Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Avriel,
Unataka kufanya mjadala katika somo usilolijua na ndiyo maana hata kuandika kwako kuna shida.

Katika uandishi dot zinakuwa tatu...
Jifunze uandishi soma ndiyo uingie katika mijadala.
 
Na kweli, penye ukweli uongo hujitenga. Mnakasha huu uliwafungua wengi macho na nawapa asante nyingi wote mlioshiriki kutoka pande zote...hii nayo itabaki kuwa historia iliyoandikwa na wengi hapa jamvini, JF idumu! Mungu awabariki!
 
Avriel,
Unataka kufanya mjadala katika somo usilolijua na ndiyo maana hata kuandika kwako kuna shida.

Katika uandishi dot zinakuwa tatu...
Jifunze uandishi soma ndiyo uingie katika mijadala.
Ndio umejibu hoja hivyo?
Aliekuambia Mimi mwandishi mzuri nani?
Bila shaka ukiachilia mbali huo uzuri wa uandishi umeelewa nilichoandika tena kwa kiswahili kisichokosewa, achana na nukta mia au elfu .........
Waislam wanapenda kulalama sana nchi hii wakati madhira ya uongozi mbovu nchini huwaathiri watu wote bila kujali dini zao,sasa mnashangaza mnapotaka kujiona ninyi ni maalumu kwa dini yenu kuliko wengine ndani ya nchi......ni ukweli usiofichika kuwa mna ajenda za kimkakati kuhakikisha mnachukua hatamu ya kidola ili mtimize matakwa yenu, jambo hilo ndilo linawatia hofu watanzania wengi wenye kuwatizama kwa jicho la tatu.

Tambueni ya kwamba taifa hili lina wananchi wengi Wa imani tofauti tofauti nanyi sio special kuliko wao na ni asili ya imani zao tu kutokulalama ndio maana kuna mambo mnayalazimisha hamuwaoni wakiwajibia bali wanawatizama tu muendelee na mikakati yenu kwani kufanikiwa kwayo ni kazi isiyo nyepesi.
 
Hakika!
Na kweli, penye ukweli uongo hujitenga. Mnakasha huu uliwafungua wengi macho na nawapa asante nyingi wote mlioshiriki kutoka pande zote...hii nayo itabaki kuwa historia iliyoandikwa na wengi hapa jamvini, JF idumu! Mungu awabariki!
 
Mimi ni Wa kike, napenda kukusahihisha hapo kidogo.
Hakuna MTU anaepingana na historia ya kweli hata kidogo tena unatupatia fursa ya kujifunza mengi ambayo hatukupata kuyasoma mashuleni, unachopingwa hapa Mzee Mohammed Said na maandiko yako kuyaelekeza zaidi katika dini yako na hisia nyingi ambazo hazina usahihi ya kwamba watu Wa dini yako wanakandamizwa, wakati huo uovu unaotendwa na viongozi madhara huwafikia watanzania wote bila kujali dini zao.......
Mnatoa wapi hizo hisia hasi?
 
Ni kweli masheikh na maustadhi walisaidia taifa kwa kupigania Uhuru na mapadri na wachungaji hawakufanya hivyo....
Tueleze sasa tufanyeje juu yao?
Watu wabadili imani waingie kwa masheikh?
Tunawashukuru waarabu walioleta utamaduni wao kwetu tukapata imani ya dini wakapatikana wananchi Wa imani hiyo waliopigania Uhuru na historia ikaandikwa nao wakamchagua mzanaki kutoka butiama kuongoza taifa kwa niaba yao...
Asanteni sana sasa ni taifa huru kabisa.
 


"Katika hotuba hiyo Chief Kidaha alikuwa anaishauri serikali ya Kiingereza kuondoa ile sheria ambayo ilikuwa inawapiga marufuku Waafrika wafanyakazi wa serikali kujishughulisha na siasa"
Kumbe hata mzungu alikataza wafanyakazi wasijishughulise na siasa!!! Hatari saaaana
 
Avriel,
Unauliza ufanyeje kwani kuna mtu amekuambia ufanye jambo?
Wala hii historia haina uhusiano wowote na Waarabu.

Wala Tanganyika haikuwa huru leo.

Lakini kwa kuwa umetaja uhuru wa Tanganyika sasa nitakuambia
kwa mara nyingine tena.

Hakuna jamii inayoweza kukubali kufutiwa historia yake.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilipoandikwa na Chuo
Cha CCM Kivukoni historia hii ilifuta mchango wa wazee wangu hiki
ndicho kilichosababisha mimi kunyanyua kalamu na kuandika historia
ya kweli ya TANU kama nilivyohadithiwa na wazee wangu na kwa
msaada wa nyaraka na picha.

Sasa wewe unauliza ufanyeje.
Jibu lako ni hili.

Unaposoma sisi tunawaadhimisha wazee wetu na kutukuza mchango
wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika wewe kaa kimya kwa kuwa
huijui historia hiyo kwa hiyo huna sababu ya kutia neno lako kupinga
labda sana sana uliza maswali kwa yale ambayo hayako wazi kwako.

Wajaluo Kenya hawawashambulii wala hawaghadhibiki Wakikuyu
wanapomuadhimisha Dedan Kimathi na Mau Mau.

Sasa wewe usighadhibike unapomsoma Sheikh Hassan bin Ameir
katika historia ya TANU au unapomsoma Sheikh Suleiman Takadir
au Sheikh Yusuf Badi au Sheikh Abdallah Rashid Sembe.

Usighadhibike kwani hawa ndiyo waliokuwa bega kwa bega na Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
katika TAA kisha TANU
na kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Ndio maana tulidai uhuru toka kwa mkoloni ili tuwe uhuru...siyo tumtoe mkoloni mweupe tumwingize mkoloni mweusi!
 
