Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nimekusoma lakini hakuna ambacho Nyerere alisea dhidi ya Uislamu au Waislamu thanks.
 
Mohamed, swali ni kuwa Nyerere alifika Dar es Salaam mwaka gani, sio lini baba yako alitambulishwa na Sykes.

Nimeshawaeleza wana ukumbi kuwa sisi watu wa pwani hatujui matusi ya moja kwa moja ila yale ya lugha. Ghafla umesahau kuwa ulisema Nyerere akija Dar wazee wako wamemuona si chochote si lolote. Haya si maneno ya stara hata kidogo. Unachokifanya kwenye makala zako kueleza kitoweo, alipolala ni kumdhalilisha ambako si lazima kuwe tusi.

Nimeonyesha hapa Jamvini jinsi ulivyoelezea picha ya Dodoma. Yote ile ni kujaribu kuonyesha udhalili fulani kwa hali ya kujinasibu kipwani. Kwamba wawili wana tai wawili hawahitaji identity na Nyerere ambaye haihitaji identity ndiye umemwelezea Mwenye soksi ndefu. Halafu unasema huna matusi.

Unaposema kavunja baraza la wazee wakati hujui amekaa nani kufanya hivyo sio kumtusi huko. Hakuna tatizo ukiandika kurasa 1000 za kumtusi kwani si wewe wa kwanza, tatizo ni pale unapotaka kutufanya mazuzu. Wapo watakaosema hewala bwana lakini sio kila mmoja. Sisi tuatakwambia hapa mzee Hongera, hapa no, hapa umebofua, hili umezusha, n.k

Hakuna tusi kubwa kama kufarakanisha watu bila sababu.
 

Sasa ukija ktk hiyo point unayosema, kwanza lazima ukubali (mkubali) kwamba Nyerere ndiye aliyekuwa part of the problem.
 
Na ninyi je, hichi anachowapandikizia Mohammed Said ni nini? Mapenzi kwa Wakristo? Unapomnyooshea mtu kidole kumbuka vinne vinakunyooshea weye.

Tunawaambia tuonesheni hapo anapokosea Mohamed Said, hamtuoneshi. Mohamesd Said yupo hapa hapa hajajificha kujibu, mmekazana anapandikiza anapandikiza, mimi nawaambia nyinyi mmeshapanda, mmepalilia na sasa bado kuvuna tu. Msomeni vizuri Mohamed Said, anafanya kila jitihada mavuno yasiwepo.
 
Hik

Hik,

Kitabu kilikuja Tanzania miezi ya mwisho 1998 sijua mwezi kwa hakika mpaka nitama nakala yangu nilyotia sahihi na kilimfikia muda mfupi sana toka kitue nchini.

Nasikia nakala ipo katika maktaba yake.

Mohamed
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?
 

Mohamed Said amakuambia usijipe taabu, wala huna haja ya kuamini. Si ukafanye research zako uje na different story. Mpaka sasa umeshindwa, umekazana nani, lini, nani, lini?
 
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?

Unakumbuka katika sifa moja mbaya ya Mwalim ni kuitwa "Haambiliki"? na ambayo alikuwa haipendi kuliko zote, jiulize kwa nini?
 
Unakumbuka katika sifa moja mbya ya Mwalim ni kuitwa "Haambiliki"? na ambayo alikuwa haipendi kuliko zote, jiulize kwa nini?
Huu sasa ni "Utanzania" Faiza! Mtanzania ukimuuliza swali hakujibu. Anakuuliza lingine!
 
Mwalimu atakuwa alikusoma na kukupuuza sana tu. Unakumbuka yale majibu yake kwa mwandishi mmoja pale Nairobi?

WC,

Katika shughuli hizi za "academics" moja ya hatari yake ni hiyo. Kuna watakaokupuuza. Kuna watakaokutia maanani. Sasa msomi makini kazi yake ni kupima nani kampuuza na kwa sababu gani.

Msomi makini kazi yake ni kupima wanaomuunga mkono wanamuunga kwa sababu zipi.

Huo ndiyo usomi.

Kitabu cha Abdu Sykes kilipata "review" katika Cambridge Journal of African History. Hii ni katika mambo ambayo mimi binafsi yameniweka pazuri. Haingii humo mtu sharti alete kitu cha maana.

Mohamed Said nimo humo.

Sitaki kwa sasa kukuambia nani aliandika review hiyo nitasema wakati wake ukifika.

Marekani nako James Brenan na Jonathan Glassman wasomi vijana mabingwa wa historia ya Tanganyika nao wakafanya review ya kitabu changu katika majarida ya Kimarekani.

(Hawa wasomi bingwa wa historia ya Tanganyika nimeadhiri nao jukwaa moja Marekani).

Baada ya review hizo kitabu kikanunuliwa kama "maandazi ya moto."

Kila maktaba niliyofika Marekani na Ulaya kitabu changu wanacho.

Sasa ikiwa Nyerere kanipuuza hiyo ni bahati mbaya sana.

Kwangu mimi kwake yeye ni kuwa kanisoma na kajua wazee wangu walikuwa wamemuweka katika fungu gani.

Nitake nini zaidi ya kushukuru?

Mohamed
 
Swali liko wapi ulipoitowa hiyo? Halafu labda mwenzetu wewe si Mtanzania.
Mimi ni Mtanzania hasa Faiza. Sisumbuliwi na DINI, CHAMA, KABILA wala ufuasi kwa yeyote. Nimeuliza ulipata kusikia majibu ya Mwalimu kwa hoja ya kipuuzi kama hii ya Mohamed kwa Mwandishi mmoja pale Nairobi?
 
