ya watu ambao unaona Sheikh Mohamed said hakuwataja katika kitabu chake, nikakushauri wewe uwatafute na kuwahoji ili kuandika kile Mohamed alichosahau na kujazia pale alipochangia.

Sasa wewe anza tu Mohamed said yupo hapo pasi na shaka yoyote atakusaidia kutoa hicho kitabu chako baada ya utafiti na wengine tupo tayari kabisa kulipia gharama zote za uchapishaji wa makala yako.

Kila la kheir acha uwoga watendee khaki wa Tz wenzako.
 
Pamoja na kutokubalika BAKWATA kwa kiwango hiki tangu mwanzo na baada ya Mwalimu kuondoka madarakani miaka zaidi ya 25 iliyopita kwa nini bado ipo na kubwa kiasi hiki miongoni mwa taasisi za KiIslamu nchi hii? Waislamu wote wanaoiongoza BAKWATA na wanaoikubali bado wanahongwa?
 
Kwahiyo mkeo ni 'authority' juu waandishi mahiri Zanzibar na Tanzania nzima!

Mke wangu ana degree ya sheria (LLb) na Masters in Mass Communication. Na amazifanyika kazi taaluma zake zote yaani uandishi na uanasheria.

Kwa kumjua aliwahi kufanya kazi na Ali Nabwa, dept of COI london, na kukutana nae sehemu mbalimbali hivyo alimjua fika umahiri wake.Hivyo si ajabu kwa nguli kumjua nguli mwenzake.
 

WC,

BAKWATA?

Nani kakwambia kuwa BAKWATA ipo?
BAKWATA imekufa siku nyingi sana.

Ofisi zipo na mafaili na wafanyakazi wa BAKWATA Sheikh Mkuu na wa mikoa wote hao wapo.
Kwenye vitabu vya serikali BAKWATA ipo.

Waislam tunao sisi.
Waislam wanatusikiliza sisi.
Na hili hata serikali wanalijua.

Ngoja nikujuvye.
Litoke tangazo.

Waislam leo Mohamed Said atakuwa Starlight au Ukumbi wa Korea.
Hupati pa kutia mguu...

Itangazwe.
Waislam Sheikh Mkuu leo yuko hapo...
Hendi mtu!

Lakini haikuwa kazi nyepesi.
Alhamdulilah.

Waislam tumerejesha heshima yetu na ya dini yetu.

Mohamed
 
Utafiti wa upande mmoja, wa kuangalia watu wa aina moja, wa DINI moja, wanaoswali na kunywa kahawa pamoja, halafu ukaiita ni HISTORIA ya NCHI utanishinda. Nimesema mara nyingi DINI hainihangaishi hata kidogo kwa kuwa Mungu mwenyewe hakuwa na DINI. Tanzania alootuachia Mwalimu haina DINI. Tutapambana ibaki hivo. Siwezi kuandika historia ya aina hii ya Mohamed
 

WC,

Labda nikusaidie kidogo hapo kutokana na uzoefu wangu wakti nikiwa Serikalini hapo Dar .

Kwa mtazamo wa mwenye akili timamu. Bakwata ni chombo kilichoundwa mah'susi kabisa na Serikali ya Muungano upande wa Tanganyika kwa nia na madhumuni ya kuwadhibiti waislam. Hiyo ndio bakwata ukipata bahati ya kushika nyadhifa za Serikalini iwe kimkoa au kiwilaya utalibaini hili kwa nafasi kubwa unayotakiwa kuwapa Bakwata kwa niaba ya waislam.

Je unaweza kuamini Bakwata inashindwa hata pesa za kufanya uchaguzi wake mpaka wachangiwe na Augustono Mrema na Kanisa. Hivi kweli waislam wamekosa fedha? Mbona kuna vikundi vingi sana vya Tab'rih vinazunguka nchi nzima na nje ya nchi?

Kifupi waislam hawaitaki bakwata bali inalelewa na Serikali. Na ndio maana mfumo wa uongozi wake ni wa kiserikali. Utasikia sheikh wa mkoa, sheikh wa wilaya na kesho ukianzishwa mkoa mwingine basi anachaguliwa sheikh wa mkoa na sheikh wa wilaya kama ilivyo kwa ma RC, DC na RPC, RSO,RPO etc
 
Dah! Mohamed unaongopa sana. Ni juzi tu sikukuu yenu imepita. WAISLAMU wote wale niliowaona wakishiriki na vongozi wa BAKWATA na wa nchi hii wote si lolote, si chochote! Mohamed, hata mimi nikisema niko Starlight nitapata watu ukiwemo wewe!
 

WC,

Nyerere hakuacha Tanzania isiyo na dini.
Nyerere kaiacha nchi iko mikononi mwa Kanisa Katoliki barabara.

Kuweka hili wazi na kwa kuandika kitabu ndiko kulikonitia mie katika orodha ya wataalamu wa historia ya Tanganyika.
Hili ndilo linalonifanya nialikwe kote huko kwenye mikutano na makongamano kama mzungumzaji.

