Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


wale watoto waliomuua gadaffi walikuwa wanatamka neno ambalo gadafi alikuwa analitamka wakati anapigwa ....Alah Akbar
kwa hiyo nina uhakika waislamu wa Tanzania(waliopo madarakani) wanawakandamiza waislamu wenzao(kina MS ) ..sasa ili kutafuta pa kutokea wanawasingizia wakristo..sehemu kama egypt ,tunis(arap rise ) walikuwa hawana mtu wa kumsingizia kama hawa hapa wa TZ
 

Tumseme na kumcriticise JK kwa utendaji wake na sio dini yake mkuu unaniangusha Saint Ivuga ushasahau misimamo yangu kaitka ufisadi?

Ila sipendi tumzungumze JK kwasababu ya dini yake huo ni udini mkuu.

Kuna watu wamefikia kusema kukiwa na kibaragashia Ikulu mambo yanaenda kombo.

Nikuulize wewe utajisikia vp mtu akisema kukiwa na misalaba basi ujue kodi zetu zishaliwa (nimetolea mfano) sidhani kama utapendezeshwa na kauli hizi za udini.
 
Ninavyozidi kuufuatilia huu mjadala ndivyo ninavyozidi kufunguka macho na hivi sasa najiuliza swali moja - Kwa nini ukoo wa Sykes umetoa baraka zake jina lao litumiwe na huyu mchochezi kuvuruga amani na mshikamano wa Watanzania kwa misingi ya dini ? Nasema hivi kwa sababu naamini kama Mohamed Said anafanya haya anayoyafanya kwa baraka zao, basi ni heri hata hiyo historia inayodaiwa imesahauliwa ibaki huko huko. Nasema hivyo kwa sababu moja kuu, kama Nohamed Said atafanikiwa katika mpango wake huo ovu, jina la ukoo wa Sykes kuna siku historia itabidi iwahukumu.

Lakini, naomba nitoe onyo, hata kama hatafanikiwa, na hilo nina hakika nalo asilimia 100% kwa sababu Watanzania wengi ninaowafahamu hawawezi kumuunga mkono mchochezi wa aina ya Mohamed Said, bado jina la ukoo wa Sykes utakuwa umepakwa matope ambayo yatachukua siku nyingi kufutwa. Hebu tuwe great thinkers kidogo, tuseme yatokee machafuko watakaofaidika si vigumu kukisia ni watu gani - ni hao hao watu wa mataifa ya nje ambao wala hawasiti kumsifia mtu kama Mohamed Said, mzaliwa wa Gerezani Dar es Salaam, kwani watavuna matunda ya machafuko anayoyachochea.

Wana JF msione ajabu watu kukesha humu 24/7 ! Tunalala tukiamka wapo tu, tunakwenda kibaruani tukirejea wapo tu, vipi hawa ? Ni kitu gani kinawanyima watu usingizi kiasi hiki, kutetea simulizi na hadithi za Wazee wa Gerezani wa Mohamed Said ? Huyu mtu kaonyesha wazi kuwa ama hajui au anadanganya kuhusu kuanzishwa kwa AA na madhumuni yake. Anamtaja katibu wa kwanza wa AA lakini hamgusii kiongozi wa kwanza wa TAA ambaye angeweza kuwa mmoja tu, hawawezi kuwa wawili. Moja wa Wazee wake anayemtaja alipewa uongozi wa TAA kwa muda mfupi tu mwaka 1952 na akaboronga.

Sasa subirini hadithi nyingine ndeeeefffuu !
 
nimekupata mkuu..ila nadhani wenye mambo hayo ya udini ni 1 kati ya watu 100..
jua kuwa wakristo wapo wa aina nyingi mimi ukristo wangu sio wa kuvaa misalaba...
 
Ndio maana Mwanakiji nikashauri Truth and reconciliation committee iwekwe ili wajadiliane mbele ya jamii ukweli ujulikane na uongo ufahamike.

hili mimi nami nilishalishauri zamani tu; japo kwangu sikutaka iwe Truth and Reconciliation bali Historical Commission on Truth and Unity..

Its complicated Mwanakijiji udini upo na Kanisa lina maovu yake. Asiye muislamu ni ngumu kulifahamu au kulielewa kwani alikuwa analelewa na mfumo huo ndani na hivyo ngumu kuyaona nje ya box.

Hili halina shaka na siwezi kushangaa kwani ni mwanafunzi mzuri tu wa historia ya Kanisa katoliki pote duniani. Lakini kuishia kusema hivyo hakutoshi kwa sababu mtu mwingine anaweza kusema kuwa kutokana na madhara ya utumwa "Uislamu" ulikuwa na maovu yake kisa tu wahusika wake wengine walikuwa ni "Waislamu". Hata unaposema "maovu" ya kanisa yanaweza kabisa kuonesha ni jinsi gani pia Kanisa hilo hilo limefanya mengi sana kwenye jamii ya Watanganyika hadi leo hii na linaendelea kufanya hivyo.

