Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nyambala,

Tafadhali tuelewane.
Kitabu ambacho si sahihi katika historia ya TANU ni hiki:
"Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981."

Ikiwa umefuatilia makala zangu katika Mwananchi na ukaja kusoma kitabu
hicho utapigwa na butwaa maana hiyo yao sio historia ya TANU. Historia
ya TANU hayumo Abdulwahid Sykes, Ally Sykes Dossa Aziz, Sheikh Hassan
bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Bi Titi Mohamed, Bi Tatu
bint Mzee nk. hiyo siyo historia ya TANU ni kitu kingine kabisa.

Hicho kitabu ulichotaja kwa bahati mbaya sijakisoma kwa hiyo siwezi kusema kitu. Ila
ni hivi vitabu vingi vilivyoandikwa kuhusu historia Tanganyika na kugusia
"nationalist politics" haya niliyoandika hayamo ingawa wemeeleza mengi
kwa kupitia kijuujuu tu ukiondoa The Making of Tanganyika cha Judith Listowel, 1965.

Asante sana Mohamed Said kwa kuliweka hili wazi kuhusu kitabu hiki cha "Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981." Kusema ule ukweli jina tu la hicho kitabu linanifanya hata nisiwe na hamu ya kukisoma au kukitafuta. Kitabu nilichokielezea hapo juu nimekikuta kwenye makabrasha flani na nimekisoma fasta fasta maana sikuwa na muda. Weekend hii nikipata nafasi ntakipitia tena mstari kwa mstari maana kuna vitu interesting ningependa tujadili.

Lakini pia kwa kukumbusha umewahi kutuhumu kwamba vitabu vinavyotumika mashuleni kusomeshea historia navyo vimepotosha unaweza kututajia mifano tafadhali ukiondoa huki cha CCM.
 
Hapa ndipo penye mgongano; wewe unachukulia nafasi ya Nyerere kama nafasi ya wengine; kwamba wote walitoa mchango ulio sawa. NI vizuri kwanza utambue na kukiri nafasi ya pekee ya Nyerere katika harakati za Uhuru na kutoka hapo ndipo tunaweza kuzungumzia kwa kina kabisa nafasi za wengine wote bila kujali dini, rangi, au mahali wanakotoka. Walikuweo wengi waliotoa mchango wao katika harakati za Uhuru lakini hakuna aliyekuwa na nafasi ya pekee na mchango wa pekee kama Julius Nyerere. Wazee wa Dar walijua hili, historia imerekodi hili na ushahidi wa hili uko wazi kabisa. Tukikubaliana katika hili niko radhi kabisa tushirikiane zaidi katika kuwatambua waasisi wetu wengine na michango yao mbalimbali.

Unasemaje?

Ingawa umemuuliza hili swali Mohamed Said, yeye atalijibu kivyake kama mwana historia na wengine tutalijibu kivyetu kama wapenzi na wasomaji wa historia.

Kumbuka, Mohamed Said na mwingine yoyote yule hakuna mahali amesema kuwa Nyerere hakuwa na "role" katika kudai madaraka na ukaelezwa (na mimi) alipoyapata madaraka hata mwanawe akampa jina "Madaraka". Mohamed Said anasema walioandika "historia" ya TANU na hicho kitabu kakitaja humu, hawakutenda haki amma kwa makusudi kabisa amma kwa kulazimishwa walipowaacha watu waliompokea Nyerere na watu walioanzisha vyama vya harakati za kisiasa kabla ya Nyerere na chimbuko la chama cha TANU lilianzia kwao na si kwa Nyerere kama wengi wanavyotaka iwe.

Na kila ulipojaribu kupotosha (rejea post yako #162) ukajibiwa vilivyo (rejea post #167) hukuweza kutanabahi kuwa ulipotoka au ulipotoshwa kwa uliyoyaeleza na ukashindwa kuwa hata muungwana kukiri au kuomba msamaha kwa kutaka kupotosha wengi wanaosoma humu. Japo ungerudi ukayapinga kuwa hayo uliyojibiwa si kweli ukaueleza ukweli uujuwao wewe "kwa dalili" ungetutendea haki wasomaji.

