Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Pole FaizaFoxy - Kwanza, Mag ni kifupi cha jina langu halisi. Pili, mimi ni mtoto watatu kwenye familia yetu. Tatu, nimesema sijibizani na Mohamed Said, inawezekana ikawa taabu kuona hiyo tofauti. Hebu kwanza soma EAMWS ilianzishwa na nani na kwa misingi ipi, matatizo gani alikumbana nayo Agakhan baada ya kuianzisha, aina gani ya ushirikiano alipewa na Waislaam Watanganyika na kwa nini mnadai shule za Agakhan zilizotaifishwa kuwa zenu huku mnamkana kwa biashara zake kwamba hazifuati misingi ya Kiiislamu. Mpaka hapo Mwalimu Nyerere anaingiaje katika ugomvi huo ambao haihitaji shahada kujua uliwahusisha akina nani. Kama mpaka hapo hujaona uwongo wa Mohamed Said nasema siwezi kukusaidia kwa sababu wewe ni mojawapo wanaoangalia kila kitu katika misingi ya Kidini. Pole sana FaizaFoxy, ni mimi Mag3.
Najua kuna roho za watu zinauma kweli kweli kwamba wazee wa Gerezani ilibidi wampigie magoti wakuja, mvaa kaptula, mkatoliki awaongoze katika harakati za kudai uhuru na akaendelea kuwaongoza hata baada ya uhuru. FaizaFoxy, hiyo historia hata ungetumia mabomu ya nuclear huwezi kuifuta, just bear it and like it !
 

Kuhusu jina langu ukizipitia posts za hizi nyuzi mbili vizuri huko nyuma kuna mtu kauliza na nimeelezea vizuri nikatoa mpaka anuani ya kwetu, sina cha kuficha. Faiza ni jina langu halisi nililopewa na wazazi wangu na Foxy ni umaarufu wangu niliopachikwa nyumbani kwetu, kwa kuwa nilipotoka tuko Faiza wengi nikapachikwa hilo la Foxy ili iwe rahisi kututofautisha anapoongelewa Faiza kwani kina Faiza mdogo tulishakuwa zaidi ya watatu. Foxy kutokana na mcheza sinema wa enzi hizo Foxy Brown (Pam Grier) au Black Mama na nilifanana nae ujanani si utani.

Hata kama anajibu kuhusu kitabu cha Mohamed Said kilichoandika kuhusu hiyo EAMWS , si atueleze hapa ndivyo alivyoandika Mohamed Said na ndio uongo wenyewe huu na hapa ndipo usahihi wenyewe. Jee wewe umeliona hilo? na unaweza ukaliweka sawa kwa faida ya wengi? maana mwenzako kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika walioianzisha yeye kamtaja Nyerere tu kama vile ni mali ya Nyerere na si chama halafu karukia ANC kamtaja Mtemvu tu halafu karukia AMNUT halafu karukia EAMWS na kaanza kwa shutuma za uongo halafu hajatuonesha huo uongo uko wapi na ukweli uko wapi. Jee, unaweza kumsaidia?
 

Mag3 ndio jina lako? Unanchekesha, jibu na mengine, mbona umerukia hilo tu?

Kama hujibizani na Mohamed Said utafikia kumtukana kuwa ni "mpuuzi" na kumuita "muongo"? Unasema hujibishani na MS wakati hata kichwa cha habari cha hii mada kina kusuta? unanchekesha!

Halafu hilo la uongo unalolirudia rudia ndio hilo linakurudia wewe mwenyewe mara hili mara lile. Tuoneshe uongo uko wapi na ukweli wako uko wapi? tuoneshe ni Mzee yupi wa gerezani aliyempigia magoti Nyerere?

Niliposema Nyerere kaja na kaptura na picha nimebandika kuweka ushahidi. Mbona wewe hutuoneshi ushahidi wa shutuma zako na badala yake nakuona unatokwa na povu?

Wazee wa gerezani ukipenda usipende hawafutiki kwenye historia ambayo mlidhani kuwa watafutika au mlikuwa hamuijui kabisa lakini katokea kijana wao wa hapo hapo anaewajua fika, anawaelezea na kuitanabahisha dunia na kila mtu hustuka kama mstuko uliokupata wewe. Na hao wazee ndio waliompokea Nyerere na ndio walioanzisha harakati za Uhuru na Nyerere ndio akaja kuwasaliti, hilo halipingiki wala huna uwezo huo, kwa kuwa huna ukijuwacho zaidi ya kutafuta kwenye mtandao kukopy na kupaste.. Kaa hapa uwajuwe hao wazee wa gerezani ni kina nani na wameifanyia nini hii nchi.

Wacha hasira huwezi kuifuta historia, utaipindisha tu, lakini kichwani mwako utabaki unaujuwa ukweli ni upi.
 
Ni wapi Mag3 kasema Nyerere alianzisha TANU peke yake? Bibie, Mandela hakuanzisha ANC. Kilianzishwa kabla hata ya kuzaliwa kwake. Lakini leo ukizungumzia na kutukuza mchango wa Mandela katika ANC si kwamba huwatendei haki wale waliokianzisha chama. Kwa bahati nzuri, wakati TANU inaanzishwa 1954 Nyerere alikuwepo na ni Nyerere huyu huyu aliyesaidia kuisambaza TANU Moshi, Mbeya, Iringa, Arusha, Shinyanga, Tabora na wala sio akina Sykes na wazee wenu wa Gerezani. Mpeni Nyerere heshima yake hata kama wakazi wa Gerezani walichangia kwa hali na mali uanzilishwaji wa harakati za ukombozi, ni Nyerere ndiye aliyesaidia kuzisambaza harakati hizo Tanganyika nzima. Na kama ingekuwa movie, basi Nyerere ndiye sterring na wale wengine wote wanaitwa extras.
 

Soma vizuri post yangu usipindishe maneno.
 
NONDO anazomwaga MS,sio mchezo,tunaweza ku connect dots nyingi tu-tatizo linakuja pale anapotaka kuikamata"audience" kwa ku sacrifice baadhi ya dini na mashujaa ambacho ni kitu hatari sana kwa umoja wa nchi

Yawezekana kwako nondo anazomwaga Mohamed zikawa si mchezo kama unavyodai lakini aache kudanganya Watanzania kuwa anaandika historia ya harakati za uhuru za Tanganyika. Hatungekuwa na ugomvi naye kama angekiri kuwa historia anayoiandika ni ya wazee wake wa Dar es Salaam na hasa eneo la Gerezani na katu si ya Tanganyika kama anavyodai.

