Kwa wale wanaopinga maneno ya MS tunaomba watoe ushahidi wa VITENDO ambavyo Nyerere alivifanya kuwatendea HAKI Waislamu.
Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini Wakristo ndiyo walikuwa wanaongoza ktk Idara Serikalini?
Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini kila Waziri ktk wizara ya Elimu alikuwa Mkiristo?
Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini Wakristo wanamwita "Mtakatifu" kwa kumpa fadhila alozowafanyia?
Kama Nyerere hakuwa MDINI mbona mnakasirika akiambiwa MDINI?
Mkuu hapa hatutafuti kuamini rai za mag3 na kukataa za sheikh mohamed. Kinachotafutwa hapa ni ukweli kutoka katika masimulizi ya hao wote pamoja na wachangiaji wengine.
Kama kuna ukweli ndani ya maelezo ya mag3 tunauchukua na kama kuna upotoshaji tunaachana nao. Vivyo hivyo kama kuna ukweli kwenye masimulizi ya sheikh mohamed tunauchukua na kama kuna upotoshaji tunaachana nao.
We are just looking for the facts!
Nyie hivi mnaona kuwa Mag3 anasimulia? Mbona hamumuulizi yeye simulizi zake na matusi juu, ni kama nani? "Credibility issue", mtu ambae anaficha hata jina lake, wasifa na wadhifa wake mnamuamini kuliko aliyejitambulisha yeye nani na anafanya nini?
Faiza,
Mag3 ameshalitolea maelezo swali lako la kutaka ajitambulishe kwa majina yake halisi kama alivyofanya sheikh mohamed. Na hata wewe umeulizwa swali hilo hilo na ukalitolea maelezo. Kwa jinsi ulivyojieleza na jinsi mag3 alivyojieleza, maelezo yenu yamefanana, kwani hata wewe hatujakufahamu kikamilifu, kwani si wote tunaoishi kariakoo hadi tujue kwamba faizafoxy ndiye faiza omary ama vinginevyo!
Kwa mujibu wa taratibu za JF, kila mmoja yuko huru kujiandikisha kwa jina analolitaka. Na hapa tumekuwa tukijadili mambo mengi sana bila kutaka kufahamu majina halisi ya wachangiaji, tunachoangalia hapa ni source na credibility ya habari husika. Hakuna ushahidi wa wazi hapa JF kwamba wanaotumia majina yasiyohalisi (nicknames) kwamba si credible ama reliable source. Wala hakuna ushahidi wa wazi kwamba wanaotumia majina yao halisi ndio pekee wanakuwa credible ama reliable source.
Suala la cheo na kazi ya mwanaJF yeyote si lazima aviseme hapa, ni hiari yake kama akiamua kujitambulisha ama kutojitambuylisha hiyo si hoja ya msingi ya kujadili hapa. Kama unadhani hiyo ni hoja ya msingi, hapa si mahali pake, unaweza kuifungulia thread na utapata majibu yake. Ni vizuri ukafahamu kuwa si suala la kumuamini huyu na kutomuamini yule. Tunachotafuta hapa ni "facts" kutoka kwenye masimulizi yao. Mambo yanayosemwa hapa si kwamba yote ni mageni masikioni mwetu bali kuna baadhi ni mageni na ndiyo hayo tunayotaka yajisimamie kwa ushahidi madhgubuti ili tuweze kuyaamini na kuyapokea.
Mwanakijiji,
Nina hakika hadi hapa tulipofika mimi na wewe USHANIJUA usitegemee mimi kubishana na wewe staili ya nipe nikupe. Mimi ukiniuliza swali nakwenda kwenye picha kubwa na kutoa jibu nikikusudia hasa jibu lenyewe linufaishe.
Nadhani muda wote tumekaa jamvini umeona kuwa mimi situmii maandishi ya wasomi wengine natumia maandishi ya mkono wangu. Hii ndiyo tofauti kubwa kati yangu na wengine walioingia katika mnakasha huu.
Mimi nia yangu si nikushinde, la hasha. Nia yangu kubwa ni kukupa kile ambacho kwako ni kigeni lakini zaidi ya hapo kukufahamisha kuwa somo langu nalijua vyema.
