Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,171
Nyambala,
Tafadhali tuelewane.
Kitabu ambacho si sahihi katika historia ya TANU ni hiki:
"Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981."
Ikiwa umefuatilia makala zangu katika Mwananchi na ukaja kusoma kitabu
hicho utapigwa na butwaa maana hiyo yao sio historia ya TANU. Historia
ya TANU hayumo Abdulwahid Sykes, Ally Sykes Dossa Aziz, Sheikh Hassan
bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Bi Titi Mohamed, Bi Tatu
bint Mzee nk. hiyo siyo historia ya TANU ni kitu kingine kabisa.
Hicho kitabu ulichotaja kwa bahati mbaya sijakisoma kwa hiyo siwezi kusema kitu. Ilani hivi vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusu historia Tanganyika na kugusia"nationalist politics" haya niliyoandika hayamo ingawa wemeeleza mengikwa kupitia kijuujuu tu ukiondoa The Making of Tanganyika cha Judith Listowel, 1965.
Asante sana Mohamed Said kwa kuliweka hili wazi kuhusu kitabu hiki cha "Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981." Kusema ule ukweli jina tu la hicho kitabu linanifanya hata nisiwe na hamu ya kukisoma au kukitafuta. Kitabu nilichokielezea hapo juu nimekikuta kwenye makabrasha flani na nimekisoma fasta fasta maana sikuwa na muda. Weekend hii nikipata nafasi ntakipitia tena mstari kwa mstari maana kuna vitu interesting ningependa tujadili.
Lakini pia kwa kukumbusha umewahi kutuhumu kwamba vitabu vinavyotumika mashuleni kusomeshea historia navyo vimepotosha unaweza kututajia mifano tafadhali ukiondoa huki cha CCM.