Kati ya hao wazee wote anaowataja pamoja na kukoleza chumvi nyingi hakuna hata moja aliyeongoza chama cha siasa kilichopigania uhuru na kama walishiririki katika harakati za kudai haki za msingi na kupinga uonevu basi wako wengi tena waliotoa changamoto kubwa kuliko za kwao lakini hawatajwi inapofika kudai uhuhru kupitia chama cha siasa.

Chama cha TAA hakikua peke yake katika harakati hizi na tumejaribu kuorodhesha watu, vyama na vikundi mbalimbali vilivyowapa wakoloni changamoto nyingi tu kupitia kilichoitwa petitions kwa serikali ya kikoloni. Anapotaja wazee wake tena wa Dar es Salaam na kudai anaandika historia baada ya kufanya utafiti nchini Tanganyika anasema uwongo.

Mathalani mwulizeni kama anaijua iliyoitwa Meru Citizen Union na wapiganaji wake kama Munya Lengoroi, Gamaliel Sablak na kama amewahi kuwasikia kwa nini hawatajwi. Jibu jepesi linalopatikana ni kuwa hawa kwanza si wazee wake, pili hawakuzaliwa wala kuishi Gerezani na tatu si Waislaam. Udini ndio unamsukuma zaidi Mohamed Said katika maandishi yake karibu yote.
 

Mag3
Please usituletee data za kutengenezwa, TUMEZICHOKA; KWA SABABU ZIMETENGENEZWA. Tunataka credible sources please!!
 

Well said!!
Kila wakati namwambia Mag3 aache kutuwekea hizo HOLLYWOOD STORY zilizotengenezwa na Pro-Nyerere.
 
Nilidhani tunaandikia wino. Haya maneno ya nani, Bibie?
maana mwenzako kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika walioianzisha yeye kamtaja Nyerere tu kama vile ni mali ya Nyerere na si chama halafu karukia ANC kamtaj
 
Nyerere katika Utangulizi wa Kitabu chake cha Uhuru na Umoja* (naweza kusema historia fupi ya harakati za uhuru kwa maneno yake Nyerere mwenyewe) anasema hivi kuhusu historia ya harakati za uhuru Tanganyika:

The Tanganyika African National Union was born in July 1954, and modern political development in Tanganyika really begins from that date. But it would be absurd to imagine that this organization, which gathered strength so quickly and so quickly achieved its preliminary goal of independence sprang out of thin air. Nor its triumph attributable to any special abilities or virtues of the people this part of Africa.

Katika sehemu hiyo ya utangulizi Nyerere anaeleza vitu vikubwa vitatu ambavyo si vigumu kuviona, kwanza ni kwamba TANU kama chama cha siasa kuundwa kwake mwaka 1954 kulileta harakati za ukombozi na uhuru katika kiwango tofauti kabisa na kubadilisha kabisa historia ya Tanganyika. La pili ni kwamba, mafanikio ya TANU hayakuja hivi hivi tu yalikuwa na asili yake na tatu siyo ujuzi fulani wa watu wa Tanganyika au uwezo wao fulani ndio ulifanya mafanikio ya TANU yawe ya haraka hivyo.

Anaelezea mambo mbalimbali ambayo yaliifanya TANU kufanikiwa kwa haraka namna hiyo. Nyerere anaelezea vitu vifuatavyo ambavyo baadaye alitumia muda kuvifafanua kwa kina:


  1. Historical circumstances favored Tanganyika (it was a TrusteeshipTerritory under British Administration)
  2. The groundwork of political organization existed in the form of a multitude of very small welfare and tribal organizations (hapa anajumlisha cooperatives na TAA na vyama vya kikabila)
  3. Lack of general economic or social development in the country had at least the incidental advantage that there existed no real strong local vested interests supporting the maintenance of colonialism or privilege.
  4. Swahili was understood by the majority of the people – especially men
  5. No one tribal group dominated all others in size, wealth and education


Nyerere anafafanua kwa kina jinsi gani mambo hayo yalisaidia sana kujenga mwamko wa kitaifa ambao uliwahakikishia wananchi wote kuwa njia ya amani iliyopendekezwa na TANU kutafuta "uhuru" ilikuwa ni bora. Anasema hii ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo kwani kumbukumbu ya kuzimwa kwa juhudi za kukataa watawala zilikuwa bado kwenye fikra za wazee wengi (walioona mwamko wa Maji Maji kwa mfano). Anasema hivi:

This does not mean that the people of this country were cowardly or particularly fond of non-violence; no, they knew fighting; they had been badly defeated and ruthlessly suppressed. As realists, therefore, they wanted to know why TANU thought we could win even without guns.

Mwalimu anaelezea katika utangulizi huo kuwa nchi ilikuwa na matatizo na anakiri wazi kabisa kuwa nchi ilikuwa imegawanyika kidini. Na kinyume na madai ya Mohammed Said Nyerere alikubali kabisa nafasi ya pekee ya wazee wa Kiislamu wa Pwani ambao walitoa mchango mkubwa wa kuifanya TANU ikubalike maeneo mengi nchini. Anasema hivi:

This thumbnail sketch must not be taken to imply that there were no problems for TANU. The country is divided in religion (angalia neno "is") and it would have been very easy for TANU to have fallen into a religious hostility.

Hili ni muhimu kidogo hasa tukisoma masimulizi Mzee Said kwamba katika mgogoro kati ya wale waliotaka kuona TANU inafanya upendeleo wa pekee kwa Waislamu (kina Shehe Takadir) na wale ambao hawakutaka TANU iingie kwenye suala la udini (Mashehe wa Tanga) linaonekana wazi. Nyerere anaendelea hapo hapo:

That it did not do so is a tribute to religious leaders in this country, but in particular to the adherents of the Moslem faith in the coastal belt – where TANU started.

Hii inavunja vunja mara moja na daima madai kuwa Nyerere alitaka kujulikana ni yeye pekee aliyeanzisha TANU na kuwa hakutambua mchango wa wazee wa Kiislamu katika harakati za Uhuru. Ikumbukwe kuwa kitabu cha Uhuru na Umoja kimepigwa chapa mara ya kwanza mwaka 1966 – baada ya Uhuru, baada ya matukio ya jeshi kuasi na watu kuwekwa kizuizini. Kama Nyerere angekuwa na chuki na Waislamu au Uislamu baada ya uhuru kama Mohammed Said anataka watu waamini maneno haya yasingetoka kinywani mwake. Ni maneno ambayo yanatoa heshima kwa viongozi wa kidini lakini "in particular" anasema ni Waislamu wa Pwani! Lakini anakiri kabisa kuwa TANU ilianzia Pwani. Kama Nyerere hakuwa na tatizo kuwapa heshima Waislamu mwaka 1966 haiwezekani basi kuwa alikuwa na chuki na Waislamu kwani angeweza kabisa kutotaja hilo. Alikuwa ni mkweli wa historia na akaitaja kama ilivyo.

