Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Kama hukuelewa ninachozungumza ustaarabu ni kuomba ufafanuzi sio kunitukana.

Katika sentensi yangu hapakuwa na tusi lakini haya tuwaachie wanaukumbi waamue
kati yetu nani katukana.

Mohamed
Alaa ukiitwa kwa kazi uloifanya imekuwa tusi? unachojaribu kufanya hapa kitu gani haswa kama wewe una hakika na kazi yako ambayo kwetu sisi ni matusi makubwa unashangaa kipi?

Wewe huoni kama umetutukana nami sioni kama nimekutukana isipokuwa umewafanyia kazi kubwa wazungu, na wamekusifia kwani tusi hilo. Au neno Nyapala maanake supervisor nalo tusi?
 
Hili sio swala la chuki hata kidogo,inaonekana somo la MS halijaeleweka.
Nyerere mpaka Mwinyi ana stahafu bado ananguvu nchii ametuchagulia mpaka rais wa awamu ya tatu kama mmesahau na alihaidi kabla ya kwenda London kutibiwa kwamba angemwona hata rais wa awamu ya nne.
Mzee MS,amewaambia kwa fumbo hapo juu "mwinyi alikuwepo tu ila "watu" walisha form a mechanism ya kuendesha mambo yao

Hapa ndipo mnaonekana mna agenda ya udini na chuki dhidi ya Nyerere. Somo la kupandikiza chuki za kidini hatuwezi kulielewa wala kulikubali.
Kama mwinyi akiwa raisi alishindwa kuiongoza nchi na kutegemea watu walioko nje ndio waiongoze huo ni uzembe wake mwenyewe.

Maraisi wote wa nchi hii wamekuwa wakichaguliwa na wananchi, Nyerere alikuwa na kura moja tu kama nilivyo mimi. Lakini kwa sababu ya chuki zenu za kidini mnamtupia hata lawama asizostahili.
 
Sanda Matuta,

Hali ya Mwinyi ilikuwa kama Insha Allah utakavyoona hapo chini:
"This was the time that Mwinyi confided to Prof. Malima that there werepeople within the office of the president who had duplicates keys to hisdrawers and were stealing documents. Mwinyi, Prof. Malima confided to my informantlooked scared and while he was reporting this to Prof. Malima, Mwinyi wasspeaking in very low tones, whispering as if fearing his office was bugged.Prof. Malima advised President Mwinyi to transfer that entire staff and bringin new people who would have allegiance to him. At this time Prof. Malimastarted to receive hate mails which he turned over to the Intelligence forinvestigation but nothing came out of those investigations."

Mohamed

Mzee Mohamed,
Suala la mzee mwinyi kumnong'oneza malima juu ya kuingiliwa ofisini kwake tangu awali umeombwa umhoji ili upate habari toka kwa mhusika mwenyewe badala ya kutumia habari za kuambiwa na mtu mwingine.

Kumbuka hapa mzee mwinyi alikuwa ananong'ona, nani aliufahamu huo mnong'ono?
 
Mkuu Mkandara,
Heshima kwako, miaka michache iliyopita nilipojiunga na JF nilijaribu kwa mbali ku-rise issue hii ya Nyerere ukani crash pamoja na wachangiaje wengine na kuniambia nilikua na "labda Nyerere kuna kitu alinifanya mimi binafsi au familia yangu" na kwakua sikua na utafiti wowote (kama Muhamed Said) nikaliwacha jambo lile. Nilijaribu kuleta kile ambacho nikua nikielezwa na kukisikia.

Ila kama lilivyo kila jambo dunia lazima litapata wa kulisemea hata kama mbele zaidi miaka mia, wakati wake umefika sasa kwa jambo hili. Labda uniambie wewe hukutani na maneno ya namna ya Muhamed Said huko uliko ila ni kitu cha kawaida sana wanapokaa watu wa imani sawa kuzungumzia mustakabari wa imani yao.

Usipate shida sana kutetea jambo lililo wazi muda ni muafaka upande ule mwingine kujua kwamba upand e huu wanalijua hili na wanalizungumza labda itasaidia kupunguza ama kuondoa tofauti hizi.

As for Muhamed Said,yeye ni mtu mdogo sana kuleta machafuko kwenye nchi hii,na nina imani hiyo sio nia yake kuletea vurugu baina yetu ila yafaa kuzungumza ile tupate common ground which will be based on mtual understanding for a lasting peace kama mababu zetu walivyo ishi zamani.Lakini kung'ang'ania kila kitu kiko sawa ni kuletelea msiba.
 
Mkuu Mkandara,
Heshima kwako,miaka michache iliyopita nilipojiunga na JF nilijaribu kwa mbali ku-rise issue hii ya Nyerere ukani crash pamoja na wachangiaje wengine na kuniambia nilikua na "labda Nyerere kuna kitu alinifanya mimi binafsi au familia yangu" na kwakua sikua na utafiti wowote (kama Muhamed Said) nikaliwacha jambo lile.Nilijaribu kuleta kile ambacho nikua nikielezwa na kukisikia.
Ila kama lilivyo kila jambo dunia lazima litapata wa kulisemea hata kama mbele zaidi miaka mia,wakati wake umefika sasa kwa jambo hili.Labda uniambie wewe hukutani na maneno ya namna ya Muhamed Said huko uliko ila ni kitu cha kawaida sana wanapokaa watu wa imani sawa kuzungumzia mustakabari wa imani yao.
Usipate shida sana kutetea jambo lililo wazi muda ni muafaka upande ule mwingine kujua kwamba upand e huu wanalijua hili na wanalizungumza labda itasaidia kupunguza ama kuondoa tofauti hizi.
As for Muhamed Said,yeye ni mtu mdogo sana kuleta machafuko kwenye nchi hii,na nina imani hiyo sio nia yake kuletea vurugu baina yetu ila yafaa kuzungumza ile tupate common ground which will be based on mtual understanding for a lasting peace kama mababu zetu walivyo ishi zamani.Lakini kung'ang'ania kila kitu kiko sawa ni kuletelea msiba....

Sheikh Mohamed keshaeleza kwamba hii mbiu ya mfumo kristo ni muendelezo wa kile alichojifunza kwa masheikh wake na 16/10/2011 mlikuwa na mkutano kupanga mikakati ya kuukomesha, hiyo sio kuchochea vurugu?
 
Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.

Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwataja kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.

Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !

How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.

Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.

Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea na si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.

Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.
 
Mzee Mohamed,
Suala la mzee mwinyi kumnong'oneza malima juu ya kuingiliwa ofisini kwake tangu awali umeombwa umhoji ili upate habari toka kwa mhusika mwenyewe badala ya kutumia habari za kuambiwa na mtu mwingine.
Kumbuka hapa mzee mwinyi alikuwa ananong'ona, nani aliufahamu huo mnong'ono?

MM,

Yaani unataka vyanzo vyangu vya habari nivianike katika jamvi?
Nifanye hivyo na nibaki mtafiti...

Mohamed
 
Mag 3 Kwanini unaona tukubari RAI zako na tukatae hadithi na Muhamed Said!!!?

Unahisi kwa kijana wa miaka arobaini kila siku ana amka asubui na wimbo wa "Nyerere ni mpungufu wa fadhira" kila siku kutoka kwa wazazi na ndugu wa karibu na anakutana na "ngano" za MS na RAI zako ataamini kipi?