Naomba uje hapa na utuambie anaowataja Moghamed Said na nyadhifa zao kabla na baada ya kuja Nyerere Dar kuwa si kweli hawakuwepo na hawakuyafanya anayoelezea Mohamed Said na utupe mbadala. Lakini leo kuja humu na ku "twist" bila dalili hata moja uliyoileta kugaragazwa na kukufanya ubaki kinywa wazi halafu unataka kutuaminisha kipi?

Please, be real! Come with valid and concrete arguments, do not beat around the bushes.
 
Ingawa umemuuliza hili swali Mohamed Said, yeye atalijibu kivyake kama mwana historia na wengine tutalijibu kivyetu kama wapenzi na wasomaji wa historia.

Kumbuka, Mohamed Said na mwingine yoyote yule hakuna mahali amesema kuwa Nyerere hakuwa na "role" katika kudai madaraka na ukaelezwa (na mimi) alipoyapata madaraka hata mwanawe akampa jina "Madaraka".

Kama hujui kwanini anaitwa Madaraka usikisie, nina uhakika hata M. Said anajua vyema tu.

Mohamed Said anasema walioandika "historia" ya TANU na hicho kitabu kakitaja humu, hawakutenda haki amma kwa makusudi kabisa amma kwa kulazimishwa walipowaacha watu waliompokea Nyerere na watu walioanzisha vyama vya harakati za kisiasa kabla ya Nyerere na chimbuko la chama cha TANU lilianzia kwao na si kwa Nyerere kama wengi wanavyotaka iwe.

Kwani historia ya TANU iliandikwa kwenye kurasa za mawe?
 
Kama hujui kwanini anaitwa Madaraka usikisie, nina uhakika hata M. Said anajua vyema tu.

Kwani historia ya TANU iliandikwa kwenye kurasa za mawe?

Ndio hayo ninayoyasema, "hiding behind the bush" na inaonesha hukuipenda "theory" yangu ya jina la "Madaraka"? pole sana. Huyo unaemshutumu kuwa ayaandikayo kuwa "si kweli" unanirudisha kwa huyo huyo nikaujuwe ukweli. Ahsante sana, nakuomba na wewe sasa rudi kwa Mohamed Said upate ukweli.

Mohamed Said kisha jibu kuhusu kitabu wewe unauliza kama kimeandikwa kwenye mawe? Hiki hapa kimetajwa:

Tafadhali tuelewane.
Kitabu ambacho si sahihi katika historia ya TANU ni hiki:
"Kivukoni Ideological College, Historia yaChama Cha TANU 1954-1977,
Dar es Salaam, 1981."
 
Mohamed said naomba unieleze kwa nini hutaki kutueleza ilikuwaje Nyerere akapewa kadi namba moja ya TANU badala ya hao wazee wako, Ally na Abdul Sykes ambao walipewa kadi namba 2 na 3? Na ni kwa nini ulitoka Namba 4 ya Kadi ya Dossa hadi kadi 25. Hujatueleza ni kwa nini hao wengine wenye hizo kadi za 5 hadi 25 walikuwa ni kina nani?
 
Hivi Nyerere kabla ya kuja Dar alikuwa anatokea wapi?
MKJJ,
Katika kitabu "Aliye buni jina Tanzania"-Mahmoud Hamis kurasa ya 13 na 14 anaandika.."Wanao msifia Nyerere wanadeni kwa Sheikh Karuta Amri Abeid baada ya "mjadara" wa URAIA kupamba moto na kuokoa jahazi la Nyerere kiasisa lilipokuwa linakaribia kuzamana" sasa nadhani jibu unalo
 
Kigarama,

Mimi ni Muislam siwezi kutia farka katika jamii hilo ni tendo baya kabisa.

Haya nikandikayo humu ndiyo historia ya Waislam wa Tanganyika. Kuna
watu wanashangaa mbona Waislam wako nyuma hivi?