Nyerere anaelezea kwa kirefu kidogo juu ya moral principle ya usawa wa watu wote ambayo anasema ndiyo iliongoza harakati za uhuru. Anaelezea ni jinsi gani kulianza kuibuka makundi ambayo hayakutaka kuona kuwa watu ambao hawakuwa na ngozi nyeusi hawakuwa ni Watanganyika kweli na walitaka wabaguliwe. Anaelezea hili kidogo ndani yake ikifichika falsafa kubwa sana ya utu sawa kwa wote.

Until the end of the 1950s it could be said that TANU was campaigning for equality from motives of expedient self interests. As that decade drew to a close, however, the test came. Were those who claimed equality for themselves willing to accept the other side of the coin – the equality of others?

Hili ni swali jepesi lakini si dogo; lilikuwa na maana nyingi sana kwa wale waliopigania uhuru. Je, wote walipigania uhuru ili wote wawe sawa au baadhi wawe sawa zaidi. Tukumbuke pia wakati anaandika hili Jeshi lilikuwa limeshahasi karibu miaka miwili nyumba ambapo mojawapo ya madai ilikuwa ni kuondolewa kwa viongozi wasio wa Afrika weusi. Nyerere analijibu kiufundi swali hili na kwa hekima ya mzazi ambaye hataki kutaja watu kwa majina lakini wasomaji wake wakiwa na uelewa walitarajiwa kuelewa.

Inevitably there were some few members of TANU whom discrimination had made bitter, and whose basic lack of self-confidence caused them to fail in this test. And inevitably there were also those whose membership and participation in the independence struggle had been motivated by greed and jealousy. Such people still exist in Tanzania, as elsewhere in the world.

Kwa maneno mengine Nyerere anasema siyo wote waliokuwa wako kwenye harakati za uhuru walikuwa wanataka uhuru ili wote wafanikiwe au wakiongozwa na kanuni ile ya msingi na walipoona kuwa hawakufanikiwa wakatoka kwenye kanuni ile na kuwa nje. Hawa anasema walikuwa wanagombania uhuru ili wapate nafasi fulani au walipokosa nafasi walizofikiria wangezipata wakaanza kuwa ni tatizo.

Ushahidi wa kauli yake ulikuwa kwamba uchaguzi wa 1965 ulionesha Watanzania walielewa kuwa ni taifa gani walilolitaka. Anaelezea mtazamo wa matokeo ya uchaguzi ule ambapo baadhi ya wale waliokuwa washirika wa wakati wa uhuru walidondoka vibaya na majina mapya yakaangizwa katika historia (Bibi Titi Mohammed na Paul Bomani walianguka kwenye uchaguzi huu – kama kumbukumbu yangu haijanipoteza).

Nyerere akaelezea hivi matokeo ya uchaguzi ule:

Our people have shown that they accept the objective – the creation of a nation out of more than 120 tribes, out of peoples of different religions and different social groups, and a nation in which race is of less importance than a record of service and an expected ability to give service

Ikumbukwe katika uchaguzi huo Jamal alishinda huko Morogoro na wengine ambao hawakuwa weusi nao kushinda katika jamii ambayo watu weusi ni wengi – kitu ambacho kihistoria Tanzania hakijawa kigeni sana tangu wakati ule.

Lakini Nyerere alielewa vizuri sana maana ya kudai "usawa". Anaelezea kuwa wananchi wa Tanzania walitarajia kuwa serikali yao isimamie ile kanuni ambayo iliwaongoza kupigania uhuru. Anasema hivi:

TANU's emphasis on the morality of its case, and its stress on peaceful methods, has created among the people certain expectations about the actions of their independent nation and its leadership. TANU called for equality; our people now expect it. We called for human respect; our people now demand that their leaders accord it to everyone regardless of his economic or social degree. We called for equal opportunity; our people are now critical that this does not exist.

Na ndio akaelezea kuwa matarajio hayo ya wananchi ndio yalikuwa sababu ya baadhi ya changamoto nyingi na pia nafasi mpya za kujenga taifa tulitakalo. Na kutoka hapo Nyerere anaingia ndani katika falsafa nzito sana ambayo hadi wakati ule ilikuwa haijafanywa na Mwafrika. Ni kile alichokiita "A New Synthesis of Man and Society" ambayo nina uhakika matukio yanayoendelea nchini sasa hivi na hata yale yaliyotokea Libya yakiangaliwa kwa mwanga wake yanakuwa wazi sana. Nashauri watu wakitafute hicho kitabu na kusoma hiyo sehemu.

Nitaendelea na suala la "Je Nyerere alijua Waislamu walikuwa wamedhulumiwa na kuwa nyuma na kukiri hali hiyo ya tofauti katika nchi huru?" Bw. Mohammed Said anataka tuamini kuwa Nyerere hakulijua tatizo la inequality kati ya Waislamu na Wakristu. Napendekeza kuwa alijua na labda kwa kina cha kifilosofia kuliko wengi wa zama zake na maneno yake yanabakia ni ya kina hata yakisomwa leo hii.

* Maneno yaliyotiwa msisitizo ni kauli za Nyerere mwenyewe.
 
Mag3
Please usituletee data za kutengenezwa, TUMEZICHOKA; KWA SABABU ZIMETENGENEZWA. Tunataka credible sources please!!
Hivi hizi data zimetengenezwa na nani? Masimulizi ya Mohammed ya kusimuliwa na wazee wake ndizo data sahihi peke yake? Si kweli kwamba Mtemvu alijitenga na TANU kwa sababu alitaka Tanganyika iwe for Africans peke yake? Duuh!
 

FaizaFoxy, ungekuwa umepitia hii thread kutoka mwanzo hungekurupuka hivi kuhusu porojo za Mohamed Said kuhusu EAMWS,

FaizaFoxy, mwulize tu huyo Mohamed Said kwamba anapotaja shule za Agakhan, ni wanafunzi wa aina gani walikuwa wakisomea hizo shule. Je wakati huo tofauti kati ya Waislaam hao anaowataja na jumuia ya Ismailia zilikuwa zimekwisha ? Hizi ni porojo ambazo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuziamini.
 