"Panapo ukweli uongo ujitenga" Muhamed saidi si kaleta juzi tu hizo hadithi zake angalia post zangu za mwaka 2007 haya mambo yapo inabidi mkubari ili tuanze upya.

Tena kuhusu hilo la chadema ndio wala usililete hapa mimi nalijua mwanzo mwisho
 
Sheikh mohamed,
nia yangu sio unitajie vyanzo vyako vya habari, maana hizi ni nyeti zinahitaji usiri. Zile ambazo si nyeti sana umekuwa ukibainisha vyanzo vyake.

Ninachokusudia hapa ni kutaka kufahamu kama umewahi kumhoji mzee mwinyi kuhusu jambo hilo, lengo ni kutanzua huu utata. Bila shaka utakuwa umenielewa!
 
Sanda Matuta,

Hali ya Mwinyi ilikuwa kama Insha Allah utakavyoona hapo chini:
"This was the time that Mwinyi confided to Prof. Malima that there werepeople within the office of the president who had duplicates keys to hisdrawers and were stealing documents. Mwinyi, Prof. Malima confided to my informantlooked scared and while he was reporting this to Prof. Malima, Mwinyi wasspeaking in very low tones, whispering as if fearing his office was bugged.Prof. Malima advised President Mwinyi to transfer that entire staff and bringin new people who would have allegiance to him. At this time Prof. Malimastarted to receive hate mails which he turned over to the Intelligence forinvestigation but nothing came out of those investigations."

Mohamed

Hii hoja tulishaivunja kitambo sana. Mzee Mwinyi bado yuko hai na hakuna mahali umeonesha kumhoji kuhusu ukweli wa hicho. Kwa kadiri ya kwamba hujamhoji mzee Mwinyi ambaye yuko hai na anapatikana kirahisi kujua kama kweli alisema hayo unayodai alimuambia Malima ni wachache wanaweza kuamini kuwa ni kweli kwa sababu once again mtu unayemtumia kama chanzo cha kuamini ni marhemu.

Unawatumia waliokufa lakini walio hai hutaki kuwatumia. Hili ni tatizo.
 
Mag 3 Kwanini unaona tukubari RAI zako na tukatae hadithi na Muhamed Said!!!?
Unahisi kwa kijana wa miaka arobaini kila siku ana amka asubui na wimbo wa "Nyerere ni mpungufu wa fadhira" kila siku kutoka kwa wazazi na ndugu wa karibu na anakutana na "ngano" za MS na RAI zako ataamini kipi?
"Panapo ukweli uongo ujitenga" Muhamed saidi si kaleta juzi tu hizo hadithi zake angalia post zangu za mwaka 2007 haya mambo yapo inabidi mkubari ili tuanze upya.
Tena kuhusu hilo la chadema ndio wala usililete hapa mimi nalijua mwanzo mwisho

Mkuu hapa hatutafuti kuamini rai za mag3 na kukataa za sheikh mohamed. Kinachotafutwa hapa ni ukweli kutoka katika masimulizi ya hao wote pamoja na wachangiaji wengine.

Kama kuna ukweli ndani ya maelezo ya mag3 tunauchukua na kama kuna upotoshaji tunaachana nao. Vivyo hivyo kama kuna ukweli kwenye masimulizi ya sheikh mohamed tunauchukua na kama kuna upotoshaji tunaachana nao.

We are just looking for the facts!
 
Mag 3 Kwanini unaona tukubari RAI zako na tukatae hadithi na Muhamed Said!!!?
Unahisi kwa kijana wa miaka arobaini kila siku ana amka asubui na wimbo wa "Nyerere ni mpungufu wa fadhira" kila siku kutoka kwa wazazi na ndugu wa karibu na anakutana na "ngano" za MS na RAI zako ataamini kipi?
"Panapo ukweli uongo ujitenga" Muhamed saidi si kaleta juzi tu hizo hadithi zake angalia post zangu za mwaka 2007 haya mambo yapo inabidi mkubari ili tuanze upya.
Tena kuhusu hilo la chadema ndio wala usililete hapa mimi nalijua mwanzo mwisho

Sanda Matuta, na wewe ulisimuliwa na wazee wako ama ulikuwapo ili nijue namna ya kukujibu. Kama ulikuwapo kwenye miaka ya 1950 hadi uhuru ulikuwa na umri gani ? Siulizi hivi kwa lengo baya, nataka tu nijue kama unaeleza uliyoshuhudia au uliyosimuliwa.
 
Hapana swali hapo sasa unajibu nini mahali pasipokuwa na swali?

Mohamed

Swali ni ulitumia muda gani kufanya utafiti wa kuandika kitabu chako cha Abdulwahid Sykes hadi kilipochapwa mwaka 1998? kwa mfano, ilikuwa ni miezi miwili, au miezi mitatu au mwaka mmoja? Au ilikuw ani kazi uliyotumia muda mrefu kuweza kukusanya, kuchambua, kuweka katika mpango mzuri ushahidi mbalimbali kabla hujaamua kuandika manuscript yako? Au hukutumia muda wowote ule kufanya utafiti na badala yake ukarundika tu kila ulichokipata na kuweka humo ndani? Au hili ni swali ambalo halijibiki?
 
Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.

Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwata kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.

Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !

How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.

Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.

Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea ni si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.

Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.

Mag3,

Nimekwambia ukinitaja tu ujuwe nitakujibu.

Nimekusoma umeandika mengi kwa hakika ni tabu kukusoma nashusha hii hapa chini kwa faida ya wanaukumbi:

"Jina la Abdulwahid halitajwi kabisa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika au katika historia ya kuasisi TANU. Juu ya haya yote Abdulwahid ndiye aliyewasha cheche za kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Jopo la wana-historia wa Chama Cha Mapinduzi waliopewa jukumu la kutafiti na kuandika historia rasmi ya TANU, hakuna hata sehemu moja waliyotaja jina la Abdulwahid katika kitabu kizima.[1]Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa. Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule. Kitendo hiki kimeondoa hadhi na heshima ya wazalendo wengi waliopigania nchi hii na halikadhalika kimeiondolea TAA heshima ya kuitwa chama cha siasa. Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano, "Sasa inakaribia mwaka mmoja toka iundwe Tanganyika African National Union na katika kipindi hiki chama kimekua kikipata nguvu siku hadi siku, wakati mwingine chini ya upinzani mkubwa. Kama mnavyofahamu chama hiki ni badala ya Tanganyika African Union ambayo ilikuwa sawasawa na chama cha majadiliano."[1]Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii.[1]Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), [1]halikadhalika Japhet na Seaton (1966).[1]TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), [1]Nyerere (1953) [1]aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri. Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema, "Tanganyika African National Union kwa mtazamo mmoja ni chama kipya, lakini kwa mtazamo mwingine ni chama kikongwe. TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu." Wasomi wengine wameishusha TAA kufikia daraja la kuwa klabu: Mwenegoha (1976) anaandika, "Mwaka 1954, baada ya miaka ishirini na tano ya kutoweza kufanya lolote, Nyerere aliigeuza TAA kutola chama cha kijamii kuwa chama cha siasa chenye kuogopwa kilichoitwa Tanganyika African National Unioní." [1]Abdulwahid ambae alitoa mchango wa pekee katika kuunda TANU alikuwa anaiona TAA kama chama cha siasa (1951). [1]Katika kundi la waandishi na wasomi walioandika kuhusu African Association kisha wakabadili mawazo yao kuhusu nini hasa chama kile kilikuwa, ni Nyerere na Hatch ndiyo waliobadili misimamo yao ya awali. Nyerere alipoandika barua kwa Gavana wa Tanganyika, Edward Twining tarehe 10 Agosti, 1953 alieleza kuwa TAA ni chama cha siasa. [1]Lakini baadae alibadili msimamo na kusema kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe. Kauli hii ilitawala hotuba za Nyerere na maandishi yake kwa kipindi kirefu. Katika miaka ya hivi karibuni amesikika akisema kuwa TAA kilikuwa "chama cha siasa kisichokuwa na katiba ya siasaí." Hatch (1976) ameieleza TAA kama chama cha starehe [1] sehemu moja na chama cha siasa sehemu nyingine.[1]John Kabudi ameieleza African Association kama "chama cha watu binafsi wananchi kilichokuwa na mwelekeo wa kitaifa."[1]Ieleweke kuwa hata viongozi wa TAA hawathaminiwi kama wanasiasa. Kaniki, kwa kukosa neno la kuwatambulisha waasisi wa TAA, amewaita wanasiasa na kuwawekea "quatation mark": "Nyerere, kabla ya hapo akiwa hajulikani na "wanasiasa" wengi katika Tanganyika, alikuwa mwalimu katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, jirani na Dar es Salaam, na alikuwa amechaguliwa rais wa (TAA) mwaka uliopita.[1]
Kwa mtazamo huo wa Kaniki mzalendo kama Abdulwahid Sykes hakuwa mwanasiasa, ila Nyerere ndiye mwanasiasa. Iliffe (1968)[1]alidokeza kuwa historia ya TANU iliyokuwa imeandikwa hadi wakati ule ilikuwa haijakamilika na katika uchambuzi wake alisema kuwa African Association kutokana na mwelekeo na wanachama wake ilikuwa ni chama cha siasa. Kandoro na Japhet, [1]waasisi wa TANU walipata umaarufu wakati Abdulwahid akiwa rais wa TAA mwaka 1952. Hawa walikuwa ndiyo waasisi pekee ambao walifanya kazi na Abdulwahid wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru. Safari ya Kirilo kuja Dar es Salaam na kule kumweka Seaton kama mwanasheria kushughulikia mgogoro ule, kazi yote hiyo ilifanywa na Abdulwahid na uongozi a TAA wa wakati ule. Ilikuwa Abdulwahid ndiye aliyemhangaikia Kirilo kupata pasi ya kusafiria baada ya kunyimwa pasi kule Arusha. Kirilo na Seaton na halikadhalika Kandoro wamenadika kumbukumbu zao kuhusu ukoloni, lakini cha ajabu na kusikitisha ni kuwa hakuna hata sehemu moja waandishi hawa wametaja mchango wa Abdulwahid hata kwa kuparazia tu. Waandishi hawa wamejaribu kumtumbukiza Nyerere kama kiongozi aliyehusika katika Mgogoro wa Ardhi ya Wameru, wakati yeye hata kuwapo nchini wakati ule hakuwapo. Ukweli ni kuwa wakati mgogoro wa ule ulipofikishwa mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, Nyerere alikuwa masomoni Chuo Kikuu cha Edinburgh Uskochi akisomea shahada ya pili. Mwandishi aliyejipambanua na hawa wote kwa kutomtaja Abdulwahid ni mama wa Kiingereza Judith Listowel (1965) [1]ambae ingawa amemtaja kijuujuu, ameandika kwenye kitabu chake kuwa Abdulwahid alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU.
Katika miaka hii ya karibuni kumejitokeza hamu ya kutaka kuielewa historia ya siasa katika Tanzania na jina la Abdulwahid limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika majarida, [1]magazeti, [1]magazeti ya kimataifa, [1]na katika vitabu. [1]Maandiko yote haya yanamtazama Abdulwahid kwa sura tofauti. Yapo yanasema kuwa yeye ndiye alikuwa kinara katika kuunda TANU na kumtia Nyerere katika siasa. Katika maandiko haya Abdulwahid anaelezwa kama mzalendo na mwanamapinduzi. Tandon anamweleza Abdulwahid na wazalendo wengine katika Afrika ya Mashariki kama Chege Kibachia, Makham Singh, Fred Kubai, James Kivu, I.K. Musazi, Erika Fiah na Gama Pinto kama "viongozi maveterani wa watu wa Afrika ya Mashariki ambao wanahistoria wetu wa sasa wamewasahauí." [1] Wapo waandishi wanaomuona Abdulwahid kama "kabaila uchwara" kutokana na kuwa alikuwa mtoto wa mfanyabiashara Mwafrika tajiri, Kleist Sykes.
Profesa Shivji anamtuhumu Abdulwahid kwa kushirikiana na wakoloni na anamchukulia kama kabaila uchwara ambae yeye mwenyewe hatoki katika tabaka la wafanyakazi. Akitafakari nafasi ya Abdulwahid kama kiongozi wa makuli katika bandari ya Dar es Salaam wakati wa ukoloni Shivji anasema, "Serikali ilipenyeza uongozi wa makabaila uchwara katika chama. Mwezi February 1948 Abdul Sykes, mtoto wa mfanya biashara Mwafrika maarufu, aliombwa na serikali awe katibu wa chama cha makuli. Abdul Sykes hakuwa akifanyakazi bandarini wala hakuwa anatoka katika tabaka la wafanyakazi. "[1]
Hapa Shivji alikuwa anaeleza jinsi Abdulwahid alivyochaguliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza katika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika. Kwa kutoijua vyema historia ya maisha ya Abdulwahid na vilevile kwa hamaki za misimamo ya mrengo wa kushoto ya Ki-Marx, Shivji ametumia vipimo visivyo sawa katika kumchambua Abdulwahid. Engels anasema bepari uchwara ni "tabaka la makabaila wa kisasa ambao wanahodhi njia zote za uzalishaji mali za jamii na vilevile wanawaajiri na kuwalipaí."[1]Hata hivyo Sklar anasema kuwa dhana hiyo sasa imebadilika kwa hiyo hata ile maana yake ya awali imebadilika: "Hivi sasa neno hilo linatumiwa na wafuasi wa Marx kuieleza tabaka lililo juu katika jamii ambazo linafuata soko huria na kuachia kuhodhiwa kwa mali kama matokeo ya mali binafsi katika uzalishaji wake."[1]
Kama Shivji angeliyajua maisha ya Abdulwahid ni wazi kuwa angetumia kipimo kingine kabisa katika kumweleza. Lakini kwa kuwa kilichotumika ni kipimo kisicho sawa, matokeo yake hayakuweza kuwa barabara. Hakuna biashara ya Mwafrika wakati wa ukoloni inaweza kuitwa biashara ya bepari na katika mkumbo wa kujumuishwa katika dhana ya ubepari, kama ubepari ulivyokuwa ukifahamika huko Ulaya. Haya ndiyo matatizo yanayoikumba historia ya Abdulwahid na kwa kweli historia nzima ya taifa la Tanganyika.K
atika wale walioasisi TANU, ni wale tu aliokuwa makao makuu ya TAA ndiyo wanaoweza kueleza historia ya kweli ya chama hiki. Hawa ni John Rupia, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Julius Nyerere, Dome Budohi, Abdulwahid na Ally Sykes. Hawa ndugu wawili, Abdulwahid na Ally, wao ni baba yao ndiye aliyekuwa muasisi wa African Association akiwa kama katibu wake wa kwanza hapo mwaka wa 1929. Majalada ya akina Sykes kuhusu African Association na TANU yana habari muhimu sana kwa mtafiti kuhusu historia ya ukoloni na juhudi walizofanya waasisi wa taifa la Tanganyika katika kujikomboa. Majalada haya yana habari muhimu na za kutosha kuhusu Nyerere na jinsi alivyopokelewa Dar es Salaam na akina Sykes na jinsi alivyoingizwa katika siasa. Inastaajabisha kuwa kumbukumbu hizi zenye habari muhimu sana kuhusu Nyerere na TANU hazikuguswa kabisa wakati watafiti wa historia ya TANU walipokuwa wakifanya utafiti wao. Inastaajabisha vilevile kuwa, si Ally wala mdogo wake, Abbas ndugu wawili walio hai baada ya kifo cha kaka yaoAbdulwahid, walifanyiwa mahojiano yoyote na watafiti wale.
