Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mwanakijiji,

Swali hilo mbona nyie ndiyo wa kulijua zaidi kwa kuwa ndiyo mmeshika madaraka kwa 83%.

Masikini ya mungu sisi nafasi zetu wahudumu, wapika chai, madereva, shamba boy sasa hayo mambo ya huko maofisini ya ufisadi, sijui nini tutayajuaje?

Mohamed
 


Mwanakijiji,

Siasa za Nyerere na wazee wangu zinakuvuruga akili sana. Fikiri na fikiri huo ndiyo usomi. Niwezayo nitakupa majibu nitakayoshindwa ndiyo hivyo tuyaache kama yalivyo.

Yuko mtu kutoka Cambridge University kaja kufanya utafiti wa maisha ya Nyerere kanitafuta na tumezungumza kwa kifupi Insha Allah atakuja nihoji.

Alikotoka wamemwambia ukitaka kumjua Nyerere soma kitabu cha Mohamed Said.

Wasemaje nimlete kwako?

Mohamed
 
Mohammed Said,
Inaonyesha wewe unayajua mengi sana sasa nakuuliza swali hapa..

1. Kwa nini wakati wa Mwinyi Private primary schools zilianzishwa na shule za serikali za Primary waka introduce ada wakati maskini wengi ni waislaam, na matokeo yake drop off kubwa sana ya wananfunzi walijiandikisha darasa la kwanza kuharibu kabisa elimu nchini.

2. Wakati wa Mwinyi kama sikosei ndio mkata wa MoU uliwekwa wakristu wakarudishiwa shule na Hospital zao, OIC walitaka kujenga chuo kikataliwa, Saudia walitaka nao kujenga wakakataliwa chini ya jicho la Mwinyi ambaye umekuwa ukimsifia sana..
 
Simile Mkandara,

Wapi nimemsifia Mwinyi?

Sasa hayo mengine ya Mwinyi siwezi kumjibia.

Mohamed
 
Simile Mkandara,

Wapi nimemsifia Mwinyi?

Sasa hayo mengine ya Mwinyi siwezi kumjibia.

Mohamed
Alaa huyu hayupo ktk wazee wako?...samahani. Nilitegemea sana wewe mwenye taarifa za elimu nchini ungeweza kulijibu hilo kumbe tumuulize Mwinyi basi ya nini nasi kuzungumza ya Nyerere hali mtu wa kujibu hayupo duniani?
 


hao watu wanaomshauri hivyo wanampotosha. Nipe contacts zake huyo jamaa nami nitamsaidia kidogo. Nitumie kwenye ile email yangu.
 
Alaa huyu hayupo ktk wazee wako?...samahani. Nilitegemea sana wewe mwenye taarifa za elimu nchini ungeweza kulijibu hilo kumbe tumuulize Mwinyi basi ya nini nasi kuzungumza ya Nyerere hali mtu wa kujibu hayupo duniani?

Mkandara, pamoja na heshima yote kwangu kwa mzee Said hili la yeye kutumia mamlaka ya watu wasioweza kuulizika (aidha wamekufa au hawataji kwa majina au hajawauliza walio hai) linasumbua sana. kwa mfano Mkapa ni mmoja wa watu waliokuwepo tena ni kijana wakati haya mengi yanatokea na alikuwa ni Mhariri. Lakini sioni hata mara moja Bw. Said akisema kaenda kumuuliza! Mama Maria hataki kumuuliza - kwa kuogopa kumfedhehesha japo anadai mama huyo "anajua yote"; Wakati anaandika kitabu ilimchukua karibu miaka mitano kufanya utafiti wake hadi kuchapa mwaka 1998 - muda wote huo Nyerere alikuwa hai hajawahi kumuuliza badala yake anatusimulia kuwa ni Prof. Othman ambaye alienda kwa Nyerere - na Prof. Othman hayupo - hatuwezi kumuuliza!

Go figure..
 

Acha kusema hivyo na ni kashfa kwa Rais, Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi, Mkuu wa TISS, Wakuu Jeshini, Polisi n.k Wewe ni Mtanzania na unayo haki ya kudai kutoka serikali yako ya Tanzania. Hakuna "SERIKALI YA JAMHURI YA KANISA". Na hakuna mahali katika Katiba yetu panaposema "Wakristu" wana haki zaidi kuliko Waislamu. Labda hujui haki zako kama raia wa Tanzania. Viongozi wote na watendaji wote wanaoishika madaraka katika nchi hii ni kwa sababu ni Watanzania kuanzia wakati wa Nyerere hadi leo hii Waislamu, Wakristu na Wapagani wameshika nafasi mbalimbali.

