Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hotuba inasemekana haionekani sehemu yoyote kwa mujibu wa Mzee Said.
Huko kwenye archieve kumebaki ile picha Nyerere akiwa na soksi ndeefu hadi magotini.
Tulishaambiwa kuwa Sykes alitunza nyaraka zake vema sana na ameziona, sijui hakuona draft ya hotuba ya UN!
Wanasayansi wa siasa wanasema, siasa ni kitu 'fuid' kwamba kubadilika kwake ni suala la dakika na sio siku. Kuanzia mwaka 1950 hadi Nyerere alipokwenda UN kulikuwa na mabadiliko makubwa sana. Sina uhakika hiyo hotuba iliyokuwa katika mfumo wa siasa ilishindwaje kubadilika(stagnant) hadi isome vile vile.
Alipofika Dar alikuwa na MA, na alishakuwa na exposure tayari katika masula ya kimataifa.
Mwaka 1950 Nyerere alikuwa hajajulikana sana katika medani ya siasa.
Kama hotuba iliandikwa mwaka 1950, je ilikusudiwa ikasomwe lini na nani ndani ya UN?
Nguruvi3,
Ndugu yangu unaleta hoja nzuri ambazo mimi zinanisisimua tatizo unachukuliwa na hamaki kidogo.
Hii habari ya archive na soksi ndefu ya nini kaka inachafua murua wako isingelikuwa hapo.
Ngoja nikutoa shaka katika hilo la soksi ndefu.
Katika moja ya uzi wangu nilipoona hili suala kaptula linapewa uzito usiostahili nilisema mimi baba yangu akivaa kaptula na stockings akenda kazini. Abdulwahid Sykes akivaa kaptula na stockings akiwa Market Master pale Kariakoo na watu walomuona katika kivazi hicho wu hai. John Iliffe katika "A Modern Histrory of Tanganyika" ameielezea ile picha ya waasisi wa TANU na yeye kenda mbali zaidi kwa kusema kuna tofauti ya mavazi kati ya waasisi waliotoka kwenye majimbo (provinces) na akina Abdulwahid.
Nakuomba sana ndugu yangu tuliache hili la nguo kwa hakika halina tija. Tuzungumze yale yatakayotuongezea ufahamu zaidi wa historia ya nchi yetu.
Nakuomba soma Cranford Pratt, "A Critical Phase in Tanganyika" ameeleza kirefu kuhusu memorandum iliyoandikwa 1950 na TAA Political Sub Comitteee ambayo ilipelekwa kwa Gavana Edward Twinning. Hotuba iliyosomwa Umoja wa Mataifa 1955 imenyambuliwa mle ndani.
Humu ndani nimeeleza kwa kirefu kuhusu jambo hili lakini kama hamuamini wala isiwe tabu hotuba hiyo ni moja tu katika mengi katika historia ya Tanganyika ambayo niko tayari wakati wowote kueleza kwa ajili ya faida ya wanaukumbi.
Kuhusu Nyaraka za Sykes wala usifanye maskhara. Uzione kwa jicho lako ndiyo utaamini. Illife alizitumia hizo kupitia bint yake Abdu, Daisy Sykes kuandika historia ya African Association katika miaka ya katikati ya 1960 wakati Daisy alipokuwa mwanafunzi wake Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Naweka hapa "observations" zangu kuhusu hizi nyaraka kwa faida ya wanaukumbi:
...aliniruhusunisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo zaukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani yasefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini. Nikiyapitiamajalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu nakila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ulewa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli tokakwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo(Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwaAlly Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru;nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabethiliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa RaisAbdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, MwekaHazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwakutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukobakwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa;barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere,Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. Baadaye nilipofanyautafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwambatabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jaladakila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Nijambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazonilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa.Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuwezakuzifungua na kuzisoma. Vilevile vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi zaVita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe.Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfanowake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthaminimchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezocha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi yaNyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo."Waungwana hawabanani.
Mohamed