WAKRISTO wa huko ni tofauti na UKRISTO huu alookuwa nao Mwalimu wa kuwasahau wazee wako wa Kiislamu? Ni bahati mbaya tu Mwalimu alikufa bila kuandika historia ya Nchi hii. Pateni muda wa kuzisikiliza hotuba zake.
 

Nguruvu3,

Mimi nakutaka radhi kwa wewe kuumuzwa na lugha na vitendo vyangu. Lakini nakuhakikishia hiyo haikuwa nia yangu. Tusameheane na tuendelee na mjadala.

JF ni kubwa kuliko hisia zangu na zako na za yeyote yule na ndiyo maana katutandikia jamvi tumekaa kwa raha mustarehe tunajadili.

Hatuna cha kumlipa JF isipokuwa sisi tuoneshe ukomavu wa fikra.

Hisani anotufanyia JF ni kubwa kupita kiasi.

Niwie radhi ndugu yangu.

Mohamed
 
Mimi ni Mtanzania hasa Faiza. Sisumbuliwi na DINI, CHAMA, KABILA wala ufuasi kwa yeyote. Nimeuliza ulipata kusikia majibu ya Mwalimu kwa hoja ya kipuuzi kama hii ya Mohamed kwa Mwandishi mmoja pale Nairobi?

Sijapata kusikia. Halafu nioneshe huo upuuzi wa Mohamed Said uko wapi? naona unaandikia mate na wino upo, leta upuuzi wake tuuone na utuoneshe ule wako usio upuuzi.

Jee, wewe umepata kusikia kuwa Nyerere alikuwa na sifa moja mbaya akiitwa "Haambiliki"?
 
Watu wa msimamo kwa masuala ya msingi kama Mwalimu hii sifa haikwepeki.
 
WAKRISTO wa huko ni tofauti na UKRISTO huu alookuwa nao Mwalimu wa kuwasahau wazee wako wa Kiislamu? Ni bahati mbaya tu Mwalimu alikufa bila kuandika historia ya Nchi hii. Pateni muda wa kuzisikiliza hotuba zake.

WC,

Nilidhani utaendelea na mimi kupuuzwa...

Si rahisi kunipuuza mimi wengi wamejaribu wameshindwa na si kama najigamba.
Nakupa taarifa hizi ili tujuane vizuri.

Sasa tuje katika "bahati mbaya" ya Nyerere kutoandika historia. Historia iliandikwa
na Abdu Sykes na Kleruu na Nyerere ndiye aliyekua akisimamia kazi hii.

Mswada wake ulikuwapo pale Maktaba ya TANU. Mswada huu umetoweka kama
zilivyotoweka nyaraka nyingine muhimu za kihistoria.

Nyerere alikuwa anaogopa kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sababu ingebidi
yeye awe mmoja kati ya wengi.

Hili hakulipenda.

Angalia hivi tunavyopata shida leo ya kusema nani kafanya nini na nani alikuwa nani baada
ya mimi ghafla kumpachika Abdu Sykes katika historia ya kupigania uhuru.

Si unaona mnakasha ulivyokuwa mkali hapa? Hadi naitwa muongo naleta fitna nk. nk.

Jiulize kwa nini iwe hivi.

AA kaianzisha baba yake Abdu, Mzee Kleist. Ofisi ya AA kajenga baba yake Abdu, Mzee Kleist.

Abdu kawa secretary wa TAA 1950, Rais wa TAA 1952 mmoja wa waasisi wa TANU yeye na
mdogo wake Ally. Kadi ya Abdu na. 3 ya Ally na 2 Nyerere na 1.

Nyaraka zote za harakati Abdu kafa kawaachia wanawe. Iweje historia ya TANU iandikwe Abdu hayumo?

Hiki si kizungumkuti?

Tutaendelea.

Kwa sasa Wild Card tusimame hapa (jina lako linanikumbusha wakati nasoma dos commands).

Mohamed
 
Mzee Said unafikiri ni kwa kiasi gani mfumo wa ufisadi na vitendo vinavyotokea kwenye mfumo huo (wizi wa EPA, manunuzi ya ndege ya rais na rada na ubadhirifu wa mali ya umma pamoja na matumizi mabaya ya mabaraka - nikitaja vichache) umeathiri maisha ya mamilioni ya Waislamu wa Tanzania?
 
Mohamed mara nyingi haujibu ulichoulizwa. Tanganyika haikuwahi kuwa koloni la Mwingereza. Huku kupigania UHURU unakokukuza sana hapa sielewi kunatoka wapi. Najua unajua zipo Nchi zilizopigania uhuru kwelikweli. Hivi Mzee wetu Kleist alianzisha AA kwa kuwa alikuwa MUISLAMU? Mohamed, acha pia kuwasingizia marehemu wetu hawa mambo mengi kwa kuwa unajua hawapo tena duniani.
 
Nadhani hapo watu wako kwenye kupinga tu...na wala haito tufikisha kokote kama hamuwezi kuchagua haki na kuifata,hii inakumbusha ule msemo wa "mfa maji,haishi kutapata" mara hili mara lile kwa kigezo cha kujiita "censors" "see things in a big picture".
Gazeti la Mwananchi leo tena kwaniaba ya "muhandishi wetu" kuna interview ya Sihiyana Mandevu dereva wa tax aliye kuwa akimbeba Nyerere toka wakati wa mtaa wa pemba na New street,Kkoo na New street na wajumbe walele hadi St Joseph ambapo huku wajumbe walibadilika kuwa wengine ambao hakuwafahamu,sasa kama kweli we claim to see thing in that "big picture"....why then we don't connect the dots!!?? Hauitaji kwenda Bweni kujifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…