Ni uvivu wao aukitu gani? Mimi nitakuwa masuul mbele ya Allah endapo
sitosema kweli kuhusu tatizo hili la dhulma na ndiyo maana unaona nawapa
changa motowahusika wajibu. Halikadhalika ndiyo maana sikujificha jina
langu liko hapo na wengi wananijua.

Tusipuuze mambo haya.
Jamii moja kuaikalia kichwani jamii nyingine ni hatari.

Waislam sasa wanajua na ndiyo maana unasikia wasema
"Mfumo Kristo sasa basi."

Huyo unamnasihi bure hawezi kupambana na mimi kashindwa
kunijibu Nyerere yeye ataweza wapi.

Waswahili tuna msemo, "Fupa lililomshinda fisi mbwa ataliweza?"

Mohamed
Huu mjadala moto! Ila ningependa kumuomba mzee wetu Mohamed Said awe na uvumilivu kidogo,hii ni public forum yenye watu tofauti wa kila namna,mtu anaetumia lugha isiyo nzuri ampuuze tu naamini mods watakuwa wanachukua hatua haraka kulinda heshima ya mjadala huu unaofatiliwa na wanazuoni wengi hasa kutokana na heshima kubwa na upeo wa waendesha mada wakuu,Mohamed na Mwanakijiji.mjadala huu utaleta changamoto ya kuandikwa historia kwa mapana yake.binafsi sitochangia ila msomaji tu ili nisianze kuleta logic penye ukweli.walio shuhudia wakiwa na evidence wapo! Tuheshimu huu mjadala kama reference muhimu ya vizazi vijavyo.Asante wadau wote mnaoendelea kutoa elimu.
 
Mtazamo,

Ahsante kwa kututia hima.

Insha Allah tutaendesha mnakasha wa kistaarabu
kwa faida ya nchi yetu na vizazi vijavyo.

Mohamed
 
Mohamed said naomba unieleze kwa nini hutaki kutueleza ilikuwaje Nyerere akapewa kadi namba moja ya TANU badala ya hao wazee wako, Ally na Abdul Sykes ambao walipewa kadi namba 2 na 3? Na ni kwa nini ulitoka Namba 4 ya Kadi ya Dossa hadi kadi 25. Hujatueleza ni kwa nini hao wengine wenye hizo kadi za 5 hadi 25 walikuwa ni kina nani?

Kigarama,

Sijakataa kueleza kwa nini Nyerere alipewa kadi na. 1. Wewe hujanijua? Sipigiwi nacheza leo mganda unaniletea uwanjani kwangu si itakuwa hatari ingawa salama!:
"Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANUna kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilishataifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANUulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ilekadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie. Kutokamfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha zaTAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykeskwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kamaafisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwemnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wenginewalipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa beiakapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Azizkadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendokutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. BibiTiti kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25."

Mimi nikijuana na Dome Okochi Budohi. Katika kitabu kuna picha yangu na yeye tumepiga nyumbani kwake Nairobi, Ruiru mwaka 1972. Huyu kasi yake ni na 6. Nimepata mengi sana kuhusu siku za awali za TANU. Yeye alikamatwa baada ya "Operation Anvil" iliyowakumba Wakenya wote Afrika Mashariki waliotuhumiwa kuwa na Mau Mau na akarudishwa Kenya akafungwa Lamu. Baada ya uhuru alitolewa na akafanya kazi katika gazeti la Argus Uganda. Kwa masikitiko sana anasema alijitahidi sana kukuonana na Nyerere kila akija Nairobi kwa kumtumia ujumbe na kuomba wakutane. Kumbuka hawa wote walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU, wanaharakati lakini Nyerere alikataa kuonananae. Hivi ni katika vitu vilivyokuwa vikinishangaza wakati naandika kitabu cha Nyerere kujiweka mbali na watu alioanzanao harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Yako mengi taratibu tutaeleweshana Insha Allah.