Nadhani umeona hapa mtu atasema Nyerere aliandika katiba ya TANU nitamjibu kiungwana kabisa kuwa hilo si kweli katiba walinyanyambua ya CPP ya Nkrumah, atasema mwingine, wazee wako walikuwa hawana taarifa za Meru Citizens Union nikamjibu Kirilo akija Dar es Salaam mwenyeji wake Abdulwahid Sykes na nikasema nimesoma barua za Sablak kwenye nyaraka za Sykes.
Mwingine anasema Nyerere kaasisi AA Tabora nikasema si kweli nikatoa ushahidi na majina ya walioanzisha na ili kutoweka upasi nikamuhakikishia kuwa najua hilo kosa amefanya kwa bahati mbaya kwa kutokujua. Nimekwenda hata katika "anectdotes" za siku hizo hii yote kuwahakikishia wanaonisoma kuwa somo langu nalijua vyema.
Kubwa ambalo ndilo limewachanganya baadhi ya wanaukumbi hotuba ya TANU Umoja wa Mataifa 1955 nimeotoa habari zake na nimetoa hata rejea ya Pratt na nimeeleza kuwa hotuba ile imenyofolewa katika jalada Maktaba ya CCM Dodoma, na microfilm TNA imepotea nk. nk.
Mimi si mtu wa nipe nikupe majibu ya karaha na hamaki. Ingelikuwa mimi ni mtu wa nipe nikupe mnakasha huu ungelikuwa umekufa siku nyingi sana.
Umushudiwa natukanwa. Mfate psychoanalyst yoyote mueleze kuhusu mtu anaetoa matusi kumtukana mtu anaefanyanae majadiliano atakuambia ni dalili kuwa hana cha kueleza.
Mimi haya kanifunza Maalim Haruna kwenye madras. Nishamueleza shiekh wangu hapa ukumbini mara nyingi na mafunzo nlopata kwake kuhusu adab. Alikuwa akisema, "Mohamed kaa ukijua ukitoa tusi kumtukana mtu basi jua umenitukana mimi."
Mwanakijiji nimechukua muda kukueleza haya yote kwa kuwa nafsi yangu Imekupenda kwa kuwa nimetambua una hamu ya kujua mambo na kama ni hivyo hii elimu niliyonayo mie katika historia ya Tanganyika ni amana yako lazima nikupe wakati wowote ukiitaka lakini ili niweze kukupa na wewe uwe mwanafunzi mzuri.
Mohamed
At least mimi umenijuwa natoka Kariakoo, na naitwa Faiza na nyumbani kwetu ni wapi, Jee Mag3 ameeleza hayo au kasema hizo Mag ni herufi za majina yangu matatu? Unanchekesha, anyway, tuachane na haya turudi kwenye mada, nimejifunza jambo moja zuri kutoka hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anchi-miaka-50-ya-uhuru-wa-tanganyika-43.html
Mwita Maranya, naona tunatoka nje ya mjadala na mada husika na sidhani kama hii inakusaidia wewe au mimi kuijuwa Tanzania imetoka wapi, iko wapi na inakwenda wapi. Naomba sana tuache kujadili yetu binafsi na turudi kwenye mada, mimi nakupa ushindi kwa yote, wewe ni hodari sana na unastahili kila sifa, hongera sana, sasa turudi kwenye mada.
Dhulma zipi? maana unajibu kitu unachoulizwa, kama hakuna swali au hoja unatoaje majibu.
Ndiyo maana mimi huweka ushahidi wa kuthibitisha Mzee Said ana chuki au ni mdini. Haitoshi mimi kusema mzee Said ni mdini halafu nikutake utoe majibu.
Pili, mnamtuhumu nani ? Nyerere, Serikali, CCM au Wakatoliki. Tukishajua hapo, tuendelee kwa tuhuma zipi. Na tusiishie hapo tuambiwe nini kifanyike nini.
Hebu toa hoja moja tu kuhusu dhulma unaayohamasisha masheikh wakaieleze mikoani, halafu tupe ufumbuzi wake kwa mtazamo wako.