Mag3,

Uwongo wa Mohamed Said kwa darubini upo wazi.

1. Amesema namba za mitihani zilipoanza ufaulu ukaongezeka. Tukamuuliza zilianza lini, akasema hajui. Muongo!

2. Kasema Nyerere alivunja baraza la wazee wa TANU kwa kutumia kamati kuu ya chama. Tukamuuliza kamati kuu ilikuwa na akina nani?
Amejibu kuwa anaenda kufanya utafiti. Sasa alimtuhumu vipi Nyerere kama hana utafiti. Muongo !

3. Kasema uhuru umeletwa na waislam peke yao. Tukamuuliza akina Vedasto na Mtamilwa je. hana jibu. Muongo

4. Tukamwambia uhuru ni zao la watu wote katika uwiano tofauti , akasema Tanzania hakuna wapagan wala atheist! Uongo mkubwa sana

5.Kasema, Nyerere alifunga masheikh, tukamletea idadi ya watu wengine waliofungwa nae wakiwemo akina Kasanga Tumbo. Hana jibu. Muongo

6. Akasema Nyerere hataki majina ya mitaa ya wazee wake, tukamwambia aliwahi kuweka kibao kikang'olewa? hana jibu. Muongo

7. Kasema MoU ni pesa za kujenga makanisa, tukamuuliza wapi ipo documented hivyo anavyosema, hana jibu.nuongo

8. Amesema kwa kushirikiana na Ghaissany kuwa wamakonde walipelekwa Zbar kwenye mapinduzi. Tukamuuliza je Wzbar kama akina Mwinyi na Jumbe wanasemaje. Hajawahi kuwahoji. Muongo

9. Kasema Sykes ndiye aliyepigania uhuru wa Tanganyika. Tukamuuuliza aliwahi kwenda Mbeya, Musoma Mtwara kwa shughuli za kisiasa? hajibu. Muongo

10......................................1,000.

Mohamed ni mjuzi sana, anatumia uelewa wake wa lugha kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na biashara. Anajua kuwa ukitaka kufanikiwa ni gawa watu halafu kutumbukiza chuki. Anajua kuwa ni lazima kuwe na star kama ilivyo kwenye movie, so that the show goes on.
Akamteua Nyerere as star halafu kamfanya public enemy number 1. Kanasibisha imani (sio kabila) ili kujenga kambi zinazokinzana.

Anatumia siasa ku promote udini wakati huo huo anatumia dini ku protect hoja zake za kisiasa.

Kama si muongo, kwanini hajibu maswali au hoja ! hatuna interest ya kujua alikunywa chai na profesa gani ulaya, we are in better position to define and narrate about our country.
 
Mag3,

..............Anatumia siasa ku promote udini wakati huo huo anatumia dini ku protect hoja zake za kisiasa...................

Nilikuwa natafuta ni jinsi gani ya kum-describe MS..........kwa maoni yangu hiyo ni description nzuri sana ya Brother MS
 
Nilikuwa natafuta ni jinsi gani ya kum-describe MS..........kwa maoni yangu hiyo ni description nzuri sana ya Brother MS

Ogah,

Mkuu (na mimi najifunza lugha za kileo nadhani "Mkuu" ni kama kusema "Bwana") tulipoteana.
Waswahili tuna msemo, "Mdomo haumkatai bwana wake."

Insha Allah niko tayari kupokea kila aina ya jina na sifa ila mradi siktukanwi.

Mohamed
 

Nguruvi3,

Ahsante kwa mchango wako ila mimi sijasema hilo la MoU na la Abdulwahid.
Hilo la chuki nishalijibu mara nyingi.

Nakushauri tafuta kitabu chochote cha "research methodology" kitakusaidia katika
elimu ya "deduction" nimeona hapa umejitahidi kuitumia lakini bado kidogo inahitaji
kupigwa msasa.

Mwisho nakushauri huko usoni usitumie neno "muongo" sema "hasemi kweli" kauli
zako zitaonekana za kiungwana.

Huenda hufahamu lakini ukimwita mtu "muongo" unamfedhehesha ni neno zito.

Mohamed
 

Mag3,

Yale yamekwisha niulize tu ndugu yangu hapana haja ya kupitia kwa FF.

Hizo shule si shule za Aga Khan zilikuwa zikijengwa na Aga Khan kwa ajili
ya EAMWS kuwainua vijana wa Kiislam.

Mohamed
 
Hivi hizi data zimetengenezwa na nani? Masimulizi ya Mohammed ya kusimuliwa na wazee wake ndizo data sahihi peke yake? Si kweli kwamba Mtemvu alijitenga na TANU kwa sababu alitaka Tanganyika iwe for Africans peke yake? Duuh!

Jasusi,

Habari nilizoelezwa na wazee wangu naziamini kuliko vitabu elfu vya wanahistoria ambao hawakuwapo wakati wazee wangu wanapambana na ukoloni wa Waingereza.

Msome Mtemvu hapa chini:

Ilikuwamiaka ya 1980 tuko nyumbani kwa marehemu Bi. Mluguru bint Mussa, mama yake AllySykes Mtaa wa Lindi. Pametokea msiba. Bi. Mariamu, shangazi yake Bwana AllySykes amefariki. Watu wamejazana mtaa umefungwa wanasubiri muda wa mazishi.Bwana Ally mwenyewe kakaa jamvini kazungukwa na jamaa zake wa Gerezani, wamekukujakuungananae katika msiba wa shangazi yake. Watu ni wengi sana. Bwana Ally yeyemwenyewe ni mzishi sasa leo limemfika ndugu zake wa wamemwitika kwa wingi sana, wamekuja kumzika.Bwana Ally kuniona ananita nende nikakae nae mbele. Basi nanyanyuka pale nyumanilipokuwa kwa unyonge maana umma mzima unaniangalia huyu anaeitwa mbele pale anaumuhimu gani. Katika lile jamvi alokuwa Bwana Ally ni "nani aliye nani katikamji wa Dar es Salaam," Waingereza wanasema "Who is Who" wenyewe watoto waGerezani na Dar es Salaam wametanda. Sasa Bwana Ally anawanadia watu, "Nyie mnamjuahuyu? Mtoto wa Said pale Kipata mwandishi hodari sana…" Utambulishoumekwisha nakaa pembeni Ally Sykes na Zuberi Mtemvu wanashambuliana kwa maneno.Bwana Ally kalalamika kuhusu hali ya nchi mambo hayendi vyema. Zuberi Mtemvukadakia anawashahidisha watu, "Jamani mnasikia Ally analalamika ati mambohayendi sawa…" Mtemvu anaangua kicheko cha kejeli huku akitingisha kichwa. Watusasa weshakuwa hadhir wanasubiri Mtemvu atasema kitu gani? "Huyu Ally namarehemu kaka yake (Mungu amrehemu) walikuwa wanashirikiana na Nyerere kukipigavita chama changu kife, leo Ally huyu huyu keshageuka ati nchiimeharibika…"Wasikizaji wanacheka wengine wanamuunga mkono Bwana Ally wengineZuberi Mtemvu. Bwana Ally hakubali kushindwa anarudisha kombora, "Ala kumbeCongress bado mko hadi leo nilidhania tulishakumalizeni." Vicheko. Mzee mmojakwa mbali anaita, "Ally sikiza bwana, Congress tupo sana. Congress ni mwambausiovunjika." Vicheko vinaendelea. Kwangumimi pale nilikuwa nasoma na kupata mazingatio. Nilikuwa nikiifahamu vemahistoria ya Zuberi Mtemvu na mwalimu wangu alikuwa Ally Sykes. Nilikuwanimemsoma Mtemvu katika nyaraka za Sykes. Mtemvu ni mmoja wa wanachama wamwanzo shupavu na msomi kabisa kujiunga na TANU. Katika nyaraka za Sykes kuna"note" ya mwaka 1954 aliyoandika Zuberi Mtemvu kwa penseli kumpelekea AllySykes akimtaarifu kuwa kakutana na Ally Mwinyi Tambwe na amemweleza kuhusuchama kipya cha siasa kinachotaka kuanzishwa. Katika "note" ile Mtemvuanamfahamisha Ally Sykes kuwa Ally Mwinyi Tambwe kakubali kukiunga mkono chamahicho kipya. Mtemvu alimjulisha Ally Sykes kuwa Tambwe kukubali kujiunga naTANU lilikuwa jambo zuri sana. Tambwe,Mngazija wakati huo alikuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.Tambwe alimwahidi Mtemvu kuwaingiza TANU wanachama wengine wanaounga mkono harakatizile. Mtemvualimfahamu Nyerere siku zile za mwanzoalipokuwa akija Mtaa wa Kipata kwa Ally Sykes. Baba yake Mtemvu, Mzee MwinsheheManga Mtemvu, alikuwa amejenga nyumba yake nyuma ya nyumba ya Kleist Sykes babayake Ally. Mtemvu alikuwa na kipaji cha kuzungumza kama alichokuwanacho Nyerere,Bibi Titi na Sheikh Suleiman Takadir. Mtemvu alikuwa na kipaji cha kuwezakushawishi na kuwashirikisha watu katika harakati. Takriban mwezi mmoja baadaya kuundwa kwa TANU Nyerere na Mtemvu walikwenda kuifanyia kampeni TANU hukoMorogoro ambako ndiko ilipokuwa asili ya ukoo wa Mtemvu. Baba yake Mtemvu, MzeeMwinshehe, alikuwa ameongea na baadhi ya wezee wenzake kuhusu TANU. IjapokuwaNyerere alijaribu kwa uwezo wake wote kuwafikishia watu ujumbe wa TANU matokeohayakuwa mazuri. Katika barua ambayo Mtemvu alimwandikia Ally Sykes mnamoAgosti, 1954 aliwaelezea watu wa kabila lake kama "wagumu." Mtemvu alimuelezeaAlly kwa ufupi juu ya mkutano wao na Nyerere Morogoro mjini na aliomba apewemara moja kadi 200 za TANU. Allyaliwaandikia na kuwapa kadi za uanachama wa TANU, Mtemvu na Tambwe naakamwambia mdogo wake Abbas, awaalike wote wawili kwenye mkutano wa uzinduzi watawi la TANU la Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Arnatouglo ambao ulikuwaufanyike Jumamosi inayofuata. Nilipokuwanawatazama pale mazikoni Ally Sykes na Zuberi Mtemvu walivyokuwa wakitaniananilizidi kupata uhakika kuwa kwa hakika wazalendo hawa walikuwa wakijuana vyemana historia yao ni ndefu na inatoka mbali. Siwatu wengi sana wenye kujua kuwa ni Nyerere ndiye alimshauri Mtemvu aache kaziserikalini ajiriwe na TANU. Mtemvu alikubali ushauri ule na akaacha kazi. Kwa ajilihii basi Mtemvu akaja kuwa katibu wa kwanza wa TANU na Waingereza wakimchukulia Mtemvu kama mtu mwenye siasa za upande wa kushoto sana katika TANU. Hivi ndivyo ilivyokuwa Zuberi Mwinshehe MangaMtemvu akaja kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika TANU. Katika siku za mwanzo nafasi ya katibumwenezi ilikuwa ikishikwa na viongozi mbali mbali baina ya Mtemvu Denis Phombeah,Oscar Kambona, Iddi Faizi Mafongo na Stephen Mhando. Mtemvu akiwa katibumwenezi alikuwa na kazi ngumu ya kuwashawishi na kuushirikisha umma katikaharakati za kudai uhuru na kusajili matawi