Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nimekusoma lakini hakuna ambacho Nyerere alisea dhidi ya Uislamu au Waislamu thanks.
 
Mohamed, swali ni kuwa Nyerere alifika Dar es Salaam mwaka gani, sio lini baba yako alitambulishwa na Sykes.

Nimeshawaeleza wana ukumbi kuwa sisi watu wa pwani hatujui matusi ya moja kwa moja ila yale ya lugha. Ghafla umesahau kuwa ulisema Nyerere akija Dar wazee wako wamemuona si chochote si lolote. Haya si maneno ya stara hata kidogo. Unachokifanya kwenye makala zako kueleza kitoweo, alipolala ni kumdhalilisha ambako si lazima kuwe tusi.

Nimeonyesha hapa Jamvini jinsi ulivyoelezea picha ya Dodoma. Yote ile ni kujaribu kuonyesha udhalili fulani kwa hali ya kujinasibu kipwani. Kwamba wawili wana tai wawili hawahitaji identity na Nyerere ambaye haihitaji identity ndiye umemwelezea Mwenye soksi ndefu. Halafu unasema huna matusi.

Unaposema kavunja baraza la wazee wakati hujui amekaa nani kufanya hivyo sio kumtusi huko. Hakuna tatizo ukiandika kurasa 1000 za kumtusi kwani si wewe wa kwanza, tatizo ni pale unapotaka kutufanya mazuzu. Wapo watakaosema hewala bwana lakini sio kila mmoja. Sisi tuatakwambia hapa mzee Hongera, hapa no, hapa umebofua, hili umezusha, n.k

Hakuna tusi kubwa kama kufarakanisha watu bila sababu.
 
Mfano wako huu ni mzuri sana; civil rights ilikuwa siyo kwa ajiliya kuonesha chuki dhidi ya weupe bali kuonesha ubovu wa mfumo wa ukandamizaji. Matokeo yake hata watu weupe wengi walishiriki kwa sababu walikubaliana na msingi (premise) ya hoja. Kina Martin Luther walikuwa hawahubiri chuki dhidi ya watu weupe hata chembe, walikuwa hata hawahubiri chuki dhidi ya vyama vya siasa; walikuwa wanahubiri chuki ya mfumo mbaya na waliutambua mfumo huo kuwa msingi wake na sera yake ni ubaguzi wa rangi.

Hoja zao zilikuwa universal na ukweli wake ulikuwa intrinsic in nature. Ndio maana kuna post moja jana niliandika kwa M. SAid sijui hata kama aliijibu kuwa anakemea mfumo ambao haupo; Mfumo Kristu unaodaiwa haupo upo mfumo ufisadi lakini yeye na wengine wenye kukubaliana naye hawataki kuungalia. Wanapozungumzia "mfumo Kristu" utafikiri wanasema kuwa hakuna Wakristu maskini, hakuna wakristu ambao maisha yao na ya watoto na familiia zao yanaathiriwa na mfumo wa ufisadi. Kw akujaribu kuangalia matatizo ya mfumo wetu kuwa ni ya kidini badala ya corruption - M. Said na wengine wanapoteza sana.

Na bahati mbaya badala ya kuwaleta pia Wakristu waone uzito wa hoja zao na uhalali wake wanatumia muda mrefu kuwashambulia hata Wakristu ambao kimsingi wanatambua dhulma inayoletwa na ufisadi. Wenye imaTukubaliane kwanza kuwa tatizo letu kama taifa ni ufisadi ambao unaathiri Wakristu na Waislamu,ni na wasio na imani, Waswahili na Wachagga, Wazaramo na Wasukuma na kutoka hapo kwa pamoja tukitumia kanuni za haki, usawa, utu na upendo kuweza kuuvunja vunja mfumo huu ili tujenge mfumo ambao utaheshimu utu na haki ya kila Mtanzania bila kujali wazazi wake wanavaa nguo gani, wanasali wapi au majina yao yanaendana na dini gani.

Unasemaje?

Sasa ukija ktk hiyo point unayosema, kwanza lazima ukubali (mkubali) kwamba Nyerere ndiye aliyekuwa part of the problem.
 
Na ninyi je, hichi anachowapandikizia Mohammed Said ni nini? Mapenzi kwa Wakristo? Unapomnyooshea mtu kidole kumbuka vinne vinakunyooshea weye.

