Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
- Thread starter
- #41
Asante Fundi Mchundo na sasa umefika wakati wa kutoa somo kwa watu kama Mohamed Said ambao porojo za mitaani za wazee wao wa Gerezani wanaamini zingeweza kuwaletea uhuru Watanganyika.Naona wengine hawataki tu kumuelewa Mag3. Ni hivi:
Ndi maana, tunawashangaa watu wanaotaka kutuambia kuwa bila hao jamaa wa gerezani na misheni kota, mpambano usingefanikiwa. Ni matusi makubwa.
- Mwaka 1957, kulikuwa na watanganyika waafrika 8,665,336 nchi nzima.
- Wasukuma walikuwa asilimia 12.6 ya watanganyika waafrika, kwa hiyo walikuwana idadi ya 1,091,832.
- Mwaka huo huo, mji wa Dar es Salaam ulikuwa na watu 128,742; Tanga 38,053; Mwanza 19,877;Tabora 15,361; Moshi 13,726; Arusha 10,038 na Bukoba 5,276.
- Mwaka huo ni asilimia 4.4 ya wakazi wa Tanganyika ndio waliokuwa wanaishi mijini.
- Kutokana na ukweli huu, hao watu ambao Mohamed Said anawapigia debe waliokuwa wakiishi kwenye kitongoji kimoja tu cha mji wa Dar es Salaam wasingeweza kufanya lolote hata kama waswahili wote wa Dar es Salaam, Tanga na Tabora wangewaunga mkono.
- Miaka ile huku walikokuwa wakiishi watanganyika wengi, mswahili alikuwa anachukuliwa kama mtu asiyeweza kuaminika ndiyo maana wakina Sykes wasingeweza kuwashawishi watu wa huko kuungana nao. Mtu ambaye wangemwamini ni mshamba mwenzao na hasa kama atatambulishwa na watu wa kwao wanaowaamini. Mtu mwenye sifa hii alikuwa Julius Kambarage Nyerere na pengine Oscar Kambona. Sehemu za pwani, Bibi Titi Muhamed alichangia mno kuvuta wanawake na wame zao kuingia TANU.
Amandla.....
Fact No 1: TAA ilikuwa ni chama cha Wafanya kazi serikalini kama zilivyokuwa vyama vingine tu vya wafanya kazi kama wa reli, madereva, makuli, wafanyakazi viwandani n.k.
Fact No 2: TAA haikujisgughulisha katu na mambo ya kisiasa kabla ya 1952 na hiyo ilibainishwa fika katika katiba yake.
Fact No 3: Wafanyakazi wote kwa ujumla wao kwa wakati huo walikuwa ni asilimia ndogo sana ya Watanganyika.
Fact No 4: Wanachama wa TAA kwa ujumla wao walikuwa asilimia ndogo sana ya wafanyakazi nchi nzima ya Tanganyika.
Fact No 5: Ni Mwalimu Nyerere aliyeleta changamoto ndani ya TAA na hasa wazo la kupigania uhuru.
Fact No 6: Changamoto alizoleta Mwalimu ndani ya TAA ndio chanzo cha kukubalika kwake na kuchaguliwa kuwa Raisi wa kwanza wa TAA iliyokuwa na mwelekeo wa kisiasa.
Fact No 7: Mwalimu hakusita kuionya TAA kwamba kama haikuwa tayari kuwashirikisha Watanzania walio wengi basi haitafika popote. Hawa Watanganyika aliokuwa akiwasema Mwalimu ni wakulima kwa ujumla wao kupitia vyama vyao vya Ushirika.
Fact No 8: Baada ya hiyo Changamoto, Mwalimu ndiye alikabidhiwa jukumu la kuandaa katiba mpya iliyokuja kuzaa chama cha siasa kilichoshirikisha wakulima na wafanyakazi, TANU.
Fact No 9: Majimbo yaliyoongoza kwa idadi ya watu na vyama vya ushirika vya wakulima yalikuwa majimbo matatu tu - Jimbo la Ziwa, Jimbo la Kaskazini na Jimbo la Nyanda za juu Kusini.
Fact No 10: Hivyo vyama vya Ushirika vya Wakulima vilijiunga na TAA/TANU kwa ushawishi wa mtu moja tu waliyemwamini, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwaka 1955 vyama vingine vyote vya Wafanyakazi navyo vikajiunga na kukazaliwa a united front - Tanganyika Federation of Labour.
Mpaka hapo yatosha kwa leo nitaendelea...............