Katika miaka ya mwishoni ya 1960, John Iliffe akiwa Idara ya Historia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, alipoanza utafiti wake wa historia ya Tanzania, aliweza kukusanya habari nyingi sana na muhimu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake, Aisha Daisy Sykes, binti wa Abdulwahid. Ingawa Daisy alimfahamisha Iliffe kuwa habari zile alizokuwa akiandika katika semina kuhusu historia ya Tanganyika alikuwa akizipata kutoka kwa baba yake, inastaajabisha kuwa, Iliffe japo kuwa alikua muhihataji sana wa kutaka kujua historia ya Tanganyika, hakuchukua tabu ya kuonana na Abdulwahid ili apate habari zile moja kwa moja kutoka kinywani kwake.Iliffe hata hivyo kwa kujua hazina ya historia iliyokuwa katika kumbukumbu za akina Sykes, alimtia hima Daisy aandike historia ya maisha ya babu yake, Kleist Sykes. Utafiti huu Daisy aliufanya kwa ufanisi mkubwa. [1]Baba yake alipofariki dunia mwaka wa 1968, Daisy kutokana na mafanikio ya kuandika habari za babu yake sasa akataka kufanya utafiti na kuandika maisha ya marehemu baba yake. Daisy aliamua kufanya hivyo kwa uchungu alipokuja kugundua kuwa historia ilikuwa haimtendei haki baba yake. Daisy alihisi ilikuwa ni wajibu wake kuueleza ulimwengu baba yake alikuwa nani na nini mchango wake katika kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza. Hiki alikiona kitu muhimu ili kuiweka sawa historia ambayo kwa makusudi ilikuwa inapotoshwa. Daisy alikuwa na majalada na shajara zote za baba yake. Iliffe kwa sababu ambazo kwa wakati ule Daisy hakuweza kuzitambua, alimkataza asifanye hivyo kwa kuwa wakati wa kuandika historia ya baba yake ulikuwa bado. Iliffe alimwambia Daisy afanye subira hadi hapo baadae. Ni wazi kuwa Iliffe alikuwa akijua kuwa Abdulwahid alikuwa mtu muhimu na wa kuaminika katika historia ya TANU; na kuwa utafiti wowote katika maisha yake kungesaidia sana kuielewa historia ya Tanzania. Kutokana na msimamo huu wa Iliffe Daisy hakujaaliwa tena kuandika maisha ya baba yake.
Historia ya TANU siku zote imekuwa ikitawaliwa na mambo kama haya. Mwaka wa 1962 Ally Sykes alijaribu kuandika historia ya TANU katika gazeti la Mambo Leo. Mhariri wa gazeti lile M.J. Sichwale alimuandikia Ally Sykes kumfahamisha kuwa hawezi kuchapisha makala yake kwa kuwa mwandishi hana utaalamu na somo aliloliandikia.[1]TAA ilipogeuzwa kuwa TANU, wanaharakati wa TAA, labda kwa kuanza kuhisi kuwa historia yao ilikuwa inataka kupotoshwa na wale waliokuja katika siasa na TANU, walikuwa na fikra za kuandika historia ya TANU. Mwalimu Kihere, mmoja wa viongozi wa TAA Tanga, alipata wakati fulani kumwambia Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia kuwa ingekuwa vyema historia ya siasa katika Tanganyika ikaandikwa na kuhifadhiwa wakati wao wangali hai kuepusha kuingizwa uongo ndani yake na kupindisha ukweli na hao watakaokuja hapo baadae baada ya wao kutoweka. Bahati mbaya wazo hili halikupewa uzito iliostahili na hadi Mwalimu Kihere, Abdulwahid na John Rupia, Stephen Mhando na Hassan Suleiman wanafariki dunia, hakuna hata mmoja katika wale wakongwe wa siasa alikuwa wameandika kitu chochote.
Hassan Suleiman anawalaumu wanahistoria kwa kukosekana kuandikwa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwapuuza wazalendo wengine na badala yake kuandika historia ya Tanganyika kwa kuegemeza historia hiyo kwa Nyerere. Kabla hajafariki, Hassan Suleiman alichukua nyaraka zake zote binafsi za African Association wakati alipokuwa kiongozi na kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati ule Rashid Kawawa katika sherehe mahsusi iliyofanyika Makao Makuu ya CCM, Dodoma. Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na Abdulwahid mwenyewe. Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana Nyerere wakati ule Waziri Mkuu alimuomba Abdulwahid aandike historia ya harakati ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU. Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Marekani alichaguliwa na TANU asaidiane na Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa historia ile.
Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA. Nyaraka zake binafsi, za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo. Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakumpendeza Nyerere, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid ñ Kleist Sykes, lilikuwa likitawala. Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watoto wake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile. Historia hii inasemekana haikumpendeza Nyerere na baadhi ya viongozi wa TANU. Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika bali nia na azma yao ilikuwa na kumjenga Nyerere na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili. Abdulwahid alipongíamua hili haraka akajitoa katika kazi ile. Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii iansemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU. Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam. Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ëmwandishií kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake. Hata hivyo TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu na wakafanya bidii kuzuia isichapishwe. Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili. Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa. Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.
Hata hivyo kuna kasoro katika kitabu hicho ambacho ëmwandishií alishindwa kugundua na kuweza kujikinga asijulikane kama kile kitabu hakikuandikwa na kalamu yake. ëMwandishií kama tunavyoweza kumwita, akiandika katika nafsi ya kwanza, anaeleza kuwa amekiandika kitabi kile mwaka wa 1964. Katika maelezo hayo ëmwandishií anatoa habari ambazo msomaji makini anahisi kuwa ëmwandishií alikuwa marika sawa na anawafahamu vyema wale wazalendo anaoandika habari zao. Lakini mwandishi anasahau kuwa mwaka 1964 wakati yeye anadai alikuwa akiandika habari hizo yeye alikuwa mvulana mdogo na asingeweza kuwajua vile wale wazalendo na habari zilizotokea miaka ya 1950 wala asingeweza kuwa na ubongo wa kutafakari mambo kama yale. Sasa swali linakuja. Huyu aliyeandika habari zile ni nani hasa? Kutokana na maelezo ambayo kitabu hiki kimeeleza ni wazi aliyeandika habari zile hawezi kuwa Dr Kleruu kwa sababu Kleruu katika kipindi kile, hakuwapo katika harakati zile za kuunda TANU. Ni mtu mmoja tu ndiye anaeweza kuwa na habari zile na kuwa na ufahamu wa mambo yalivyokuwa miaka ile. Huyu atakuwa ni marehemu Abdulwahid akiandika mwaka 1964. ëMwandishií kwa ujinga amenakili kutoka kwenye maandishi ya Abdulwahid ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika Maktaba ya TANU, Dar es Salaam. Na huyu ëmwandishií wala hakunakili maandishi yale mwaka 1964, bali miaka mingi baada ya kifo cha Abdulwahid kutokea.
Abdulwahid alipobaini kuwa historia ya Tanganyika inaweza kuwa chanzo cha husda na hasama kati yake na Nyerere na viongozi wengine wa TANU, akaamua kutosema chochote kuhusu hilo ingawa kabla hajafa alikubali mwaliko wa Chama Cha Historia Cha Tanzania (Historical Association of Tanzania) (HAT). Imeshindikana kujua Abdulwahid alizungumza kuhusu nini katika mwaliko ule, lakini inasemekana moja ya maswali aliyoulizwa ilikuwa kuwa kama si kweli Nyerere ndiye aliyekipa chama uhai kuanzia mwaka wa 1954. Katika kujibu swali hili Abdulwahid alilirudisha swali lile kwa wasikilizajiwake kwa kutoa mfano wa John Glenn, Mmarekani wa kwanza kwenda angani kuzunguka dunia. Abdulwahid aliwauliza wasikilizaji wake, ëNani apewe sifa, wanasayansi wa Kimarekani waliotengeneza roketi ile au John Glenn aliyekuwa rubani wa chombo?í
Mwaka 1962 Judith Listowel alipokuja Tanganyika kufanya utafiti kabla hajaandika kitabu chake The Making of Tanganyika, alitaka sana kufanya mahojiano na Abdulwahid. Kwa kujua matatizo yaliyokuwa yanakabili historia ya Tanganyika mara ya kwanza ilipojaribiwa kuandikwa, Abdulwahid alijaribu sana kumkwepa Listowel. Listowel alipokuja kumkamata Abdulwahid nyumbani kwake Magomeni Mikumi, yeye hakupenda kueleza mchango wake wala wa baba yake katika kuaisisi African Association na TANU. Kwa kweli katika mahojiano yake Listowel hakupata chochote cha maana sana. Hata hivyo Listowel aliweza kuelezwa na Abdulwahid jinsi TANU ilivyokuja kuasisiwa. Listowel alikuja kuandika katika kitabu chake kuwa: "Abdul Sykes, kaka yake Ally, alisema kuwa ilibidi waamshe fikra za siasa za wananchi ili kiundwe chama cha siasaí."[1] Kutokana na mazungumzo haya na Abdulwahid, Listowel alimwandikia Ally Sykes: "Nimependezwa sana na kaka yako na ningefurahi kama ningepata wasaa wa kuwa na mazungumzo na yeye zaidií."[1]Akiwa London Listowel alimuandikia Ally Sykes mara kadhaa akitaka ufafanuzi kuhusu mambo mengi muhimu katika historia ya Tanganyika.
Abdulwahid alipofariki Wizara ya Habari ilitoa taarifa ikieleza kuwa Rais Nyerere amehudhuria maziko ya Abdulwahid Sykes.[1]Kingine kinachostaajabisha ni kuwa taarifa ile ilitoa maelezo machache ya uajiriwa wake katika serikali na kuacha maelezo muhimu ya Abdulwahid katika siasa. Ilikuwa Mwingereza, Brendon Grimshaw, mhariri wa Tanganyika Standard, ndiye aliyempa Abdulwahid heshima na hadhi anayostahili baada ya kifo chake kwa kuchapisha taaízia ambayo ilimweleza Abdulwahid kama "Mmoja wa wapangaji wa vuguvugu la kudai uhuru na mmoja wa watu waliomsaidi Nyerere kuingia katika siasa."
Taaízia ile ilitoa sifa kemkem kwa ukoo wa Sykes katika kuleta maendeleo ya siasa Tanganyika kwa kusema kuwa, "Msukumo mkubwa wa Waafrika wa Tanganyika kupata chama cha siasa chenye nguvu ulitokana na juhudi za ukoo wa Sykes" 1]Inasemekana taaízia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU. Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu kumtukuza kaka yao. Hali hii ilijitokeza tena wakati CCM ilipokuwa ikitafiti historia yake. Hassan Upeka,[1]mmoja katika wasaidizi wa utafiti ule alipeleka katika jopo lile la utafiti na uandishi wa historia ya TANU, mahojiano aliyofanya na Abdulwahid miaka mingi iliyopita kuhusu historia ya TANU. Hassan Upeka alifahamishwa kuwa historia inayoandikwa haimhusu Abdulwahid Sykes."

