Mkuu Jasusi achana na huyu mpuuzi, tatizo ni kwamba watu wengi makini wamekuwa wakiyapuuzia haya makala yake ya kichochezi na hatari yake ni kuwa uwongo ukiachiwa nafasi ya kujirudia rudia mwisho wapo watakaoamini kuwa ni kweli vile. Mimi wakati naanza shule 1953, huyo Mohamed Said alikuwa hata hajazaliwa kama alivyokiri kwenye majibu yake hapo nyuma.
Mimi ni mzaliwa wa kanda ya Ziwa na wakati tunapata uhuru mwaka nilikuwa Sekondari lakini pamoja na kuwa tulikuwa tunafuatilia sana matukio ya kisiasa, sikuwahi kuwaona au hata kuwasikia hao anaodai Mohamed kuwa walikuwa vinara wa harakati za kudai uhuru Tanganyika. Je hii ni kwa sababu nilizaliwa nje ya Dar es Salaam au kwa ni sababu hao wazee wa Mohamed hawakujulikana nje ya Dar es Salaam.
Pamoja na kwamba mwaka 1965 tayari nilikwishahamia Dar es Salaam kuendelea na masomo yangu, sikuyasikia haya majina hadi miaka ya 1970 ! Baada ya hapo nilijaribu sana kuwadadisi wazee mbali mbali, Musoma, Mwanza hadi Bukoba lakini sikuweza kumpata mzee ambaye kwa hakika angeweza kunisimulia mchango wa hawa wazee wa Gerezani alikozaliwa Mohamed Said katika kudai uhuru wa Tanganyika.
TAA kwa upande mwingine ilianzishwa na watumishi wa serikali chini ya utawala wa kikoloni na haihitaji akili yoyote ya ziada kukisia kuwa wengi wa hawa watumishi walikuwa wa aina gani. Ni vigumu sana kusema kwa uhakika ni lini TAA iliyoanzishwa mwaka 1929 ilianza kuwa na msimamo wa kisiasa lakini upepo wa uhuru kwa nchi nyingi za Kiafrika ulianza kuvuma kwa kasi miaka ishirini baadaye.
Harakati za TAA zilipoonyesha dalili ya kudai mambo nje ya haki za wafanya kazi ilibidi kuchagua moja ama ujiuzulu uunge mkono TAA bila kificho au uendelee na ajira lakini usionyeshe wazi msimamo wako. TAA ikawa imefikia kikomo chake na ikawa sasa ni lazima kizaliwe chombo cha kisiasa ambacho malengo yake na dhumuni lake ni kuiondoa serikali ya kikoloni kwa kudai uhuru kamili.
Madai ya Mohamed Said ni kama leo kudai kuwa wote walioko serikalini hawaungi mkono madai ya Chadema dhidi ya serikali, la hasha, wapo lakini wakijionyesha wazi wazi wakati huu nafikiri sote tunajua serikali ya CCM itakavyowashughulikia. Kulikuwa na faida kubwa kwa wanaharakati wengine kubaki ndani ya serikali ya mkoloni kama ilivyo sasa hivi kwa Chadema kuwa na watu wake ndani ya serikali ya CCM.
TAA ya Mwanza mpaka mwaka 1948 ilikuwa na wanachama kama 3,000 lakini mwaka 1952 kwa jitihada za Bomani wanachama wa TAA waliweza kuongezeka hadi kufikia 30,000 na ni mwaka moja baadaye ndiyo Katibu Mkuu wa TAA kama anavyodai Mohamed Said alipotembelea Mwanza. Lakini wakati huo tayari Mwalimu Nyerere anaiongoza TAA baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Raisi wake.
Walikuwapo watu kama Masanja Shija Raisi wa kwanza wa Victoria Federation Cooperative Union (VFCU) na Makamu wake akiwa Daudi Kabeya Murangira wa Majita aliyeuza boti zake za uvuvi. Jamani wana JF, Tanganyika ilikuwa zaidi ya Wazee wa Mohamed Said wa Gerezani na Kariakoo na ukweli ni kwamba Watanganyika walihitaji kuhamasishwa kutoka Mtwara hadi Sirari, Dar es Salaam hadi Kasulu !