Kama hushiriki katika kuleta mabadiliko ya kisiasa ya kuwafaa Watanzania wote utabakia kulalamika kwa kuona dhulma ambayo haipo. Shiriki katika mchakato wa mabadiliko ya kisiasa ili Watanzania wote wanufaike na matunda ya uhuru. Wakristu wa Tanzania hawaendi popote nao ni Watanzania, Wapagani hawaendi popote nao ni Watanzania na Waislamu hawaendi popote nao ni Watanzania. Kama walivyofaa wazee wetu kushirikiana kuukataa utawala wa kigeni bila wao kujiangalia dini zao au nani ana nafasi zaidi vivyo na sisi tufanye hivyo. Jiunge na wale wanaotaaka mabadiliko ya kisiasa bila ya kubagua watu; haitoshi kuwaelimisha watu tu juu ya dhulma bila kushiriki kuondoa dhulma hiyo. Usije ukajikuta kuwa wakati unatetea kuondolewa dhulma kumbe wakati huo huo unaanzisha dhulma nyingine.

Unafikiri Serikali ipunguze idadi ya Wakristu wanaoajiriwa serikalini kwa muda fulani ili Waislamu wapewe nafasi hizo?
 

Go figure...indeed strange that he thought he would get away with this...

Kwa kweli mtapata tabu labda mfanye kama alivyokushaurini FF.

Andikeni kitabu.

Nendeni kwa Mama Maria, Mkapa na wengine wengi sana.

Mimi nimekupeni "cue" nishakusafishieni njia.

Sasa hicho kitabu chenu ndiyo kitakuwa jibu la kitabu changu.

Lakini kwa kutaka kujibu kitabu changu kwa sentensi katika JF mtakesha na mimi.

Mwenzenu mimi baada ya kuona wazee wangu wametolewa katika historia nimeandika hilo buku leo unaona nyote mmemjua Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir, Rashid Sisso, Tatu bint Mzee, Bi Mluguru bint Mussa na wengine wengi.

Mmejua kuwa hotuba ya Nyerere iliandikwa toka 1950. Mmejua kuwa kuna historia ya TANU iliyoandikwa siku za mwanzo za uhuru ikapotea na mengine mengi...

Vipi mtachukua hii changamoto?

Mohamed
 
Hapa mbona umewataja Chenge na Lowassa tu? Rostum, Kikwete, Karamagi, Hussein Mwinyi, Ridhwani unawaweka wapi? Ufisadi hauna dini ndugu yangu.

Najua ufisadi hauna dini ila proportion ya mafisadi kati ya waislamu na wakristo wakristo mnaongoza kwa wingi. Kuna Lowassa, Chenge, Sitta, Mwakyembe, Magufuli, Mkapa, Mahalu, MoU etc. Tukivuka zaidi kuna yule aliyekuwapo Tanroads, kuna Mgonja, Mramba, Msuya, Sumaye etc.

Worse zaidi amesimama kiongozi wa dini Askofu mzima na kutamka mbele za watu tusiwaogope mafisadi nikuulize wewe uko tayari kucheka meza moja na mafisadi? That shows kiwango cha maadili maaskofu wengine wanacho na mustakabali mzima wa mafundisho ya kanisa kuwaandaa waumini kuwa watu wema katika jamii. Kama kiongozi wa kiroho ana sawa watu kuiba unafikiri waumini wake wakoje???
 

Kikwetee ni mpika chai?
 
Mada yetu ya historia imeisha? Maana twaanza kuona true colors..
 

Mwanakijiji,

Usiwe na haraka safari yetu Waislamu bado ni ndefu serikali haijakubali kuwa tuna tatizo. Hadi hapo watakapokiri kuna tatizo na kutaka ushauri kipi kifanyike hapo ndipo tutazungumza nini kifanyike.

Kwa sasa tujikite katika kuisihi serikali iamke tuiepushe nchi yetu na vurugu.

Mohamed
 

Baraza la iddi mjini dodoma.
Waislamu walicheka na mtakatifu?
Siyo fisadi yule?
Kumbe ni shujaa.
 
 

Kama muislamu anaongoza nchi na unalalamika itakuwaje akiwa mkristu?
 
Mwanakijiji,

Kikwete utampata katika ile 17% na uzuri wake hili na yeye analijua sana.

Ehe bwana vipi?
Unashindwa kuliona hilo mbona rahisi sana.

Mohamed
 
Baraza la iddi mjini dodoma.
Waislamu walicheka na mtakatifu?
Siyo fisadi yule?
Kumbe ni shujaa.

Una evidence kuwa JK fisadi? Mnamzushia tu JK kila siku subirini kesi ya Ridhiwani na Dr Slaa imalizike mtaelewa JK kama fisadi au la. Hao niliwataja kila mmoja ana liscandal lake kuanzia waliouza wanyama na ardhi kwa waarabu hadi kwa wauzaji wa nyumba za serikali. Turudi katika mada mnacho cha kukosoa kuhusu kazi mohamed said.
 
Mwanakijiji,

Nikusahihishe kidogo.

Diamond 2 Waislam tumekubaliana wakati wa kulalamika umekwisha.
Sasa ni wakati wa "kushughulika vizuuuri."

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…