Mimi sielewi mantikii ya wewe kudonoadonoa majina ya watu badala ya kuyaweka hapa yote. Kama umeweza kuandika paragrafu zote hizo kwa nini inakuwa ngumu kwako kuandika majina ya watu 25 TU? Halafu mbona kama la watu kusahau watu walioanza nao kitu si jambo maalum kwa Nyerere peke yake bali ni tabia za wanadamu wengi tu.Unajua kwamba lowassa na Kikwete hawako kama vile walivyoanza?

Kutafuta habari za mtu aliyesifiwa sana au aliyechukiwa sana ni kawaida ya waandishi wadadisi na kwangu mimi ni jambo jema. Tofauti yangu na wewe kwenye hili jambo ni pale unapotaka kuonyesha kwamba Nyerere "ubaya"wake ulitokana na chuki yake dhidi ya waislamu jambo ambalo si la Kweli.
 
MKJJ,
Katika kitabu "Aliye buni jina Tanzania"-Mahmoud Hamis kurasa ya 13 na 14 anaandika.."Wanao msifia Nyerere wanadeni kwa Sheikh Karuta Amri Abeid baada ya "mjadara" wa URAIA kupamba moto na kuokoa jahazi la Nyerere kiasisa lilipokuwa linakaribia kuzamana" sasa nadhani jibu unalo
Karuta Amri Abeid alimtetea Nyerere kwa sababu aliona Nyerere ni dhaifu au alimtetea Nyerere kwa sababu aliona wenzake hawajui thamani aliyokuwa nayo Nyerere?
 
Najua kuna watu wanatafuta "mema" ya Hittler na kiuhalisia kabisa lazima yatakuwepo, lakini vilevile kuna watu wanafanya utafiti kuyavumbua "makosa" ya Yesu Kristo na Mtume Mohamed (S.W.A). Watu kama Salman Rushdie ni watu wanaofanana na wewe Mohamed Said katika kuonyesha upande wa pili wa ama wa mtu aliyependwa sana au aliyechukiwa sana.
 
Kigarama,

Samahani sikuelewa kama ulikuwa unataka niorodheshe majina na kadi moja baada ya nyingine.
Niwie radhi sina majina hayo na nambari kadi zao hizo nilizoweka ndizo nilizoweza kupata. Niwie
radhi.

Kigarama,

Usiulize swali kwa hamaki. Hebu soma jinsi ulivyoniuliza utadhani tunagombana kumbe toko jamvini
tunafanya mnakasha. Nakuwekea wanachama waliohudhuria mkutano wa kwanza:

Mkutanowa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia,Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani,Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, IddiFaiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo...

Mohamed
 
Kigarama,

Samahani sikuelewa kama ulikuwa unataka niorodheshe majina na kadi moja baada ya nyingine.
Niwie radhi sina majina hayo na nambari kadi zao hizo nilizoweka ndizo nilizoweza kupata. Niwie
radhi.

Kigarama,

Usiulize swali kwa hamaki.
Mohamed bwana. Mimi nilidhani tabia yako ya kusingizia watu mambo itaishia kwa Nyerere peke yake kumbe hata kwangu!!?? mimi sijahamaki bali nilishangaa kadri mjadala unayvoendelea maswali ya msingi unayaruka.
Ila unanishangaza sana. Uwezo wako wa kupata habari za wale "waliotelekezwa, kudhulumiwa" na Nyerere unavuka mipaka hadi Kenya lakini likija suala la Heri kwa Nyerere kumbukumbu zake hakuna.
 
Najua kuna watu wanatafuta "mema" ya Hittler na kiuhalisia kabisa lazima yatakuwepo, lakini vilevile kuna watu wanafanya utafiti kuyavumbua "makosa" ya Yesu Kristo na Mtume Mohamed (S.W.A). Watu kama Salman Rushdie ni watu wanaofanana na wewe Mohamed Said katika kuonyesha upande wa pili wa ama wa mtu aliyependwa sana au aliyechukiwa sana.

Kigarama,

Unasemaje ndugu yangu. Umewaona wazee wangu?
Huna lolote la kusema kuhusu wazalendo hawa ila
kuweka mambo nje ya mada?

Unadhani walioikwepa historia hii walikuwa wajinga?

Inatisha.

