Sasa kama unajua kuwa mtafiti hawezi kufanya utafiti wa kila kitu kwenye jambo analolitafiti, sasa kwa nini mnapiga kelele kwa wazee wa Gerezani kusahauliwa, wakati na nyie watoto wa Gerezani mmewasahau wazee wa Nyamagana waliopigania Uhuru ambao nao Historia "Rasmi' iliwasahau?
Kuna mtafiti akajua kila kitu. Hebu nitajieni utafiti uliofanyika ukataja kila kitu. Mie ningelikuwa supervisor wako katika utafiti ukiniletea research ukasema umegusa kila mahali nakupa 0 kwasababu ni uongo na hujafanya kazi. Professor Albert Einstein mwenyewe ambaye wazungu wanasema ndio mtu mwenyewe akili nyingi duniani alipofanya utafiti wake wa theory of relativity alishindwa kuelezea uhusiano wa sub atomic particles and speed of light. Mwezi uliopita wanasayansi kama 10 kutoka ujerumani, us, uk na norway wameweza kugundua kuwa sub atomic particles travell faster than the speed of light. Hivyo kuleta challenge kwa theories za Einstein na mfumo mzima wa maisha yetu.
Hakuna ukamilifu katika binaadamu mkamilifu mmungu peke yake. Ila kuna kujitahidi na Mohamed Said amejitahidi kuleta aliyogundua na kuweka evidence zake na nyie andikeni ya kwenu na wazee wenu tuyasome.