Hivi wewe bado hadi sasa hujaelewa?

Athari ya Nyerere ndiko kulikoleta hili vuguvugu la Waislam wa nchi nzima kupiga kelele kuhusu mfumokristo.
Usijifanye mbuni.

Mambo yamebadilika sana ndugu yangu.
Waislam sie si wale wa 1968.

Mohamed
 

WC,

Kama unavyodai Mohamed said ameandika upande mmoja. Basi ni vizuri na wewe ukaandika upande mwingine ili kuleta au kubalance historia yenu. Kwani kwa wale waliomsoma kakala zake katika mwananchi na humu JF watajua upande mmoja wa shilingi pasi na kujua upande mwingine kunani.

Tunasubiri utafiti wako wa upande wa pili ili sote tunufaike na kujua stori ya kweli ya uhuru wenu.
 

WC,

Nyerere hakuacha Tanzania isiyokuwa na dini.
Nyerere kaiacha nchi chini ya mfumokristo na hii ndiyo chanzo cha haya yote yanayotokea hivi sasa nchini kwetu.

Tatizo hili halitoondoka kwa kutaka liondoke.
Tatizo hili litaondoka kwa nchi kukubali kuwa lipo tatizo na hatua kuchukuliwa kuliondoa.

Mohamed
 
Nadhani mnapaswa kushukuru kwamba angalau kuna chombo kama BAKWATA ambacho pamoja upinzani kinaopata bado kipo na kinapambana mfumokristo mnaousema.
 
Ali Hassan Mwinyi aliyeachiwa Urais alikuwa Cardinal au Archbishop wa Jimbo gani la Catholic Tanzania? Mtafiti kama wewe unapoongopa namna hii inakuwa haipendezi hata kidogo.
 

WC,

Pembea ya mzunguko.

Mohamed

Sheikh hawa kina Nguruvi3, Wild Card, Mag3, Mwanakijiji et.al. watakupasuwa kichwa hawa..ujumbe umeshafika na kwa ufahamu wangu darsa lazima itakuwa haadhir kwao. Hivi wanavyoandika ni kule kujitutumua tu na kuwakilisha pote lao barabbara. Na usidhani kama hawa ni watu tofauti..wanaingia kwa IDs tofauti tu.....hii habari ya multiple IDs Mwanakijiji anaijua zaidi.

Naona tumuite mwalimu na chetezo tutie fatha..na tumuombe Moderator atufungie thread yetu. Kweut sie ilikuwa ni kitivo khasa hiki na kitovu cha elimu kubwa mno. Allah akulipe kheri kwa jinsi ulivyojitoa muhanga bila kuogopa yoyote ila ukitaka hifadhi ya Allah. Mungu anasema ... '' Mkininusuru (kwa maana ya kutetea dini na muongozo wangu) na mi nitawanusuru''. Sifa yake kubwa Mungu wetu huyu nikutokhaalif ahdi zake. Naamini hili unalijua fika na ndo maana umejitoa muhanga kufanya nusra hii.

Barubaru, Mdondoaji, Ritz na ukhti Faiza mchango wenu ulikuwa na umuhimu mno katika kufikisha ujumbe huu nanyi pia nawaombea kwa Allah awalipe kheri.

Imma Nguruvi3, Mag3, Mwanakijiji, Wild Card na wengi wa mrengo unaofanana nao..nawausia kheri, upendo,kuvumiliana, kustahmiliana. Hii ndio sifa na tofauti ya Bin adam na wanyama. Namuomba Allah awaongoze katika Nuru, Aamiin.

Wakatabahuu

Kikwebo.
 
Dah! Mohamed unaongopa sana. Ni juzi tu sikukuu yenu imepita. WAISLAMU wote wale niliowaona wakishiriki na vongozi wa BAKWATA na wa nchi hii wote si lolote, si chochote! Mohamed, hata mimi nikisema niko Starlight nitapata watu ukiwemo wewe!

WC,
Umesema kweli kabisa umewaona BAKWATA katika sherehe.

Hiyo ndiyo idara yao tuliowaachia.
Futari, kunywa chai na sambusa za Ikulu na kupiga picha na viongozi wa nchi.

Masula muhimu ya maendeleo ya Waislam wanafanya viongozi wa Waislam

Chunguza.

Kuna masheikh hata siku moja hutowaona katika mambo kama hayo na ni viongozi wenye umma mkubwa nyuma yao.
Hawa wakizungumza Waislam tunasikiliza.

Jiulize Makongamano ya Mfumokristo yamefanyika nchi nzima viwanja vinafurika.
Umewasikia BAKWATA?

Mohamed
 
Mbona CHADEMA ya "WAKRISTO" inapata taabu ndani ya mfumo huu kuliko CUF ya "WAISLAMU"?
 

Kikwebo,

Ah! Sheikh wangu ulikuwapo lakini huonekani.
Amin Amin Amin.

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…