Tunawaambia tuonesheni hapo anapokosea Mohamed Said, hamtuoneshi. Mohamesd Said yupo hapa hapa hajajificha kujibu, mmekazana anapandikiza anapandikiza, mimi nawaambia nyinyi mmeshapanda, mmepalilia na sasa bado kuvuna tu. Msomeni vizuri Mohamed Said, anafanya kila jitihada mavuno yasiwepo.
 
Hik

Hik,

Kitabu kilikuja Tanzania miezi ya mwisho 1998 sijua mwezi kwa hakika mpaka nitama nakala yangu nilyotia sahihi na kilimfikia muda mfupi sana toka kitue nchini.

Nasikia nakala ipo katika maktaba yake.

Mohamed
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?
 
ooh noooo.. miye nauliza maswlai ili nijue zaidi; lakini sikubali majibu yasiyoweza kushawishi akili kwa sababu tu mtu anayeyota anadai ni ya kweli. Hatuzungumzi hesabu hapa wala hatubishanii kanuni fulani ya kupata jawabu la formula ya kikemia. Tunachozungumzia ni vitu ambavyo viko very subjective katika historia.

Sasa mtu akisema "Bw. X alisema b, c na z" tunaweza tukakubali lakini tukikubali bila kuuliza alisema wapi, lini na kwa nani na kuna ushahidi gani tutakuwa hatujitendei haki katika jitihada ya kutaka kujua zaidi. Binafsi ningependa sana Bw. Said atuambiea vile ambavyo ni factual au historical facts ambavyo mtu yeyote anaweza kuviona au kuvifuatilia na kuvithibitisha. Hapa ndipo penye kujifunza.

Bahati mbaya wengine hawataki kujifunza kutoka kwa Bw. Said wanataka tukubali kwa sababu "Bw. Said kasema".

Well, wewe ni mmoja wao?

Mohamed Said amakuambia usijipe taabu, wala huna haja ya kuamini. Si ukafanye research zako uje na different story. Mpaka sasa umeshindwa, umekazana nani, lini, nani, lini?
 
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?

Unakumbuka katika sifa moja mbaya ya Mwalim ni kuitwa "Haambiliki"? na ambayo alikuwa haipendi kuliko zote, jiulize kwa nini?
 
Unakumbuka katika sifa moja mbya ya Mwalim ni kuitwa "Haambiliki"? na ambayo alikuwa haipendi kuliko zote, jiulize kwa nini?
Huu sasa ni "Utanzania" Faiza! Mtanzania ukimuuliza swali hakujibu. Anakuuliza lingine!
 
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?

WC,

Katika shughuli hizi za "academics" moja ya hatari yake ni hiyo. Kuna watakaokupuuza. Kuna watakaokutia maanani. Sasa msomi makini kazi yake ni kupima nani kampuuza na kwa sababu gani.

Msomi makini kazi yake ni kupima wanaomuunga mkono wanamuunga kwa sababu zipi.

Huo ndiyo usomi.

Kitabu cha Abdu Sykes kilipata "review" katika Cambridge Journal of African History. Hii ni katika mambo ambayo mimi binafsi yameniweka pazuri. Haingii humo mtu sharti alete kitu cha maana.

Mohamed Said nimo humo.

Sitaki kwa sasa kukuambia nani aliandika review hiyo nitasema wakati wake ukifika.

Marekani nako James Brenan na Jonathan Glassman wasomi vijana mabingwa wa historia ya Tanganyika nao wakafanya review ya kitabu changu katika majarida ya Kimarekani.

(Hawa wasomi bingwa wa historia ya Tanganyika nimeadhiri nao jukwaa moja Marekani).

Baada ya review hizo kitabu kikanunuliwa kama "maandazi ya moto."

Kila maktaba niliyofika Marekani na Ulaya kitabu changu wanacho.

Sasa ikiwa Nyerere kanipuuza hiyo ni bahati mbaya sana.

Kwangu mimi kwake yeye ni kuwa kanisoma na kajua wazee wangu walikuwa wamemuweka katika fungu gani.

Nitake nini zaidi ya kushukuru?

Mohamed
 
Swali liko wapi ulipoitowa hiyo? Halafu labda mwenzetu wewe si Mtanzania.
Mimi ni Mtanzania hasa Faiza. Sisumbuliwi na DINI, CHAMA, KABILA wala ufuasi kwa yeyote. Nimeuliza ulipata kusikia majibu ya Mwalimu kwa hoja ya kipuuzi kama hii ya Mohamed kwa Mwandishi mmoja pale Nairobi?
 