But kwa waislamu ubaguzi unaendelea mpaka leo na kiasi imekuwa sasa hivi Tanzania ni kawaida kuwa wanaonekana ni SECOND CLASS CITIZEN.

Hili linasemwa lakini halina ushahidi wa kihistoria kwa sababu hakuna hoja ya kisayansi ambayo imewezakuoneha ikilinganishwa na vingine. Kwa mfano, ni kwa kiasi gani kwa mfano Wamang'ati na watu wa makabila mengine yanaoishia kijadi wanawakilishwa katika serikali? Je wanabaguliwa? Nani anawabagua? Je, mtu anaweza kusema kuwa Wakristu na Waislamu wanapendelewa Tanzania?

Je ni kweli Wakristu wote wananufaika na mfumo uliopo kiasi kwamba wana interests ya kuona unaendelezwa?


Ni kweli - lakini fikiria kuwa tayari mmeshafikia hitimisho kuwa kuna "dhulma" je watu watakuwa tayari kuambiwa "hakuna" kama uchunguzi yakinifu wa kisayansi na historia ukifanyika? Jibu ni kuwa "haiwezekani" kwa sababu watu wameshahitimisha kuwa kuna dhulma. Hata wewe unaweza kushangaa kabisa endapo tume kama hiyo ikaja na taarifa huru kabisa ya kuonesha kuwa hakuna "systematic discrimination of Muslims"! Utapigwa na butwaa!


Ni jambo moja kutaka kuutafuta ukweli lakini jingine kutaka kuthibitisha kinachodhaniwa kuwa ni kweli. Wengi wameshakubali hoja ya M. Said kuwa kuna dhulma nchini na hawataki kujiuliza maswali yoyote zaidi ya kurudia tu "Waislamu wanadhulumiwa, Waislamu wanadhulumiwa".

Je ndugu yangu Mdondoaji uko tayari kuona inaundwa tume huru ya Historia, Ukweli na Umoja ambayo itafanya kazi yake kwa uwazi na wazi katika kukusanya, kuchambua, kuhifadhi taarifa mbalimbali za historia yetu ikitafuta kujua majibu ya maswali mbalimbali? Je utakuwa open minded kukubali matokeo yake endapo yataenda kinyume na vile ambavyo tayari unaamini?
 
Mag3,
Nadiriki kusema kuwa Mohamed ame "hijack" jina na legacy ya Abdulwahid Sykes kwa malengo yake ya kidini. Hata mimi niko karibu na wanae Abdulwahid. They are not exactly thrilled with Mohamed's jihad.
 
Mohamed,
Hata kama hotuba unayodai aliisoma Nyerere iliandikwa mwaka 1950 tunaomjua Nyerere ni kwamba hakuwa kasuku. Hotuba aliyoisoma UN aliongezea hisia zake. Kwa hilo hatuwezi kukuachia uwajazie watu fikra zao kwamba Nyerere alienda kusoma verbatim hotuba iliyoandikwa 1950 bila kufanyiwa update au bila kuwekwa kwenye mtiririko ambao Nyerere alihisi kuwa comfortable nao. No matter how many times you say it whenever we see you making that claim we will come here to challenge you.
 
Mag3,
Nadiriki kusema kuwa Mohamed ame "hijack" jina na legacy ya Abdulwahid Sykes kwa malengo yake ya kidini. Hata mimi niko karibu na wanae Abdulwahid. They are not exactly thrilled with Mohamed's jihad.

Kama wanae Abdulwahid Sykes wapo bila shaka wanafuatilia huu mjadala unavyoendelea humu ndani ya JF na vita anavyoendesha huyu mchochezi kwa kutumia jina la baba yao mzazi na wanajua fika madhara ambayo yanaweza kusababishwa na hizi porojo za hatari, sasa mimi naomba moja wao ajitokeze atoe kauli ama ya kuunga mkono hoja za Mohamed Said au za kufanya masahihisho pale penye upotoshwaji. Kuna mengi wengine tunayajua na tungeweza kuyasema ila tunaustahi ukoo wa Sykes kwa sababu tunaamini mzee wao Abdulwahid Sykes alishiriki katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kwa nia njema kama Mtanganyika. Yawezekana kuna mahali alitofautiana na Mwalimu Nyerere, hilo lawezekana kwa sababu wote ni binadamu lakini haya madai ya Mohamed Said sasa yanavuka mpaka.
 

halafu unajua hawezi kuiweka hiyo hotuba ya 1950 ili tuilinganishe na ya Nyerere ya 1955 ambayo tunayo ili tuweze kuona ni kwa kiasi gani zinafanana.
 