ya TANU. Ili kampeni ya kuwaingizawanachama katika TANU ifanikiwe na ujumbe wake uwafikie wananchi ilibidi TANUifanye mikutano ya hadhara. Kwa bahati mbaya serikali ikawa haitaki kutoakibali kwa TANU ifanye mikutano. TANU ilijikuta katika hali ambayo haiwezikuwasiliana na umma kuutayarisha katika harakati za kudai nchi yao. Katikahatua kadhaa za ujasiri Mtemvu alifanya mikutano ya hadhara bila ya kupatakibali cha serikali. Nyerere mtu wa hadhari hakutaka kuonekana anavunja sheria.Alifahamu kwamba vitendo kama hivyo vingesababisha matatizo kutoka serikalini. Jambokama hilo lilikuwa sawa na kuikaribisha misukosuko bila sababu ambayoingeathiri TANU na uongozi wake wote. Nyerere, kama rais wa TANU, alikuwaamepokea barua kadhaa kutoka kwa Chief Secretary, T. Griffith-Jones, kuhusumikutano isiyokuwa na kibali aliyokuwa akiifanya Mtemvu. Lakini kwa hakika kwaTANU kunyimwa haki ya kuitisha mikutano ilikuwa sawasawa na kuifunga mikono.Hakukuwa na namna nyingine TANU ingeweza kufanya ili iwasiliane na watu. Kuachakufanya mikutano TANU ingebakia dhaifu na harakati zingekufa. Mtemvu alikuwaakifahamu kuwa serikali ilikuwa imedhamiria kabisa kuiua TANU ingali badochanga. Akiwa bado amenaswa katika kitendawili hicho cha kibali cha kufanyamkutano, Mtemvu alipata nakala ya mkutano wa 674 wa Baraza la Udhamini la Umojawa Mataifa ambayo Attorney General, Gratten Below, alifafanua juu ya msimamo waserikali kuhusu suala hilo. Mwanasheria Mkuu aliarifu kwamba watu wanawezakuanza shughuli za chama mara tu maombi ya usajili ya chama cha siasayatakapowakilishwa; na wanaweza kuendelea na shughuli za siasa mpaka majibukutoka kwa Msajili Mkuu yamepokelewa kwamba tasjili imekataliwa. Uongozi waTANU katika makao makuu ulisisimka kwa taarifa hiyo iliyofukuliwa na Mtemvu. TANUdaima itamkumbuka Mtemvu kwa juhudi zake za kuiingiza TANU Mafia ambako alihutubiamikutano iliyofurika watu. Nyerere alimwambia Mtemvu watu wa Mafia watakuelewawewe zaidi ya mimi. Bahatimbaya sana Mtemvu alitupana mkono na Nyerere na TANU mwaka 1958 pale serikaliya kikoloni ilipoandaa uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria ambao viti vilikuwavishindaniwe kwa misingi ya utaifa. Kulikuwa na viti kwa ajili ya Wazungu,Wahindi na Waafrika. Masharti mengine ya kumwezesha Mwafrika kupiga kurayalimtaka awe na kipato cha paundi mia nne za Kiingereza kwa mwaka, awe nakiwango cha elimu ya darasa la kumi na mbili na awe ameajiriwa katika kazimaalum. Haya yalikuwa masharti magumu na yaliyoonekana kama hayatawezakukubalika na TANU. Mtemvu hakuona mantiki ya kuwaingiza Wazungu na Waasiakatika Baraza la Kutunga Sheria na hakuficha msimamo wake na kwa hakikawanachama takriban wote wa TANU walipinga kura tatu. Wana TANU walikuwa nakauli mbiu yao wakisema kuingia kura tatu ni sawasawa na "kujipaka kinyesi." Mtemvuna wengi waliokuwa wakimuunga mkono walisisitiza, "Afrika kwa Waafrika." Lakinihili jambo likawa linasubiri uamuzi wa mkutano mkuu wa TANU wa mwaka 1958 ambaoulikuwa ufanyike Tabora. TANU ilifanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa1958 mjini Tabora kuanzia tarehe 21-26 Januari kujadili miongoni mwa mambomengine ikiwa ishiriki katika uchaguzi chini ya masharti haya ya kibaguziyaliyowekwa na Waingereza au wasuse. Mkutano ule ulitishia kuigawa TANU katikakambi mbili hasimu. Kambi moja ni ile ya wenye siasa za wastani waliopendeleakushiriki katika uchaguzi na ile ya pili ni ile ya wenye msimamo mkaliwaliotaka uchaguzi ususiwe kabisa. TANU ilinusurika na kile ambacho kingewezakuwa mgogoro ndani ya chama ambao ungewafanya wale wenye msimamo mkali kamaSheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU katika makaomakuu, na Zuberi Mtemvu, wakati huo katibu mwenezi wa TANU, kufanya mapinduziambayo yangekigawa chama kama isingelikuwa busara ya Julius Nyerere, Rais waTANU na mkakati wa siri alioupanga na viongozi wa TANU Tanga, Mwalimu Kihere naSheikh Rashid Sembe. Lakinikumuelewa Mtemvu na hisia za wanachama wa TANU, fikra za uongozi wake na nguvuzilizokuwa zikidhibiti siasa Tanganyika wakati ule wa ukoloni, na ili kuelewakwa nini kura tatu ilileta mgogoro na kutoelewana katika uongozi hata kupelekeaTANU kumegeka kwa mara ya kwanza na Mtemvu kuanzisha chama kingeine cha siasa,inatubidi turudi nyuma tufuatilie mwanzo wa siasa mjini Tabora, mahala ambapoTANU ilifanya uamuzi wake ya kihistoria na kuwanasa Waingereza katika mtego waowenyewe. Tunahitaji kuyatazama mambo kwanza kuanzia Tanga mahali ambapo Nyererena uongozi wa TANU pale Tanga walikutana kwa siri kuweka mikakati ya mkutano waTabora. Baada ya kufanya hivyo tufichue jambo moja baada ya jingine katika ulemkutano ambao wajumbe wa TANU walikutana katika ukumbi wa Parish wa KanisaKatoliki, Tabora. Hii itatuwezesha kujua kwa nini mkutano mkuu huu ulikuwamuhimu. Akiiandikia Fabian Colonial Bureau, Katibu Mwenezi wa TANU, ZuberiMtemvu ambae alikuwa amelichambua jambo hili la utatanishi wa kura tatu