Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

mimi nimesoma sana historia hii.nashangaa wanakuja watu wanasema historia hii uongo oooh wazee wake!! sasa historia hii kama kweli unaiona sio ya kweli leta zenu na facts tusome tuone nan kasema sio sahihi!! naona kinachouma watu hapa kinajulikana hutuwez kujidanganya nafsi zinajua shida ipo wap hapa wote tunajua."yaliyo nyoyon ni mabaya kushinda wadhihirishayo"
kama historia na facts za Mohamed said unayepinga unaona sio leta facts zako .hivi ni vitu vya kielimu.ukipinga sema wewe sasa ipi ya kweli sio kukaa tu analeta historia ya wazee wake ooh nin ukiulizwa leten bas zenu tuone mnagwaya gwaya.
 
Hakuna mahali katumia neno "Uislam", hilo sasa lako wewe unatulisha "tango pori". Rudia kusoma uje na neno sahihi alilotumia Mohamed Said.

Nini kilichoumiza mpaka unabadili maneno?
 
Julai...
Hawawezi kuwa na hstoria nyingne ya African Association.
Hstoria hii ni moja na inatoka mbali sana na hawa wazee waasisi walioko leo ni vitukuu.

Angalia pcha hiyo hapo chini ni mimi na Kleist Abdul Sykes.
Babu zetu wakati wanaasisi African Association 1929 walikuwa na umri wa miaka ya katikati 25.

Mimi na Kleist mwenzangu ametangulia mbele ya haki hapo tunapiga hii picha ya kwanza sote tayari tulikuwa na wajukuu.

Picha ya pili wa kwanza kulia ni mimi na Kleist ni watatu.

Huu ulikuwa mwaka wa 1968 miezi michache baada ya baba yake Kleist, Abdul Sykes kufariki.

Watoto wetu sisi wameijua historia hii kwa kutusikia sisi baba zao tunaihadithia kutoka kwa baba na babu zetu.

Hawa hawawezi kuwa na kumbukumbu hizi.
Wazitoe wapi?


 
Hakuna mahali katumia neno "Uislam", hilo sasa lako wewe unatulisha "tango pori". Rudia kusoma uje na neno sahihi alilotumia Mohamed Said.

Nini kilichoumiza mpaka unabadili maneno?
Rudia kusoma kwa makini andiko langu la hujalielewa fuatilia tena kwa makini mjadala toka mwazo.

Ahsante.
 
Rudia kusoma kwa makini andiko langu la hujalielewa fuatilia tena kwa makini mjadala toka mwazo.

Ahsante.
Kaangalie wewe uoneshe wapi Mohamed Said kaandika "Uislam"?
Kwanini ubadilishe maneno, ni walewale tu msopenda kusikia au kusoma neno Waislam.

Wewe tuelezee hapa, wazee wako wana historia ipi kudai uhuru wa Tanganyika? Mohamed Said ndiyo kishaandika historia ya wazee wake, sasa wewe weka ya wa kwako, wacha porojo.
 
Maalim Faiza,
Hawakuwako na ndiyo sababu wakaamua kuifuta historia ya wazee wetu.
Sisi tuna kila aina ya ushahidi kuanzia nyaraka hadi picha.

Wala sisi hatawalaumu wao kwa nini hawakuwako.
Tusingeweza sote kufanya jambo lile.

Huyo hapo chini Ali Msham na Mwalimu Nyerere.
Alitoa nyumba yake kuwa ofisi ya TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hakupata kujulikana Ali Msham hadi nilipoandika historia yake.

 
Dada Foxy naona kama imekupa shida kidogo no need to panic. Tukisema hoja za unayemtetea zina shaka mnalipuka nashangazwa na wewe kuuliza swali kama hilo.

Si mara moja wala mara mbili anatumia neno hilo katika kujibu hoja mbali mbali za wanabodi

Kuna kingine labda?
 
Kuna watu kama marehemu Lupembe na Rupia hawa walikuwa wafanyabiashara wakubwa kabla ya Uhuru na walichangia kiasi kikubwa safari ya Nyerere kwenda UN lakini huwa sisikii wakitajwa
 
Kuna watu kama marehemu Lupembe na Rupia hawa walikuwa wafanyabiashara wakubwa kabla ya Uhuru na walichangia kiasi kikubwa safari ya Nyerere kwenda UN lakini huwa sisikii wakitajwa
Rod...
Kitabu cha Historia ya TANU kimeshaandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni na Abdul Sykes hakutajwa.

Haishangazi kuwa Rupia, Lupembe na wazalendo wengine hawamo.
 
Barubaru,
Miaka mingi imepita na mjadala huu haujapata kutokea.

Waliingia watu wengi kuja kunijibu.

Uwanja ulijaa.
Tulifanya mjadala kwa miezi sita mfululizo watu wanokaribia 1m walishiriki.

Hivi sasa uwanja ni mtupu watu wanokuja kukabiliana na mimi ni wachache sana.

Nimebakia peke yangu uwanjani.

Walidhani mimi nafanya maskhara nilipowaambia kuwa historia ya Waislam katika kuuunda AA, TAA, TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ni ya kipekee.

Wengi hawakuniamini lakini jinsi mjadala ulivyokuwa unaendelea na mimi kuwa nakuja na vitu vipya kila ninaponyanyua kalamu akili zao za ndani zikawa sasa zinauliza iweje hapa tunaona picha na maelezo yanoyofanana na picha na kubwa hii historia haikuwa inafahamika?

Leo ukweli umedhihiri kuwa historia iliyokuwa inachukuliwa kuwa ndiyo historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika siyo.

Hii ndiyo sababu ya kuandikwa kitabu cha Julius Nyerere, ''Nyerere Biography'' na jopo la waandishi wasomi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakiongozwa na Prof. Issa Shivji.

Penye ukweli uongo hujitenga.

Mtu akikuonyesha fimbo yake iliyopindika akasema fimbo hiyo imenyooka jibu lake si kupigizana makelele kwa kubishana.

Jibu ni wewe kumwonyesha fimbo yako iliyonyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…