Hapa nanusa kaarufu ka chuki binafsi Kwa Mwalimu Nyerere, anyway kama historia" imewasahau" hawa wazee wa gerezani nina uhakika wako wengi "waliosahauliwa" sehemu nyingine pia katika ukombozi wa nchi yetu hii. Mohamed Said anafanya kila anachoweza kumulika hilo lakini tatizo lake ni kuweka udini kidogo kwenye hili na ndiyo hapo utafiti" objective" unarushwa nje na hisia binafsi kutawala zaidi. Ningependa kuongea mawili matatu kumjibu Mr Said kama ifuatavyo;
Vita ya ukombozi Afrika yetu hii mara nyingi ilianzishwa na wakazi wa mijini kama wafanya kazi wa serikali, madereva, makuli, wafanya biashara ndogo ndogo, waandishi n.k kwa hapa kwetu walikua wapwani, watu wa DSM, na haswa pale gerezani, sawa sawa, lakini hawa wote iwe Tanganyika, Nigeria, au Ghana ilibidi wapate nguvu za mikoa ya ndani yenye wananchi wengi ili kukamilisha kile walichokianza na hapa sasa ndiyo akina Bomani na Nyerere na wasukuma, wanyamwezi, wahaya,wapare, na wanyakyusa wanapokuja. Sijui Mo Said alitaka historia iwaadikaje hao lakini kila mwenye mchango muhimu kwenye ukombozi wa nchi hii ameguswa na wengine wengi wameachwa siyo hawa tu wa gerezani
Kingine pamoja na yote kuanzisha kitu na kumalizia kitu ni vitu viwili tofauti sana katika maisha haya ya mwana adam na wote nafikiri tunajua hili. Napenda kuungana na mag3 kuhusu mchango wa Watanganyika wa sehemu zingine zisizokua Pwani, huu mchango ulikua mkubwa na wenye chachu kubwa katika kuleta uhuru, pwani pekee yao wasingeweza, ila hawa wa maeneo mengine wangeweza bila ya Pwani, hilo Mo Said inabidi kulijua na hapa siongelei udini ila ukanda kama naweza kuuita hivyo. Na hili linaondoa umuhimu wa kipekee au kama Mo said angependa kuiweka umuhimu wa uanzishaji wa kitu na nafasi ya muanzishaji kwenye historia, hivi tunajua nani alianzisha motor engine? hapana Kila mtu anasema ni huyu au Yule, na je ina maana yeyote au umuhimu gani kumjua katika jamii? Nafikiri hapana labda tu kama wewe ni mwanahistoria na unataka kuandika kuhusu hilo la mashine. Mchango wa Syskes, Bomani, wasukuma, Abushiri Salum, Nyerere, wanyakyusa, wapare, wachaga na wengine uko wazi na kwa hili sisi siyo wana historia na waanzilishi wa TAA tusiowajua hawatunufaishi kama jamii kwa lolote, bwana Said angalia hili kwa mawazo mapana.
Na napenda kuongeza hata kama hawa wa gerezani wangekua wanashirika katika ukoloni kama tabaka la pili la kinyonyaji bado mapambano yangeanzishwa tu na wengine wasomi wa mikoa ya ndani kwani si wangeona ndugu zao wengine wa Afrika wanafanya nini kwa hiyo hapa hii "indignation" yako haina maana ya hawa kupewa nafasi kubwa na muhimu katika historia ya ukombozi wetu wakati wako wengi tu waliosahaulika kama unavyodai wao.
Shukhran,