WAKRISTO wa huko ni tofauti na UKRISTO huu alookuwa nao Mwalimu wa kuwasahau wazee wako wa Kiislamu? Ni bahati mbaya tu Mwalimu alikufa bila kuandika historia ya Nchi hii. Pateni muda wa kuzisikiliza hotuba zake.
 
Mohamed, swali ni kuwa Nyerere alifika Dar es Salaam mwaka gani, sio lini baba yako alitambulishwa na Sykes.

Nimeshawaeleza wana ukumbi kuwa sisi watu wa pwani hatujui matusi ya moja kwa moja ila yale ya lugha. Ghafla umesahau kuwa ulisema Nyerere akija Dar wazee wako wamemuona si chochote si lolote. Haya si maneno ya stara hata kidogo. Unachokifanya kwenye makala zako kueleza kitoweo, alipolala ni kumdhalilisha ambako si lazima kuwe tusi.

Nimeonyesha hapa Jamvini jinsi ulivyoelezea picha ya Dodoma. Yote ile ni kujaribu kuonyesha udhalili fulani kwa hali ya kujinasibu kipwani. Kwamba wawili wana tai wawili hawahitaji identity na Nyerere ambaye haihitaji identity ndiye umemwelezea Mwenye soksi ndefu. Halafu unasema huna matusi.

Unaposema kavunja baraza la wazee wakati hujui amekaa nani kufanya hivyo sio kumtusi huko. Hakuna tatizo ukiandika kurasa 1000 za kumtusi kwani si wewe wa kwanza, tatizo ni pale unapotaka kutufanya mazuzu. Wapo watakaosema hewala bwana lakini sio kila mmoja. Sisi tuatakwambia hapa mzee Hongera, hapa no, hapa umebofua, hili umezusha, n.k

Hakuna tusi kubwa kama kufarakanisha watu bila sababu.

Nguruvu3,

Mimi nakutaka radhi kwa wewe kuumuzwa na lugha na vitendo vyangu. Lakini nakuhakikishia hiyo haikuwa nia yangu. Tusameheane na tuendelee na mjadala.

JF ni kubwa kuliko hisia zangu na zako na za yeyote yule na ndiyo maana katutandikia jamvi tumekaa kwa raha mustarehe tunajadili.

Hatuna cha kumlipa JF isipokuwa sisi tuoneshe ukomavu wa fikra.

Hisani anotufanyia JF ni kubwa kupita kiasi.

Niwie radhi ndugu yangu.

Mohamed
 
Mimi ni Mtanzania hasa Faiza. Sisumbuliwi na DINI, CHAMA, KABILA wala ufuasi kwa yeyote. Nimeuliza ulipata kusikia majibu ya Mwalimu kwa hoja ya kipuuzi kama hii ya Mohamed kwa Mwandishi mmoja pale Nairobi?

Sijapata kusikia. Halafu nioneshe huo upuuzi wa Mohamed Said uko wapi? naona unaandikia mate na wino upo, leta upuuzi wake tuuone na utuoneshe ule wako usio upuuzi.

Jee, wewe umepata kusikia kuwa Nyerere alikuwa na sifa moja mbaya akiitwa "Haambiliki"?
 
Watu wa msimamo kwa masuala ya msingi kama Mwalimu hii sifa haikwepeki.
 
WAKRISTO wa huko ni tofauti na UKRISTO huu alookuwa nao Mwalimu wa kuwasahau wazee wako wa Kiislamu? Ni bahati mbaya tu Mwalimu alikufa bila kuandika historia ya Nchi hii. Pateni muda wa kuzisikiliza hotuba zake.

WC,

Nilidhani utaendelea na mimi kupuuzwa...

Si rahisi kunipuuza mimi wengi wamejaribu wameshindwa na si kama najigamba.
Nakupa taarifa hizi ili tujuane vizuri.

Sasa tuje katika "bahati mbaya" ya Nyerere kutoandika historia. Historia iliandikwa
na Abdu Sykes na Kleruu na Nyerere ndiye aliyekua akisimamia kazi hii.

Mswada wake ulikuwapo pale Maktaba ya TANU. Mswada huu umetoweka kama
zilivyotoweka nyaraka nyingine muhimu za kihistoria.

Nyerere alikuwa anaogopa kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sababu ingebidi
yeye awe mmoja kati ya wengi.

Hili hakulipenda.

Angalia hivi tunavyopata shida leo ya kusema nani kafanya nini na nani alikuwa nani baada
ya mimi ghafla kumpachika Abdu Sykes katika historia ya kupigania uhuru.