Ndio maana tulidai uhuru toka kwa mkoloni ili tuwe uhuru...siyo tumtoe mkoloni mweupe tumwingize mkoloni mweusi!
Huu mnakasha ni adimu sana. Ndio maana napitia madini ya huyu babbu kila nipatapo wasaa. Tumetoka mbaaaali sana. Ila fikra zetu bado zinatawaliwa na mawazo ya wale tuliowang'oa
 
Mohamed,

Waislam siku zote lazima wahisi kuwa wanadhulumiwa kwa sababu:

1. Uislam sio dini tu, bali ni mfumo wa kisiasa pia. Uislam unataka ushike dola ndo ukamilike. Kama dola sio ya Kiislam Uislam hauwezi kukamilika. Kwa hiyo kwenye nchi yoyote ambayo Uislam haujashika dola, Waislam lazima watajiona wanaonewa.

2. Kudhani Quran ndo kila kitu. Kuna Waislam wengi wana mtazamo wa kwamba Quran ndo kila kitu. Kwamba ina elimu yote inayotakiwa kwa binadamu kuweza kuishi na kufanikiwa. Hili linawaletea ufukara Waislam wengi maana wanapitwa na elimu bora zaidi ambazo zingeweza kuwasaidia kwenye maisha yao. Hili huwa ni tatizo zaidi pale ambapo elimu mpya inapokinzana na Quran.
 
Dadi...
Hapana hulifahamu tatizo hiki si kitu ambacho wewe unaweza ukafanya mjadala wa maana.

Inataka kwanza uisome historia ya Tanganyika kabla na baada ya uhuru ndipo utaelewa tatizo lenyewe.

Serikali inatambua tatizo hili.
 
Dadi...
Hapana hulifahamu tatizo hiki si kitu ambacho wewe unaweza ukafanya mjadala wa maana.

Inataka kwanza uisome historia ya Tanganyika kabla na baada ya uhuru ndipo utaelewa tatizo lenyewe.

Serikali inatambua tatizo hili.

Hamna kitu kama hicho. Fanya toba umrejee mola wako salama. Usitake kutuharibia amani nchini mwetu kwa propaganda za kipuuzi.
 
Mohamed Said anataka tuiamini zaidi Historia isiyoandikiwa, hadithi alizosimuliwa zaidi na wazee wake, ni vigumu sana kuiamini Historia ya aina hiyo hata kama kuna ukweli fulani kwenye maelezo yake ya Historia na kasoro nyingi kwenye Historia yenye mkono wa TANU.
 
Hukumsikia nyerere alichoeleza aliongea na wazee wa dar,kwamba wengi walikua waislam,mkiristu yeye na rupia tu,na Mara moja moja Nani sijui
 
Basi leteni ya ukweli bila chenga

Hivi walioandika kuwa red indians waliuwawa na nchi yote kuchukuliwa au Aborigines wa Australia kumalizwa
Halafu wakaja watoto wasooijua historia wakasema ilikuwa ya kutunga hamjui wengi wataamini kweli walitunga?

Hata leo kuna watu hawaamini kama vita ya kwanza na ya pili iliwahi kutokea unabisha Google

Wengine wanabisha kuwa holocaust haikutolea na hakuna wayahudi waliuwawa

Kila mmoja aamini anachoamini maana wengine wamezaliwa juzi juzi na dini wanazikataa pia kutwa unaambiwa leta ushahidi
 
Huyu mzee amejaa hila na ni tapeli mkubwa! Binafsi namchukulia kama mhalifu ngazi za kina Osama
 
Huyu mzee amejaa hila na ni tapeli mkubwa! Binafsi namchukulia kama mhalifu ngazi za kina Osama
Mzizi...
Kuna ibra moja kubwa sana katika historia hii.

Kuna wanaonisikiliza nikilimaza wakati wa maswali huonyesha mshangao kuwa imekuwaje historia ya ukombozi wa nchi ikabadilishwa (doctored) na ikawekwa historia nyingine ambayo kwa miaka mingi ikawa inasomeshwa shuleni na vyuoni?

Mimi hutoa majibu.

Lakini wapo wengi kutoka hapa nyumbani historia hii huwatia ghadhabu kiasi hutoa matusi, vitisho na kusema maneno yasiyopendeza.

Mara ya kwanza mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London) lilipochapa makala yangu ''In Praise of Ancestors,'' ambayo ndani nilimtaja Abdul Sykes, Ally Sykes, John Rupia, Saadan Abdu Kandoro na Al Jamiatul Islamiyya katika harakati za TANU toleo zima la gazeti lilikusanywa.

Toleo lililofuatia ikachapwa makala kutoka kwa Dr. Mayanja Kiwanuka wa CCM Dodoma iliyojaa kebehi na vitisho dhidi yangu.

Alihitimisha kwa kunitukana na kuniita ''pygmy.''

Matusi, kejeli na vitisho yote nimeyakusanya kwa kipindi cha miaka 20 na In Shaa Allah iko siku tutayachapa hapa barzani.

Mzizi...ananiita ''tapeli mkubwa,'' ''mhalifu.''
Akili imemruka anatoa matusi na haya ni kawaida kwa mtu aliyeghadhibika.

Hawezi kufikiri hadi atulie na akili yake irejee.
Hujiuliza kwa nini wanakasikrika kwa mimi kuandika historia ya wazee wangu?

Nini kinawachoma?
Wangependa kama historia hii nisingeiandika na tukawa na historia ambayo haina ukweli?

Hiki ndicho kiichokusudiwa mwanzo walipofuta historia ya kweli ya TANU na kupachika nyingine?

Sasa historia ya kweli ipo.
Tufanyeje?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…