Mohamed

Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.

Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwataja kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.

Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !

How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.

Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.

Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea na si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.

Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.

"Jina la Abdulwahid halitajwi kabisa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika au katika historia ya kuasisi TANU. Juu ya haya yote Abdulwahid ndiye aliyewasha cheche za kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Jopo la wana-historia wa Chama Cha Mapinduzi waliopewa jukumu la kutafiti na kuandika historia rasmi ya TANU, hakuna hata sehemu moja waliyotaja jina la Abdulwahid katika kitabu kizima.[1]Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa. Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule. Kitendo hiki kimeondoa hadhi na heshima ya wazalendo wengi waliopigania nchi hii na halikadhalika kimeiondolea TAA heshima ya kuitwa chama cha siasa. Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano, "Sasa inakaribia mwaka mmoja toka iundwe Tanganyika African National Union na katika kipindi hiki chama kimekua kikipata nguvu siku hadi siku, wakati mwingine chini ya upinzani mkubwa. Kama mnavyofahamu chama hiki ni badala ya Tanganyika African Union ambayo ilikuwa sawasawa na chama cha majadiliano."[1]Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii.[1]Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), [1]halikadhalika Japhet na Seaton (1966).[1]TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), [1]Nyerere (1953) [1]aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri. Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema, "Tanganyika African National Union kwa mtazamo mmoja ni chama kipya, lakini kwa mtazamo mwingine ni chama kikongwe. TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu." Wasomi wengine wameishusha TAA kufikia daraja la kuwa klabu: Mwenegoha (1976) anaandika, "Mwaka 1954, baada ya miaka ishirini na tano ya kutoweza kufanya lolote, Nyerere aliigeuza TAA kutola chama cha kijamii kuwa chama cha siasa chenye kuogopwa kilichoitwa Tanganyika African National Unioní." [1]Abdulwahid ambae alitoa mchango wa pekee katika kuunda TANU alikuwa anaiona TAA kama chama cha siasa (1951). [1]Katika kundi la waandishi na wasomi walioandika kuhusu African Association kisha wakabadili mawazo yao kuhusu nini hasa chama kile kilikuwa, ni Nyerere na Hatch ndiyo waliobadili misimamo yao ya awali. Nyerere alipoandika barua kwa Gavana wa Tanganyika, Edward Twining tarehe 10 Agosti, 1953 alieleza kuwa TAA ni chama cha siasa. [1]Lakini baadae alibadili msimamo na kusema kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe. Kauli hii ilitawala hotuba za Nyerere na maandishi yake kwa kipindi kirefu. Katika miaka ya hivi karibuni amesikika akisema kuwa TAA kilikuwa "chama cha siasa kisichokuwa na katiba ya siasaí." Hatch (1976) ameieleza TAA kama chama cha starehe [1] sehemu moja na chama cha siasa sehemu nyingine.[1]John Kabudi ameieleza African Association kama "chama cha watu binafsi wananchi kilichokuwa na mwelekeo wa kitaifa."[1]Ieleweke kuwa hata viongozi wa TAA hawathaminiwi kama wanasiasa. Kaniki, kwa kukosa neno la kuwatambulisha waasisi wa TAA, amewaita wanasiasa na kuwawekea "quatation mark": "Nyerere, kabla ya hapo akiwa hajulikani na "wanasiasa" wengi katika Tanganyika, alikuwa mwalimu katika shule ya Mtakatifu Francis, Pugu, jirani na Dar es Salaam, na alikuwa amechaguliwa rais wa (TAA) mwaka uliopita.[1]
Kwa mtazamo huo wa Kaniki mzalendo kama Abdulwahid Sykes hakuwa mwanasiasa, ila Nyerere ndiye mwanasiasa. Iliffe (1968)[1]alidokeza kuwa historia ya TANU iliyokuwa imeandikwa hadi wakati ule ilikuwa haijakamilika na katika uchambuzi wake alisema kuwa African Association kutokana na mwelekeo na wanachama wake ilikuwa ni chama cha siasa. Kandoro na Japhet, [1]waasisi wa TANU walipata umaarufu wakati Abdulwahid akiwa rais wa TAA mwaka 1952. Hawa walikuwa ndiyo waasisi pekee ambao walifanya kazi na Abdulwahid wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru. Safari ya Kirilo kuja Dar es Salaam na kule kumweka Seaton kama mwanasheria kushughulikia mgogoro ule, kazi yote hiyo ilifanywa na Abdulwahid na uongozi a TAA wa wakati ule. Ilikuwa Abdulwahid ndiye aliyemhangaikia Kirilo kupata pasi ya kusafiria baada ya kunyimwa pasi kule Arusha. Kirilo na Seaton na halikadhalika Kandoro wamenadika kumbukumbu zao kuhusu ukoloni, lakini cha ajabu na kusikitisha ni kuwa hakuna hata sehemu moja waandishi hawa wametaja mchango wa Abdulwahid hata kwa kuparazia tu. Waandishi hawa wamejaribu kumtumbukiza Nyerere kama kiongozi aliyehusika katikaMgogoro wa Ardhi ya Wameru, wakati yeye hata kuwapo nchini wakati ule hakuwapo. Ukweli ni kuwa wakati mgogoro wa ule ulipofikishwa mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, Nyerere alikuwa masomoni Chuo Kikuu chaEdinburgh Uskochi akisomea shahada ya pili. Mwandishi aliyejipambanua na hawa wote kwa kutomtaja Abdulwahid ni mama wa Kiingereza Judith Listowel (1965) [1]ambae ingawa amemtaja kijuujuu, ameandika kwenye kitabu chake kuwa Abdulwahid alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU.
Katika miaka hii yakaribuni kumejitokeza hamu ya kutaka kuielewa historia ya siasa katika Tanzania na jina la Abdulwahid limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika majarida, [1]magazeti, [1]magazeti ya kimataifa, [1]na katika vitabu. [1]Maandiko yote haya yanamtazama Abdulwahid kwa sura tofauti. Yapo yanasema kuwa yeye ndiye alikuwa kinara katika kuunda TANU na kumtia Nyerere katika siasa. Katika maandiko haya Abdulwahid anaelezwa kama mzalendo na mwanamapinduzi. Tandon anamweleza Abdulwahid na wazalendo wengine katika Afrika ya Mashariki kama Chege Kibachia, Makham Singh, Fred Kubai, James Kivu, I.K. Musazi, Erika Fiah na Gama Pinto kama "viongozi maveterani wa watu wa Afrika ya Mashariki ambao wanahistoria wetu wa sasa wamewasahauí." [1] Wapo waandishi wanaomuona Abdulwahid kama "kabaila uchwara" kutokana na kuwa alikuwa mtoto wa mfanyabiashara Mwafrika tajiri, Kleist Sykes.