Si unaona mnakasha ulivyokuwa mkali hapa? Hadi naitwa muongo naleta fitna nk. nk.

Jiulize kwa nini iwe hivi.

AA kaianzisha baba yake Abdu, Mzee Kleist. Ofisi ya AA kajenga baba yake Abdu, Mzee Kleist.

Abdu kawa secretary wa TAA 1950, Rais wa TAA 1952 mmoja wa waasisi wa TANU yeye na
mdogo wake Ally. Kadi ya Abdu na. 3 ya Ally na 2 Nyerere na 1.

Nyaraka zote za harakati Abdu kafa kawaachia wanawe. Iweje historia ya TANU iandikwe Abdu hayumo?

Hiki si kizungumkuti?

Tutaendelea.

Kwa sasa Wild Card tusimame hapa (jina lako linanikumbusha wakati nasoma dos commands).

Mohamed
 
Mzee Said unafikiri ni kwa kiasi gani mfumo wa ufisadi na vitendo vinavyotokea kwenye mfumo huo (wizi wa EPA, manunuzi ya ndege ya rais na rada na ubadhirifu wa mali ya umma pamoja na matumizi mabaya ya mabaraka - nikitaja vichache) umeathiri maisha ya mamilioni ya Waislamu wa Tanzania?
 
WC,

Nilidhani utaendelea na mimi kupuuzwa...

Si rahisi kunipuuza mimi wengi wamejaribu wameshindwa na si kama najigamba.
Nakupa taarifa hizi ili tujuane vizuri.

Sasa tuje katika "bahati mbaya" ya Nyerere kutoandika historia. Historia iliandikwa
na Abdu Sykes na Kleruu na Nyerere ndiye aliyekua akisimamia kazi hii.

Mswada wake ulikuwapo pale Maktaba ya TANU. Mswada huu umetoweka kama
zilivyotoweka nyaraka nyingine muhimu za kihistoria.

Nyerere alikuwa anaogopa kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sababu ingebidi
yeye awe mmoja kati ya wengi.

Hili hakulipenda.

Angalia hivi tunavyopata shida leo ya kusema nani kafanya nini na nani alikuwa nani baada
ya mimi ghafla kumpachika Abdu Sykes katika historia ya kupigania uhuru.

Si unaona mnakasha ulivyokuwa mkali hapa? Hadi naitwa muongo naleta fitna nk. nk.

Jiulize kwa nini iwe hivi.

AA kaianzisha baba yake Abdu, Mzee Kleist. Ofisi ya AA kajenga baba yake Abdu, Mzee Kleist.

Abdu kawa secretary wa TAA 1950, Rais wa TAA 1952 mmoja wa waasisi wa TANU yeye na
mdogo wake Ally. Kadi ya Abdu na. 3 ya Ally na 2 Nyerere na 1.

Nyaraka zote za harakati Abdu kafa kawaachia wanawe. Iweje historia ya TANU iandikwe Abdu hayumo?

Hiki si kizungumkuti?

Tutaendelea.

Kwa sasa Wild Card tusimame hapa (jina lako linanikumbusha wakati nasoma dos commands).

Mohamed
Mohamed mara nyingi haujibu ulichoulizwa. Tanganyika haikuwahi kuwa koloni la Mwingereza. Huku kupigania UHURU unakokukuza sana hapa sielewi kunatoka wapi. Najua unajua zipo Nchi zilizopigania uhuru kwelikweli. Hivi Mzee wetu Kleist alianzisha AA kwa kuwa alikuwa MUISLAMU? Mohamed, acha pia kuwasingizia marehemu wetu hawa mambo mengi kwa kuwa unajua hawapo tena duniani.
 
Nadhani hapo watu wako kwenye kupinga tu...na wala haito tufikisha kokote kama hamuwezi kuchagua haki na kuifata,hii inakumbusha ule msemo wa "mfa maji,haishi kutapata" mara hili mara lile kwa kigezo cha kujiita "censors" "see things in a big picture".
Gazeti la Mwananchi leo tena kwaniaba ya "muhandishi wetu" kuna interview ya Sihiyana Mandevu dereva wa tax aliye kuwa akimbeba Nyerere toka wakati wa mtaa wa pemba na New street,Kkoo na New street na wajumbe walele hadi St Joseph ambapo huku wajumbe walibadilika kuwa wengine ambao hakuwafahamu,sasa kama kweli we claim to see thing in that "big picture"....why then we don't connect the dots!!?? Hauitaji kwenda Bweni kujifunza
 
Back
Top Bottom