Ndugu yangu Kigarama, ni swali la muda tu na ukumbuke kuwa kabla ya kuchangia yabidi usome mambo mbali mbali ambayo yametolewa na washiriki mbali mbali ili usiyarudie tena. Hata hivyo kuna moja muhimu la kulitilia maanani nalo ni kwamba Wazee wa Mohamed walimhitaji Mwalimu Nyerere kuliko alivyowahitaji wao na ni bahati kwao waligundua hilo mapema sana na kumkabidhi Uraisi mara moja. Watu wa muhimu sana walikuwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao ilibidi wateuliwe wawe viongozi wa TANU mikoani na hasa kwenye majimbo muhimu ambako ndiko hasa harakati za kupambana na mkoloni zilikoanzia. Vyama hivyo vya Ushirika vingi vikiwa vimeanzishwa kabla ya TAA na vilitumika kuwahamasisha wananchi kuliko vyama vya wafanyakazi kwa sababu vilikuwa karibu na wananchi walio wengi.
Vyama vya Ushirika vya Wakulima vikuu vilikuwa kama;
- Kilimanjaro Co-operative Union Ltd (1933)
- Lake Province Native Growers Association (1949) - baadaye ikaanzishwa Victoria federation of Co-operative Unions
- Bukoba Co-operative Union Ltd. (1950)
- Ngoni Matengo Co-operative Union Ltd. (1936)
- Rungwe African Co-operative Union Ltd. (1949)
Dar es Salaam ilikuwa na wakazi wasiofika 200,000 na hata tukisema asilimia kumi walikuwa wafanyakazi sana sana watafikia watu 20,000. Hii idai ukigawanya kwa vyama vyote ni kwamba wakati Mwalimu Nyerere anachaguliwa kuiongoza TAA, mojawapo ya vyama vya wafanyakazi Dar es Salaam, labda ilikuwa na wanachama wasiofika hata elfu mbili. Sasa linganisha idadi hii na Chama cha Ushirika kama Victoria Federation of Coperative Unions ya Mwanza ambayo tayari ilikuwa na wanachama zaidi ya 30,000.
Kuna riwaya iliwahi kuandikwa na mtunzi moja mwenye jina la James Hadley Chase ikiwa na title - Believe this and you will believe anything ! Hivyo ndivyo navyovichukulia porojo za Mohamed Said ila tatizo ni kuwa ni porojo zenye hatari kwani zinapandikiza chuki miongoni mwa wananchi. Hapana, lazima aambiwe bila kumung'unya maneno aache mara moja kuivuruga jamii kwa hizi chuki zake na mimi nawaomba wote wenye nia njema na taifa letu kumpa a big NO ! Mbona haorodheshi majina ya hawa vinara walioongoza hivyo vyama vya Uchirika na badala yake amekaa kutusimulia soga za Gerezani ?