Profesa Shivji anamtuhumu Abdulwahid kwa kushirikiana na wakoloni na anamchukulia kama kabaila uchwara ambae yeye mwenyewe hatoki katika tabaka la wafanyakazi. Akitafakari nafasi ya Abdulwahid kama kiongozi wa makuli katika bandari ya Dar es Salaam wakati wa ukoloni Shivji anasema, "Serikali ilipenyeza uongozi wa makabailauchwara katika chama. Mwezi February 1948 Abdul Sykes, mtoto wa mfanya biashara Mwafrika maarufu, aliombwa na serikali awe katibu wa chama cha makuli. Abdul Sykes hakuwa akifanyakazi bandarini wala hakuwa anatoka katika tabaka la wafanyakazi. "[1]
Hapa Shivji alikuwa anaeleza jinsi Abdulwahid alivyochaguliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza katika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika. Kwa kutoijua vyema historia ya maisha ya Abdulwahid na vilevile kwa hamaki za misimamo ya mrengo wa kushoto ya Ki-Marx, Shivji ametumia vipimo visivyo sawa katika kumchambua Abdulwahid. Engels anasema bepari uchwara ni "tabaka la makabaila wa kisasa ambao wanahodhi njia zote za uzalishaji mali za jamii na vilevile wanawaajiri na kuwalipaí."[1]Hata hivyo Sklar anasema kuwa dhana hiyo sasa imebadilika kwa hiyo hata ile maana yake ya awali imebadilika: "Hivi sasa neno hilo linatumiwa na wafuasi wa Marx kuieleza tabaka lililo juu katika jamii ambazo linafuata soko huria na kuachia kuhodhiwa kwa mali kama matokeo ya mali binafsi katika uzalishaji wake."[1]
Kama Shivji angeliyajua maisha ya Abdulwahid ni wazi kuwa angetumia kipimo kingine kabisa katika kumweleza. Lakini kwa kuwa kilichotumika ni kipimo kisicho sawa, matokeo yake hayakuweza kuwa barabara. Hakuna biashara ya Mwafrika wakati wa ukoloni inaweza kuitwa biashara ya bepari na katika mkumbo wa kujumuishwa katika dhana ya ubepari, kama ubepari ulivyokuwa ukifahamika huko Ulaya. Haya ndiyo matatizo yanayoikumba historia ya Abdulwahid na kwa kweli historia nzima ya taifa la Tanganyika.K
atika wale walioasisi TANU, ni wale tu aliokuwa makao makuu ya TAA ndiyo wanaoweza kueleza historia ya kweli yachama hiki. Hawa ni John Rupia, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Julius Nyerere, Dome Budohi, Abdulwahid na Ally Sykes. Hawa ndugu wawili, Abdulwahid na Ally, wao ni baba yao ndiye aliyekuwa muasisi wa African Association akiwa kama katibu wake wa kwanza hapo mwaka wa 1929. Majalada ya akina Sykes kuhusu African Association na TANU yana habari muhimu sana kwa mtafitikuhusu historia ya ukoloni na juhudi walizofanya waasisi wa taifa la Tanganyika katika kujikomboa. Majalada haya yana habari muhimu na za kutosha kuhusu Nyerere na jinsi alivyopokelewa Dar es Salaam na akina Sykes na jinsi alivyoingizwa katika siasa. Inastaajabisha kuwa kumbukumbu hizi zenye habari muhimu sana kuhusu Nyerere na TANU hazikuguswa kabisa wakati watafiti wa historia ya TANUwalipokuwa wakifanya utafiti wao. Inastaajabisha vilevile kuwa, si Ally wala mdogo wake, Abbas ndugu wawili walio hai baada ya kifo cha kaka yaoAbdulwahid, walifanyiwa mahojiano yoyote na watafiti wale.
Katika miaka ya mwishoni ya 1960, John Iliffe akiwa Idara ya Historia ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, alipoanza utafiti wake wa historia ya Tanzania, aliweza kukusanya habari nyingi sana na muhimu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake, Aisha Daisy Sykes, binti wa Abdulwahid. Ingawa Daisy alimfahamisha Iliffe kuwa habari zile alizokuwa akiandika katika semina kuhusu historia ya Tanganyika alikuwa akizipata kutoka kwa baba yake, inastaajabisha kuwa, Iliffe japo kuwa alikua muhihataji sana wa kutaka kujua historia ya Tanganyika, hakuchukua tabu ya kuonana na Abdulwahid ili apatehabari zile moja kwa moja kutoka kinywani kwake.Iliffe hata hivyo kwa kujua hazina ya historia iliyokuwa katika kumbukumbu za akina Sykes, alimtia hima Daisy aandike historia ya maisha ya babu yake, Kleist Sykes. Utafiti huu Daisy aliufanya kwa ufanisi mkubwa. [1]Baba yake alipofariki dunia mwaka wa 1968, Daisy kutokana na mafanikio ya kuandika habari za babu yake sasa akataka kufanya utafiti na kuandika maisha ya marehemu baba yake. Daisy aliamua kufanya hivyo kwa uchungu alipokuja kugundua kuwa historia ilikuwa haimtendei haki baba yake. Daisy alihisi ilikuwa ni wajibu wake kuueleza ulimwengu baba yake alikuwa nani na nini mchango wake katika kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza. Hiki alikiona kitu muhimu ili kuiweka sawa historia ambayo kwa makusudi ilikuwa inapotoshwa. Daisy alikuwa na majalada na shajara zote za baba yake. Iliffe kwa sababu ambazo kwa wakati ule Daisy hakuweza kuzitambua, alimkataza asifanye hivyo kwa kuwa wakati wa kuandika historia ya baba yake ulikuwa bado. Iliffe alimwambia Daisy afanye subira hadi hapo baadae. Ni wazi kuwa Iliffe alikuwa akijua kuwa Abdulwahid alikuwa mtu muhimu na wa kuaminika katika historia ya TANU; na kuwa utafiti wowote katika maisha yake kungesaidia sana kuielewa historia ya Tanzania. Kutokana na msimamo huu wa Iliffe Daisy hakujaaliwa tena kuandika maisha ya baba yake.
Historia ya TANU siku zote imekuwa ikitawaliwa na mambo kama haya.Mwaka wa 1962 Ally Sykes alijaribu kuandika historia ya TANU katika gazeti la Mambo Leo. Mhariri wa gazeti lile M.J. Sichwale alimuandikia Ally Sykes kumfahamisha kuwa hawezi kuchapisha makala yake kwa kuwa mwandishi hana utaalamu na somo aliloliandikia.[1]TAA ilipogeuzwa kuwa TANU, wanaharakati wa TAA, labda kwa kuanza kuhisi kuwa historia yao ilikuwa inataka kupotoshwa na wale waliokuja katika siasa na TANU, walikuwa na fikra za kuandika historia ya TANU. Mwalimu Kihere, mmoja wa viongozi wa TAA Tanga, alipata wakati fulani kumwambia Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia kuwaingekuwa vyema historia ya siasa katika Tanganyika ikaandikwa na kuhifadhiwa wakati wao wangali hai kuepusha kuingizwa uongo ndani yake na kupindisha ukweli na hao watakaokuja hapo baadae baada ya wao kutoweka. Bahati mbaya wazo hili halikupewa uzito iliostahili na hadi Mwalimu Kihere, Abdulwahid na John Rupia, Stephen Mhando na Hassan Suleiman wanafariki dunia, hakuna hata mmoja katika wale wakongwe wa siasa alikuwa wameandika kitu chochote.
Hassan Suleiman anawalaumu wanahistoria kwa kukosekana kuandikwa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika kwa kuwapuuza wazalendo wengine na badala yake kuandika historia ya Tanganyika kwa kuegemeza historia hiyo kwa Nyerere. Kabla hajafariki, Hassan Suleiman alichukua nyaraka zake zote binafsi za African Association wakati alipokuwa kiongozi na kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati ule Rashid Kawawa katika sherehe mahsusi iliyofanyika Makao Makuu ya CCM, Dodoma. Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na Abdulwahid mwenyewe. Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana Nyerere wakati ule Waziri Mkuu alimuomba Abdulwahid aandike historia ya harakati ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza. Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU. Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Marekani alichaguliwa na TANU asaidiane na Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa historia ile.
Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA. Nyaraka zake binafsi, za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo. Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakumpendeza Nyerere, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid ñ Kleist Sykes, lilikuwa likitawala. Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watotowake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile. Historia hii inasemekana haikumpendeza Nyerere na baadhi ya viongozi wa TANU. Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika bali nia na azma yao ilikuwa na kumjenga Nyerere na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili. Abdulwahid alipongíamua hili haraka akajitoa katika kazi ile. Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii iansemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU. Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam. Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ëmwandishií kufanya mabadiko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake. Hata hivyo TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu na wakafanya bidii kuzuia isichapishwe. Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili. Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa. Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.
Hata hivyo kuna kasoro katika kitabu hicho ambacho ëmwandishií alishindwa kugundua na kuweza kujikinga asijulikane kama kile kitabu hakikuandikwa na kalamu yake. ëMwandishií kama tunavyoweza kumwita, akiandika katika nafsi ya kwanza, anaeleza kuwa amekiandika kitabi kile mwaka wa 1964. Katikamaelezo hayo ëmwandishií anatoa habari ambazo msomaji makini anahisi kuwa ëmwandishií alikuwa marika sawa na anawafahamu vyema wale wazalendo anaoandika habari zao. Lakini mwandishi anasahau kuwa mwaka 1964 wakati yeye anadai alikuwa akiandika habari hizo yeye alikuwa mvulana mdogo na asingeweza kuwajua vile wale wazalendo na habari zilizotokea miaka ya 1950 wala asingeweza kuwa na ubongo wa kutafakari mambo kama yale. Sasa swali linakuja. Huyu aliyeandika habari zile ni nani hasa?Kutokana na maelezo ambayo kitabu hiki kimeeleza ni wazi aliyeandika habari zile hawezi kuwa Dr Kleruu kwa sababu Kleruu katika kipindi kile, hakuwapo katika harakati zile za kuunda TANU. Ni mtu mmoja tu ndiye anaeweza kuwa na habari zile na kuwa na ufahamu wa mambo yalivyokuwa miaka ile. Huyu atakuwa ni marehemu Abdulwahid akiandika mwaka 1964. ëMwandishií kwa ujinga amenakili kutoka kwenye maandishi ya Abdulwahid ambayo yalikuwa yamehifadhiwa katika Maktaba ya TANU, Dar es Salaam. Na huyu ëmwandishií wala hakunakili maandishi yale mwaka 1964, bali miaka mingi baada ya kifo cha Abdulwahid kutokea.
Abdulwahid alipobaini kuwa historia ya Tanganyika inaweza kuwa chanzo cha husda na hasama kati yake na Nyerere na viongozi wengine wa TANU, akaamua kutosema chochote kuhusu hilo ingawa kabla hajafa alikubali mwaliko wa Chama Cha Historia Cha Tanzania (Historical Association of Tanzania) (HAT). Imeshindikana kujua Abdulwahid alizungumza kuhusu nini katika mwaliko ule, lakini inasemekana moja ya maswali aliyoulizwa ilikuwa kuwa kama si kweli Nyerere ndiye aliyekipa chama uhai kuanzia mwaka wa 1954. Katika kujibu swali hili Abdulwahid alilirudisha swali lile kwa wasikilizajiwake kwa kutoa mfano wa John Glenn, Mmarekani wa kwanza kwenda angani kuzunguka dunia. Abdulwahid aliwauliza wasikilizaji wake, ëNani apewe sifa, wanasayansi wa Kimarekani waliotengeneza roketi ile au John Glenn aliyekuwa rubani wa chombo?í
Mwaka 1962 Judith Listowel alipokuja Tanganyika kufanya utafiti kabla hajaandika kitabu chake The Making of Tanganyika, alitaka sana kufanya mahojiano na Abdulwahid. Kwa kujua matatizo yaliyokuwa yanakabili historia ya Tanganyika mara ya kwanza ilipojaribiwa kuandikwa, Abdulwahid alijaribu sana kumkwepa Listowel.Listowel alipokuja kumkamata Abdulwahid nyumbani kwake Magomeni Mikumi, yeye hakupenda kueleza mchango wake wala wababa yake katika kuaisisi African Association na TANU. Kwa kweli katika mahojiano yake Listowel hakupata chochote cha maana sana. Hata hivyo Listowel aliweza kuelezwa na Abdulwahid jinsi TANU ilivyokuja kuasisiwa. Listowel alikuja kuandika katika kitabu chake kuwa: "Abdul Sykes, kaka yake Ally, alisema kuwa ilibidi waamshe fikra za siasa za wananchi ili kiundwe chama cha siasaí."[1]Kutokana na mazungumzo haya na Abdulwahid, Listowel alimwandikia Ally Sykes: "Nimependezwa sana na kaka yako na ningefurahi kama ningepata wasaa wa kuwa na mazungumzo na yeye zaidií."[1]Akiwa London Listowel alimuandikia Ally Sykes mara kadhaa akitaka ufafanuzi kuhusu mambo mengi muhimu katika historia ya Tanganyika.
Abdulwahid alipofariki Wizara ya Habari ilitoa taarifa ikieleza kuwa Rais Nyerere amehudhuria maziko ya Abdulwahid Sykes.[1]Kingine kinachostaajabisha ni kuwa taarifa ile ilitoa maelezo machache ya uajiriwa wake katika serikali na kuacha maelezo muhimu ya Abdulwahid katika siasa. Ilikuwa Mwingereza, Brendon Grimshaw, mhariri wa Tanganyika Standard, ndiye aliyempa Abdulwahid heshima na hadhi anayostahili baada ya kifo chake kwa kuchapisha taaízia ambayo ilimweleza Abdulwahid kama "Mmoja wa wapangaji wa vuguvugu la kudai uhuru na mmoja wa watu waliomsaidi Nyerere kuingia katika siasa."
Taaízia ile ilitoa sifa kemkem kwa ukoo wa Sykes katika kuleta maendeleo ya siasa Tanganyika kwa kusema kuwa, "Msukumo mkubwa wa Waafrika wa Tanganyika kupata chamacha siasa chenye nguvu ulitokana na juhudi za ukoo wa Sykes" 1]Inasemekana taaízia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU. Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu kumtukuza kaka yao. Hali hii ilijitokeza tena wakati CCM ilipokuwa ikitafiti historia yake. Hassan Upeka,[1]mmoja katika wasaidizi wa utafiti ule alipeleka katika jopo lile la utafiti na uandishi wa historia ya TANU, mahojiano aliyofanya na Abdulwahid miaka mingi iliyopita kuhusu historia ya TANU. Hassan Upeka alifahamishwa kuwa historia inayoandikwa haimhusu Abdulwahid Sykes."