Kama tunamzushia Kikwete ufisadi vile vile Sumaye na Lowassa wanazushiwa. Kuanzia IPLT, mikataba ya madini, Richmond, Kikwete ni msafi kweli kweli.
 
Kaitafute ile bahasha ya Mang'ula ambayo Mkapa alisema isifunguliwe mbele ya mkutano wa CCM kumjadilia Kikwete. Mkapa aliidismiss kwa kusema kuwa wote CCM ni wachafu. Tunajua kilichomtokea Mang'ula baada ya Kikwete kuukwaa urais. Lakini dondoo na records zipo. Nani alijua Watanzania wangeambiwa juu ya ufisadi wa Mkapa? Ni wachache sana waliobaki wasafi CCM na Kikwete si mmoja wao.
 
Hotuba inasemekana haionekani sehemu yoyote kwa mujibu wa Mzee Said.
Huko kwenye archieve kumebaki ile picha Nyerere akiwa na soksi ndeefu hadi magotini.
Tulishaambiwa kuwa Sykes alitunza nyaraka zake vema sana na ameziona, sijui hakuona draft ya hotuba ya UN!

Wanasayansi wa siasa wanasema, siasa ni kitu 'fuid' kwamba kubadilika kwake ni suala la dakika na sio siku. Kuanzia mwaka 1950 hadi Nyerere alipokwenda UN kulikuwa na mabadiliko makubwa sana. Sina uhakika hiyo hotuba iliyokuwa katika mfumo wa siasa ilishindwaje kubadilika(stagnant) hadi isome vile vile.

Alipofika Dar alikuwa na MA, na alishakuwa na exposure tayari katika masula ya kimataifa.
Mwaka 1950 Nyerere alikuwa hajajulikana sana katika medani ya siasa.
Kama hotuba iliandikwa mwaka 1950, je ilikusudiwa ikasomwe lini na nani ndani ya UN?
 
Alipofika Dar alikuwa na MA, na alishakuwa na exposure tayari katika masula ya kimataifa.
Mwaka 1950 Nyerere alikuwa hajajulikana sana katika medani ya siasa.
Kama hotuba iliandikwa mwaka 1950, je ilikusudiwa ikasomwe lini na nani ndani ya UN?

Tunaambiwa alipofika Dar alikuwa mshamba mshamba hata kuvaa suruali hajui sijui maisha yote aliyokuwa akiishi Scotland alikuwa anavaa nini au wanafunzi wa shule aliyosoma ya Mwisenge na baadaye Tabora walikuwa wanavaa nguo gani!
 
Tunaambiwa alipofika Dar alikuwa mshamba mshamba hata kuvaa suruali hajui sijui maisha yote aliyokuwa akiishi Scotland alikuwa anavaa nini au wanafunzi wa shule aliyosoma ya Mwisenge na baadaye Tabora walikuwa wanavaa nguo gani!
Alipofika Dar alikuwa anavaa Lubega, Unabisha? Ni kuletee ushahidi wa mtu aliyempa pesa za kununua kitambaa cha suruali yadi 3.5.
Fundi aliyemshonea akiitwa naniii. Shati alinunua mtaa wa Narung'ombe senti 15. Hii nimeelezewa na marhum fundi na marhumu muuza duka.
 

Your sense of wit just charmed me!
 
Ndugu zanguni kashfa, kejeli na matusi si sifa ya JF huko mnakoelekea siko mnavunja heshima ya hili jamvi.

Hebu mlanini shetani tulizeni hamaki zenu na tujadili mambo makubwa ya mustkbali ya nchi yetu.

Vinginevyo huu ukumbi utaonekana wa wahuni.

Mohamed
 
hapana miye ndiye nimesema hawezi:

a. Hawezi kuwa nayo - haipo - na hivyo tuamini maneno yake
b. Hata angekuwa nayo hawezi kuiweka kwa sababu hailingani kwa kiasi kikubwa na hotuba aliyoitoa Nyerere UN ambayo tunayo..

Mwanakijiji,

Uzuri wa utafiti na kuandika ndiyo huu.

Vipi nimetoa changamoto ya wewe na wenzako kuandika historia kujibu kitabu changu.

Je mmeipokea hiyo changamoto au mmetoa mbukwa?


Mohamed
 
Mwanakijiji,

Uzuri wa utafiti na kuandika ndiyo huu.

Vipi nimetoa changamoto ya wewe na wenzako kuandika historia kujibu kitabu changu.

Je mmeipokea hiyo changamoto au mmetoa mbukwa?


Mohamed

Kusema kweli ni changamoto nzuri sana na ni matumaini yangu watakuwepo watu ambao wataijibu siku moja na kuonesha kuwa ulichoandika siyo historia kama ilivyokuwa bali historia kama ulivyosimuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…