FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Nimejaribu sana kupata majibu ya maswali myepesi sana kwa Mag3 au wanaomuunga mkono, lakini mpaka sasa sikuambulia kitu. Hivi kuna msomi akajificha asijulikane halafu anakuja kupingana na mwana historia aliojiweka wazi kabisa?
Maswali yangu yalikuwa haya:
Msomi alioweka post kwa mbwembwe eti anaeweza kuelezea history ya Tanganyika anashindwa kujieleza yeye ni nani? Hapa panaleta raha sana.
Maswali yangu yalikuwa haya:
FaizaFoxy https://www.jamiiforums.com/members/faizafoxy.html Yesterday 17:44 #30
Mohamed Said anapotaja wazee wake anaonesha na nini walikifanya na dalili anaziweka wazi, sasa huyo aliyeambiwa na wazee wake bila kutupa dalili za hao wazee walikuwa kina nani walikuwa na harakati zipi, tumuamini vipi?
FaizaFoxy Yesterday 17:55 #33
Tumeona Mohamed Said akitubwagia kinaga ubaga vitabu alivyoandika na "papers" alizoandika, mihadhara aliyoitowa / hudhuria vyuo mbali mbali duniani, Jee, na wewe upo tayari kutuwekea hapa ili tujuwe "credibility" yako katika historia? au ndio wakudonyoa donyoa mtandaoni? na ya kuhadithiwa na wazee wako ambao hata dalili hautupi walikuwa na harakati zipi katika siasa au jamii wakati huo? Tuwekee wazi ili tusikuone kama ni mpiga porojo tu.
FaizaFoxy Yesterday 23:59 #48
Mohamed Said kaelezea vitabu alivyokwishaandika, papers zake, vyuo na makongamano tofauti duniani alivyohudhuria.
Kawataja wazee wake ni kina nani na walikuwa wanafanya nini.
Huyo Mag3 hakuna kimoja katika haya aliyotuwekea wazi hata jina lake na nasaba yake hajaiweka wazi.
Hatuna reference yake hata moja ya amma kwa kitabu au paper ya history. Isitoshe, ameanza kwa kejeli na matusi, jee hapo kuna "credibility" yoyote ambayo kwa ujasusi wako unaweza kuitetea?
FaizaFoxy Today 08:35 #70
Hicho ulichonibandikia, huyo ni Mag3? nilichoulizia ni credibility ya Mag3 na atueleze hapa yeye ni nani hao wazee wake anawanukuu ni kina nani? walifanya nini katika harakati za kudai madaraka / nyadhifa za kijamii / siasa wakati huo? Yeye kishaandika au hajaandika kitabu chochote? kama kaandika ni kitabu kipi? au "paper" zipi za usomi kishaandika? vyuo alivyohudhuria, makongamano au kualikwa kuongea, kutetea maandiko yake?
Kwa ufupi ni nani?
Naona mpaka sasa bado anatafuta "data" zake kwa haya maswali.
Msomi yoyote mwema, hujitambulisha au hutambulishwa na amma usomi wake, amma kazi zake, amma utu wake (kwa wamjuao). sasa msomi Mag3 sijayaona yote hayo. Mnaweza mkamsaidia mumjuwae.
Msomi alioweka post kwa mbwembwe eti anaeweza kuelezea history ya Tanganyika anashindwa kujieleza yeye ni nani? Hapa panaleta raha sana.