Duuuh!! Facts na research!!
Kwanza sensa siyo fact, ni estimate inayobase na raw data. TZ hatuna fact; kwa sababu hatuna true information kwa sababu hatuna IT. Facts unahitaji kuwa na IT in order kuwa na true information. Unaposema TZ kuna watu Million 40 ni estimate na SIYO facts. Population haina facts bali ina estimate.
Research ina base na credible sources ambazo walengwa wanazitumia kwa ajili ya kusatisfy their arguments. Wewe na wenzako, pamoja na Mwkjj mnatumia sources ambazo zina pro-Nyerere kusatisfy argument mnazoziweka.
Kama mngekuwa mnatumia sources ambazo hazina base ya upande mmoja, basi msingekuwa na ubishi na hoja ambazo MS anajaribu kuelezea. Sources za MS zipo credible zaidi kwa sababu anatumia information direct kutoka kwa wale walioshiriki ktk Uhuru.
Sources zenu, zipo upande mmoja kwa sababu mnatumia data kutoka serikalini, au Pro-Nyerere ambazo tayari zipo FILTER ktk kuelezea ukweli.
Niweke sawa na kwa lugha rahisi kabisa isiyoleta utata na kubadilli mada. Mlima kilimanjaro upo Tanzania- Facts.
Kwanini Klimanjaro, kagera na Mbeya watu wanaelimu kuliko sehemu nyingine- yatakauwa matokeo ya research.
Baada ya hapo nifafanulie Pro-Nyerere ni akina nani na je ndio Pro-TANU?
Maiaka 10 iliyopita CCM ilikuwa madhalimu walio kandamiza waislam. Hiyo kauli imeishia wapi? si ndio ilikuwa kauli mbiu ya kuunga mkono falsafa ya 'Haki- Sawa' ya CUF. Lini uswahiba umerudi na ni kwa historia gani tofauti na ile iliyowakandamiza.
Kama source za Mohamed ni credible kama unavyodai, kwanini hakumhoji Fundikira, Rais wa EAMWS na right hand man wa Nyerere?
Kwanini hakumhoji mama Maria Nyerere kuhusu samaki aliopelekewa na marhum mzee Kiyate.
Kwanini hakumhoji marhum Rajab Diwani na Kitundu mapema(anasema alifariki masaa machache kabla ya mahojiano).
Kwanini hamhoji Sakim Ahmed Salim au Butiku wa NF
Kama ni credible, kwanini asikanushe au kukubali ushiriki wa Wanawake wa Pare katika kuanzisha chem chem ya kisiasa.
Kwanini asikanushe au kukubali uwepo wa harakati nje ya Dar es salaam kama Mwanza n.k
Kwanini majina ya akina Kisenge na Mashambo waliokuwa na hadhi katika TANU hayajitokezi
Kama ni credible kwanini asihoji namba za mtihani wizara husika
Kwanini asihoji madiwani wa kariakoo na gerezani waliobadili majina ya wapigania uhuru.
Kwanini asimhoji Silvano aliyeandika kitabu anacho kinukuu mara zote
Kwanini hakumhoji marhum Kawawa kama mwislam na mshiriki wa Nyerere, na mbona ushiriki wa Kawawa kama kiongozi katika vyama vya wafanyakazi hauonekani licha ya kuwa alikuwa Mwislam.
Soma post yangu ya awali, Mohamed anakiri kwa maneno kuwa 'anahadithia' maneno aliyosikia ili aweke sawa historia ya Waislam. Amekiri hivyo, sasa wewe unaposema ya Tanganyika umeitoa wapi zaidi ya Mohamed wenyewe.
Nina uhakika hujasoma vitabu vya Mohamed au makala zake. Nasema hivi kwasababu ametumia neno 'Inasemekana' mara nyingi sana. Credibility ya source zake iko wapi?
Unaweza kuwa na credible source halafu useme inasemekana!!! Inasemekana kutoka kwa nani maana yeye amesikia na hivyo ilipaswa aseme nimeambiwa. Ukishasema 'inasemekana' hiyo ni third party. Credibility ipo wapi.
Narudia, data na info zingine tunazofanyia kazi zimeletwa na 'credible' source kama aliyofanya Mohamed na Mdondoaji. Kwanini tulaumiwe kwa kuuliza au kuhoji.