Mwalimu Nyerere hakuwa mtoto yatima, alizaliwa katika ukoo wa kichifu na familia kubwa iliyojaa wazee wa busara wa Kizanaki ambao walimpa baraka zao zote awakabili wakoloni bila woga. Mwalimu Nyere kila aliporudi Musoma hakusahau kufika kuvuka mto Mara kwenda kumsalimia Chifu Odemba Kagose wa Buturi Ujaluoni kupata ushauri wake kwa mambo mbali mbali.
Wana JF, ni wakati sasa wa kuwakataa hawa wachochezi, ni wakati wa kumwambia Mohamed Said kuwa hata uvumilivu una mwisho. Wamekuwa wakipata free ride wakipanda hizi mbegu za chuki miongoni mwa wananchi huku sisi great thinkers tukikaa kando, no enough is enough, ukweli lazima waambiwe hata kama unauma kiasi gani.
Majuzi hapa tumeshuhudia Marekani, watu wa kilichoitwa tea party wakiibua mambo yasiyo na ukweli na kuyarudia rudia hadi wakawateka wale wenye uwezo mdogo wa kufikiri ! Mohamed Said ni wa kuogopwa kama ukimwi ! Mohamed Said sasa aanze kuorodhesha majina ya wazee wake waliojiuzulu kwenye utumishi serikalini ili kupigania uhuru wa Tanganyika ili wajadiliwe hapa JF kwa sababu TAA ilikuwa ya Watumishi wa serikali.
nafurahi kuwa zile hoja zinazostahili kujadiliwa na watu wenye hadhi ya forum hii zimeanza kujitokeza tena na kwa kweli zinachokonoa bongo na fikra za watu hadi inatia msisimko.
kuna ushahidi wa wazi kuwa kuna vipande vya historia vimezuiwa ama kupotoshwa kwa makusudi(sielewi ni kwa maslahi ya nani) na tumekuwa miaka yote tukiaminishwa kwamba harakati za kupigania uhuru ziliasisiwa,kuratibiwa na hata kufanikishwa na MWALIMU!! siku zote tumeshindwa kujiuliza maswali madogo tu kuwa kwa nchi kubwa kama TZ ambayo ilikuwa haina miundombinu kama ilivyo sasa, mwalimu aliwezaje kupata fedha,wenyeji n.k mpaka TANUikaweza kukubalika nchi nzima.
nisingepedna kuingia ndani zaidi lakini naamini kitu kimoja ambacho hata mwalimu nyerere alikuwa anakiamini nacho ni wakati makabila madogomadogo, masikini na yasiyo na elimu ya tanzania yakiunganisha nguvu na fedha zao kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukoloni,, na wakati mwalimu nyerere akiwa sambamba na wananchi wenzke toka katika jamii hizi masikini,, yale makabila yanayojiona leo hii kuwa ni makabila ya wasomi,wenye fedha na madaraka ndio yaliyokuwa hayataki kujishughulisha na harakati za kupigania uhuru na hawakuwa tayari hata kutoa michango ya fedha kusaidia harakati hizo,kwa vile wengi wao walikuwa wanafanya kazi katika serikali ya kikoloni, hawakuona ubaya wa ukoloni na hivyo hawakuona maana ya uhuru,
wale wachache wenye upeo na uelewa wa hali ya juu( nyerere,paul bomani,rashid kawawa,abbas mtemvu, abdul sykes.oscar kambona n.k) walikuwa wanapata support kubwa toka makabila madogodogo na yasiyo maarufu hivi sasa.
ushahidi uko wazi kwani hata mikutano muhimu kabisa ya TANU ilikuwa ikifanyika maeneo hayo,ofisi za kwanza kabisa za TANU zilifunguliwa maeneo hayo na hata wanaharakati wa mwanzo kabisa wa sisa za kudai uhuru walitoka maeneo hayo.
Hata mwalimu angekuwa hai leo na umuulize kama ni busara sisi wa TZ tumchague raisi kutoka makabila fulanifulani(siyataji) mwalimu angesema HAPANA tena kwa herufi kubwa kabisa kwani makabila haya yana sifa kubwa tatu nazo ni
1.usaliti-haswa kama usaliti wake utampa faida ya kifedha
2.uoga- haswa kama uoga wake utamfaya asipoteze kile anachokipata kwa muda huo.
3. ubinafsi- kwa kuamini kwa sababu wao wengi wamesoma na wanafedha basi wao ndio bora na haki kuliko wengine na kudhani kwamba wao ndio mabwana nasisi wengine tubaki kuwa watwana