Lakini mzee Said, si unajua kuwa busara si la lazima kuongea hata kukaa kimya ni busara.
Nguruvi3,
"Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himayayake ambayo inahodhi 75% za viti katika Bunge la Tanzania.Kati ya viti hivyo 70% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobakivimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine."
Hebu fananisha ingekuwaje kama Waislam wangehodhi 75% na Wakristo 25% mngeliweza kustahamili?
Hii ndiyo dhulma tuipigiayo kelele na tumezunguka nchi nzima kuwaeleza Waislam kuwa wakati wa kuondoa hii dhulma umefika.
Vyombo vya habari chini ya mfumokristo umetupiga "blackout."
Mohamed
Let us assume kuwa 'nidhulma kama unavyodai', solution gani unapendekeza ili kuondoaNguruvi3,
"Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himayayake ambayo inahodhi 75% za viti katika Bunge la Tanzania.Kati ya viti hivyo 70% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobakivimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine."
Hebu fananisha ingekuwaje kama Waislam wangehodhi 75% na Wakristo 25% mngeliweza kustahamili?
Hii ndiyo dhulma tuipigiayo kelele na tumezunguka nchi nzima kuwaeleza Waislam kuwa wakati wa kuondoa hii dhulma umefika.
Vyombo vya habari chini ya mfumokristo umetupiga "blackout."
Mohamed
OPPORTUNITY COST ya hii kitu ni ELIMU ambayo wanafilosopia wanasema ni ufunguo wa maisha
Brother MS,
Hiyo nukuu/argument hapo juu.....its too low and weak ku-rely upon...........unless useme na uthibitishe kuwa watu walikuwa wakilazimishwa kuchaguwa wakristo........
Ukiangalia Jiografia ya Tanzania tu unaweza pia kupata jibu kwa huyo mwandishi wako uliyemnukuu............
Let us assume kuwa 'nidhulma kama unavyodai', solution gani unapendekeza ili kuondoa
initiation ceremonies put a brake on developments and at worst r degrading
Nguruvi3,
"Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himayayake ambayo inahodhi 75% za viti katika Bunge la Tanzania.Kati ya viti hivyo 70% vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobakivimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine."
Hebu fananisha ingekuwaje kama Waislam wangehodhi 75% na Wakristo 25% mngeliweza kustahamili?
Hii ndiyo dhulma tuipigiayo kelele na tumezunguka nchi nzima kuwaeleza Waislam kuwa wakati wa kuondoa hii dhulma umefika.
Vyombo vya habari chini ya mfumokristo umetupiga "blackout."
Mohamed
Hawezi kuwa na jibu hata kidogo kwa sababu hajui yeye anataka nini isipokuwa kitu gani kiondoke. Yaani kwa madai yao mfumo Kristu uondoke na hawana cha ku replace kwa sababu kwa kila utakachokiweka ni mfumo kristu kwao, as a matter of fact hata demokrasia ni mfumo kristu.Let us assume kuwa 'nidhulma kama unavyodai', solution gani unapendekeza ili kuondoa
Hawezi kuwa na jibu hata kidogo kwa sababu hajui yeye anataka nini isipokuwa kitu gani kiondoke. Yaani kwa madai yao mfumo Kristu uondoke na hawana cha ku replace kwa sababu kwa kila utakachokiweka ni mfumo kristu kwao, as a matter of fact hata demokrasia ni mfumo kristu.
Binafsi nisichokipenda kutoka kwa hawa jamaa zetu ni pale wanapoitumia dini kueneza siasa zao, nimeshamwambia Mohammed Said, Islaam ni dini inayosimama peke yake na kwa wanadamu wote, tunachogombea sote ni UTU wetu ambao uko well defined ktk kuran na mtu yeyote anatakiwa kupigania haki hizo kama binadamu. Lakini haiwezekani mtu ukapigania haki zako wewe kwa sababu ya jina lako la dini ama imani yako isipokuwa pale dini inapokatazwa...