aliandikamaneno haya,"Katika nchi kama Tanganyika, utajiri na elimu vimo mikononi mwawageni. Mwafrika ni maskini na hana elimu. Upigaji kura wenye masharti magumuyaliyoegemezwa kwenye mali na elimu utawaathiri Waafrika peke yao bila kuwagusaWazungu na Waasia hata kidogo. " Ungoziwa TANU makao makuu kulikuwa na watu wengi ambao wasingeweza hata kidogokusimama kama wagombea katika uchaguzi chini ya masharti yale. Makao makuu yaTANU palikuwa na viongozi kama hawa, Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir,Bibi Titi Mohamed, John Rupia, Elias Kissenge, Dossa Aziz, Julius Mwasanyangi,Michael Lugazia, Ramadhani Chaurembo, Hussein Mbaruk, Clement Mtamila, IddTulio, Mzee Salum, Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Haidari Mwinyimvua na RajabuDiwani.Katika hawa ni wachache tu ndiyo waliokuwa na sifa za kusimama kupigiwakura au kupiga kura. Na hali ilikuwa kama hivi Tanga, Tabora, Dodoma na mahalapengine kwingi nchini Tanganyika. Kwahiyo ilikuwa ni jambo la wazi kabisa kuwa TANU ingesusia uchaguzi wa kura tatu.Mkutano wa Tabora ulikuwa uamue ikiwa TANU itashiriki katika uchaguzi nakushindana na UTP au ingesusia uchaguzi huo na hivyo kumpa mshindani wakemkubwa na hasimu wake ushindi wa bure bila jasho. Mkutanowa Tabora kwa shida sana uliamua kuwa TANU ishiriki katika kura tatu. Baada ya kutia saini kwa Azimio la TaboraMzee Fundi Mhindi, Nyerere, Dossa, Mwalimu Kihere na Mohamed Mangiringiriwaliondoka pale Parish Hall na kwenda mjini kutafuta simu ili kumpigia ZuberiMtemvu makao makuu Dar es Salaam kumuagiza awatangazie wananchi kuwa TANUimepiga kura kuingia katika uchaguzi wa kura tatu. Mangiringiri alimchukuaNyerere hadi kwa mwajiri wake wa Kiasia, G. B. Somji kupiga simu kwa Mtemvu.Siku iliyofuata wakati mkutano bado ukiendelea Mtemvu alituma simu ya maandishikwa rais wa TANU, Nyerere kupitia ofisi ya TANU Tabora, akitangaza kujiuzulukwake kutoka TANU na kuanzishwa kwa chama kipya - African National Congress(ANC). Chama cha Mtemvu kilikuja kujulikana kama "Congress" neno ambalokutokana na vyama vyote viwili jina hili lilikuja kunasibishwa na usaliti.Mtemvu akimshutumu Nyerere kwa kusaliti dhamana aliyokabidhiwa na TANU nawananchi; na Nyerere akimshutumu Mtemvu kwa kuacha mapambano na kujiunga naupinzani ili kudhoofisha TANU, na hivyo kusaliti harakati za kudai uhuru.Msimamo wa Mtemvu ulikuwa "Afrika Kwa Waafrika" - hakuna mgeni atakayekubaliwakuitawala Tanganyika. Mtemvualikuwa amelenga kwenye serikali ya Waafrika watupu ndani ya Tanganyika huru.Ujumbe wa Mtemvu ulipokelewa katika ofisi ya TANU mjini Tabora na mara mojatarishi alipanda baiskeli kupeleka ujumbe ule mkutanoni kule Parish Hall.Nyerere aliwasomea wajumbe wa mkutano mkuu ile simu kwa sauti. Ilikuwa nihabari za kustusha. Hatua hii ya Mtemvu ilikuwa ya pekee katika historia fupiya TANU. Hapakuwahi kutokea kiongozi wa chama kujiuzulu na kuanzisha chama chaupinzani. Mtemvu alikuwa mpinzani wa kura tatu toka mwanzo na Nyererealiufahamu msimamo wake. Katika maandalizi ya mkutano wa Tabora ilikuwa Mtemvundiye atakaeongoza hoja ya "kwa nini lazima TANU ikatae pendekezo la kura tatu".Lakini baadae Nyerere alimshawishi Mtemvu abaki nyuma Dar es Salaam kuendeshamakao makuu kwa kuwa haitakuwa busara kwa viongozi wote kuondoka na kuiachaofisi bila kiongozi wa juu ofisini. Nyerere alimshawishi Mtemvu akubaliane naushauri wake na kuhusu hoja ya upinzani wa kura tatu, Nyerere alishauri hojahiyo aachiwe Amon Kissenge aiwasilishe kwenye mkutano wa Tabora. Vitakati ya Mtemvu na Nyerere inasemekana ilikuwa imeanza siku nyingi na Nyererealijaribu kushinikiza atolewe Kamati Kuu ya TANU lakini hili lilipingwa vikalina John Rupia, kwa hiyo Nyerere hakufanikiwa lengo lake. Miezi michache kablaya uhuru Rais wa Congress, Zuberi Mtemvu akiwahutubia wanafunzi wa Chuo KikuuCha Karl Marx mjini Leipzig, Ujerumani ya Mashariki, Mtemvu alibashiri kuwakutolewa kwa uhuru wa Tanganyika kwa uongozi wa TANU, hautabadili chochote kwakuwa wanaoingia madarakani wameamua kushirikiana na walewale wanyonyaji wazamani na hii itavunja nguvu za wazalendo na matumaini yao. Siku za mwisho zaMzee Mtemvu alikuwa anakuja nyumbani kwa mwanae Abbas Mtemvu akitokea Morogoroambae tukiishi jirani. Nikitoka kazini njia ya kwenda kwangu ilikuwa inapitambele ya nyumba yake. Nyakati za jioni Mzee Mtemvu alikuwa akipenda kukaa njekupunga upepo. Nikifika pale nilikuwa nakwenda kumwamkia na hapo tutaanzagumzo. Ilikuwa akinishinda kwa hoja basi mimi humchokoza kwa kumwambia, "Lakinibaba unajua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imekuweka wewe katika kundi lawasaliti?" Hapo ninakuwa nimechokoza nyuki. Mzee Mtemvu atanijibu, "Msalitimimi au Nyerere aliyetoa nchi kwa walewale waliokuwa wakitutawala?" Hapoatazungumza sana na mwisho huagana nikenda zangu. Mtemvu na Nyerere kuanziamwaka wa 1958 walinuniana hawakuzungumza hadi mwisho wa maisha yao na kisa chaugomvi wao kilikuwa ni kura tatu.