Wazalendo wale hawakuwa watu wa kawaida...
Hapo Amiri Kweyamba (Special Baranch) anarandaranda
kuwachimba.

Hapo zinamwagwa dua na makafara utaogopa wewe.

Basi pitisha mchango uone ari waliyokuwanayo...

Mama Daisy anasimulia ananambia, "Baba yako alikuwa na
kabati lake la fedha basi wakija watu wa TANU yeye anaingia
ndani na kutoa tu...namwambia Bwana Abdu taratibu bwana
taratibu...wala hanisikii... hadi uhuru umepatikana. Alhmdulilah..."

Leo TANU inaandika historia yake Abdulwahid Sykes katupwa nje!
Jamani kweli tukae kimya tukisema Oh huo uchochezi, Oh huo udini...

Hili haliwashangazeni kuna nini hapa. Anaandikwa Abdulwahid na
mchango wake katika kudai uhuru wa Tanganyika magazeti
yanakusanywa yanapigwa moto.

Mohamed
 
mohamed said,
mimi nilipata kumfahamu marehemu Saleh Massasi,sikuweza kumuuliza haya ninayosoma humu sababu nilikuwa siyajui.UMESEMA kwamba alikuwemo kwenye msafara wa kutafuta hela za chuo wa EAMWS kwa dhumuni la kuwaendeleza waislam-mbona huyu mzee ambaye alikuwa ni mcheshi sana,kila akitoka msikitini usimama kijiweni na UMSIFIA sana Nyerere?????
 
SOA

Saleh Masasi (Mungu amsamehe) ndiyo waliomsaidia Nyerere kuivunja EAMWS.
Huwa napata tabu sana kuzungumza juu ya hawa watu khasa kwa kuwa wako
mbele ya haki.

Mohamed
 
Mohamed bwana. Mimi nilidhani tabia yako ya kusingizia watu mambo itaishia kwa Nyerere peke yake kumbe hata kwangu!!?? mimi sijahamaki bali nilishangaa kadri mjadala unayvoendelea maswali ya msingi unayaruka.
Ila unanishangaza sana. Uwezo wako wa kupata habari za wale "waliotelekezwa, kudhulumiwa" na Nyerere unavuka mipaka hadi Kenya lakini likija suala la Heri kwa Nyerere kumbukumbu zake hakuna.

Niwie radhi nilipata hisia kama umehamaki.
Tafadhali niulize tena hilo swali Insha Allah
kama nina majibu nitakupa.

Mohamed
 
Karuta Amri Abeid alimtetea Nyerere kwa sababu aliona Nyerere ni dhaifu au alimtetea Nyerere kwa sababu aliona wenzake hawajui thamani aliyokuwa nayo Nyerere?

Swili halikuwa "udhaifu" wa Nyerere hata kidogo..Mwanakijiji aliuliza "Nyerere alitokea wapi" angalia kwenye post yake
Labda Mzee Muhamed Said akiona inafaa basi atalizungumzia hili au umuombe afanye hivyo
 
SOA

Saleh Masasi (Mungu amsamehe) ndiyo waliomsaidia Nyerere kuivunja EAMWS.
Huwa napata tabu sana kuzungumza juu ya hawa watu khasa kwa kuwa wako
mbele ya haki.

Mohamed
Kwa tafsiri yangu inaonyesha mambo ya Saleh Masasi huwezi kuyazungumza kwa sababu yuko mbele ya haki kwa maana kwamba amefariki. Kama kifo ni kuwa mbele ya haki ina maana Nyerere unayemzungumza kila uchao na uchawao na usiku kucha yeye hayuko mbele ya Haki?

Au kuwa mbele ya haki ni kwa Waslamu peke yao? kama kwenye maandishi yako unadai kwamba Nyerere ndiye aliyeivunja EAMW kwa msaada wa watu wengine, kati ya hao watu wengine waliomsaidia Nyerere kuivunja EAMW, wazee "wako" waliopigania Uhuru na kuanzisha TANU hawamo. Historia yao hiyo pia imesahauliwa?
 
Back
Top Bottom