Mfano mzuri wa Islaam ni kama demokrasia..Leo hii dunia nzima vita vinatokea kwa sababu ya kukosekana kwa demokrasia, hivyo wananchi wataidai demokrasia ilokosekana ili kurekebisha mapungufu yoyote yaliyopo ya kiutawala na sii kutazama makundi ya watu kujaribu kupendelea kundi moja ama kudhoofisha kundi jingine ili kufikia usawa wa kiutawala. Sijui kama nimeeleweka!
Wanachokiomba kina Mohammed Said, ni Udini yaani ktk siasa za kibaguzi ni kama vile kabila fulani linabaguliwa, hivyo ili nao wapate kutesa kwa zamu kama wenzao, wanataka wampate kiongozi ama viongozi wao ambao watawawezasha kubadilisha upepo wa kimfumo kutoka kabila moja kwenda lao, kama Kenya walivyokuwa wakidai Wajaluo miaka ya Kenyatta.
Kwa sura hii, Wajaluo hawakutaka hujenga Demokrasia isipokuwa ni ktk mfumo ule ule wa ukabila, yaani Wajaluo nao wanataka kushika nchi ili wawakandamize Wakikuyu wakati wao wakipanda kimaisha ili kufikia usawa...Na wala sii swala la kuwatazama wao kama wanaokandamizwa ili wawezeshwe, hapana wanachokitafuta ni kuanguka kwa Mkikuyu..Na huyo mkikuyu hawezi kukubali akielewa kwamba utawala ukiwa chini ya Mjaluo yeye ndiye atakuwa muathirika...Kinacholkiliwa hapa ni ule mfumo wa kupokezana yaani na sisi sasa ni ZAMU YETU.
Kwa hiyo, kwa mtu mwenye upeo mkubwa ataelewa kwamba kinacholiliwa hapa na waislaam njaa hawa ni kwamba ilikuwa zamu yao, pengine wakati wa Uhuru au kabla ya Uhuru na Nyerere akawanyang'anya tonge mdomoni. Na kila napowasoma Waislaam wenye siasa kali it's all about when is our turn?.. hakuna anayelilia demokrasia iliyopotea na wala hawataki kujihusisha na siasa kuhakikisha Ukabila au Udini ndio unapigwa vita na sii apendelewe nani na kwa zamu zipi..
Hili ni tatizo ambalo tunalo sii tu kwa dini zetu bali lipo hata ktk Muungano wetu na Zanzibar. Watu wanatazama hizi zamu na ndio maana wanahesabu Wazanzibar wangapi, waislaam wangapi, wachagga wangapi yote haya ni matokeo ya imani mbovu za kibaguzi kinyume cha Uislaam au niseme demokrasia.
Hizi ndizo siasa za Waislaam wa Tanzania ambao wanataka sana kuitumia dini vibaya wakati wao wenyewe wanashindwa kuona kwamba demokrasia imepotea nchini na viongozi wao wa kiislaam ndio vipaza sauti na wanafiki wakubwa ktk uchochezi. Mwinyi ndiye aliyefungua mahusiano ya kitafa na Israel, Mwinyi ndiye aliua Balukta na kuwafunga ama kuua viongozi wake, Mwinyi ndiye aliyeweka mkataba wa MoU na misamaha ya kodi, Mwinyi ndiye aliyeruhusu Ma Casino na kadhalika lakini pembeni hudai ati kuna mfumo kristu wakati yeye ndiye mjenzi wa mfumo huo huo..
Mkuu hawa waislaam njaa ndio wanaifanya kazi yetu sisi tunaotoa Dawa iwe ngumu zaidi. Na kibaya zaidi wameingia hata ktk kazi zetu kiasi kwamba Uislaam leo unaonekana kama ni Ugaidi, ni imani inayotawaliwa na Udini kwa sababu wanashindwa kupigania haki zao hapo walipo isipokuwa kwa kutumia jina la dini ili wapate wanachama wengi wakipitia jina la dini..Lakini pamoja na yote haya, Islaam italindwa na Mwenyezi Mungu pale Waislaam wenyewe wameshindwa kuilinda...
Let us assume kuwa 'nidhulma kama unavyodai', solution gani unapendekeza ili kuondoa