Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Avriel,Sijui ni mods au nini kinatokea thread michango yangu inafutwa hapa..
Sio mbaya
Nashauri ufanye uchunguzi wa kitaalam kujua kwanini wanafunzi wanafeli nadhani kifeli kwao hakuna uhusiano na dini zao..
Mmekuwa na viongozi wengi tena wasomi wa hiyo dini yenu sijajua kwanini hawaoni hayo unayaoyaita malalamiko ya dhuluma dhidi ya dini yenu
Mimi binafsi niwe mkweli, nawachukulia watu wa dini ya kiislam Tanzania kuwa ni walalamikaji sana na wasioridhika daima mpaka washike hatamu ndipo watajiona hawaonewi, wakati huo nchi ina makundi mengi ya kidini sijawahi ona wakilalama kama waislam, halafu sizioni hizo fursa za kiuchumi, kijamii au kisiaasa anazopata MTU kutokana na kuwa wa dini ile au hii kikubwa nayaona madhira ya watanzania kukosa huduma stahiki hayabagui dini, watu hawana maji, madawa hospitalini, shule hazina vitendea kazi, wafanyakazi hawana malipo mazuri, na kadhia nyingine nyingi bila kujali dini...
Sasa hii dhana ya dhuluma kwa waislamu bado inanitia mashaka sana wakati huo hao waislamu ndio wamekuwa wakipewa Mali za serikali kwa upendeleo, sijaona wasabato wakipewa majengo bure waanzishe chuo kikuu bali waislamu hupewa, sijawahi ona ndani ya taasisi ya kiislamu kuna MTU wa dini nyingine atapewa Uhuru wa kuabudu bali wailasmu wamepewa misikiti ndani ya majengo ya wakristo, ni ikitokea kuna taasisi ya serikali kiongozi wa juu ni muislam basi tegemea atakoleza ajenda ya kuwakusanya waislamu toka pande zote wafanye kazi kwenye taasisi hiyo na watajitahidi hata kama kuna msikiti mita mia mbili kutoka ofisi iliko watataka humo ndani ujengwe mwingine na zifuatwe sheria za kiislam eneo hilo....
Huu ndio uislam ninaoushuhudia mtaani niishipo....
Teteeni imani zenu msikandamize wengine kwa hila ya aina yoyote, suala la imani MTU halazimishwi ni Uhuru wa kuchagua, na wakati mwingine MTU anaweza iga imani kwa kufurahishwa na matendo ya muumini....Mungu akiamua kuwataka watu wawe wa imani Fulani hakuna force ya nje itakayozuia...ishini kwa upendo...
Unataka kufanya mjadala katika somo usilolijua na ndiyo maana hata kuandika kwako kuna shida.
Katika uandishi dot zinakuwa tatu...
Jifunze uandishi soma ndiyo uingie katika mijadala.