Mohamed
 
Sanda Matuta, na wewe ulisimuliwa na wazee wako ama ulikuwapo ili nijue namna ya kukujibu. Kama ulikuwapo kwenye miaka ya 1950 hadi uhuru ulikuwa na umri gani ? Siulizi hivi kwa lengo baya, nataka tu nijue kama unaeleza uliyoshuhudia au uliyosimuliwa.

Wala usipate shida mkuu,mimi nilisimuliwa na aliye nisumulia bado yuko hai.
Wakati Nyerere ameenda kwa Sheikh Ramia B'moyo huyu aliyenisimulia ni kijana wa miaka zaidi ya kumi na tano akipanga viti vya mkutano
 
"Jina la Abdulwahid halitajwi kabisa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika au katika historia ya kuasisi TANU. Juu ya haya yote Abdulwahid ndiye aliyewasha cheche za kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Mohamed

Hii ilishafutwa kwani harakati za uhuru Tanganyika hazikuanzia Dar-es-Salaam kulikuwa na watu wengine nje ya Dar ambao nao katika maeneo yao walianzisha cheche za kudai uhuru. Ni sahihi kusema tu kuwa kwa eneo la Dar mzee Sykes yumkini ndiye aliyekuwa mwanzo wa cheche za uhuru.
 
Sheikh mohamed,
nia yangu sio unitajie vyanzo vyako vya habari, maana hizi ni nyeti zinahitaji usiri. Zile ambazo si nyeti sana umekuwa ukibainisha vyanzo vyake.

Ninachokusudia hapa ni kutaka kufahamu kama umewahi kumhoji mzee mwinyi kuhusu jambo hilo, lengo ni kutanzua huu utata. Bila shaka utakuwa umenielewa!

MM,

Siingii katika hilo dema.

Mohamed
 
Hii ilishafutwa kwani harakati za uhuru Tanganyika hazikuanzia Dar-es-Salaam kulikuwa na watu wengine nje ya Dar ambao nao katika maeneo yao walianzisha cheche za kudai uhuru. Ni sahihi kusema tu kuwa kwa eneo la Dar mzee Sykes yumkini ndiye aliyekuwa mwanzo wa cheche za uhuru.

Mwanakijiji,

Hilo linawezekama sana lakini litasimama vizuri na kuingizwa katika historia kama utapatikana ushahidi. Kila siku sishi kusema kuwa kama nanyi mna wazee wenu waliopigania uhuru itakuwa vyema kama mtaandika habari zao tuzisome hapa ukumbini.

Inaelekea hili limekushindeni maana naona maswali ya kupinga historia yangu iliyofanyiwa utafiti na na nyaraka zipo hadi leo.

hivi wale unaowaita ni "wazee wako" sisi Watanzania wengine hatuwezi kuwatambua kuwa ni "wazee wetu" pia... ? au wazee wako ni wako tu maana kama ni wako tu kwanini sisi wengine tutakiwe kuwasoma?
 
Back
Top Bottom