Let us assume kuwa 'nidhulma kama unavyodai', solution gani unapendekeza ili kuondoa
Hawezi kuwa na jibu hata kidogo kwa sababu hajui yeye anataka nini isipokuwa kitu gani kiondoke. Yaani kwa madai yao mfumo Kristu uondoke na hawana cha ku replace kwa sababu kwa kila utakachokiweka ni mfumo kristu kwao, as a matter of fact hata demokrasia ni mfumo kristu.
Binafsi nisichokipenda kutoka kwa hawa jamaa zetu ni pale wanapoitumia dini kueneza siasa zao, nimeshamwambia Mohammed Said, Islaam ni dini inayosimama peke yake na kwa wanadamu wote, tunachogombea sote ni UTU wetu ambao uko well defined ktk kuran na mtu yeyote anatakiwa kupigania haki hizo kama binadamu. Lakini haiwezekani mtu ukapigania haki zako wewe kwa sababu ya jina lako la dini ama imani yako isipokuwa pale dini inapokatazwa...
Mfano mzuri wa Islaam ni kama demokrasia..Leo hii dunia nzima vita vinatokea kwa sababu ya kukosekana kwa demokrasia, hivyo wananchi wataidai demokrasia ilokosekana ili kurekebisha mapungufu yoyote yaliyopo ya kiutawala na sii kutazama makundi ya watu kujaribu kupendelea kundi moja ama kudhoofisha kundi jingine ili kufikia usawa wa kiutawala. Sijui kama nimeeleweka!
Wanachokiomba kina Mohammed Said, ni Udini yaani ktk siasa za kibaguzi ni kama vile kabila fulani linabaguliwa, hivyo ili nao wapate kutesa kwa zamu kama wenzao, wanataka wampate kiongozi ama viongozi wao ambao watawawezasha kubadilisha upepo wa kimfumo kutoka kabila moja kwenda lao, kama Kenya walivyokuwa wakidai Wajaluo miaka ya Kenyatta.
Kwa sura hii, Wajaluo hawakutaka hujenga Demokrasia isipokuwa ni ktk mfumo ule ule wa ukabila, yaani Wajaluo nao wanataka kushika nchi ili wawakandamize Wakikuyu wakati wao wakipanda kimaisha ili kufikia usawa...Na wala sii swala la kuwatazama wao kama wanaokandamizwa ili wawezeshwe, hapana wanachokitafuta ni kuanguka kwa Mkikuyu..Na huyo mkikuyu hawezi kukubali akielewa kwamba utawala ukiwa chini ya Mjaluo yeye ndiye atakuwa muathirika...Kinacholkiliwa hapa ni ule mfumo wa kupokezana yaani na sisi sasa ni ZAMU YETU.
Kwa hiyo, kwa mtu mwenye upeo mkubwa ataelewa kwamba kinacholiliwa hapa na waislaam njaa hawa ni kwamba ilikuwa zamu yao, pengine wakati wa Uhuru au kabla ya Uhuru na Nyerere akawanyang'anya tonge mdomoni. Na kila napowasoma Waislaam wenye siasa kali it's all about when is our turn?.. hakuna anayelilia demokrasia iliyopotea na wala hawataki kujihusisha na siasa kuhakikisha Ukabila au Udini ndio unapigwa vita na sii apendelewe nani na kwa zamu zipi..
Hili ni tatizo ambalo tunalo sii tu kwa dini zetu bali lipo hata ktk Muungano wetu na Zanzibar. Watu wanatazama hizi kutesa kwa zamu na ndio maana wanahesabu Wazanzibar wangapi, waislaam wangapi, wachagga wangapi yote haya ni matokeo ya imani mbovu za kibaguzi kinyume cha Uislaam au niseme demokrasia. Na ndio maana Maalim Seif Hamad, Bilal, Nahoda, Shamhuna wote hawa baada ya kupewa nafasi ya kutesa mashambulizi hakuna tena.. It's all about them ktk kutesa kwa zamu!
Hizi ndizo siasa za Waislaam wa Tanzania ambao wanataka sana kuitumia dini vibaya wakati wao wenyewe wanashindwa kuona kwamba demokrasia imepotea nchini na viongozi wao wa kiislaam ndio vipaza sauti na wanafiki wakubwa ktk uchochezi. Mwinyi ndiye aliyefungua mahusiano ya kitafa na Israel, Mwinyi ndiye aliua Balukta na kuwafunga ama kuua viongozi wake, Mwinyi ndiye aliyeweka mkataba wa MoU na misamaha ya kodi, Mwinyi ndiye aliyeruhusu Ma Casino na kadhalika lakini pembeni hudai ati kuna mfumo kristu wakati yeye ndiye mjenzi wa mfumo huo huo, lakini waulize watakwambia hakuna rais kama Mwinyi.
Mkuu hawa waislaam njaa ndio wanaifanya kazi yetu sisi tunaotoa Dawa iwe ngumu zaidi. Na kibaya zaidi wameingia hata ktk kazi zetu kiasi kwamba Uislaam leo unaonekana kama ni Ugaidi, ni imani inayotawaliwa na Udini kwa sababu wanashindwa kupigania haki zao hapo walipo isipokuwa kwa kutumia jina la dini ili wapate wanachama wengi wakipitia jina la dini..Lakini pamoja na yote haya, Islaam italindwa na Mwenyezi Mungu pale Waislaam wenyewe wameshindwa kuilinda...