Mohamed
 
Mag3,

Yale yamekwisha niulize tu ndugu yangu hapana haja ya kupitia kwa FF.

Hizo shule si shule za Aga Khan zilikuwa zikijengwa na Aga Khan kwa ajili
ya EAMWS kuwainua vijana wa Kiislam.

Mohamed

Mimi nina maswali mawili tu hapa:

a. Aga Khan ni Muislamu?
b. Je, jumuiya ya Aga Khan ilipigwa marufuku na Nyerere mwaka gani?
 
Mag3,

Meru Citizens Union na Abdulwahid Sykes soma hapa chini:

"Baadaya Dr Kyaruzi kuhamishiwa Nzega nafasi ya rais ikawa wazi. Abdulwahid Sykesakakaimu nafasi hiyo na kuwa katibu na kaimu rais wa TAA. Katika uchaguzi wa mwakawa 1952, uliofanyika Arnautoglo Hall akiwa na umri wa miaka 28 Abdulwahidalichaguliwa kuwa rais wa chama cha TAA. Wakati ule mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwaumekwishaanza lakini bado haujalipuka kuwa suala lililowahusu Watanganyikawote. Umoja wa Mataifa ulipotuma ujumbe wake wa pili kuzuru Tanganyika mwaka wa1950, Wameru waliwasilisha rasmi malalamiko yao kwa ujumbe huo. Abdulwahidaliwaomba wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria washirikiane na TAA katikakutatua baadhi ya matatizo yanayokabili jamii ya Waafrika. Abdulwahidalifadhaishwa na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria palewaliposhindwa kuipinga Wilson Report ambayo ilipendekeza kuondolewa kwawananchi wa Meru kutoka kwenye ardhi yao. Katika barua aliyoiandikia MeruCitizenís Union, Abdulwahid, kwa niaba ya makao makuu ya TAA, aliwahakikishiawatu wa Meru kuwa tatizo lao llilikuwa tatizo la Watanganyika wote. Abdulwahidaliamua kutumia mgogoro wa ardhi ya Wameru kuwaunganisha Watanganyika wotedhidi ya serikali ya kikoloni. Barua hizi kati ya Abdulwahid na viongozi waMeru Citizens’s Union, Kirilo na Sablak walizoandikiana kati ya Septemba naDesemba 1952 zinatoa picha halisi ya jinsi hali ya siasa ilivyokuwa Tanganyika.(Barua hizi zinapatikana katika katika Nyaraka za Kirilo Tanzania NationalArchives (TNA), Dar es Salaam). Uamuziwa serikali juu ya mapendekezo ya TAA kwa Constitutional Development Committeeulikuwa bado umo akilini mwake. Alitambua kwamba uamuzi wa Gavana ulikuwa nimpango wa muda mrefu wa kuwadhalilisha Waafrika katika utumwa wa daima.Abdulwahid sasa akiwa na ghera kubwa alianza kufanya kazi ya kuwahamasisha watuwa Tanganyika chini ya vuguvugu la kuunganisha umma dhidi ya utawala waWaingereza. Abdulwahid aliwasiliana na Earle Seaton mjini Moshi kutaka ushauriwa kisheria juu ya tatizo la Meru. Seaton alikuja Dar es Salaam na kukutana naAbdulwahid na uongozi wa TAA. Ilikubaliwa na pande zote mbili kuwa makao makuuya TAA, Meru Citizenís Union ikiongozwa na Japhet Kirilo na Seaton lazimawaunganishe shughuli zao katika kesi hiyo na kwa pamoja watume rufaa yao kwenyeBaraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York. Kwa sasa uongozi wa chamacha TAA ulitambua kwamba nusura yao ilitegemea uwezo wao wa kudhibiti nakushawishi matukio na maamuzi ndani ya Baraza la Kutunga Sheria. Ili kuweza kufanya hayo shinikizo lilitakiwakuwekwa katika Baraza la Udhamini huko New York, nchini Amerika na siyo katikaOfisi ya Makoloni pale London Uiengereza. Katikamatawi ya TAA yaliyokuwa na nguvu sana Tanganyika mojawapo lilikuwa tawi laTabora. Tawi la chama cha TAA la Tabora lilichukua changamoto la Mgogoro waArdhi ya Wameru kwa ghera kubwa na kwa kupitia juhudi za Saadani Abdu Kandoro yeyealilibeba tatizo lile kama jukumu lake binafsi. Kandoro aliitisha mkutano wamatawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo. Mwanzailiwakilishwa na Bhoke Munanka, Mzee Mkama Mlaji na Mohamed Kihaka Kitenge;kutoka Kigoma mjumbe aliyekuja alikuwa Jumanne Mawimbi na Tabora iliwakilishwana Sheikh Kinana, Kandoro na George Magembe kama rais wa TAA tawi laTabora. Mkutano wa Tabora uliahidimshikamano wa pamoja na watu wa Meru katika mapambano dhidi ya walowezi. Mgogorowa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitiakatika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seatonkama mkalimani na mshauri wa sheria wa TAA, kwa mara ya kwanza alizungumzambele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyeshaudhalimu wa ukoloni. Waingerezawalikataa kumpa Kirilo pasi ya kusafiria kwenda Amerika na ikabidi Abdulwahidna uongozi wa TAA uingilie kati na mwishowe serikali ikatoa pasi. November, 1952 Kirilo alizungumza mbele yaKamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York. Watu wa Tanganyikasasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi zaUmoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikonomitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali. Kiriloaliuhakikishia Umoja wa Mataifa kuwa watu wake kamwe hawatachukua silahakuikomboa ardhi yao kama Wakikuyu wa Kenya walivyojaribu kufanya. Kwa kwelihapakuwa na sababu ya kutoa kauli hii, kwa kuwa uhakikisho wa kutokuwepomapambano uliwafanya walowezi washushe pumzi na kujiona wako salama. Tangumwanzo wa mgogoro wazalendo nchini Kenya kama Fred Kubai na Kung'u Karumbawalikuwa wakitoa ushauri kwa Meru Citizenís Union kwa kuwa wao walikuwa naujuzi zaidi wa matatizo ya walowezi kuliko watu wa Tanganyika. Kwa mtazamo wajuu juu mtu anaweza kudhani kuwa TAA ilikuwa akipata kipigo kutoka sehemu zoteilipojaribu kujipenyeza. Kushindwa huku si kwa sababu TAA ilikuwa ina viongozidhaifu au ilikuwa haiuingwi mkono na umma. TAA ilikuwa haifanikiwi katika madaiyake kwa sababu serikali ya kikoloni ilikuwa imeamua kutosikiliza lolote kuhusumatatizo ya Waafrika. Matokeo ya hali hii iliifanya TAA Iamue kuwa njiailiyobakia ya Tanganyika kujitoa katika makucha ya Waingereza ni kuuandaa ummawa Tanganyika chini ya chama cha siasa. Maratu baada ya Kirilo kurejea kutoka New York, mpango wa kuanzisha chama cha siasacha kushirikisha umma wote ulianza kiongozi wa mpago huu alikuwa Abdulwahid Sykes na ile kamati ya siasandani ya TAA. Uongozi wa TAA Makao Makuuulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo Umojawa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha zakupeleka msafara mwingine Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyikailikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuruwao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na AbbasSykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAAchini ya John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kamanauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaahapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjiniambako Kirilo alizichukua. Kuanziatarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea nakuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba,Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa,Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamojanao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wotemjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo. TAA iliunda sekretarieti ya kudumu katika ofisi ya NewStreet kushughulikia kazi za kila siku za chama.KIjana mmoja aliyejulikana kamaAlexander Tobias aliajiriwa kama mfanyakazi wa kwanza wa TAA. Kwa bahati mbayasana Alexander Tobias aliisaliti TAA kwaWaingereza."

Mohamed



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…